Njoo, Unifuate
Septemba 2–8. 1 Wakorintho 14–16: ‘Mungu Si Mungu wa Machafuko, bali wa Amani’


‘Septemba 2–8. 1 Wakorintho 14–16: ‘Mungu Si Mungu wa Machafuko, bali wa Amani’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Septemba 2–8. 1 Wakorintho 14–16,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
kisima cha maji ya ubatizo cha Hekaluni

Septemba 2–8

1 Wakorintho 14–16

“Mungu Si Mungu wa Machafuko, bali wa Amani”

Unaposoma 1 Wakorintho 14–16, Roho Mtakatifu atakusaidia kujua nini cha kuwafundisha watoto katika darasa lako. Pitia upya muhtasari huu kwa ajili ya mawazo ya ziada.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Unaweza kuanza somo la wiki hii kwa kusoma 1 Wakorintho 14:26 kwa sauti. Weka angalizo kwamba tunapokuja pamoja Kanisani, tunaweza kuwainua (au kuwajenga na kuwasaidia) wengine wakati tunaposhiriki. Je, watoto wanaweza kushiriki nini cha kumjenga mtu fulani katika darasa leo?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

1  Wakorintho 3:12–22

Ninaweza kuishi na Baba wa Mbinguni baada ya mimi kufa kwa sababu Yesu Kristo alifufuka.

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwafundisha watoto katika darasa lako kwamba kwa sababu Yesu Kristo alifufuka sisi tunaweza kuishi tena?

Shughuli Yamkini

  • Rudia kirai kifuatacho mara kadhaa pamoja na watoto: “Katika Kristo wote watahuishwa” (1 Wakorintho 15:22). Onyesha picha ya Mwokozi aliyefufuka (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia.). Elezea kwamba sisi wote tutakufa siku moja, lakini kwa sababu Yesu alifufuka, sisi pia tutaishi tena baada ya kufa.

  • Tumia somo linalofundishwa kwa vielelezo kama hili kufundisha kuhusu Ufufuko: Waoneshe watoto jaketi, ambalo linawakilisha miili yetu ya asili. Wakati tunapoishi, roho zetu zipo ndani ya miili yetu, na miili yetu inaweza kutembea (livae jaketi). Tunapokufa, roho zetu zinaiacha miili yetu ya asili, na miili yetu haiwezi kutembea (vua jaketi na liweke juu ya meza au kiti kuwakilisha mwili bila roho yake). Tutakapofufuka, roho zetu zinarudi ndani ya miili yetu (vaa jaketi tena), na kamwe havitengani tena. Waache watoto wachukuwe zamu kulivaa jaketi na kulivua wakati mtoto mwingine anaelezea nini kinatokea wakati tutakapofufuka.

1 Wakorintho 15:29

Ninaweza kubatizwa kwa ajili ya watu waliokufa.

Watoto unaowafundisha wanaweza kujitayarisha sasa kwenda hekaluni na kubatizwa kwa niaba ya wafu wakati watakapokuwa na umri wa miaka 12. Paulo anataja mafundisho haya muhimu katika waraka wake kwa Wakorintho.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya vitu wasivyoweza kujifanyia wenyewe (kama vile kubeba kitu kizito au kufikia kitu fulani juu ya kabati refu). Nani anawasaidia kufanya vitu hivyo? Onyesha picha ya mmoja wa mababu zako aliyekufa bila kubatizwa. Waambie watoto kuhusu mtu huyu, na eleza kwamba mtu huyu hawezi kubatizwa bila msaada kutoka kwa mtu fulani duniani.

  • Waulize watoto kama wana mwana familia yoyote ambaye amewahi kuwa hekaluni kufanya ubatizo kwa ajili ya wafu. Onyesha picha za kisima cha maji ya ubatizo cha hekaluni. Je, watoto wanajua nini kinatokea hapa? Elezea kwamba ndani ya hekalu tunaweza kubatizwa kwa niaba ya watu waliokufa bila kubatizwa. Kisha watu hao wanaweza kuchagua kama kukubali ubatizo huo.

1 Wakorintho 15:40–41

Baba wa Mbinguni ananitaka mimi kuishi pamoja Naye katika ufalme wa selestia.

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwafundisha watoto kuhusu falme za selestia, terestia, na telestia? Shughuli hizi zinaweza kukusaidia.

Shughuli Yamkini

  • Andika ubaoni selestia, terestia na telestia. Wasaidie watoto kujifunza kusema maneno haya.

  • Onyesha picha za jua, mwezi, na nyota. Je, ni kipi kilicho angavu zaidi? Soma 1 Wakorintho 15:40–41 kwa watoto (ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, 1 Wakoritho 15:40, tanbihi a). Eleza kwamba jua, mwezi, na nyota vinawakilisha falme tunazoweza kuishi baada ya kufufuliwa. Katika ufalme wa selestia, tunaweza kuishi na Baba wa Mbinguni.

  • Chora jua ubaoni na weka vipande vidogo vya karatasi, au ngazi, ardhini kuelekea kwenye jua. Kila karatasi inaweza kuwakilisha kitu fulani tunachohitajika kufanya ili kuingia ufalme wa selestia (ona M&M 76:50–53). Waruhusu watoto washiriki mawazo yao na kuchukua hatua kuelekea ufalme wa selestia.

Picha
macheo

Paulo alifananisha utukufu wa selestia na jua.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

1  Wakorintho 3:12–22

Kwa sababu ya Yesu Kristo na Ufufuko Wake, nami nitafufuliwa.

Je, watoto unaowafundisha wanaelewa umuhimu wa kufufuka kwa Yesu Kristo? Mawazo haya yanaweza kukusaidia.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kuchukua zamu kusoma aya katika 1 Wakorintho 15:12–22, wakitafuta majibu kwa swali “kingetokea nini kama kusingekuwa na ufufuko?”

  • Waalike watoto kuigiza jinsi ya kueleza ufufuko kwa mtu fulani. Kwa mawazo, ona ujumbe wa Mzee Thomas S. Monson “Mrs. Patton—hadithi inaendelea” (Ensign au Liahona, Nov. 2007, 21–24). Ona pia video “Mpaka Tutakapokutana Tena” (LDS.org). Toa ushuhuda wako juu ya Ufufuko wa Kristo.

1 Wakorintho 3:12–13, 20–22, 29

Ninaweza kujiandaa kwenda hekaluni kubatizwa kwa niaba ya wafu.

Wakati watoto wakifikia umri wa miaka 12, wanaweza kupata kibali cha hekalu na kufanya ubatizo kwa niaba ya wafu ndani ya hekalu. Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kujitayarisha?

Shughuli Yamkini

  • Soma 1 Wakorintho 15:29. Je, Watakatifu katika siku ya Paulo walikuwa wakifanya nini ambacho sisi pia tunafanya leo?

  • Waulize watoto kwa nini tunabatizwa kwa niaba ya wafu. Kama ni muhimu, eleza kwamba mababu zetu wengi hawakuwa na nafasi ya kubatizwa na kuthibitishwa wakati wa maisha haya. Katika hekalu tunaweza kubatizwa na kuthibitishwa kwa ajili yao.

  • Siku chache kabla ya darasa, muombe mzazi wa mmoja wa watoto kuja akiwa amejitayarisha kuelezea mti wa familia yake, au kusimulia hadithi kuhusu babu yake. Unaweza pia kushiriki kuhusu mababu zako.

  • Mwalike mshiriki wa uaskofu kuelezea baadhi ya mambo ambayo watoto wanaweza kufanya ili kustahili kuingia hekaluni. Waulize watoto kile wanachoweza kufanya ili kukumbuka kufanya vitu hivi. Andika mawazo yao ubaoni. Waalike kuweka lengo la kwenda hekaluni siku moja.

1 Wakorintho 15:40–41

Baada ya kufufuka, ninaweza kuishi katika ufalme wa selestia.

Kuwafundisha Wakorintho kuhusu miili tutakayopata katika ufufuko, Paulo alitaja madaraja matatu ya utukufu: selestia, terestria, na telestia.

Shughuli za Yakini

  • Soma 1 Wakorintho 15:40–41 na mwalike mtoto kuchora jua, mwezi, na nyota ubaoni. Waombe washiriki wa darasa kutambua aina gani ya mwili uliofufuka unawakilishwa na kila mchoro.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu mahekalu, kama vile “The Lord Gave Me a Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 153). Wimbo huu unafundisha nini kuhusu kujitayarisha kuishi katika utukufu wa selestia?

  • Eleza kwamba Joseph Smith alipata maono ambayo aliona falme tatu ambazo zinafanana na aina ya miili Paulo anayoelezea. Wasaidie watoto kupata virai kutoka Mafundisho na Maagano 76:50–53, 70; 76:71–79; 76:81–82 ambavyo vinaelezea falme hizi tatu.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuwaomba wazazi wao kuwaeleza hadithi kuhusu mmoja wa mababu zao. Wanaweza kushiriki hadithi hiyo pamoja na darasa wiki ijayo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wahimize watoto kuuliza maswali “Jitahidi kuona maswali ya [watoto] kama fursa, sio kama usumbufu au vizuizi kwa somo lako. … Maswali kama haya, yanakupa utambuzi muhimu wa kujua kile watoto wanachofikiria, wasiwasi walio nao, na jinsi wanavyoitikia mambo wanayojifunza. Wasaidie kuona kwamba majibu ya maswali yao yanaweza kupatikana katika maandiko na maneno ya manabii walio hai” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25–26).

Chapisha