Njoo, Unifuate
Januari 20–26. 1 Nefi 11–15: “Kujikinga kwa Utakatifu na kwa Nguvu za Mungu”


“Januari 20–26. 1 Nefi 11–15: ‘Kujikinga kwa Utakatifu na kwa Nguvu za Mungu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Januari 20–26. 1 Nefi 11–15” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
watu wakila tunda la mti wa uzima

Tamu Zaidi ya Utamu Wote, na Miguel Angel González Romero

Januari 20–26

1 Nefi 11–15

“Kujikinga kwa utakatifu na kwa Nguvu za Mungu”

Soma 1 Nefi 11–15 ukiwa na watoto unaowafundisha mawazoni mwako, na uandike misukumo yoyote unayopokea.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha ya ono la Lehi la mti wa uzima, na waalike watoto kushiriki kile wanachokumbuka walipojifunza kuhusu ono hili wiki iliyopita. Waulize kama wamejifunza jambo lolote jipya kuhusu ono tangu wakati huo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

1 Nefi 11:16–33

Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo duniani kwa sababu ananipenda.

Nefi aliona maisha na huduma ya Yesu Kristo katika ono. Tafakari kile watoto katika darasa lako wangeweza kujifunza kuhusu Mwokozi kutoka 1 Nefi 11.

Shughuli za Yakini

  • Mpe kila mtoto picha ambayo huelezea kwa mfano mojawapo ya matukio kutoka kwenye maisha ya Mwokozi lililotabiriwa katika 1 Nefi 11:20, 24, 27, 31, na 33 (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 30, 35, 39, 4257). Unaposoma mistari hii, waombe watoto kunyanyua juu picha zao pale wanaposikia mstari unaolandana nao.

  • Waambie watoto kuhusu baadhi ya mambo Nefi aliyojifunza ambayo Yesu Kristo angefanya kipindi cha maisha Yake (ona 1 Nefi 11:16–33, na waonyeshe picha kadhaa za baadhi ya matukio haya (ona, kwa mfano, Kitabu cha Sanaa za Injili, namba. 41, 46, 47, 49, 56, 57, 58, 59). Shiriki kile ambacho Mwokozi amekutendea. Onyesha picha kuwasaidia watoto kufikiria jinsi tunavyoweza kushiriki upendo wa Mungu (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 109, 110, 115).

1 Nefi 13:26–29, 35–36, 40

Kitabu cha Mormoni Kinafundisha kweli zenye thamani.

Kwa nini una shukrani kwa sababu ya Kitabu cha Mormoni? Fikiria jinsi unavyoweza kushiriki ushuhuda wako wa Kitabu cha Mormoni pamoja na watoto.

Shughuli za Yakini

  • Chora picha ubaoni, na waalike watoto kubadili au kuondoa sehemu za picha kuifanya ionekane tofauti. Wasaidie kuelewa kwamba, kama vile picha hii, baadhi ya vitu ndani ya Biblia vilibadilishwa na kuondolewa baada ya muda. Soma sehemu za 1 Nefi 13:40 ambazo zinafundisha jinsi Kitabu cha Mormoni (ambacho Nefi anakiita “haya maandishi ya mwisho”) hutusaidia kuelewa “vitu vilivyo wazi na vyenye thamani” ambavyo vilipotea kutoka kwenye Biblia.

  • Ficha kuzunguka chumba picha zinazowakilisha kweli za injili ambazo zimefafanuliwa ndani ya Kitabu cha Mormoni, kama vile ubatizo, sakramenti, na ufufuo. Waalike watoto kutafuta picha hizi. Elezea kwamba Kitabu cha Mormoni kilirudisha kweli za injili ambazo zilikuwa zimepotea.

1 Nefi 15:23–25

Neno la Mungu hunipatia nguvu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia mfano wa fimbo ya chuma kuwafundisha watoto kuhusu nguvu, ulinzi na nguvu ya neno la Mungu?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha ya ndoto ya Lehi, kama ile iliyoko kwenye muhtasari wa wiki iliyopita katika Njoo Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waalike watoto kutafuta fimbo ya chuma kwenye picha, na wasaidie kujua ni kwa jinsi gani kushikilia neno la Mungu kunaweza kutulinda (ona 1 Nefi 15:23–24). Wape watoto kitu kinachofanana na fimbo ya chuma washikilie, kama vile bomba au fimbo, wakati ukisoma mstari wa 24. Wapi tunapata neno la Mungu? Tunaweza kufanya nini kulifanya neno la Mungu sehemu ya maisha yetu kila siku?

  • Wasaidie watoto kupaka rangi na kukamilisha ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Ni kwa jinsi gani tuna “zingatia” neno la Mungu? (1 Nefi 15:24).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

1 Nefi 11:16–33

Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo duniani kwa sababu ananipenda.

Nefi alipata ono ambapo alishuhudia mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yetu, na Yesu Kristo alikuwa ni kiini cha ono hilo.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kufananisha mistari kutoka 1 Nefi 11:16–33 na picha zinazofafanua kile mistari inachoelezea (kama vile 1 Nefi 11:20, 24, 27, 29, 31, 33; ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 30, 35, 38, 39, 4257). Ni nini watoto wanajifunza kuhusu Kristo kutoka kwenye mistari na picha?

  • Waulize watoto kwa nini Yesu Kristo ni muhimu kwao. Imbeni wimbo kuhusu Mwokozi, kama vile “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35), na waulize watoto ni nini wimbo huu hufundisha kuhusu Yesu. Waalike watoto kutenga muda katikati ya wiki kutafakari kuhusu Yesu Kristo na kushiriki uzoefu wao darasani wiki inayofuata.

Picha
nakala za Kitabu cha Mormoni katika lugha tofauti

Kitabu cha Mormoni kina injili ya Yesu Kristo.

1 Nefi 13:26–29, 35–36, 40

Kitabu cha Mormoni Kinafundisha kweli zenye thamani.

Je, watoto wanajua nini kuhusu Ukengeufu? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kuelewa umuhimu wa Kitabu cha Mormoni katika kurejesha kweli za injili zilizopotea wakati wa Ukengeufu?

Shughuli za Yakini

  • Someni 1 Nefi 13:26–29 kwa pamoja, na waalike watoto kutafuta kile kinachotokea wakati watu hawana kweli za injili “zilizo wazi na zenye thamani”. Ni kwa jinsi gani Bwana hurejesha kweli ambazo zilikuwa zimepotea? (ona mistari 35–36, 40). Waalike watoto kushiriki shuhuda zao za kweli walizojifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni, au shiriki wa kwako mwenyewe.

  • Onyesha video “Kitabu cha Mormoni—Kitabu kutoka kwa Mungu” (ChurchofJesusChrist.org) kueleza kwa mfano jinsi Biblia na Kitabu cha Mormoni vinavyofanya kazi pamoja kufundisha ukweli. Kwa nini inasaidia kuwa na shahidi zaidi ya mmoja? Chora nukta ubaoni, na uipe jina Biblia, na umwalike kila mtoto kuchora mstari tofauti ulionyooka ukipita katikati ya nukta kuonyesha kwa mfano kwamba mafundisho ndani ya Biblia yanaweza kufafanuliwa katika njia nyingi wakati Biblia ikiwa yenyewe. Futa mistari, na chora nukta ya pili yenye jina Kitabu cha Mormoni. Mwalike mtoto kuchora mstari ulionyooka unaopita kwenye nukta zote kuonyesha kwamba kuna njia moja tu ya kufafanua injili pale Biblia na Kitabu cha Mormoni vinapotumika kwa pamoja.

  • Wasaidie watoto kukariri makala ya imani ya nane.

1 Nefi 15:23–25

Neno la Mungu hunipa nguvu ya kushinda majaribu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuimarisha shuhuda zao za maandiko? Tafakari swali hili unaposoma 1 Nefi 15:23–25, na tumia shughuli hapa chini kuongezea kwenye mawazo yako.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto kufanya ufupisho wa ono la mti wa uzima (ona 1 Nefi 811). Nini kiliwazuia watu wasifikie mti? Nini kiliwasaidia kuufikia? Waalike watoto kusoma 1 Nefi 15:23–25. Ni kwa jinsi gani fimbo ya chuma huwasaidia watu kupenya ukungu wa giza? Ni kwa jinsi gani kusoma neno la Mungu hutusaidia kushinda majaribu na giza leo?

  • Kamilisha ukurasa wa shughuli pamoja na watoto. Wakati wakifanya hilo, waombe wazungumze kuhusu baadhi ya majaribu wanayopata watoto. Ni kwa jinsi gani wanaweza kukumbuka kushikilia fimbo ya chuma kila siku? Imbeni “The Iron Rod” (Nyimbo za Dini, na. 274)

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kuwaonyesha familia zao “fimbo za chuma” walizotengeneza kutoka kwenye ukurasa wa shughuli na kushiriki jinsi wanavyoweza kushikilia fimbo ya chuma kwa kusoma maandiko.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia Sanaa Kuwashirikisha Wanafunzi. Unapowafundisha watoto hadithi ya maandiko, tafuta njia za kuwasaidia kupata taswira yake. Ungeweza kutumia picha, video, vikaragosi, mavazi, na kadhalika.

Chapisha