Njoo, Unifuate
Septemba 21–27. 3 Nefi 12–16: “Mimi Ndiye Sheria, na Nuru”


“Septemba 21–27. 3 Nefi 12–16: ‘Mimi Ndiye Sheria, na Nuru,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Septemba 21–27. 3 Nefi 12–16,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Yesu akiwaonyesha Mitume Kumi na Wawili

Nefi wa Tatu: Hawa Kumi na Wawili Ambao Nimewachagua, na Gary L. Kapp

Septemba 21–27

3 Nefi 12–16

“Mimi Ndiye Sheria, na Nuru”

Unapojifunza 3 Nefi 12–16, tafuta kweli ambazo zitakuwa na maana kwa watoto unaowafundisha. Muhtasari huu unapendekeza baadhi ya kweli, lakini Roho anaweza kukuongoza kwenye zingine.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Pitisha picha ya Yesu. Acha watoto wafanye zamu kushikilia picha na kushiriki jambo moja Yesu alilofundisha, kama vile jambo walilojifunza nyumbani wiki hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

3 Nefi 12:14–16

Ninaweza kuwa mfano mzuri kwa wengine.

Wakati mwingine watoto wanaweza wasitambue ni kwa kiasi gani mifano yao inaweza kuwabariki wengine. Tumia mistari hii kuwatia moyo kuruhusu nuru yao iangaze.

Shughuli za Yakini

  • Waambie watoto kwamba 3 Nefi 12:14–16 ni kuhusu wao, na kisha isome kwa sauti. Popote unaposoma “wewe” au “yako,” waonyeshe kwa kidole watoto, na waombe kujionyeshea wenyewe kwa kidole.

  • Waonyeshe watoto tochi, na mwalike mmoja wao kuiwasha. Elezea kwamba tunapomfuata Mwokozi, ni kama kuwasha nuru ambayo inaweza kuwasaidia wengine kumfuata Yeye pia. Kisha funika au ficha nuru, na waombe watoto kutaja baadhi ya mambo wanayoweza kufanya kuwa mfano mzuri kwa wengine. Kila mara wanapofanya hivyo, waruhusu kufunua nuru (ona pia ukurasa wa shughuli ya wiki hii).

  • Imbeni pamoja wimbo unaohamasisha watoto kung’ara kama nuru, kama vile “Shine On” au “I Am like a Star” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 144, 163). Waambie watoto kuhusu nuru unayoona ndani yao wakati wanapofanya “matendo mema,” na elezea jinsi nuru na mifano yao inavyowasaidia wengine na kukupa msukumo wa kufanya kazi nzuri pia.

3 Nefi 14:7

Baba wa Mbinguni hujibu sala zangu.

Mstari huu unaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Mungu atasikia na kujibu sala zao.

Shughuli za Yakini

  • Unaposoma 3 Nefi 14:7, waalike watoto kufanya matendo ambayo huwakilisha kila moja ya mialiko ya Mwokozi katika mstari huu. Kwa mfano, wangeweza kuinua mikono yao (omba), kutengeneza darubini kwa mikono yao (tafuta), au kutengeneza mwendo wa kubisha (bisha). Wasaidie watoto kufikiria juu ya mambo wanayoweza kusema na kuomba katika sala zao. Elezea kwamba tunaweza kumwambia Baba wa Mbinguni chochote, na Yeye atasikiliza kwa sababu Anatupenda.

  • Waalike watoto wakuonyeshe kile wanachokifanya kwa mikono yao, macho, na kichwa wakati wanaposali. Tumia wimbo kama “We Bow Our Heads” ili kusaidia (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 25). Tunazungumza na nani tunaposali? Toa ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni husikia sala zetu.

3 Nefi 14:24–27

Mwokozi ananitaka mimi kusikia na kutenda kile Yeye anachofundisha.

Kusikia tu maneno ya Mwokozi hakutoshi. Ni wale tu wanaoishi mafundisho Yake wanaweza kuhimili dhoruba za maisha.

Shughuli za Yakini

  • Imbeni pamoja “The Wise Man and the Foolish Man” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 281), au someni 3 Nefi 14:24–27. Wasaidie watoto kuweka majina yao kwenye “mwenye busara” wakati wanapoimba. Kwa nini nyumba ya mwenye busara ilibaki imesimama wakati wa dhoruba? Rejea mstari wa 24 kusisitiza kwamba alisikiliza na kutenda kile Mwokozi alichosema.

  • Waonyeshe watoto mwamba na mchanga. Waombe waonyeshe kwa kidole mwamba wakati ukielezea uchaguzi wa kumfuata Mwokozi na kuonyesha mchanga wakati ukielezea uchaguzi wa kutomfuata Yeye. Shuhudia kwamba tunapofanya kile Mwokozi anachosema, tunakuwa imara kama nyumba iliyojengwa juu ya mwamba.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

3 Nefi 12:6

Ninapaswa kuwa na njaa na kiu ya haki.

Kila mmoja anaweza kupata njaa na kiu; Mwokozi alizungumzia hisia hizi ili kutufundisha jinsi tunavyopaswa kuhisi kuhusu kutafuta haki.

Shughuli za Yakini

  • Bila kuwaruhusu watoto wengine kusikia, muombe mtoto mmoja kujifanya anakula au kunywa, na waruhusu watoto wengine kubahatisha ni nini anafanya. Tunapata hisia gani kwa kula chakula kizuri au kunywa maji safi? Ni kwa jinsi gani tunalisha roho zetu? Waalike watoto kusoma 3 Nefi 12:6 kutafuta Mwokozi anataka tuwe na “njaa na kiu” ya nini. Ni kwa jinsi gani tunaonyesha kwamba tunataka haki zaidi kama tunavyotaka chakula na kinywaji?

  • Leta picha za chakula na kinywaji, na wekea alama kila moja kwa marejeleo ya maandiko kama Zaburi 119:103; Yohana 6:35; 2 Nefi 32:3; Enoshi 1:4; au 3 Nefi 20:8. Waombe watoto wasome vifungu vya maneno na kuelezea kile vinachofundisha kuhusu kile tunachoweza kufanya kuonyesha kwamba tuna njaa na kiu ya haki. Shiriki uzoefu ambapo ulihisi “kujazwa na Roho Mtakatifu,” na waalike watoto kushiriki uzoefu wao.

3 Nefi 13:1–8, 16–18

Ninapaswa kufanya mambo sahihi kwa sababu sahihi.

Mistari hii huonyesha kwamba matendo mema hayatoshi—matendo yetu lazima yavuviwe na upendo kwa Mungu na hamu ya kumtumikia Yeye.

Shughuli za Yakini

  • Muombe kila mtoto kutafuta 3 Nefi 13:1–4, 5–8, au 16–18 na kutambua matendo mema yaliyotajwa katika mistari hii (elezea kwamba kutoa “sadaka” humaanisha kuwapa masikini). Kwa nini Mwokozi alisema tusiwe kama baadhi ya watu wanaofanya mambo haya?

  • Mpe kila mtoto kipande cha karatasi chenye tendo la haki juu yake (au waruhusu wafikirie mifano yao wenyewe). Waombe wafikirie sababu nzuri na sababu mbaya za kufanya mambo hayo. Wahimize daima kufanya mambo sahihi kwa sababu sahihi.

3 Nefi 14:21–27; 15:1

Usalama wa kiroho huja kwa kusikia na kutenda kile Mwokozi anachofundisha.

“Mvua” na “mafuriko” huja kwetu sote katika maisha, lakini tunaweza kunusurika majaribu kama tutasikia na kutenda kile Yesu anachofundisha.

Shughuli za Yakini

  • Kama darasa, someni 3 Nefi 14:21–27 na 15:1, na waombe watoto wasimame kila mara unaposoma neno “kufanya.” Kwa nini Mwokozi anasisitiza kufanya mafundisho Yake, na siyo tu kusikia au kukumbuka? Waalike watoto kuchora picha ya mstari wa 24–25 na kuandika juu ya mwamba “Yesu” na jambo Yesu alilotufundisha kufanya. Imbeni pamoja “The Wise Man and the Foolish Man” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,281).

  • Waalike watoto kusimama, na waombe wafikirie kwamba mguu mmoja huwakilisha kusikia maneno ya Mwokozi na mwingine huwakilisha kuyafanya. Waalike wainue mguu wa “kufanya” na kuuweka sawasawa na mguu wa “kusikia”. Nini kingetokea kama upepo mkali ungevuma katika chumba? Tumia mfano huu kuelezea kwa nini ni salama zaidi kufanya kile Mwokozi anachosema na siyo tu kusikia maneno Yake.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuchagua kitu kimoja walichojifunza kuhusu mafundisho ya Yesu leo na kuamua jinsi watakavyokifanyia kazi. Ni kwa jinsi gani matendo yao yatawasaidia kuwa nuru kwa familia zao na marafiki?

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tohoa shughuli kutosheleza mahitaji. Usione mihutasari hii kama maelekezo ambayo ni lazima kuyafuata. Badala yake, itumie kama chanzo cha mawazo ya kuchochea hisia zako mwenyewe unapotafakari mahitaji ya watoto unaofundisha. Katika baadhi ya hali, ungeweza kuhisi msukumo wa kutohoa mawazo kwa ajili ya watoto wadogo ili kuwafundisha watoto wakubwa, au kinyume chake.

Chapisha