“Septemba 16–22. 2 Wakorintho 8–13: ‘Mungu Humpenda Yeye Atoaye kwa Moyo wa Ukunjufu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Septemba16–22. 2 Wakorintho 8–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Septemba 16–22
2 Wakorintho 8–13
“Mungu Humpenda Yeye Atoaye kwa Moyo wa Ukunjufu”
Mawazo yako bora kwa ajili ya kuwafundisha watoto katika darasa lako yatakuja unapojifunza kwa maombi 2 Wakorintho 8–13 na wao wakiwa akilini mwako. Mafundisho ya ziada yanaweza kupatikana katika muhtasari huu.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Njia moja mzuri ya kualika kushiriki miongoni mwa watoto ni kuwakumbusha juu ya kitu fulani ulichowataka wafanye wakati wa somo lililopita. Waombe washiriki uzoefu wao.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Ninaweza kutoa kwa moyo wa ukunjufu kwa watu wenye shida.
Daima ni vizuri kuwahudumia wengine, lakini ni bora zaidi kuhudumia kwa moyo wa ukunjufu. Fikiria nini kitamvutia kila mtoto kuwa “mtoaji mwenye moyo wa ukunjufu.”
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto kurudia kirai “Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” (2 Wakorintho 9:7). Inamaanisha nini kuwa “mtoaji kwa moyo wa ukunjufu”? Onyesha picha ya uso wenye furaha na uso wenye huzuni, na waulize watoto upi unaonekana kama atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
-
Imbeni pamoja wimbo kuhusu huduma, kama vile “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto 198), mara kadhaa. Mara ya kwanza, waombe watoto waimbe kwa furaha; kisha waombe waimbe wimbo kwa mihemko au mitazamo, kama vile huzuni, kuchoka, hasira, au hofu. Wakumbushe watoto kwamba Baba wa Mbinguni anatutaka kusaidia wengine kwa furaha. Kisha imba wimbo huo tena kwa furaha.
-
Wape watoto picha za sura zinazotabasamu. Waombe waziinue juu picha zao wakati wanaposikia maneno tabasamu au kutabasamu wanapoimba ”Smiles” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 267). Wanaweza kufanya kitu kile kile na picha za sura za kununa na maneno chukia na kuchukia. Waambie watoto kwamba sura iliyonuna sio yenye furaha; njia moja ya kuwa mwenye furaha na kuhudumia wengine ni kutabasamu na kuwasaidia wengine nao watabasamu.
-
Panga shughuli ya darasa ili kuhudumia mtu fulani, kama vile mtoto asiyehudhuria darasa la msingi au mshiriki wa kata au jirani mwenye shida. Mnaweza kupanga kumtembelea nyumbani kwa mtu huyu, kuandika barua za huruma au kuchora picha, au kutengeneza kitafunywa cha kushiriki.
-
Mwalike kila mtoto kupanga tendo la huduma ya furaha kwa mmoja wa wanafamilia yake. Wakati wa somo la wiki ijayo, waombe waelezee kile walichofanya.
Baba wa Mbinguni siku zote anajibu sala, lakini sio siku zote atanipa kila ninachomwomba.
Uzoefu wa Paulo wa kusali kwa “mwiba wake katika mwili” uondolewe inatufundisha kwamba Mungu wakati mwingine anaonyesha upendo Wake kwa ajili yetu kwa kutokutupa kile tunachokitaka.
Shughuli Yamkini
-
Onyesha watoto mmea wenye miiba (au picha yake). Wasaidie kufikiria jinsi watakavyojisikia kuwa na mwiba uliokwama katika miili yao kwa muda mrefu. Fanyia muhtasari 2 Wakorintho 12:7–10 kwa watoto, kwa kutumia maneno watakayoelewa vyema. Eleza kwamba “mwiba katika mwili” wa Paulo ilikuwa jaribu, kama vile udhaifu wa kimaumbile. Hata kama Paulo alimwomba Mungu kuondoa jaribu, Mungu hakufanya hivyo. Badala yake, Mungu alimfundisha Paulo kwamba changamoto zinaweza kutusaidia kujifunza kuwa wanyenyekevu na kumwamini Yeye. Kisha Mungu anaweza kutufanya kuwa imara.
-
Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni anajua kipi kilicho bora kwa ajili yetu, na atatupa kile tunachohitaji, hata kama ni tofauti na kile tunachodhani tunahitaji. Unaweza pia kushiriki uzoefu wakati sala zako zilipojibiwa katika njia au wakati ambao ulikuwa tofauti na ule uliotegemea. Hadithi “Usisahau Kuomba kwa ajili ya Eric” (Friend, Jan.2017, 36–37) inaweza pia kusaidia.
-
Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu Upendo wa Baba wa Mbinguni, kama vile “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto 12–13). Waulize watoto kile watakachosema kwa mtu fulani anayeshangaa kama Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala. Imbeni wimbo tena, na onyesha mistari ambayo inaeleza jinsi Baba wa Mbinguni anavyojisikia kutuhusu sisi.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Ninaweza kutoa kwa moyo wa ukunjufu kwa watu wenye shida.
Paulo alitaka kuwapa mwongozo wa kiungu Watakatifu wa kutoa ziada yao ili kuwasaidia maskini. Je, ni kwa jinsi gani wewe utatumia maneno yake kuwapa mwongozo wa kiungu watoto ili kuhudumia wengine?
Shughuli Yamkini
-
Andika maneno ya 2 Wakorintho 9:7 ubaoni, na huku ukiacha mapengo ya maneno muhimu. Waalike watoto kukisia ni maneno gani yanayokosekana. Kisha waache wasome aya katika maandiko ili kujaza mapengo. Inamaanisha nini kutoa “kwa kunung’una, au kwa lazima”? Inamaanisha nini kuwa “mtoaji kwa moyo wa ukunjufu”?
-
Waalike watoto wakusaidie kutafuta picha za Mwokozi akiwahudumia watu wengine (zipo kadhaa katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waulize wanaona nini katika picha hizi ambacho kinawasaidia kujua kwamba Yesu aliwahudumia wengine kwa upendo. Wekeni lengo kama darasa kusema ndiyo wakati wanafamilia au wengine wanatuomba kuhudumia katika wiki ijayo, kama vile kwa kusaidia nyumbani au kushughulikia wengine.
-
Wasaidie watoto kupamba mawe madogo. Waalike kubeba “mawe yao ya huduma“ mifukoni mwao wiki hii ili kuwasaidia kukumbuka kuwahudumia wengine kwa moyo wa ukunjufu.
-
Wasaidie watoto kuja na mistari mipya ya wimbo kuhusu huduma, kama vile “Fun To Do” (Kitabu Cha Nyimbo Za Watoto, 253), ambao unafundisha kwamba ni furaha kuhudumia wengine katika njia tofauti.
Baba wa Mbinguni siku zote anajibu sala, lakini sio siku zote atanipa kila ninachomwomba.
Paulo alimwomba Mungu kuondoa udhaifu wake, lakini Mungu alijua kwamba udhaifu wa Paulo utamfanya awe myenyekevu na kumfanya kuwa imara.
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto kufananisha 2 Wakorintho 12:9–12 na Etheri 12:27. Je, ni maneno gani au virai vilivyorudiwa? Je, aya hizi zinafundisha nini? (Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba Paulo alikuwa anafananisha changamoto yake na mwiba katika mwili wake.) Mungu alimfundisha nini Paulo kuhusu majaribu?
-
Waalike watoto kuorodhesha baadhi ya majaribu ambayo watu huwa nayo katika maisha. Wasaidie kufikiria jinsi mtu fulani anavyoweza kujifunza kutokana na majaribu haya na kubarikiwa nayo.
-
Soma pamoja na watoto “Je, Baba wa Mbinguni Daima Atajibu Maombi Yangu?” (Friend, Jan. 2017, 12–13 ). Waombe watoto kushiriki uzoefu wakati walipoomba kwa ajili ya kitu fulani na hawakukipata. Waombe washiriki kile walichojifunza kutokana na uzoefu wao. Unaweza kuwa na uzoefu wako binafsi wa kushiriki. Toa ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni siku zote anajibu sala zetu katika njia na katika wakati ambao tutabarikiwa zaidi.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kuwa watoaji kwa moyo wa ukunjufu katika nyumba zao wiki hii na kuja darasani wiki ijayo wakiwa wamejitayarisha kutoa taarifa juu ya jinsi walivyomhudumia mtu fulani mwenye shida.