“Oktoba 19–25. 3 Nefi 27–4 Nefi: ‘Hakujakuwa na Watu ambao Wangekuwa na Furaha Zaidi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Oktoba 19–25. 3 Nefi 27–4 Nefi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Oktoba 19–25
3 Nefi 27–4 Nefi
“Hakujakuwa na Watu ambao Wangekuwa na Furaha Zaidi”
Unaposoma 3 Nefi 27–4 Nefi, fikiria uzoefu, mawazo, maandiko, na hadithi ambazo zingeweza kuwasaidia watoto kuelewa dhana katika milango hii.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Wasaidie watoto kukumbuka kile walichojifunza wiki chache zilizopita kuhusu kile Yesu alichofundisha watu katika nchi ya Neema. Elezea kwamba Kitabu cha Mormoni kinatuambia jinsi watu walivyobarikiwa wakati walipotii kile Yesu alichowafundisha.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo.
Ni kwa jinsi gani maneno ya Mwokozi kwa wanafunzi Wake yanawasaidia watoto kuelewa umuhimu wa kuwa wa Kanisa la Yesu Kristo?
Shughuli za Yakini
-
Muombe kila mtoto kusema jina lake. Kwa nini majina yetu ni muhimu? Waambie kwamba wanafunzi wa Yesu walitaka kujua waliiteje Kanisa la Kristo. Wasomee jibu la Mwokozi katika 3 Nefi 27:7. Nani Yesu alisema Kanisa Lake liitwe kwa jina lake?
-
Tengeneza beji ambayo inasema “Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho” kwa kila mtoto ili akavae nyumbani. Waache watoto wapake rangi beji zao. Imbeni “The Church of Jesus Christ” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77) kama darasa. Waambie kwa nini una shukuru kuwa Kanisani, na waulize watoto kwa nini wana shukrani kwa ajili ya Kanisa.
-
Wasaidie watoto kuweka pamoja fumbo katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Elezea kwamba Yesu anataka Kanisa Lake lijengwe juu ya injili Yake, na tumia ukurasa wa shughuli kuzungumza na watoto kuhusu hilo lina maana gani.
Kuishi Injili kunanipa shangwe.
Furaha ya watu iliyoelezewa katika 4 Nefi inaweza kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu shangwe inayokuja kwa kuishi injili.
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto kuzungumza kuhusu kile kinachowapa furaha. Ili kuwaambia watoto kuhusu furaha ya watu katika 4 Nefi, soma vifungu muhimu vya maneno kutoka mstari wa 2–3 na 15–17. Ungeweza pia kurejelea “Mlango wa 48: Amani katika Amerika” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 136–37, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Sisitiza kwamba watu walikuwa wenye furaha kwa sababu waliongoka kwa Bwana, waliishi kulingana na amri, na walipendana.
-
Onyesha picha za watu wenye furaha. Elezea kwamba watu katika 4 Nefi walikuwa na takribani miaka 200 ya furaha kwa sababu wote walijaribu kwa kadiri ya uwezo wao kuishi injili. Wasaidie watoto kufikiria baadhi ya amri ambazo wangeweza kutii. Kwa mfano, ungeweza kuwasomea 4 Nefi 1:15 kufundisha kwamba watu hawakupigana tena wao kwa wao. Waalike watoto kuigiza kutii amri walizozifikiria. Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu shangwe inayokuja kutokana na kuishi injili, kama vile “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198).
-
Soma vifungu vya maneno kutoka 4 Nefi 1:24–29, 34–35, na 43 ambavyo vinaeleza kile kilichotokea wakati baadhi ya Wanefi walipoacha kutii amri. Unapofanya hivyo, waalike watoto kufanya uso wa huzuni wakati wanaposikia jambo ambalo halileti furaha. Shuhudia kwamba kutii amri huongoza kwenye furaha.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo.
Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kutambua baraka kuu zinazokuja kutokana na kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo.
Shughuli za Yakini
-
Wasaidie watoto kusoma 3 Nefi 27:3, mkitafuta swali wanafunzi wa Yesu walilomuuliza Yesu. Kisha waalike kutafuta katika 3 Nefi 27:5–8 kwa ajili ya jibu. Kulingana na mistari hii, kwa nini jina la Kanisa ni muhimu?
-
Wasaidie watoto kufikiria makundi mbalimbali waliyopo, kama vile familia au darasa la Msingi. Waombe wakuambie kile wanachokipenda kuhusu kila kikundi. Waombe watoto wakusaidie kuandika kila neno la jina la Kanisa kwenye kipande tofauti cha karatasi. Kisha changanya karatasi, na waalike watoto kupanga maneno haya katika mpangilio mzuri. Ni baraka zipi tumepokea kwa sababu sisi ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho?
Kanisa la Yesu Kristo limejengwa juu ya injili Yake.
Mwokozi alifanya ufupisho wa injili Yake katika 3 Nefi 27. Ni kwa jinsi gani maneno Yake yangeweza kuwasaidia watoto kuelewa injili ni nini?
Shughuli za Yakini
-
Elezea kwa watoto kwamba neno injili humaanisha “habari njema” (ona Kamusi ya Biblia, “Injili”). Wasaidie watoto kutafuta 3 Nefi 27:13–15 kupata jambo ambalo linasikika kama habari njema kwao. Je, ni kwa nini tuna shukrani kuijua injili ya Yesu Kristo?
-
Andika ubaoni kanuni za injili kama imani, toba, ubatizo, Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho. Waalike watoto kutafuta 3 Nefi 27:19–21, wakitafuta maneno haya au maneno sawa na haya katika maelezo ya Yesu ya injili Yake.
-
Waombe watoto kuvuta taswira kwamba wana rafiki anayewauliza kile wanachoamini kama muumuni wa Kanisa. Wasaidie kupata kweli katika 3 Nefi 27:13–21 ambazo wangeweza kushiriki ili kufupisha kile wanachoamini.
-
Waalike watoto kuchagua moja ya kweli za injili Mwokozi alizofundisha katika 3 Nefi 27:13–21 ambazo wanataka kujifunza zaidi kuzihusu. Wasaidie kutumia tanbihi chini ya ukurasa, Mwongozo wa Mada, au Mwongozo kwenye Maandiko ili kupata andiko moja au mawili yanayohusiana na ukweli huo. Waalike kushiriki maandiko yao wao kwa wao na kile walichojifunza. Je, ni kwa nini tuna shukrani kuijua injili ya Yesu Kristo?
Kuishi Injili kunanipa shangwe.
Kwa sababu waliongoka kwa Yesu Kristo na injili Yake, watu walioelezewa katika 4 Nefi waliweza kuanzisha jamii ya amani na umoja. Ni nini watoto wanaweza kujifunza kutoka kwao?
Shughuli za Yakini
-
Andaa vipande vya karatasi vyenye vifungu vya maneno kutoka 4 Nefi 1:2–3, 5, na 15–17 ambavyo huelezea baraka watu walizopokea (kama vile “hakukuwepo na mabishano katika nchi”). Weka vipande vya karatasi ndani ya chombo, na mwache kila mtoto achukue kimoja na kukisoma. Wahimize watoto kutafuta kifungu chao cha maneno katika mistari hii kutoka 4 Nefi. Tunajifunza nini kutoka kwenye vifungu hivi vya maneno? Ni mfanano upi tunauona kati ya mistari hii na maana ya Sayuni katika Musa 7:18?
-
Ili kuwasaidia watoto kufanyia kazi kile kilichofundishwa katika 4 Nefi 1:15–16, wape mazingira ambapo watu wamekasirikiana wao kwa wao. Waalike kuigiza nafasi hali ingekuwaje kama wangejaribu kuishi bila “mabishano.” Kwa nini ni rahisi kuepuka mabishano wakati tunapokuwa na “upendo wa Mungu” mioyoni mwetu?
-
Soma pamoja na watoto mistari ifuatayo, na waombe watafute sababu za Wanefi na Walamani kutokuwa tena na amani na furaha: 4 Nefi 1:20, 24–29, 34–35, na 43. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuepuka hatari hizi? Wasaidie watoto kugundua njia tunazoweza kuepuka kuwa wenye kiburi kwa kurejea Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Ezra Taft Benson (2014), 238–39.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wahimize watoto kuamua juu ya jambo moja watakalofanya ili kuleta amani zaidi na furaha katika nyumba zao na kulishiriki na familia zao.