Njoo, Unifuate
Jumapili ya Nne


“Mikutano ya Jumapili ya Nne,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Ukuhani wa Melkizedeki na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama (2017)

Mikutano ya Jumapili ya Nne

Mikutano ya Jumapili ya Nne

Jumapili ya nne ya kila mwezi, akidi, vikundi, na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama watajadili mada iliyochaguliwa na Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Mada hizi zitatengenezwa upya kwa kila mkutano mkuu. Mada itakayokuwa hadi mkutano mkuu ujao itakuwa siku ya Sabato. Viongozi au waalimu wanaweza kuchagua kutoka kwa mafundisho na shughuli za kujifunza zifuatazo, waunganishe baadhi, au wajitengenezee yao wenyewe kulingana na mahitaji ya washiriki.

Sabato ni siku ambayo tunakumbuka kile ambacho Mungu ametutendea.

Kote katika historia, Mungu amehusisha kazi fulani kuu na Sabato. Kazi hizi kuu ni pamoja na Uumbaji (ona Mwanzo 2:1–3), kutoka kwa wana wa Israeli kutoka Misri (ona Kumbukumbu la Torati 5:15), na Ufufuo wa Mwokozi (ona Yohana 20:1–19; Matendo 20:7). Waalike washiriki watathmini vifungu hivi na kujadiliana jinsi kukumbuka kila moja ya matukio haya inaweza kutusaidia kuheshimu siku ya Sabato. Ni yapi baadhi ya mambo makuu ambayo Mungu ametutendea? Tunawezaje kukumbuka mambo haya siku ya Sabato vipi? Inavyofaa, waalike washiriki wajadiliane maswali kama haya katika familia zao.

Yesu Kristo ndiye Bwana wa Sabato.

Sabato pia inaitwa siku ya Bwana (ona Ufunuo 1:10). Kwa nini unafikiri Yesu Kristo anaitwa Bwana wa siku ya Sabato? (ona Mathayo 12:8). Fanyeni tathmini kwa aya kadhaa ambazo zinaweza kuwasaidia waumini kufikiria kuhusu mbinu za kulenga uzoefu wao wa siku ya Sabato kwa Yesu Kristo (kwa mfano, Helamani 5:12; Etheri 12:41; Moroni 10:32; na M&M 6:36–37). Ni aya gani zingine ambazo waumini wanaweza kushiriki ambazo zinaweza kuwasaidia kufanya Sabato kulenga Kristo zaidi. Ni malengo gani tunayoweza kuweka ili yatusaidie kulenga Mwokozi siku mzima ya Sabato?

Yesu Kristo ndiye Mfano wetu wa kuheshimu Sabato.

Wakati wa huduma Yake duniani, Mwokozi alichukua nafasi kufundisha kuhusu siku ya Sabato. Waulize waumini wasome simulizi hizi na watengeneze orodha ya vitu ambavyo Yesu alifanya siku ya Sabato na kanuni ambazo alifundisha: Luka 6:1–11; 13:11–17; Yohana 5:1–20; 9:1–16. Ni kanuni gani zingine kuhusu Sabato tunazojifunza kutoka katika aya zifuatazo.? Kutoka 20:8–11; 31:12–18; Isaya 58:13–14; and M&M 59:9–19. Waalike waumini washiriki kile wanachoweza kufanya ili kufuata mfano wa Mwokozi.

Ona pia Russell M. Nelson, “The Sabbath Is a Delight,” Ensign au Liahona, Mei 2015, 129–32.

Sabato ni siku ya kuabudu.

Andika neno abudu kwenye ubao na uulize washiriki wa darasa waandike maneno mengine yanayohusiana nalo. Kisha watengeneze minara mitatu ya maneno hayo kabla, wakati wa, na baada juu ya kila mnara. Ni nini tunachoweza kufanya kabla, wakati wa, na baada ya kanisa ili kumwabudu Bwana kwa siku Yake takatifu? Washiriki wa darasa wanaweza kusoma pamoja Mosia 18:17–29 na Moroni 6 kwa mawazo. Waalike waumini watafakari jinsi mitazamo na vitendo vyao siku ya Sabato inawasaidia kuabudu Bwana siku hiyo (ona Kutoka 31:16–17). Ni nini tunachoweza kufanya ili kuboresha hali ya kuabudu ya familia zetu na waumini wa kata ambacho wanapata wakati wa mikutano ya kanisa?

Kupokea sakramenti kunaturuhusu sisi kuwa na Roho daima.

Andika swali lifuatalo ubaoni: Ni kwa namna gani sakramenti inaathiri maisha yako? Kujibu swali hili, waalike waumini kushirikiana wawili wawili kuchagua na kujadili kirai kimoja kutoka kwa sala za sakramenti katika Mafundisho na Maagano 20:77, 79 na ushauri kutoka Mafundisho na Maagano 59:9. Patia kila kikundi muda wa kutafuta maandiko ambayo yatawasaidia kuelewa bora kirai chao na kujadili jinsi watalijibu swali lililo ubaoni. Waweza pia kuwaalika washiriki wa darasa kuchagua nyimbo za injili wanazozipenda zaidi na kuziimba pamoja.

Ona Pia Cheryl A. Esplin, “The Sacrament—a Renewal for the Soul,” Ensign au Liahona, Nov. 2014, 12–14.

Sabato ni siku ya kuwahudumia wengine.

Ni nini tunachoweza kujifunza kuhusu kuwahudumia wengine siku ya Sabato kutokana na njia ambazo Mwokozi aliwahudumia na kuwabariki wale waliokuwa karibu naye? Wahimize washiriki watathmini na kujadili Mathayo 9:10–13; Luka 19:1–9; Yohana 11:32–46; 13:1–5, 12–17; na 3 Nefi 17:5–10. Waulize washiriki wafikirie kuhusu maandiko haya huku wakizingatia jinsi wanavyoweza kuhudumu siku ya Sabato. Kwa mfano, wanaweza kuwahudumia wanafamilia, kutoa usaidizi kwa watu na familia wanazohudumia kama waalimu wa nyumbani na wa kutembelea, washughulikie historia ya familia, wawatembelee wagonjwa, au washiriki injili. Pengine washiriki wanaweza kuwa na baraza la familia kupanga njia ambazo wanaweza kuwahudumia wengine siku ya Sabato’

Picha
Kumhudumia mwanamke mzee mgonjwa kitandani

Chapisha