“Januari 13–19. 1 Nefi 8–10: ‘Waje na Kula Tunda,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Januari 13–19. 1 Nefi 8–10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020
Januari 13–19
1 Nefi 8–10
“Waje na Kula Tunda”
Unaposoma 1 Nefi 8–10, fikiria ni jumbe zipi kutoka kwenye ono la Lehi zina manufaa kwako. Andika misukumo ya kiroho unayopata katika maandiko yako, kitabu, au nyenzo hii.
Andika Misukumo Yako
Ndoto ya Lehi—na fimbo yake ya chuma, ukungu wa giza, jengo kubwa, na mti wenye matunda “matamu zaidi ya yote”—ni mwaliko wa kutia msukumo wa kupokea baraka za upendo na dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi. Kwa Lehi, hata hivyo, ono hili pia lilihusu familia yake: “Kwa sababu ya kitu ambacho nilikuwa nimekiona, nina sababu ya kutoa shukrani kwa Bwana kwa sababu ya Nefi na pia Samu. … Lakini tazama, Lamani na Lemueli, ninaogopa sana kwa sababu yenu” (1 Nefi 8:3–4). Wakati Lehi alipomaliza kuelezea ono lake, aliwasihi Lamani na Lemueli “wasikilize maneno yake, na pengine Bwana angewarehemu” (1 Nefi 8:37). Hata kama umejifunza ono la Lehi mara nyingi, mara hii lifikirie jinsi Lehi alivyofanya—fikiria kuhusu mtu unayempenda. Unapofanya hivyo, usalama wa fimbo ya chuma, hatari za jengo kubwa, na utamu wa tunda vitakuwa na maana mpya. Na utaelewa kwa kina zaidi “huruma zote za mzazi mwenye upendo” ambaye alipata ono hili la ajabu.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi
Neno la Mungu linaniongoza kwa Mwokozi na kunisaidia kuhisi upendo Wake.
Ono la Lehi linatoa mwaliko wa kufikiria kuhusu mahali ulipo—na kule uendako—katika safari yako ya kibinafsi kumjua Mwokozi na kuhisi upendo Wake. Rais Boyd K. Packer alifundisha: “Unaweza kufikiria kwamba ndoto ya Lehi au ono halina maana maalumu kwako, lakini linayo. Uko ndani yake; sisi wote tupo ndani yake (ona 1 Nefi 19:23). Ndoto au ono la Lehi juu ya fimbo ya chuma ina kila kitu ndani yake … Mtakatifu wa Siku za Mwisho anahitaji kuelewa mtihani wa maisha” (“Ndoto ya Lehi’ na Wewe,” New Era, Jan. 2015, 2).
Njia moja ya kujifunza 1 Nefi 8 yaweza kuwa kujaza chati kama hii iliyoonyeshwa hapa. Ili kuelewa maana ya ishara, inasaidia kurejelea ono ambalo Nefi alipata wakati aliposali apate kuelewa ono la Baba yake—ona hasa 1 Nefi 11:4–25, 32–36; 12:16–18; na 15:21–33, 36. Unapojifunza ono la Lehi, zingatia kile ambacho Bwana anataka ujifunze.
Ishara kutoka kwenye ono la Lehi |
Maana |
Maswali ya kutafakari |
---|---|---|
Ishara kutoka kwenye ono la Lehi Mti na matunda yake (1 Nefi 8:10–12) | Maana | Maswali ya kutafakari Ni nini nafanya kuwaalika wengine kushiriki upendo wa Mungu? |
Ishara kutoka kwenye ono la Lehi Mto (1 Nefi 8:13) | Maana | Maswali ya kutafakari |
Ishara kutoka kwenye ono la Lehi Fimbo ya Chuma (1 Nefi 8:19–20, 30) | Maana | Maswali ya kutafakari |
Ishara kutoka kwenye ono la Lehi Ukungu wa giza (1 Nefi 8:23) | Maana | Maswali ya kutafakari |
Ishara kutoka kwenye ono la Lehi Jengo kubwa na pana (1 Nefi 8:26–27, 33) | Maana | Maswali ya kutafakari |
Ishara kutoka kwenye ono la Lehi | Maana | Maswali ya kutafakari |
Ona pia David A. Bednar, “Ndoto ya Lehi: Kushikilia Daima Fimbo ya Chuma,” Ensign au Liahona, Okt. 2011, 33–37.
Ni kwa nini Nefi alitengeneza seti mbili za bamba?
“Kusudi lenye hekima” la Bwana kumtaka Nefi atengeneze seti mbili ya kumbukumbu lilikuja kuwa wazi karne nyingi baadaye. Baada ya Joseph Smith kutafsiri kurasa za kwanza 116 za muswada za Kitabu cha Mormoni, alimpatia Martin Harris kurasa hizo, naye akazipoteza (ona M&M 10:1–23). Lakini seti ya pili ya bamba za Nefi ilijumuisha wakati ule pia, na Bwana akamuamuru Joseph Smith kutafsiri bamba hizi badala ya kutafsiri tena kile kilichokua kimepotea (ona M&M 10:38–45).
Kwa maelezo zaidi kuhusu bamba zilizotajwa katika 1 Nefi 9, ona “Maelezo Mafupi Kuhusu Kitabu cha Mormoni”; 1 Nefi 19:1–5; 2 Nefi 5:29–32; na Maneno ya Mormoni 1:3–9.
Manabii wa kale walijua kuhusu misheni ya Yesu Kristo na walishuhudia juu Yake.
Historia ya ono la Lehi hakika iliacha athari kwa familia yake, lakini bado alikuwa na kweli zingine za milele za kuwafundisha kuhusu misheni ya Mwokozi. Unaposoma 1 Nefi 10:2–16, fikiria ni kwa nini Bwana angeitaka familia ya Lehi—na sisi wote—kuzijua kweli hizi. Zingatia kile unachoweza kuwaambia wapendwa wako kuwaalika kumrudia Mwokozi. Baada ya kujifunza ono na mafundisho ya Lehi, ni nini wewe, kama Nefi, umetiwa msukumo kujifunza “kwa nguvu ya Roho Mtakatifu”? (1 Nefi 10:17).
Mungu atanifunulia ukweli ikiwa nitautafuta kwa bidii.
Wewe huitikia kwa namna gani unapokumbana na kanuni ya injili ambayo hauielewi? Tilia maanani tofauti kati ya jinsi ambavyo Nefi aliitikia ono la Lehi (ona 1 Nefi 10:17–19; 11:1) na jinsi ambavyo Lamani na Lemueli walivyoitikia (ona 1 Nefi 15:1–10). Ni kwa nini waliitikia katika njia hizi, na ni nini yalikuwa matokeo ya muitikio wao?
Zingatia kuandika kuhusu wakati ambapo ulitaka kujua kama funzo la injili lilikuwa la kweli. Ni jinsi gani mchakato ulioufuata unalingana na kile Nefi alichofanya?
Ona pia 1 Nefi 2:11–19; Mafundisho na Maagano 8:1–3.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.
Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.
1 Nefi 8
Wanafamilia wako wanaweza furahia kuigiza ono la Lehi au kuchora picha na kutumia michoro yao kuelezea juu yake. Au unaweza kuonyesha mchoro wa mwana sanaa wa ono la Lehi ambao unaambatana na somo hili na waalike wanafamilia kuonyesha utondoti na kutafuta maandiko ambayo yanaeleza vitu hivi vinawakilisha nini. Wimbo wa dini “Fimbo ya Chuma” (Nyimbo za Dini, no. 274) unaambatana vizuri sana na sura hii. Pia unaweza kutazama video inayoonyesha ono la Lehi (ona mkusanyiko wa video za Kitabu cha Mormoni kwenye ChurchofJesusChrist.org au the Gospel Library app).
1 Nefi 8:10–16
Ni nani tunaweza kumualika kuja karibu na Yesu Kristo na kuhisi utamu wa upendo Wake? Nini tunaweza kufanya “[kuwapungia mkono]”?
1 Nefi 9:5–6
Ni lini tumetii amri bila kuelewa kikamilifu sababu zake? Ni namna gani tulibarikiwa?
1 Nefi 10:20–22
Ni kwa jinsi gani kuwa mchafu kimwili kunaweza kufananishwa na kuwa mchafu kiroho? Tunaweza kufanya nini ili kuhakikisha tunabaki wasafi kiroho?
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.