“Januari 20–26. 1 Nefi 11–15: ‘ Wamejikinga kwa Utakatifu na kwa Nguvu za Mungu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Januari 20–26. 1 Nefi 11–15,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020
Januari 20–26
1 Nefi 11–15
“ Wamejikinga kwa Utakatifu na kwa Nguvu za Mungu”
Je, unaweza kujiona katika 1 Nefi 11–15? Je, vifungu gani ni vya thamani kubwa zaidi kwako na kwa familia yako?
Andika Misukumo Yako
Wakati Mungu anayo kazi kubwa kwa nabii Wake kufanya, Mara nyingi Yeye humpa nabii huyo ono kubwa ambalo linamsaidia kuelewa mipango ya Mungu kwa watoto Wake. Musa aliona ono la “dunia hii, na wakazi wake, na pia mbingu” (Musa 1:36). Mtume Yohana aliona historia ya dunia na Ujio wa Pili wa Mwokozi (ona kitabu cha Ufunuo). Joseph Smith alimuona Baba na Mwana (ona Historia ya—Joseph Smith 1:17–18). Lehi aliona ono ambalo lilionyesha safari ambayo tunapaswa kufanya kuelekea kwa Mwokozi na upendo Wake.
Kama ilivyoandikwa katika 1 Nefi 11–14, Nefi aliiona huduma ya Mwokozi, siku za baadae za uzao wa Lehi katika nchi ya ahadi, na hatima ya kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Ono hili lilisaidia kumtayarisha Nefi kwa kazi iliyokuwa mbele yake, na pia linaweza kusaidia kukutayarisha wewe—kwa maana Mungu ana kazi unayohitajika kufanya katika ufalme Wake. Wewe ni mmoja wa “watakatifu wa kanisa la Mwanakondoo” lililoonekana na Nefi, “ambao walitawanyika kote usoni mwa dunia; na walikuwa wamejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu katika utakatifu mkuu” (1 Nefi 14:14).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi
Mungu alimtuma Yesu Kristo kama njia ya kuonyesha upendo Wake.
Ili kumsaidia Nefi kuelewa maana ya mti ambao baba yake alikuwa ameuona, malaika alimuonyesha “Mwana wa Baba wa Milele” (1 Nefi 11:21). Hili lilipelekea Nefi kuhitimisha ya kwamba mti unawakilisha upendo wa Mungu. Lakini ono lilikuwa bado halijakamilika. Unaposoma na kutafakari 1 Nefi 11, umepata nini ambacho kinakusaidia kuelewa ni kwa nini yesu Kristo ni onyesho kubwa zaidi la upendo wa Mungu?
Ili kujifunza kuhusu ishara zingine katika ndoto ya Lehi, ona 1 Nefi 11:35–36; 12:16–18; na 15:21–30.
Ona pia Yohana 3:16.
Bwana alitayarisha njia kwa ajili ya Urejesho.
Nefi kamwe asingeishi kushuhudia kile alichoona katika ono lake. Kwa nini unafikiri ilikuwa muhimu kwa Nefi kujua vitu hivi? Kuna umuhimu gani kwako wewe kuvijua vitu hivi? Pengine unaweza kuuliza swali hili kila mara unaposoma kuhusu kitu ambacho Nefi aliona katika ono lake.
Haya ni baadhi ya matukio ambayo Nefi aliyaona: siku za baadae za watu wake (ona sura ya 12), ukoloni wa Amerika na Mapinduzi ya Marekani (ona sura ya 13:12–19), Ukengeufu Mkuu (ona sura ya 13:20–29), na Urejesho wa injili (ona sura ya 13:32–42).
Ni nini “kanisa kuu na la machukizo” ambalo Nefi aliona?
Mzee Dallin H. Oaks alieleza kwamba lile “kanisa kuu la machukizo” lililozungumziwa na Nefi linawakilisha “falsafa yoyote au shirika linalopinga imani katika Mungu. Na ‘utumwa’ ambamo hili ‘kanisa’ linatafuta kuwaleta watakatifu hautakuwa kuzuiliwa kimwili bali utumwa wa dhana za uwongo” (“Kusimama Kama Mashahidi wa Mungu,” Ensign, Mac. 2015, 32).
Ni nani ambaye Nefi aliona Roho “alimshawishi” asafiri “kwa yale maji mengi”?
Nefi aliona kwamba Roho Mtakatifu angemtia msukumo Christopher Columbus kufanya safari yake maarufu kwenda Amerika. Mnamo Machi 14, 1493, Columbus aliandika kuhusu safari hii: “Matokeo haya makuu na ya ajabu hayafai kudhaniwa kwamba ni kwa ajili ya ustahili wangu … ; kwa kuwa kile ambacho bila usaidizi akili ya mwanadamu pekee haingweza kutimiza, Roho wa Mungu amezijalia juhudi za mwanadamu, kwani Mungu ana desturi ya kusikia maombi ya watumishi Wake ambao wanayapenda mawaidha yake hadi kuweza kutekeleza vitu vinavyoonekana kutowezekana” (The Annals of America [Encyclopedia Britannica, Inc., 1976], 1:5).
Maandiko ya siku za mwisho yanarejesha “vitu vilivyo wazi na vyenye thamani.”
Nefi aliona katika ona kwamba Biblia—ambayo aliielezea kama “maandishi ya Wayahudi”—ingekuwa na “vitu vilivyo wazi na vyenye thamani vilivyoondolewa [kutoka kwenye maandishi hayo]” (1 Nefi 13:23, 28). Hata hivyo, pia aliona kwamba Mungu angerejesha vitu hivi kupitia “vitabu vingine”—Kitabu cha Mormoni na maandiko mengine ya siku za mwisho (ona 1 Nefi 13:39–40). Ni nini baadhi ya kweli za thamani ambazo Kitabu cha Mormoni kinatusaidia sisi kuzielewa vizuri zaidi? Maisha yako ni tofauti kiasi gani kwa sababu vitu hivi vilivyo wazi na vya thamani vimerejeshwa?
Ona pia “Vitu Vilivyo Wazi na Vya Thamani,” Ensign, Mac. 2008, 68–73; Russell M. Nelson, “Kitabu cha Mormoni: Maisha Yako Yangekuaje Bila kuwa Nacho?” Ensign au Liahona, Nov. 2017, 60–63.
Bwana atanijibu pale ninapoomba kwa imani, na moyo wa upole?
Je, umewahi kuhisi kana kwamba ulikuwa hupokei ufunuo binafsi—kwamba Mungu alikuwa hazungumzi nawe? Ni ushauri gani Nefi aliwapa ndugu zake walipohisi hivi? Ni jinsi gani unaweza kutumia ushauri wa Nefi maishani mwako, na ni jinsi gani unaweza kutumia ushauri wake kuwasaidia wengine?
Ona pia Yakobo 4:8; Alma 5:46; 26:21–22.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.
Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.
1 Nefi 11–14
Familia yako inaposoma sura hizi, mara kwa mara tua na uulize maswali kama haya: ni nini Nefi alikiona katika ono lake ambacho kilimfurahisha? Ni kipi chaweza kuwa kulimhuzunisha? Kwa nini?
1 Nefi 13:20–42
Ili kuwasaidia wanafamilia kuelewa thamani ya kweli “zilizo wazi na za thamani” katika Kitabu cha Mormoni, linganisha ujumbe ulioandikwa wazi na ujumbe ulioparaganywa. Ni kwa nini Baba wa Mbinguni anataka kweli Zake zifundishwe kwa uwazi? Wanafamilia wanaweza kutoa ushuhuda juu ya kweli “zilizo wazi na za thamani” ambazo wamejifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni.
1 Nefi 14:12–15
Ni kwa nini sisi “tumejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu” wakati tunapoishi kulingana na maagano yetu na Mungu?
1 Nefi 15:8–11
Ni uzoefu gani familia yako inaweza kushiriki wakati ambapo “wamemuuliza Bwana”? Tunajifunza nini kutokana na mfano wa Nefi?
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.