Njoo, Unifuate
Agosti 26–Septemba 1. 1 Wakorintho 8-13: ‘Ninyi Mmekuwa Mwili wa Kristo’


“Agosti 26–Septemba1. 1 Wakorintho 8-13: ‘ Ninyi ni Mwili wa Kristo’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Agosti 26–Septemba 1. 1 Wakorintho 8-13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
mkutano wa Sakramenti

Agosti 26–Septemba 1

1  Wakorintho 8–13.

Ninyi Mmekuwa Mwili wa Kristo”

Unaposoma 1 Wakorintho 8–13, sikiliza ushawishi kutoka kwa Roho kuhusu jinsi ya kufundisha kanuni zilizoko katika sura hizi. Kumbuka kwamba wazo la shughuli yoyote linaweza kutoholewa kwa watoto wote wakubwa na wadogo.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto washiriki kitu fulani walichofanya wakati wa mkutano wa Sakramenti leo kufikiria kuhusu Yesu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

1 Wakorintho 10:13

Baba wa Mbinguni atanisaidia mimi kufanya maamuzi sahihi.

Siyo rahisi kila mara kuchagua yaliyo mema, lakini Baba wa Mbinguni atatusaidia kufanya maamuzi sahihi.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee 1 Wakorintho 10:13 watoto, ukiwaalika wageukie upande mwingine tofauti na wako wanaposikia maneno “alijaribiwa” au ”majaribu.”

  • Tengeneza alama ndogo za simama kwa ajili ya watoto. Simulia baadhi ya hadithi kwa ufupi za watu ambao wako karibu kufanya uchaguzi usio sahihi. Wakati watoto wanasikiliza, waalike kuinua juu ishara zao wakati mtu katika hadithi anafanya uchaguzi usio sahihi. Je, uchaguzi sahihi ungekuwa upi? Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni atawasaidia kuchagua yaliyo sahihi.

  • Onyesha picha ya Yesu, na imba pamoja na watoto wimbo kuhusu Yesu Kristo, kama vile “I’m Trying to Be Like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 79–79). Je, ni kwa jinsi gani kumkumbuka Yesu kunatusaidia kufanya chaguzi nzuri? Onyesha picha za vitu vingine ambavyo vinatusaidia kufanya chaguzi sahihi, kama vile wazazi au maandiko. Waulize watoto ni nini kinachowasaidia kufanya chaguzi sahihi.

1 Wakorintho 12:4, 7–11

Baba wa Mbinguni amenibariki na karama za kiroho.

Baba wa Mbinguni amewapa watoto wake wote karama za kiroho. Ni karama gani za kiroho unazoziona katika watoto unaowafundisha?

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja 1 Wakorintho 12:7–11, na tambua karama za kiroho Paulo alizozitaja. Wasaidie watoto wafikirie vitendo ambavyo vinaendana na karama hizi za kiroho, na kutumia vitendo kuwasaidia watoto kukumbuka karama.

  • Waombe watoto wachore picha ya karama waipendayo waliyoipata. Eleza kwamba Baba wa Mbinguni anatupa karama za kiroho ili kuimarisha imani yetu na kutusaidia kuwabariki wengine.

  • Andika barua kwa kila mtoto, ukieleza karama ya kiroho uliyoiona kwake (au unaweza kuwataka wazazi waandike barua hizi). Funga barua kama zawadi. Waruhusu watoto wafungue zawadi zao, na wasaidie kusoma karama zao za kiroho.

Picha
Masanduku ya zawadi

Baba wa Mbinguni amewapa watoto wake wote karama za kiroho.

1 Wakorintho 13:1–8

Naweza Kuwapenda Wengine

Maandiko yanafundisha kwamba hisani ni “upendo msafi wa Kristo” (Moroni 7:47). Unawezaje kuwasaidia watoto kuendeleza na kueleza upendo kama wa Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Soma 1 Wakorintho 13:8 na Moroni 7:47, na wasaidie watoto kurudia kirai “Hisani ni upendo msafi wa Kristo.” Onyesha picha za Yesu akiwa mwenye upendo na mpole, na waulize watoto jinsi gani alionesha upendo kwa wengine (ona Kitabu cha Sanaa cha Injili kwa ushauri).

  • Mchague mtoto asimame mbele ya chumba. Muulize mtoto jinsi gani atamhudumia mtu mwingine katika darasa. Eleza kwamba hii ni njia moja tunayoweza kuonyesha hisani kwa wengine. Waalike watoto wengine kuchukua zamu kuonyesha hisani.

  • Imbeni wimbo kuhusu kuwapenda wengine, kama vile “Jesus Said Love Everyone “ au Love One Another (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61, 136), pamoja na watoto. Onyesha picha za watu tofauti (kama vile mzazi, mwalimu, au rafiki), na waombe watoto kushiriki jinsi gani wanaweza kumhudumia mtu yule. Waombe watoto kufikiria juu ya mtu fulani ambaye wanaweza kumhudumia na kuandika barua au kuchora picha ya kumpa mtu yule. Kama unataka mawazo mengine, onyesha video “Peleka kwa Mwingine” (LDS.org).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

1 Wakorintho 10:13

Baba wa Mbinguni atanisaidia mimi kupinga majaribu.

Ahadi katika aya hizi zinaweza kuwapa watoto kujiamini kwamba Baba wa Mbinguni atawasaidia watakapokuwa wanajaribiwa.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wasome 1 Wakorintho 10:13 wawili wawili na kufanya muhtasari wa aya katika maneno yao. Waombe watoto kushiriki uzoefu ambapo Baba wa Mbinguni aliwasaidia kuepuka au kupinga majaribu. Je, tunaweza kufanya nini ili kumtegemea Baba wa Mbinguni wakati tunapojaribiwa?

  • Andika katika vipande vya karatasi majaribu ambayo watoto wanaweza kukabiliana nayo leo. Waalike watoto kila mmoja kuchagua karatasi na kushiriki kile Baba wa Mbinguni alichotoa kutusaidia kuepuka au kupinga majaribu haya. Kwa baadhi ya mawazo; someni pamoja Alma 13:28–29.

1 Wakorintho 11:23–29

Wakati wa Sakramenti, naweza kufikiri kuhusu jinsi ninavyomfuata Mwokozi.

Sakramenti ina umuhimu wa ziada kwa watoto ambao wamebatizwa. Wasaidie kuona ibada hii takatifu kama nafasi ya “kujihoji” wenyewe na kufanya upya maagano yao kwa Mwokozi (1 Wakorintho 11:28).

Shughuli Yamkini

  • Muombe mtoto asome 1 Wakorintho 11:28. Ina maana gani “kujihoji” wenyewe kabla ya kupokea sakramenti? Waombe watoto kufikiria juu ya watu wengine ambao wanapima vitu, kama madaktari, wapelelezi, au wanasayansi (kwa mfano, madaktari hupima miili yetu kwa ajili ya vidonda au magonjwa ambayo yanahitaji kuponywa). Je, kazi zao zinatufundisha nini sisi kuhusu jinsi tunavyotakiwa kujipima wenyewe wakati tunapopokea sakramenti?

  • Waombe watoto kutengeneza orodha ya vitu wanavyoweza kufikiria juu yake wakati wanapopokea sakramenti. Waalike watumie orodha zao kama ukumbusho wa kujihoji wenyewe wakati wa sakramenti.

1 Wakorintho 12:4, 7–12,31; 13:1–8

Ninazo karama za kiroho.

Paulo alifundisha kwamba karama za kiroho “zinatolewa kwa kila mtu” (1 Wakorintho 12:7). Kanuni hii inaweza kuwasaidia watoto kujenga hisia za kujithamini, hususani wanapotumia karama zao kubariki wengine.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kuandika ubaoni karama za kiroho wanazopata katika 1 Wakorintho 12:7–11; 13:2. Waalike watafute karama yoyote ya nyongeza iliyotajwa katika Moroni 10:8–18 na Mafundisho na Maagano 46:13-26. Shiriki pamoja nao karama za kiroho za nyongeza zilizotajwa na Mzee Marvin J. Ashton: Karama ya kuomba; karama ya kusikiliza; … karama ya kuepuka mabishano; … karama ya kutafuta kile kilicho cha haki; karama ya kutohukumu; karama ya kumtegemea Mungu kwa ajili ya mwongozo; … karama ya kujali wengine; … karama ya kutoa sala; karama ya kutoa ushuhuda wenye nguvu” (“Kuna Karama Nyingi, Ensign, Nov. 1987, 20) Waalike watoto wazungumze kuhusu karama za kiroho wanazoziona katika wao kwa wao.

  • Kabla ya darasa, waulize wazazi kuhusu karama wanazoziona kwa watoto wao, au fikiria kuhusu karama zao wewe mwenyewe. Waambie watoto kuhusu karama hizi, na waombe kukisia mtoto yupi ana karama hiyo. Waombe watoto kuandika njia moja watakayotumia karama zao kumbariki mtu fulani wiki hii.

  • Shiriki hali tofauti ambazo watu wanaweza kutumia karama ya kiroho kutoka 1 Wakorintho 12:7–10. Waalike watoto kutambua karama za kiroho ambazo zinaweza kutumika katika kila hali.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki karama zao za kiroho pamoja na familia zao na wawaulize wanafamilia karama zao ni zipi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa Mialiko ambayo Inaheshimu haki ya Kujiamulia Unapowaalika watoto kufanya juu ya kile wanachojifunza, fikiria njia ya kuheshimu haki yao ya kujiamulia. Kuliko kutoa mwaliko maalulmu, fikiria kuwataka wawazie njia zao wenyewe za kutumia kile walichojifunza.

Chapisha