“Februari 17–23. 2 Nefi 11–25: ‘Tunafurahia katika Kristo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Februari 17–23. 2 Nefi 11–25,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Februari 17–23
2 Nefi 11–25
“Tunafurahia katika Kristo”
Maandalizi yako ya kufundisha yanaanza unaposoma 2 Nephi 11–25. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa sura hizi, na muhtasari huu unaweza kukupa mawazo ya kufundisha.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Kwa kifupi pitia tena pamoja na watoto kile walichojifunza kuhusu Mwokozi na Upatanisho Wake wiki iliyopita. Kama walishiriki kile walichojifunza pamoja na familia zao, wahimize kuzungumza kuhusu hilo.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Hekalu ni nyumba ya Bwana.
Unabii wa Isaya kuhusu “mlima wa nyumba ya Bwana” ingeweza kuwa fursa ya kufundisha watoto kuhusu hekalu na kuwasaidia kutazamia kwenda huko siku moja.
Shughuli za Yakini
-
Acha mtoto ashikilie picha ya hekalu (muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia ina picha hiyo), na waombe watoto kushiriki kile wanachofahamu kuhusu hekalu. Soma 2 Nefi 12:3, na elezea kwamba katika mstari huu nabii aitwaye Isaya alitoa unabii kwamba kutakuwa na mahekalu katika siku za mwisho. Soma mstari kwa mara ya pili, na sisitiza kwamba tunapokwenda hekaluni, Bwana “atatufunza njia zake” na kutusaidia “kutembea katika mapito yake.”
-
Tengeneza njia sakafuni, na mwisho wa njia, weka picha ya hekalu ikiwa imefunikwa. Acha watoto watembee kwenye njia, na wanapofanya hivyo, wasaidie kurudia kifungu “tembea katika mapito yake.” Watoto wanapofika mwisho wa njia, waache wafunue picha. Inamaanisha nini kutembea katika mapito ya Mungu?
-
Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu hekalu, kama vile “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95). Wasaidie watoto kutafuta maneno na vifungu vya maneno katika wimbo ambavyo hufundisha hekalu ni nini na kile tunachofanya hekaluni.
“Tunafurahia katika Kristo.”
Nefi na Isaya walikuwa na shuhuda za Mwokozi, na shuhuda zao ziliwafanya wawe na furaha. Wasaidie watoto waone kwamba una “furahia katika Kristo.”
Shughuli za Yakini
-
Mwalike mtoto kushikilia picha ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo (kama vile Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 30), na wasaidie watoto kumtafuta mtoto Yesu katika picha. Soma 2 Nefi 19:6 au onyesha video “Mwokozi Amezaliwa—Video ya Krismasi” (ChurchofJesusChrist.org), na waombe watoto kuonyesha kwa kidole Yesu pale wanaposikia maneno mtoto na mwana. Elezea kwamba nabii Isaya, aliyeandika maneno katika 2 Nefi 19:6, alijua kuhusu kuzaliwa kwa Yesu mamia ya miaka kabla hakujatokea.
-
Simulia hadithi kuhusu Yesu Kristo akileta furaha kwa wengine, au onyesha video kama vile “Yesu Anamponya Mtu Aliyezaliwa Kipofu” au Waacheni Watoto Wadogo Waje Kwangu” (ChurchofJesusChrist.org). Onyesha nyakati za furaha katika hadithi au video. Soma 2 Nefi 25:26 na zungumza kuhusu kwa nini una “furahia katika Kristo.” Waombe watoto wazungumzie kuhusu jinsi Yesu anavyowaletea furaha.
Milania itakuwa ni wakati wa amani na furaha.
Baada ya ujio Wake wa pili, Yesu Kristo ataishi na watu Wake wakati wa kipindi cha amani kiitwacho Milania.
Shughuli za Yakini
-
Waonyeshe watoto picha za wanyama waliotajwa katika 2 Nefi 21:6–7, na waombe watoto kuwapa majina wanyama. Elezea kwamba wanyama hawa kwa kawaida ni maadui, lakini Isaya alifundisha kwamba baada ya Yesu Kristo kurudi tena, kutakuwa na kipindi cha amani, kiitwacho Milania, ambapo wanyama hawataleteana madhara. Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa wanyama hawa katika namna tunavyotendeana? Waalike watoto kuchora picha za wanyama hawa wakiishi pamoja kwa amani.
-
Soma 2 Nefi 22:5, na waombe watoto wakusaidie kutafuta wimbo ambao unaelezea “vitu vyema” Bwana alivyotenda. Baadhi ya mifano yaweza kujumuisha “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29) au “How Great Thou Art” (Nyimbo za Dini, na. 86). Imbeni wimbo kwa pamoja. Elezea kwamba katika Milania, kila mtu atajua kuhusu “vitu vyema” Bwana alivyotenda.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Hekalu ni nyumba ya Bwana.
Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia mistari hii kuwasaidia watoto kutazamia siku watakapoweza kuhudhuria hekaluni?
Shughuli za Yakini
-
Onyesha picha ya hekalu (muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia. ina picha hiyo). Muombe mtoto asome 2 Nefi 12:2–3, na waalike watoto wengine kusikiliza sababu za kwa nini Isaya alisema tunahitaji hekalu. Ungeweza kuelezea kwamba Isaya aliita hekalu “mlima wa nyumba ya Bwana.” Kwa nini mlima ni alama nzuri kwa ajili ya hekalu?
-
Waalike watoto wajichore picha zao wakienda hekaluni. Kama itawezekana, waombe mmoja wa wavulana au wasichana katika kata awaambie watoto jinsi ilivyo kufanya ubatizo kwa ajili ya wafu hekaluni. Kijana huyu au mtu mwingine yeyote katika kata angeweza kuwafundisha watoto jinsi ya kutafuta majina ya mababu zao wanaohitaji ibada za hekaluni.
Shetani anajaribu kunikanganya kuhusu wema na uovu.
Tunaishi katika ulimwengu ambapo, kama Isaya alivyotoa unabii, watu huita uovu wema na wema uovu. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kutambua udanganyifu huo?
Shughuli za Yakini
-
Waonyeshe watoto kitu kichungu au kichachu, kama vile achali au limao, ndani ya karatasi ya peremende. Someni pamoja 2 Nefi 15:20, na elezea kwamba shetani hujaribu kufanya vitu viovu kuonekana vyema. Wasaidie watoto kufikiria njia ambazo Shetani hutumia kufanya hili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kugundua udanganyifu wake?
-
Onyesha dakika ya kwanza na nusu ya video “Utakuwa Huru” (ChurchofJesusChrist.org). Kwa nini mvuvi alibadili ndoana yake? Kwa nini Shetani hubadili dhambi?
2:58
“Tunafurahia katika Kristo.”
Watoto wanahitaji kujua kwamba injili ya Yesu Kristo ni ya furaha. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia “kufurahia katika Kristo”?
Shughuli za Yakini
-
Wasaidie watoto kupata majina ya Yesu Kristo katika 2 Nefi 17:14 na 19:6. Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba “Imanueli” ni moja ya majina haya, na linamaanisha “Mungu pamoja nasi.” Ni nini kila moja ya majina haya hutufundisha kuhusu Yeye?
-
Weka picha ya Mwokozi ubaoni, na someni pamoja 2 Nefi 25:26. Kwa nini Nefi aliandika na kuzungumza mengi kuhusu Yesu Kristo? Acha kila mtoto aandike ubaoni, karibu na picha ya Yesu, jambo moja kuhusu Mwokozi ambalo huwaletea furaha.
-
Waombe watoto kufikiria juu ya mtu ambaye wangependa ku “mshawishi … kumwamini Kristo” (2 Nefi 25:23). Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwaelezea wengine furaha ambayo Mwokozi huleta ndani ya maisha yetu? Waache watoto waandike au kuigiza baadhi ya mambo wangeweza kufanya kumsadia mtu waliyemfikiria kumwamini Yesu Kristo.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kufikiria jambo wanaloweza kufanya kuonyesha familia zao kwamba wana “furahia katika Kristo.”