Njoo, Unifuate
Januari 27–Februari 2. 1 Nefi 16–22: “Nitaandaa Njia Mbele Yako”


“Januari 27–Februari 2. 1 Nefi 16–22: ‘Nitaandaa Njia Mbele Yako,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

Januari 27–Februari 2. 1 Nefi 16–22,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Lehi akitazama Liahona

Lehi na Liahona, na Joseph Brickey

Januari 27–Februari 2

1 Nefi 16–22

“Nitaandaa Njia Mbele Yako”

Hadithi zenye ushawishi katika 1 Nefi 16–22 hufundisha kweli ambazo zinaweza kuwabariki watoto katika darasa lako. Soma sura hizi na andika misukumo unayopokea.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Andika maneno yafuatayo ubaoni, au onyesha picha zake: Liahona, upinde , na merikebu. Waalike watoto watatu kila mmoja achukue mojawapo ya maneno au picha na kushiriki sehemu ya hadithi ya Nefi ambayo inahusisha kitu kile. Toa msaada kama itahitajika.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

1 Nefi 16:10, 28–29; 18:8–13, 20–22

Bwana anaweza kuniongoza na kunielekeza.

Wafundishe watoto kwamba hata wakati wanapokumbana na changamoto ngumu, Bwana anaweza kuwaongoza (ona 1 Nefi 16:29).

Shughuli za Yakini

  • Waonyeshe watoto dira, ramani, au kitu kingine chochote kinachotusaidia kuipata njia, na elezea jinsi ya kutumia vifaa hivi. Fananisha vifaa hivi na Liahona unapofanya ufupisho wa hadithi katika 1 Nefi 16:10, 28–29 na 18:9–13, 20–22. Onyesha kwamba wakati familia ya Lehi hawakuwa waaminifu, Liahona haikufanya kazi (ona pia 1 Nefi 18:9–12, 20–22). Ni nini hutusaidia leo kuipata njia yetu ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni?

  • Leta boksi lililo na dokezo kadhaa ambazo huelezea mahali maalumu ndani au kuzunguka jengo la kanisa. Tumia boksi na dokezo kuwakilisha Liahona, na waache watoto wafanye zamu kuchagua dokezo na kubashiri wapi ni mahali maalumu. Kisha nendeni pamoja mahali hapo. Elezea kwamba tunapoonyesha imani na kufuata maelekezo Bwana anayotupatia, Yeye atatusaidia kurudi Kwake (ona Alma 37:38–42). Ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni hutuongoza katika safari yetu ya kurudi Kwake?

1 Nefi 16:14–32

Ninaweza kuwa mfano mzuri kwa familia yangu.

Muingiliano wa Nefi na familia yake wakati wa kipindi kigumu kunaweza kuwasaidia watoto kuona kwamba japokuwa ni wadogo, wanaweza kuwa mifano kwa familia zao.

Shughuli za Yakini

  • Mpangie kila mtoto kuchora picha ya kitu kutoka kwenye hadithi ya kuvunjika kwa upinde wa Nefi (ona 1 Nefi 16:14–32), kama vile Nefi, upinde, au Liahona. Kisha tumia picha kusimulia hadithi kwa darasa, na waache watoto wafanye zamu kufanya vivyo hivyo. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama Nefi pale familia zetu zinapopitia nyakati ngumu?

  • Waalike watoto kila mmoja kukata karatasi ya duara na kuchora uso wa huzuni upande mmoja na uso wa furaha upande mwingine. Unaposimulia hadithi ya kuvunjika kwa upinde wa Nefi, waalike kutumia nyuso kuonyesha jinsi familia ya Nefi ilivyokuwa ikihisi wakati wa sehemu tofauti za hadithi. Ni kwa jinsi gani Nefi alisaidia kuifanya familia yake iwe na furaha? Tunaweza kufanya nini kuzifanya familia zetu ziwe na furaha?

1 Nefi 17:7–19; 18:1–4

Baba wa Mbinguni anaweza kunisaidia kufanya mambo magumu.

Kama Nefi, watoto unaowafundisha wanajifunza kufanya mambo ambayo yanaonekana magumu. Uzoefu wa Nefi unaweza kuwasaidia kujua kwamba Baba wa Mbinguni atawasaidia pale wanapoomba.

Shughuli za Yakini

  • Wasimulie watoto hadithi ya Nefi akiamriwa kujenga merikebu, kwa kutumia 1 Nefi 17:7–19 na 18:1–4. Unaweza pia kutumia “Sura ya 7: Kujenga Merikebu” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 21–22) au video inayohusiana katika mkusanyiko wa Video za Kitabu cha Mormoni kwenye ChurchofJesusChrist.org. Ukurasa wa shughuli ya wiki hii unaweza kuimarisha kanuni kwamba Baba wa Mbinguni alimsaidia Nefi, na Yeye atatusaidia sisi.

  • Imbeni kwa pamoja aya ya pili ya “Nephi’s Courage” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 120–21). Nini kilimsaidia Nefi kuwa na ujasiri wakati kaka zake walipomfanyia mzaha kwa kujaribu kujenga merikebu?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

1 Nefi 16:10, 28–29; 17:13–15; 18:8–13, 20–22

Wakati ninapotii amri, Bwana huniongoza.

Tumia tukio la familia ya Lehi kuongozwa na Liahona kuwaonyesha watoto jinsi Bwana atakavyowaongoza pale wanapojitahidi kufanya mapenzi Yake.

Shughuli za Yakini

  • Chagua moja au zaidi ya vifungu vya maneno vifuatavyo kusoma pamoja na watoto: 1 Nefi 16:10, 28–29; 17:13–15; na 18:8–13, 20–22. Waombe watafute kile tunachopaswa kufanya kupata mwongozo na maelekezo kutoka kwa Mungu na jadilini kile walichojifunza.

  • Baada ya kupitia tena hadithi katika 1 Nefi 16–18, wafanyie usahili watoto kadhaa kama vile wamesafiri pamoja na familia ya Lehi. Ungeweza kuuliza maswali kama haya: kwa nini ulikuwa na shukrani kwa ajili ya Liahona? Nini ulihitaji kufanya ili kwamba Liahona iweze kufanya kazi? (Ona 1 Nefi 16:28–29). Alika darasa kujadili vitu ambayo Bwana ametoa kutuongoza katika siku yetu.

  • Waombe watoto kufikiria jinsi ambavyo wangeweza kutumia hadithi ya Liahona kumsaidia rafiki ambaye anahitaji kufanya uamuzi wa muhimu. Pendekeza kwamba kwa kuongezea kwenye 1 Nefi 16:10, 26–31 na 18:9–22, wangeweza pia kurejea kwenye Alma 37:38–44. Shiriki uzoefu ambapo Baba wa Mbinguni alikusaidia kupita wakati mgumu, au waalike watoto kushiriki uzoefu huo. Tunapaswa kufanya nini ili kupokea usaidizi Wake?

1 Nefi 16:14–39; 18:1–5

Mtazamo na chaguzi zangu vinaweza kuwa na ushawishi mzuri kwa familia yangu.

Imani ya Nefi ilikuwa ni baraka kubwa wakati familia yake ilipokabiliwa na majaribu. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza kutoka kwenye mfano huu?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto wachore picha inayofafanua hadithi ya kuvunjika kwa upinde wa Nefi (ona 1 Nefi 16:14–39). Pitia tena hadithi pamoja nao, kama itahitajika. Wakati wakishiriki michoro yao, wasaidie kuainisha njia ambazo kwazo uaminifu wa Nefi ulibariki familia yake. Waalike watoto kutafakari changamoto ambazo wao au familia zao hukumbana nazo. Ni nini wanaweza kufanya kufuata mfano wa Nefi?

  • Someni kwa pamoja mistari kutoka 1 Nefi 16:21–32. Jadilini baadhi ya malengo familia za watoto wanaweza kuwa nayo, kama vile kuwa na mazoea ya jioni za familia nyumbani au sala za familia. Ni kwa jinsi gani watoto wanaweza kuzisaidia familia zao kufikia malengo haya? Waalike kupanga kufanya jambo moja kuzisaidia familia zao kufikia malengo yao wiki hii.

1 Nefi 19:22–24

Ninaweza kulinganisha maandiko na Maisha yangu.

Wasaidie watoto kuona kwamba matukio katika maandiko ni zaidi ya hadithi—yana kanuni ambazo zinaweza kubariki maisha yao.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto wasome 1 Nefi 19:22–24 kwa sauti, na waulize watoto kile wanachodhani inamaanisha “kulinganisha maandiko yote” nasi. Wasaidie kugundua jinsi Nefi alivyolinganisha matukio ya kimaandiko na uzoefu wake wa kupata mabamba ya shaba (ona 1 Nefi 4:1–4; ona pia Kutoka 14). Ni kwa jinsi gani kukumbuka hadithi hii kulimsaidia Nefi na kaka zake?

  • Pitia tena baadhi ya hadithi ambazo watoto wamejifunza kuhusu Lehi na familia yake kutoka 1 Nefi, na waalike kushiriki kile walichojifunza kutoka kwenye hadithi hizi. Wasaidie kufikiri juu ya hali katika maisha yao ambazo zinaweza kuwa sawa na hadithi hizi. Kwa mfano, Bwana kumwamuru Nefi kujenga merikebu kungeweza kuwakumbusha nyakati ambapo walihitaji kufanya kitu kigumu na kutafuta msaada wa Bwana.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuchagua hadithi kutoka 1 Nefi 16–22 na kushiriki na familia zao jinsi wanavyoweza “kulinganisha” hadithi hiyo na maisha yao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia hadithi. Hadithi huwasaidia watoto kuelewa kanuni za injili kwa sababu zinaonyesha kwa mifano jinsi wengine wanavyoishi kanuni hizo.

Chapisha