Njoo, Unifuate
Kuna Tofauti Gani?


“Kuna Tofauti Gani?” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Ukuhani wa Melkizedeki na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama (2017)

Kuna Tofauti Gani?

Kuna Tofauti Gani?

Katika hizi siku za mwisho, Mungu amerejesha ukuhani na kupanga akidi za ukuhani na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ili kumsaidia kukamilisha kazi Yake (ona Musa 1:39). Kwa hivyo, kila Jumapili wakati tunapokutana katika mikutano ya Ukuhani wa Melkizedeki na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, tunakutana kujadili na kupanga jinsi tutakavyotimiza kazi Yake. Hii ndiyo sababu mikutano hii inahitaji kuwa zaidi ya madarasa. Pia ni nafasi za kushauriana kuhusu kazi ya wokovu, jifunzeni pamoja kutoka kwa mafundisho ya viongozi wa Kanisa kuhusu kazi hiyo, na kupanga kuitimiza. Mabadiliko haya katika mikutano yetu ya Jumapili yatatusaidia kutimiza madhumuni haya.

Ratiba ya Kila Mwezi

Mikutano ya Jumapili ya Ukuhani wa Melkizedeki na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama itafuata ratiba hii ya kila mwezi:

Wiki

Madhumuni

Jumapili ya Kwanza

Fanyeni mashauriano pamoja juu ya majukumu, fursa na changamoto na mfanye mipango ya kutenda

Jumapili ya Pili na ya Tatu

Jifunze jumbe za mkutano mkuu wa hivi karibuni zilizochaguliwa na urais au kiongozi wa kundi au, wakati fulani, na askofu au rais wa kigingi

Jumapili ya Nne

Jadili mada maalum iliyochaguliwa na Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

Jumapili ya Tano

Shughulikia mada iliyochaguliwa na uaskofu

Mkutano wa Baraza la Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Utaratibu Wa Mikutano Yetu

Katika kila mojawapo ya mikutano ya Ukuhani wa Melkizedeki na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, tunafuata utaratibu kutimiza kazi ya Mungu.

  1. Shiriki Uzoefu unaotokana na mawazo na mialiko iliyopokelewa katika mikutano ya ukuhani na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama (ikiongozwa na urais au kiongozi wa kundi).

  2. Fanyeni ushauri pamoja (Jumapili ya Kwanza, ikiongozwa na urais au mshiriki katika kundi) au mjifunze pamoja (Jumapili ya pili, tatu, na ya nne, ikiongozwa na mwalimu aliye na mwito).

  3. Fanya mpango wa kutenda kama kundi au kama watu binafsi (mkiongozwa na urais au kiongozi wa kundi).