Njoo, Unifuate
Jumapili ya Kwanza


“Mkutano wa Baraza wa Jumapoili ya Kwanza,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Ukuhani wa Melkizedeki na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama (2017)

Mikutano ya Jumapili ya Kwanza ya Baraza

Mikutano ya Jumapili ya Kwanza ya Baraza

Jumapili ya kwanza ya kila mwezi, mikutano ya akidi, kundi, na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama haitajumuisha somo linalofundishwa na mwalimu. Badala yake, urais na viongozi wa makundi wataongoza mkutano wa baraza. Kila akidi, kundi, au Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama watashauriana kwa pamoja kuhusu majukumu ya sehemu zao, nafasi, na changamoto; wanajifunza kutoka kwa ufahamu na uzoefu; na kupanga njia za kushughulikia misukumo iliyotoka kwa Roho.

“Ufunuo umeenea miongoni mwetu.”1

Mzee Neil L. Andersen

Kabla ya Mkutano wa Baraza

  • Viongozi wanatambua majukumu enyeji, fursa, na changamoto na kwa maombi kuchagua mada itakayojadiliwa.

  • Kila mtu hutafuta ushauri wa Roho.

  • Kila mtu hujitayarisha kushiriki mawazo na uzoefu.

Picha
Kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wakikutana pamoja

Wakati wa Mkutano wa Baraza

  • Viongozi wanawaalika waumini kushiriki uzoefu wakifuata mawazo waliyopata kutoka kwa mikutano ya awali.

  • Kila mtu anashauriana kwa pamoja kuhusu mada hiyo, wanawasikiliza wenzao, na kutafuta ushauri wa Roho.

  • Viongozi hujumlisha hoja kuu na kutoa mialiko kwa utendaji

Picha
Mkutano wa Baraza la Ukuhani wa Melkizedeki

Baada ya Mkutano wa Baraza

  • Kila mtu anashughulikia misukumo na mialiko, kwa pamoja na kama mtu binafsi.

  • Kila mtu anajiandaa kushiriki uzoefu wao katika mikutano ijayo.

Picha
Kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wakikumbatiana.

“Sisi ni Mikono Yake.”2

Rais Dieter F. Uchtdorf

Picha
Taarifa ya mchoro wa njoo, unifuate

Taswira ya Sala kutoka Getty Images

Kanuni za Kushauriana Pamoja

Sio mikutano yote ya baraza inafanana. Acha Bwana awafundishe. Hizi ni kanuni kadhaa za kukuwezesha kuanza:

  1. Kusudi la mkutano wa baraza ni kushauriana kwa pamoja kuhusu majukumu enyeji, nafasi, na changamoto; wanajifunza kutoka kwa ufahamu na uzoefu; na kupanga njia za kushughulikia misukumo iliyotoka kwa Roho.

  2. Mkutano wa baraza unapaswa kusababisha kitendo—mipango ya kibinafsi au kundi, ambayo imeongozwa na Roho, kutenda nje ya mkutano kutimiza kazi ya Bwana (ona M&M 43:8–9).

  3. Mabaraza yanapaswa kutumia maandiko na maneno ya manabii na mitume wa siku za mwisho, Viongozi wengine Wakuu, na Maafisa Wakuu kuongoza na kusaidia majadiliano. Kwa njia hii, maneno yenye msukumo ya viongozi wa Kanisa yanaweza kusaidia akidi, makundi, na Miungano ya Usaidizi ya Kina Mama kushughulikia mahitaji muhimu.

  4. Majadiliano hayapaswi kugusia siri au maswala nyeti kuhusu watu binafsi au familia.

  5. Hata ingawa mkutano wa baraza unaongozwa na mshiriki wa urais au uongozi wa kundi, yeye hatawali ushiriki. Kiongozi anawasilisha hoja ya kujadiliwa na kualika kila mtu kushiriki mawazo na uzoefu, akiongozwa na Roho.

  6. Ingawa hapapaswi kuwa na yeyote anayehisi kushinikizwa ashiriki, kila mtu anafaa kuhisi salama kushiriki maoni na mawazo bila ya kuogopa kukosolewa.

  7. Inapowezekana, kuketi kwenye duara kunaweza kukuza roho ya kushiriki na majadiliano yenye uwazi.

Mada Zinazoweza Kufaa kwa Mikutano ya Baraza la Jumapili ya Kwanza.

Mawazo ya mada za kujadili katika mikutano ya baraza yanaweza kutoka kwa baraza la kata, mikutano ya urais, mpango wa eneo, mawazo ya kiongozi yanayotokana na kuwahudumia waumini, na misukumo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Mada zifuatazo ni mapendekezo tu. Viongozi wanaweza kufahamu kuhusu mahitaji mengine ambayo wanahisi wametiwa msukumo kushughulikia.

  • Tunawezaje kuyapatia majukumu yetu yote kipaumbele vyema kwa njia tofauti zinazowezekana?

  • Tunawezaje kumkaribia Mungu na kupokea ushauri zaidi kutoka kwa Roho maishani mwetu na nyumbani kwetu?

  • Ni kwa namna gani tutashiriki injili pamoja na marafiki na majirani zetu? (ona Alma 17).

  • Tunawezaje kujilinda wenyewe pamoja na familia zetu dhidi ya njia mbovu za mawasiliano na ponografia? (ona M&M 42:22-23).

  • Je, tutafanya nini kusaidia kuwashauri na kuwaimarisha watoto wetu na vijana katika kata yetu?

  • Tunawezaje kuzidisha umoja katika akidi yetu, kundi letu, au Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama? (Ona Mosia 18:19-22.)

  • Ni kwa namna gani tunaweza kushiriki katika kazi ya historia ya familia na ibada ya hekalu?

  • Ni kwa namna gani tunaweza kualika usaidizi wa Bwana kutafuta majibu kwa maswali yetu na kuelewa kwa kina injili?

  • Ni kwa namna gani wazazi wanaweza kuwa viongozi bora nyumbani?

  • Tunawezaje kuimarisha ushuhuda wetu wa Bwana na Injili Yake na kusaidia familia zetu kujitegemea kiroho?

  • Huduma ina maana gani? Tunawahudumia kwa njia gani wale walio karibu nasi? (ona 1 Petro 4:11).

Ikiwezekana, viongozi waweza kutaka kuwajulisha washiriki mapema kuhusu mada ili waweze kuja wakiwa tayari kuijadili.

Muhtasari

  1. Neil L. Andersen, in Adam C. Olson, “Handbook Training Emphasizes Work of Salvation,” Ensign or Liahona, Apr. 2011, 76.

  2. Dieter F. Uchtdorf, “You Are My Hands,” Ensign or Liahona, Mei 2010, 68.

Chapisha