Agano la Kale 2022
Julai 18–24. Ezra 1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8: “Hii ni kazi kubwa ninayoifanya mimi”


“Julai 18–24. Ezra 1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8: ‘Hii ni kazi kubwa ninayoifanya mimi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Julai 18–24. Ezra 1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

hekalu la Zerubabeli

Kielelezo cha wa hekalu la Zerubabeli, na Sam Lawlor

Julai 18–24

Ezra 1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8

“Hii ni kazi kubwa ninayoifanya mimi”

Rais Ezra Taft Benson alifundisha, “Neno la Mungu … lina nguvu za kuwaimarisha Watakatifu na kuwakinga wao kwa Roho ili waweze kushinda uovu, kushikilia kwa nguvu wema, na kupata shangwe katika maisha haya” (Teachings of Presidents of the Church: Ezra Taft Benson [2014], 118).

Andika Misukumo Yako

Wayahudi walikuwa wamechukuliwa mateka katika Babeli kwa takribani miaka 70. Walikuwa wameipoteza Yerusalemu na hekalu, na wengi walikuwa wamesahau ahadi kwenye sheria za Mungu. Ila Mungu hakuwa amewasahau wao. Kimsingi, Yeye alikuwa ametangaza kupitia manabii Wake, “Nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa” (Yeremia 29:10). Kuwa mkweli kwa unabii huu, Bwana alitengeneza njia kwa Wayahudi kurudi, na kuinua watumishi waliotimiza “kazi kubwa” kwa ajili ya watu Wake (Nehemia 6:3). Hawa watumishi walikuwa ni pamoja na gavana aliyeitwa Zerubabeli, ambaye alisimamia kujengwa upya kwa nyumba ya Bwana; Ezra, kuhani na mwandishi aliyebadilisha mioyo ya watu kurudi katika sheria ya Bwana; na Nehemia, gavana wa mwisho wa Yuda aliyeongoza kazi ya kujenga upya kuta za ulinzi kuzunguka Yerusalemu. Walikumbana na upinzani, hakika, lakini pia walipokea usaidizi kutoka katika chanzo kisichotarajiwa. Uzoefu wao unaweza kutufahamisha na kutupa misukumo, kwa sababu sisi pia tunafanya kazi kubwa. Na kama kazi yao, kazi yetu ina mengi ya kufanya kuhusiana na nyumba ya Bwana, sheria ya Bwana, na ulinzi wa Kiroho tunaoupata Kwake.

Kwa ajili ya muhtasari wa vitabu vya Ezra na Nehemia, ona “Ezra” na “Nehemia” katika Kamusi ya Biblia.

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Ezra 1

Bwana huwapa misukumo watu kutekeleza makusudi Yake.

Baada ya Uajemi kuishinda Babeli, Mfalme wa Uajemi, Koreshi, alipata msukumo kutoka kwa Bwana kutuma kundi la Wayahudi Yerusalemu kujenga upya hekalu. Unaposoma Ezra 1, angalia kile ambacho Koreshi alikuwa radhi kufanya ili kuwaunga mkono Wayahudi katika kazi hii muhimu. Ni kwa jinsi gani unamwona Bwana akifanya kazi kupitia wanaume na wanawake wanaokuzunguka, ikijumuisha wale ambao si waumini wa Kanisa? Hii inapendekeza nini kwako kuhusu Bwana na kazi Yake?

Ona pia Isaya 44:24–28.

Ezra 3:8–13; 6:16–22

Mahekalu yanaweza kuniletea Shangwe.

Wakati Wababeli walipoivamia Yerusalemu, walipora na kuchoma hekalu na kuliteketeza kabisa (ona 2 Wafalme 25:1–10; 2 Mambo ya Nyakati 36:17–19). Unafikiri ungejihisi vipi kama ungekuwa miongoni mwa Wayahudi walioshuhudia hili? (ona Zaburi 137). Gundua jinsi Wayahudi walivyojisikia, miongo mingi baadae, wakati waliporuhusiwa kurudi nyumbani na kujenga upya hekalu (ona Ezra 3:8–13; 6:16–22). Tafakari hisia zako kuhusu hekalu. Kwa nini mahekalu ni chanzo cha shangwe. Unawezaje kuonyesha shukrani zako kwa Bwana kwa ajili ya mahekalu?

Kwa mifano ya siku za leo ya kufurahi wakati wa ujenzi wa mahekalu, ona video “Practice, Celebration, Dedication: Temple Blessings in El Salvador” na “The Laie Hawaii Temple Youth Cultural Celebration” (ChurchofJesusChrist.org).

5:51
3:13
familia ikitembea katika viwanja vya hekalu

Mahekalu yanaweza kuwa chanzo cha shangwe katika maisha yetu.

Ezra 4–6; Nehemia 2; 46

Ninaweza kusaidia kazi ya Mungu kusonga mbele licha ya upinzani.

Kazi ya Bwana mara chache huenda bila pingamizi, na hii ilikuwa hakika kwa juhudi zilizoongozwa na Zerubabeli na Nehemia. Katika hali zote mbili, “adui za Yuda” (Ezra 4:1) walikuwa Wasamaria—uzao wa Waisraeli ambao walichanganyikana na Watu wa Mataifa. Kusoma kuhusu upinzani wao kuhusu kujenga hekalu (ona Ezra 4–6) kunaweza kukuongoza wewe kutafakari upinzani ambao kazi ya Mungu inaupata leo na jinsi unavyoweza kuitikia wakati upinzani unapokuja.

Sawa na hilo, kusoma kuhusu kazi za Nehemia akikarabati kuta za Yerusalemu (ona Nehemia 2; 46) kunaweza kukufanya wewe kuakisi juu ya kazi ambazo Mungu anakutaka uzifanye. Je, unajifunza nini kutoka katika mfano wa Nehemia?

Ona Dieter F. Uchtdorf, “Tunafanya Kazi Kubwa na Hatuwezi Kutulia,” Liahona, Mei 2009, 59–62.

Ezra 7; Nehemia 8

Ninabarikiwa pale ninaposoma maandiko.

Hata baada ya hekalu kujengwa upya, watu wa Yerusalemu waliendelea kuhangaika kiroho, kiasi fulani kwa sababu, kwa vizazi vingi, walikuwa na nafasi finyu ya kupata “kitabu cha torati ya Musa” (Nehemia 8:1). Ezra mwandishi alipokea ruhusa kutoka kwa Mfalme wa Uajemi kwenda Yerusalemu, ambapo yeye alileta torati mbele ya kusanyiko” (Nehemia 8:2). Unawezaje kufuata mfano wa Ezra kama ilivyoelezwa katika Ezra 7:10? Unaposoma Nehemia 8, ambayo inakupa maelezo ya Ezra akiwasomea watu torati, ni mawazo gani unakuwa nayo kuhusu nguvu za neno la Mungu katika maisha yako?

Ona pia Mafundisho: Ezra Taft Benson, 115–24.

ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Ezra 3:8–13; 6:16–22.Ni kwa jinsi gani Wayahudi walionyesha shangwe yao kwa ajili ya hekalu lilipokuwa linajengwa upya na wakati linawekwa wakfu? Je, tunafanya nini ili kuonyesha shangwe yetu kwa ajili ya hekalu? Labda familia yako ingeweza kutazama picha za mahekalu na kuzungumza kuhusu mahekalu yanavyoweza kuwaletea shangwe (ona temples.ChurchofJesusChrist.org).

Ezra 7:6, 9–10, 27–28.Mara nyingi katika mistari hii, Ezra aliandika kwamba mkono wa Bwana ulikuwa juu yake alipokuwa akisafiri kwenda Yerusalemu. Kirai hiki kinaweza kumaanisha nini? Ni kwa jinsi gani tumehisi mkono wa Bwana juu yetu? Pengine wanafamilia wanaweza kushiriki mifano kutoka kwenye maisha yao wenyewe.

Nehemia 2; 46.Hadithi ya Nehemia inaweza kuwapa msukumo wanafamilia wanapokabiliana na upinzani wanapokuwa wanafanya “kazi kubwa” (Nehemia 6:3). Wanafamila wanaweza kujenga ukuta kutoka katika vitu vinavyowazunguka hapo nyumbani wakati mnaposoma kwa pamoja vifungu muhimu (kama vile Nehemia 2:17–20; 4:13–18; 6:1–3). Ni nini tunajifunza kutoka kwa Nehemia kuhusu kukabiliana na upinzani? Ni kazi ipi kubwa Bwana anatutaka sisi tuifanye? Je, ni kwa jinsi gani Bwana ametuimarisha kushinda upinzani kwenye kazi hii?

Nehemia 8:1–12.Katika Nehemia 8, Ezra anasoma torati ya Musa kwa watu waliokuwa na shauku ya kusikia neno la Mungu. Kusoma mistari 1–12 kunaweza kuimarisha kuthamini kwa familia yako katika neno la Mungu. Ni kwa namna gani watu walihisi kuhusu sheria ya Mungu? Tunawezaje kusaidiana “kuelewa yaliyosomwa”? (mstari wa 8).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Shirikini maandiko kama familia. Wakati wa kujifunza kwenu maandiko kama familia, waruhusu wanafamilia kushiriki vifungu vya maandiko ambavyo vina maana kwao hasa.

Ezra akiwasomea watu maandiko

Kielelezo cha Ezra akiwasomea watu maandiko huko Yerusalemu, na H. Willard Ortlip, © Providence Collection/licensed from goodsalt.com