Njoo, Unifuate
Desemba 30–Januari 5 Kurasa za utangulizi za Kitabu cha Mormoni: “Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo”


“Desemba 30–Januari 5. Kurasa za utangulizi za Kitabu cha Mormoni: ‘Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Desemba 30–Januari 5. Kurasa za utangulizi za Kitabu cha Mormoni,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
mabamba ya dhahabu.

Desemba 30–Januari 5

Kurasa za utangulizi za Kitabu cha Mormoni

“Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo”

Anza maandalizi yako ya kufundisha kwa kusoma Kitabu cha Mormoni ukurasa wa jina na dibaji; shuhuda za Mashahidi Watatu, Mashahidi Wanane, pamoja na Nabii Joseph Smith; na “Maelezo Mafupi kuhusu Kitabu cha Mormoni.” Tafakari jinsi unavyoweza kuwapa muongozo wa kiungu watoto kujifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kushiriki hadithi wanazozijua kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni, kwa kutumia picha 67–86 kwenye Kitabu cha Sanaa za Injili au picha zingine ulizonazo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni kinaweza kunisaidia mimi kuwa na imani katika Yesu Kristo.

Wasaidie watoto kujua kwamba lengo la Kitabu cha Mormoni ni kutoa ushuhuda wa Yesu Kristo.

Shughuli za Yakini

  • Nyanyua juu Kitabu cha Mormoni, na uonyeshe kichwa cha habari kidogo, Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo. Acha watoto wafanye zamu kusema, “Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo.” Kwa ufupi waambie watoto jinsi gani Kitabu cha Mormoni kimeimarisha imani yako katika Yesu Kristo.

  • Simulia hadithi kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni ambayo hufundisha kuhusu Yesu Kristo, kama vile tukio la Samueli Mlamani akitoa unabii wa Kristo (ona Helamani 14–16), Mwokozi akiwabariki watoto (ona 3 Nefi 17), au Kaka wa Yaredi akimwona Yesu Kristo (ona Etheri 2–3). Milango kutoka kwenye Hadithi za Kitabu cha Mormoni (na video zinazohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org) zinaweza kusaidia. Waonyeshe watoto kile tunachojifunza kuhusu Yesu kutoka kwenye hadithi hizi. Waambie kwamba watajifunza mambo mengi kuhusu Yesu Kristo kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni mwaka huu.

  • Imbeni wimbo kuhusu Kitabu cha Mormoni, kama vile “Hadithi za Kitabu cha Mormoni” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 118 ). Imbeni wimbo huo pamoja mara kadhaa, na acha watoto wafanye zamu kushikilia picha ya Mwokozi wakati mkiimba.

Dibaji ya Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni ni jiwe la katikati la tao la dini yetu.

Rais Thomas S. Monson alielezea: “Kama [Kitabu cha Mormoni] ni cha kweli—na mimi kwa dhati ninashuhudia kwamba ndipo—hapo Joseph Smith alikuwa nabii … , Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni Kanisa la Bwana duniani, na ukuhani mtakatifu wa Mungu umerejeshwa” (“Nguvu ya Kitabu cha Mormoni,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 86–87).

Shughuli za Yakini

  • Wasomee watoto maelezo yafuatayo ya Joseph Smith ndani ya dibaji ya Kitabu cha Mormoni: “Kitabu cha Mormoni [ni] jiwe la katikati la tao la dini yetu.” Elezea kwamba kama vile jiwe la pembeni linavyounganisha sehemu zote za tao, ushuhuda wetu wa Kitabu cha Mormoni huunganisha na kuimarisha ushuhuda wetu wa mambo mengine, kama Joseph Smith na injili.

  • Mwalike mzazi wa mmoja wa watoto kushiriki uzoefu wa jinsi gani alipokea ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni. Soma pamoja na watoto mwaliko unaopatikana mwisho wa dibaji ya Kitabu cha Mormoni, na wasaidie kuigiza mambo wanayoweza kufanya ili kupata shuhuda zao.

Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith

Kitabu cha Mormoni kilitolewa kwetu kwa nguvu ya Mungu.

Ushuhuda wa Joseph Smith unaweza kuwasaidia watoto kuelewa lengo takatifu la Kitabu cha Mormoni.

Shughuli za Yakini

  • Kwa ufupi wasimulie watoto hadithi ya ujio wa Kitabu cha Mormoni kama ilivyoelezewa katika “Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith.” Unaweza pia kutumia “Mlango wa 1: Jinsi Tulivyopata Kitabu cha Mormoni” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 2–4, au video inayohusiana katika ChurchofJesusChrist.org). Wasaidie watoto kuigiza hadithi mara kadhaa pale unaporudia kuisimulia.

  • Waonyeshe watoto mfano wa michoro kutoka kwenye mabamba ya dhahabu. Elezea kwamba Mungu alimsaidia Joseph kutafsiri michoro hii kwenda kwenye maneno ambayo tunaweza kusoma na kuelewa.

    Picha
    Bamba mbili za shaba zikionyesha michoro iliyoandikwa

    Joseph Smith alitafsiri michoro iliyoandikwa kwenye mabamba ya shaba.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni hunisaidia kuwa na imani katika Yesu Kristo.

Kumbuka kwamba lengo lako katika kuwafundisha watoto kuhusu Kitabu cha Mormoni ni kujenga imani yao katika Mwokozi.

Shughuli za Yakini

  • Gawa darasa katika jozi. Alika kila jozi kusoma aya ya pili ya ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni, ukitafuta kitu ambacho kinawaambia ni nini Kitabu cha Mormoni kimekusudiwa kufanya. Kisha alika kila jozi kushiriki pamoja na darasa.

  • Wasaidie watoto kupata katika ukurasa wa jina kirai “kuwathibitishia Myahudi na Myunani kwamba Yesu ndiye Kristo.” Ni kwa jinsi gani Kitabu cha Mormoni hututhibitishia kwamba Yesu ndiye Kristo? Waalike kushiriki hadithi kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni ambayo imeimarisha imani yao katika Kristo, au shiriki hadithi yako mwenyewe.

Dibaji ya Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni ni jiwe la katikati la tao la dini yetu.

Kupata ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni kutawasaidia watoto kujua kwamba Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni Kanisa la kweli la Mungu.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto wajichukulie kana kwamba hujawahi kamwe kusikia juu ya Kitabu cha Mormoni kabla. Waalike kufanya kazi na mwenza kufikiria juu ya njia ambazo wangeweza kutumia kukuelezea Kitabu cha Mormoni ni nini na wapi kilitoka, wakitumia maelezo kutoka kwenye dibaji. Kisha acha kila jozi ifanye zamu kukufundisha. Picha Biblia na Kitabu cha Mormoni hushuhudia juu ya Kristo (ChurchofJesusChrist.org) ingeweza pia kusaidia.

  • Mwalike mtoto asome maelezo ya Joseph Smith katika aya ya sita ya dibaji. Kwa kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki, elezea jinsi jiwe la katikati linavyounganisha tao. Kulingana na aya ya mwisho ya dibaji, ni mambo gani mengine tunajua pale tunapopata ushuhuda kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli?

Ushuhuda wa Mashahidi Watatu”; “Ushuhuda wa Mashahidi Wanane

Ninaweza kuwa shahidi wa Kitabu cha Mormoni.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kupata na kushiriki shuhuda zao za Kitabu cha Mormoni?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuelezea kitu ambacho wameona ambacho hakuna mwingine yeyote darasani amekiona. Elezea kwamba Kitabu cha Mormoni kina shuhuda za watu 11 tofauti na Joseph Smith ambao waliona mabamba ya dhahabu ambayo kwayo Kitabu cha Mormoni kilitafsiriwa. Someni shuhuda pamoja. Kwa nini mashahidi hawa walitaka watu wengine wajue kuhusu shuhuda zao?

  • Uliza kama mtoto yeyote angependa kushiriki ni kwa jinsi gani wanajua Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Someni pamoja Moroni 10:3–5, na mwalike kila mtoto kusoma Kitabu cha Mormoni mwaka huu na kupata au kuimarisha ushuhuda wake kwamba ni cha kweli. Waambie watoto jinsi ulivyopata ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kama inawezekana, hakikisha kwamba kila mtoto ana nakala ya Kitabu cha Mormoni, na waalike kuanza kukisoma wao wenyewe na pamoja na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tafuta mwongozo wako mwenyewe. Badala ya kuichukulia mihutasari hii kama maelekezo ambayo ni lazima uyafuate pale unapofundisha, itumie kama chanzo cha mawazo kuanzisha mwongozo wako wa kiungu unapotafakari mahitaji ya watoto unaowafundisha.

Chapisha