Agano la Kale 2022
Julai 11–17. 2 Wafalme 17–25: “Alimtumaini Bwana, Mungu wa Israeli”


“Julai 11–17. 2 Wafalme 17–25: ‘Alimtumaini Bwana, Mungu wa Israelii,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Julai 11–17. 2 Wafalme 17–25,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

watu wakiondoka kwenye mji ulioangamizwa

Kutoroka kwa Wafungwa, na James Tissot na wengine

Julai 11–17

2 Wafalme 17–25

“Alimtumaini Bwana, Mungu wa Israeli”

Wakati Yosia aliposikia maneno kutoka katika kitabu cha torati, aliitikia kwa imani. Ni kwa jinsi gani unaweza kuitikia kwa imani kwenye kile ulichokisoma katika 2 Wafalme 17–25?

Andika Misukumo Yako

Licha ya huduma nzuri ya nabii Elisha, maisha ya kiroho ya Ufalme wa Kaskazini wa Israeli yaliendelea kudorora. Wafalme waovu walikuza kuabudu sanamu, na vita na ukengeufu vilishamiri. Mwishowe Himaya ya Ashuru ilishinda na kuyatawanya makabila kumi ya Israeli.

Wakati huohuo, Ufalme wa Kusini wa Yuda ulikuwa haufanyi vizuri sana; kuabudu sanamu kulikuwa kumesambaa huko pia. Ila pamoja na uozo wote huu wa kiroho, maelezo ya maandiko yanataja wafalme wawili wenye haki ambao, kwa muda, waliwageuza watu wao kwa Bwana. Mmoja alikuwa Hezekia. Wakati wa utawala wake, Waashuru, wakiwa ndiyo wametoka kwenye ushindi wao huko kaskazini, waliitwaa sehemu kubwa ya kusini. Ila Hezekia na watu wake walionyesha imani katika Bwana, aliyeikomboa Yerusalemu katika njia ya muujiza. Baadae, baada ya kipindi kingine cha ukengeufu, Yosia alianza kutawala. Akisukumwa kwa sehemu na ugunduzi wa kitabu cha torati, Yosia alileta mabadiliko yaliyoamsha maisha ya kidini ya wengi wa watu wake.

Je, tunajifunza nini kutoka katika hizi nyakati angavu mbili kinyume na miaka ya giza ya historia ya Yuda? Miongoni mwa mambo mengine, unaweza kutafakari nguvu za imani na za neno la Mungu katika maisha yako. Kama Israeli na Yuda, wote tunafanya chaguzi nzuri na mabaya. Na tunapohisi kwamba mabadiliko yanahitajika katika maisha yetu, labda mifano ya Hezekia na Yosia inaweza kutusukuma “kumtumaini Bwana Mungu wetu” (2 Wafalme 18:22).

Ona pia 2 Mambo ya Nyakati 29–35; sehemu ya “Mawazo ya Kuweka Akilini” “Yesu Atasema kwa Israeli Yote, ‘Njooni Nyumbani.’”

Learn More image
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

2 Wafalme 18–19

Ninaweza kubaki mwaminifu kwa Bwana nyakati zote za changamoto.

Wengi wetu tumepitia nyakati ambazo hujaribu imani yetu. Kwa Hezekia na watu wake, mojawapo ya nyakati hizo zilikuja wakati jeshi la Ashuru lilipovamia Yuda, kuharibu miji mingi, na kuisogelea Yerusalemu. Unaposoma 2 Wafalme 18–19, fikiria kwamba uliishi Yerusalemu wakati wa nyakati hizo. Ungeweza kujisikiaje, kwa mfano, kusikia dhihaka za Waashuru kama ilivyoandikwa katika 2 Wafalme 18:28–37 na 19:10–13? Unajifunza nini kutokana na kile Hezekia alichofanya katika kuitikia? (ona 2 Wafalme 19:1–7, 14–19). Ni kwa namna gani Bwana alimhimili Hezekia? (ona 2 Wafalme 19:35–37). Tafakari namna ambavyo amekuhimili wewe katika nyakati za changamoto.

Pia ungeweza kutafakari maelezo ya Hezekia katika 2 Wafalme 18:5–7. Ni nini aya hizi zinapendekeza kuhusu kwa nini Hezekia aliweza kubaki mwaminifu wakati majaribu yalipokuja? Ni kwa jinsi gani unaweza kufuata mfano wake?

Ona pia 3 Nefi 3–4; D. Todd Christofferson, “Thabiti na Imara katika Imani ya Kristo,” Liahona, Nov. 2018, 30–33.

2 Wafalme 19:20–37

Mambo yote yapo katika mikono ya Bwana.

Senakeribu, mfalme wa Ashuru, alikuwa na sababu nzuri kuamini kwamba jeshi lake lingeweza kuishinda Yerusalemu. Ashuru ilikuwa imeyashinda mataifa mengi, ikijumuisha Israeli—kwa nini Yerusalemu pawepo na tofauti yoyote? (ona 2 Wafalme 17; 18:33–34; 19:11–13). Ila Bwana alikuwa na ujumbe kwa Senakeribu, uliotolewa kupitia nabii Isaya, na umeandikwa katika 2 Wafalme 19:20–34. Ni kwa jinsi gani ungeweza kufanyia muhtasari ujumbe huu? Ni kweli zipi unazipata katika mistari hii ambazo zinakusaidia kuwa na imani katika Bwana na mpango Wake?

Ona pia Helamani 12:4–23; Mfundisho na Maagano 101:16.

2 Wafalme 21–23

Maandiko yanaweza kugeuza moyo wangu kumwelekea Bwana.

Je, umewahi kuhisi kwamba ulikuwa umepungukiwa kitu fulani kiroho? Labda ulihisi kwamba uhusiano wako na Mungu ungeweza kuwa wenye nguvu zaidi. Ni nini kilikusaidia kugeuka na kurudi Kwake? Tafakari maswali haya unaposoma kuhusu jinsi Ufalme wa Yuda ulivyoanguka mbali kutoka kwa Bwana chini ya Mfalme Manase (ona 2 Wafalme 21) na jinsi Mfalme Yosia alivyowasaidia wao kujikabidhi tena Kwake (ona 2 Wafalme 22–23). Ni kitu gani kilimshawishi Yosia na watu wake? Maelezo haya yanaweza kukushawishi wewe kufanya upya msimamo wako wa “kumfuata Bwana … kwa moyo [wako] wote, na kwa roho [yako] yote,” (2 Wafalme 23:3).

Unaposoma sura hizi, fikiria pia kujifunza sura ya 6 katika Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball ([2006], 59–68), ambapo Rais Kimball alipendekeza kwamba hadithi ya Mfalme Yosia “ni mojawapo ya hadithi bora katika maandiko yote” (ukurasa wa 62). Kwa nini Rais Kimball alihisi hivyo? Unapata nini katika maneno ya Rais Kimball, hasa maoni yake kuhusu Mfalme Yosia, ambayo yanakusaidia wewe kuitumia 2 Wafalme 22–23 kwenye maisha yako?

Ona pia Alma 31:5; Takashi Wada, “Kusherehekea Maneno ya Kristo,” Liahona, Mei 2019, 38–40; “Josiah and the Book of the Law” (video), ChurchofJesusChrist.org.

familia ikisoma maandiko

Maandiko yanaweza kugeuza mioyo yetu kwa Bwana.

ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

2 Wafalme 19:14–19.Nini tunaweza kujifunza kutokana na mfano wa Hezekia ambacho kinaweza kutusaidia wakati tunapokuwa na matatizo au maswali magumu? Ni kwa jinsi gani Bwana amejibu sala zetu kwa ajili ya msaada? Pengine kila mwanafamilia angeweza kutengeneza kitu cha kuonyesha nyumbani ambacho kinawakumbusha wao kumgeukia Bwana

2 Wafalme 22:3–7.Wafanyakazi wanaoelezewa katika 2 Wafalme 22:3–7 waliaminiwa kwa kupewa hela zilizotumika kujenga upya hekalu “kwa sababu walitenda kazi kwa uaminifu” (msitari wa 7). Baada ya kusoma mistari hii, ungeweza kuwaomba wanafamilia kutaja vitu ambavyo wameaminiwa navyo. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa waaminifu kama wafanyakazi katika mistari hii?

2 Wafalme 22:8–11, 19; 23:1–3.Ni kitu gani kinatuvutia sisi kuhusu namna Yosia na watu wake walivyoitikia neno la Mungu? Ni kwa jinsi gani tunaitikia neno la Mungu katika maandiko? Wanafamilia wako wanaweza kushiriki vifungu vya maandiko au hadithi ambazo zimeongeza hamu yao ya kumfuata Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

2 Wafalme 11:25.Je, ni kitu gani kinajitokeza kwetu kuhusu maelezo ya Yosia katika mstari huu? Wanafamilia yako wangeweza kuchora katika mioyo ya karatasi vitu wanavyoweza kufanya wiki hii kumgeukia Bwana kwa mioyo yao yote.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekeza:“As I Search the Holy Scriptures,” Nyimbo za Kanisa, na. 277.

Kuboresha Kujifunza Binafsi.

Tafuta maneno na virai vyenye mwongozo. Unaposoma, Roho anaweza kuleta maneno fulani au virai kwenye umakini wako. Yanaweza kukupa msukumo na kukushawishi wewe; yanaweza hata kuonekana kama vile yaliandikwa kwa ajili yako.

mtu akileta karatasi lililokunjwa kwa mfalme

Kielelezo cha mwandishi akileta karatasi lililokunjwa la maandiko kwa Mfalme Yosia, na Robert T. BarrettY