“Januari 6–12. 1 Nefi 1–7: ‘Nitaenda na Kutenda,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
Januari 6–12. 1 Nefi 1–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Januari 6–12
1 Nefi 1–7
“Nitaenda na kutenda”
Unaposoma 1 Nefi 1–7, fikiria kuhusu mistari, uzoefu, maswali, na nyenzo nyingine unazohisi kupata msukumo kutumia kufundishia watoto. Shughuli kwenye muhtasari huu zinaweza kutoholewa kwa ajili ya watoto wakubwa au wadogo.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Baadhi ya watoto darasani kwako wanaweza kuwa tayari wamesikia kuhusu au kusoma uzoefu wa familia ya Nefi katika 1 Nefi 1–7. Waalike washiriki kile wanachojua. Kama watoto hawajui mengi kuhusu uzoefu wa Nefi, wape fursa mwisho wa somo kushiriki kile walichojifunza.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Ninahitaji ushuhuda wangu binafsi.
Nefi alikuja kuamini maneno ya baba yake kwa sababu alikuwa na hamu ya kujua mwenyewe na aliomba kwa Bwana. Wasaidie watoto kujifunza kutoka kwenye mfano wake.
Shughuli za Yakini
-
Leta boksi lililofungwa lenye picha ya Mwokozi ndani yake, na mpe kila mtoto zamu ya kujua mwenyewe nini kilichomo ndani ya boksi. Waambie watoto kwamba Nefi alitaka kuwa na ushuhuda wake binafsi kwamba Bwana alikuwa ameiamuru familia yake kuondoka Yerusalemu. Waombe watoto wasikilize kile Nefi alichofanya kupata ushuhuda wake binafsi wakati unaposoma 1 Nefi 2:16. Shuhudia kwamba kama vile sisi kila mmoja alivyopaswa kufungua boksi kujua nini kilikuwa ndani yake, sote tunahitaji kumuomba Mungu ili kupata ushuhuda wetu wenyewe.
-
Leta picha au vitu vinavyowakilisha mambo ambayo watoto wangeweza kutafuta ushuhuda kwayo, kama vile picha ya Yesu Kristo, Kitabu cha Mormoni, au picha ya nabii anayeishi. Waalike watoto kuchagua picha au kitu na kushiriki pamoja na darasa shuhuda zao juu ya kile kitu.
Mungu atanisaidia kutii amri Zake.
Unawezaje kutumia maelezo haya kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Mungu hutusaidia kutii amri Zake, hata wakati zikionekana ngumu kutii?
Shughuli za Yakini
-
Soma 1 Nefi 2:2–4 kwa watoto, na uonyeshe picha kadhaa za vitu ambavyo familia ya Lehi iliweza kuwa ilivichukua kuelekea nyikani, kama vile hema, mablanketi, na pinde na mishale. Waombe wafikirie kile ambacho wangeweza kuhisi kama wangepaswa kuacha nyumba zao na kwenda nyikani. Je, Bwana anatutaka sisi tufanye nini ili kumtii leo?
-
Wasaidie watoto kupaka rangi na kukata michoro ya karatasi kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii; kisha waombe kutumia maumbo ya karatasi kufupisha maelezo ya Nefi na kaka zake kuchukua bamba za shaba (ona 1 Nefi 3–4). Wimbo “Nephi’s Courage” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 120–21) na “Mlango wa 4: Bamba za Shaba” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 8–12; ona pia video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org) vinaweza kukusaidia kusimulia hadithi hii.
-
Tumia picha 103–15 ndani ya Kitabu cha Sanaa ya Injili kuwasaidia watoto kufikiria juu ya vitu ambavyo Bwana ametuamuru sisi kufanya. Je, tunabarikiwa vipi tunapomtii Yeye? Wasaidie kupamba beji za kuvaa zinazosema Nitaenda na kutenda vitu ambavyo Bwana ameamuru (1 Nefi 3:7). Rudieni kirai mara kadhaa kwa pamoja.
Maandiko ni hazina kuu.
Unawezaje kuwapa watoto msukumo kuthamini maandiko, au neno la Mungu?
Shughuli za Yakini
-
Waonyeshe watoto kitu (au picha ya kitu) ambacho kina thamani kubwa kwako. Zungumza kuhusu jinsi unavyokichukulia na kukijali. Elezea kwamba kwa familia ya Lehi, maandiko yalikuwa na thamani kubwa, kama hazina.
-
Waalike watoto wakusaidie kusimulia au kuigiza kile ambacho Nefi na kaka zake walifanya ili kupata bamba za shaba: walisafiri umbali mrefu, wakatoa dhahabu na fedha zao, na kujificha ndani ya pango ili kuokoa maisha yao. Soma 1 Nefi 5:21. Kwa nini maandiko yalikuwa na thamani kwa familia ya Lehi? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuchukulia maandiko kama hazina?
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Ninaweza kuwa na ushuhuda wangu binafsi.
Unajifunza nini kutoka kwenye mfano wa Nefi kuhusu kupata ushuhuda wako mwenyewe? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza kutokana na mfano wake?
Shughuli za Yakini
-
Waombe watoto kutafuta 1 Nephi 2:16, 19 ili kugundua jinsi Nefi alivyopata ushuhuda wa maneno ya baba yake. Waalike kuandika matendo ya Nefi kwenye vitofali au vitu vingine na kisha kujenga kitu kwa kutumia vitu hivyo kuwakilisha jinsi vitu hivyo vinavyotusaidia kujenga ushuhuda.
-
Waambie watoto jinsi ulivyopata ushuhuda wako wa injili. Waalike kushiriki shuhuda kama hizo ambazo wamekuwa nazo, na wahamasishe kufuata mfano wa Nefi kuendelea kujenga shuhuda zao. Ni kwa jinsi gani kuwa na ushuhuda wetu wenyewe kunatusaidia?
Ninaweza kuitikia kwa imani maagizo ya Bwana.
Kukuza mtazamo kama wa Nefi kutawasaidia watoto wakati Bwana anapowataka kufanya kitu ambacho kinaonekana kigumu.
Shughuli za Yakini
-
Gawa darasa katika makundi mawili. Alika kundi moja kusoma mwitikio wa Lamani na Lemueli kwa Lehi (ona 1 Nefi 3:2–5) na kundi lingine kusoma mwitikio wa Nefi (ona 1 Nefi 3:2–4, 7). Mwalike mtoto ajifanye kama Lehi na kuwaomba watoto wengine kujifanye kama wanarudi Yerusalemu kuchukua bamba za shaba. Alika kila kundi kujibu kwa maneno yao wenyewe kama vile walikuwa watu waliowasoma. Nini baadhi ya mambo Mungu ametuamuru sisi kufanya? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama Nefi?
-
Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu utiifu, kama vile “Nephi’s Courage” au “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 120–21, 146–47), na waombe watoto kusikiliza vifungu vya maneno ambavyo hufundisha jinsi tunavyopaswa kumwitikia Bwana.
Roho Mtakatifu ataniongoza pale ninapotafuta kufanya mapenzi ya Bwana.
Nefi alimfuata Roho, “bila kujua kimbele vitu ambavyo [yeye] angefanya” (1 Nefi 4:6). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu?
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto kuigiza hadithi ya Nefi na kaka zake wakijaribu kupata bamba za shaba (ona 1 Nefi 3–4). Alika mtoto asome 1 Nefi 4:6, na liombe darasa lisikilize kile Nefi alichofanya kile kilichowaruhusu kufanikiwa.
-
Shiriki na watoto baadhi ya mifano ya mambo ambayo Mungu angewataka wafanye, kama vile kuwa rafiki wa mtu shuleni ambaye anaonekana mpweke, kumsamehe ndugu, au kusema ukweli baada ya kutenda kosa. Waombe watoto kushiriki jinsi gani Roho Mtakatifu angeweza kuwasaidia katika hali hizo. Ni kwa jinsi gani tunaweza kumwalika Roho Mtakatifu kutusaidia kumtii Mungu?
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kushiriki uzoefu pamoja na familia zao wakati walipobarikiwa kwa kutii amri. Watie moyo wawaombe wanafamilia wao kushiriki uzoefu sawa na huo.