Njoo, Unifuate
Septemba 28–Oktoba 11. 3 Nefi 17–19: “Tazama, Shangwe Yangu Imetimia”


“Septemba 28–Oktoba 11. 3 Nefi 17–19: ‘Tazama, Shangwe Yangu Imetimia,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Septemba 28–Oktoba 11. 3 Nefi 17–19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Kristo anawatokea Wanefi

Nuru ya Mwonekano Wake Iling’ara juu Yao, na Gary L. Kapp

Septemba 28–Oktoba11

3 Nefi 17–19

“Tazama, Shangwe Yangu Imetimia”

Unaposoma 3 Nefi 17–19, fikiria ni maandiko yapi, uzoefu upi, shughuli zipi, na hadithi zipi zingeweza kuwasaidia watoto kuelewa kweli katika milango hii.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha ya Mwokozi, na waalike watoto kushiriki jinsi ambavyo wangeweza kuhisi kama Angewatembelea jinsi alivyofanya kwa Wanefi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

3 Nefi 17:7, 20–25

Mwokozi anampenda kila mmoja wa watoto wa Baba wa Mbinguni.

Yesu alionyesha upendo Wake kwa watoto wakati Alipowabariki na kusali kwa ajili yao. Unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kuhisi upendo Wake kwa ajili yao?

Shughuli za Yakini

  • Fanyia ufupisho maelezo kwenye 3 Nefi 17 wakati ukionyesha picha kama ile iliyoko kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia. Au ungeweza kutumia “Mlango wa 44: Yesu Kristo Anawabariki Watoto” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 124–25, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Soma vifungu vya maneno na mistari kutoka 3 Nefi 17 ambavyo vinasisitiza upendo wa Mwokozi kwa watu (kama vile mstari wa 7 na 20–25). Acha watoto wafanye zamu kushikilia picha na kusimulia kile Yesu alichofanya kwa sababu Aliwapenda watu.

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kuchora picha yao wenyewe wakiwa na Yesu. Wanapofanya hivyo, wasaidie kufikiria njia ambazo Yesu ameonyesha upendo Wake kwao.

    Picha
    Yesu Anawabariki Watoto wa Wanefi

    Tazama Watoto Wenu, na Gary L. Kapp

3 Nefi 18:1–12

Ninaweza kumfikiria Yesu wakati ninapopokea sakramenti.

Kuna mambo mengi yanayoweza kumvuruga mtoto wakati wa sakramenti. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto darasani mwako kuelewa umuhimu wa kumfikiria Mwokozi na upendo Wake kwao wakati wa ibada hii takatifu?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto wakuambie nini kinatendeka wakati wa sakramenti. Soma mistari kutoka kwenye tukio la Yesu akihudumia sakramenti kwa Wanefi (ona 3 Nefi 18:1–12), na waombe watoto kusimama wanaposikia jambo ambalo linafanana na kile tunachofanya wakati wa sakramenti. Ni nini Yesu Kristo anatutaka “tukumbuke” au kufikiria wakati wa sakramenti? (ona 3 Nefi 18:7, 11).

  • Imba hali midomo imefungwa, imba maneno, au piga wimbo wa Kanisa au wimbo wa Msingi wakati watoto wakipaka rangi picha ambazo zitawasaidia kumkumbuka Mwokozi wakati wa sakramenti (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Wahimize kutazama picha hizi ili ziwasaidie kumkumbuka Yesu wakati wanapopokea sakramenti.

3 Nefi 18:15, 20–21, 24; 19:16–17, 30

Yesu hunifundisha jinsi ya kusali.

Je, unajifunza nini kuhusu sala unaposoma 3 Nefi 17–19? Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia kile unachojifunza kuwafundisha watoto jinsi ya kusali?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha za watu wakisali (kama vile zile zilizoko kwenye “Mlango wa 46: Yesu Kristo Anafundisha na Kusali pamoja na Wanefi” katika Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 128–30). Waalike watoto kuonyesha maelezo katika picha yanayoonyesha kwamba watu hawa wanasali. Soma 3 Nefi 19:16–17 kuelezea kwamba Yesu alitufundisha jinsi ya kusali. Waruhusu watoto wakuambie jinsi wanavyohisi wakati wanaposali.

  • Soma 3 Nefi 18:21, na waalike watoto wachore picha yao wenyewe au familia zao zikisali. Wahimize watoto kuwaalika wanafamilia wao kusali pamoja nao.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu sala, kama vile “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13). Waombe watoto kushiriki kile wanachojifunza kuhusu sala kutoka kwenye wimbo. Shiriki ushuhuda wako juu ya sala.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

3 Nefi 17

Mwokozi anawapenda watoto wa Baba wa Mbinguni.

Rais Ezra Taft Benson alifundisha: “Ninawaahidi, watoto wapendwa, kwamba malaika watawahudumia pia. Mnaweza msiwaone, lakini watakuwepo pale kuwasaidia, na mtahisi uwepo wao” (“Kwa Watoto wa Kanisa,” Ensign, Mei 1989, 83).

Shughuli za Yakini

  • Someni pamoja mistari kadhaa kutoka 3 Nefi 17 ambayo unahisi itakuwa na maana kwa watoto unaowafundisha. Unaposoma kila mstari, waombe watoto wachague neno au kifungu cha maneno ambacho wanahisi ni cha muhimu na kisha kushiriki kwa nini maneno hayo yalikuwa na maana kwao. Shuhudia kwamba Yesu anawapenda sana watoto, na hii ndiyo sababu Yeye aliwabariki na kusali kwa ajili yao.

  • Waalike watoto kushiriki ni kwa jinsi gani wangehisi kama wangekuwa kati ya watoto ambao Mwokozi aliwabariki. Ikiwezekana, onyesha video “My Joy Is Full” (ChurchofJesusChrist.org) kuwasaidia kupata taswira ya tukio hili. Je, ni nini Mwokozi alifanya kuonyesha upendo Wake? Ni nini tunaweza kufanya kujiandaa kuwa na Yeye wakati Atakapokuja tena?

3 Nefi 18:1–12

Ninapopokea sakramenti, ninaweza kujazwa na Roho Mtakatifu.

Tunaweza kujifunza kutoka 3 Nefi 18 jinsi sakramenti ilivyo muhimu kwa Mwokozi. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuhisi kwamba sakramenti ni muhimu kwao?

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kusoma 3 Nefi 18:1–12. Unajifunza nini kuhusu sakramenti kutokana na mistari hii? Wasaidie kusoma sala ya sakramenti katika Mafundisho na Maagano 20:77 na 79 na utafute maneno na vifungu vya maneno katika sala ambavyo pia vinapatikana katika 3 Nefi 18:1–12. Maneno na vifungu hivi vya maneno vinamaanisha nini? Tunawezaje kujiandaa wenyewe kupokea sakramenti? Ni nini tunaahidi, au kuweka agano kufanya tunapo pokea sakramenti?

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu unyenyekevu, kama vile “Reverently, Quietly” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 26). Ni kwa namna gani kupokea sakramenti kwa unyenyekevu hutusaidia kuhisi Roho? Ni kwa jinsi gani kunatusaidia kufanya chaguzi za haki?

3 Nefi 18:15–24; 19:6–9, 15–36

Kusali kutanisaidia kuwa karibu na Baba wa Mbinguni.

Tunaweza kumhisi Baba wa Mbinguni karibu nasi kupitia sala. Ni jumbe zipi kuhusu sala katika 3 Nefi 18–19 zitawasaidia watoto unaowafundisha kuboresha sala zao?

Shughuli za Yakini

  • Andika marejeleo yafuatayo ya maandiko kwenye vipande vya karatasi, na vitoe kwa kila mtoto au kwa makundi madogo ya watoto: 3 Nefi 18:15; 3 Nefi 18:20; 3 Nefi 18:21; 3 Nefi 19:19; na 3 Nefi 19:24. Waalike watoto kusoma maandiko, wakitafuta mambo Yesu Kristo au wanafunzi Wake waliyofundisha kuhusu sala. Waombe waripoti kile wanachojifunza kwa darasa.

  • Ubaoni, andika Ninakushukuru kwa . Wape watoto dakika moja ya kufikiria mambo mengi kadiri wawezavyo ili kujaza nafasi zilizo wazi. Kwa nini ni vizuri kwetu kuonyesha shukrani kwa Baba wa Mbinguni? Kisha andika Ninakuomba ubaoni, na someni pamoja 3 Nefi 18:18–21 na 19:9, 23, mkitafuta mawazo kuhusu kile tunachopaswa kukiombea.

  • Shiriki ushuhuda wako au uzoefu binafsi kuhusu nguvu ya sala, na wahimize watoto kushiriki shuhuda zao au uzoefu wao.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kuzungumza na wazazi wao au wanafamilia wengine kuhusu jinsi wanavyoweza kuwa na uzoefu wenye maana zaidi wa sakramenti Jumapili inayofuata.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto wadogo kujifunza kutoka kwenye maandiko. Ili kuwasaidia watoto wadogo kujifunza kutoka kwenye maandiko, fokasi katika mstari mmoja wa maandiko au hata maneno muhimu tu. Unaweza kuwaalika watoto kusimama wakati wanaposikia neno maalumu au kifungu cha maneno.

Chapisha