“Septemba 23–29. Wagalatia: ‘Enendeni katika Roho’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Septemba 23–29. Wagalatia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Septemba 23–29
Wagalatia
“Enendeni katika Roho”
Unaposoma Wagalatia, je, ni misukumo gani unayokuwa nayo kuhusu kile watoto katika darasa lako wanahitaji kujifunza?
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Wape watoto dakika chache kuchora kitu fulani walichojifunza kutoka majadiliano ya hivi karibuni ya injili nyumbani au Kanisani. Kusanya michoro, na waache watoto wajaribu kukisia kile kinachowakilishwa na kila mchoro.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Roho Mtakatifu hunisaidia kujisikia mwenye upendo, furaha, na amani.
Watoto wadogo wanaweza kutambua matunda ya Roho. Hii itawatayarisha kutafuta ushawishi wa Roho Mtakatifu maisha yao yote.
Shughuli Yamkini
-
Tundika au onyesha picha kadhaa za aina ya matunda, na waalike watoto kuelezea kila tunda lina ladha gani. Eleza kwamba jinsi matunda yalivyo na ladha tofauti, tunaweza kumsikia Roho Mtakatifu katika njia tofauti kama vile upendo na amani. Waombe waelezee jinsi wao wanavyomhisi Roho Mtakatifu.
-
Soma Wagalatia 5:22–23 pamoja na watoto, na fafanua maneno wasiyoweza kuwa na uzoefu nayo. Mwalike kila mtoto kuchagua tunda la Roho lililotajwa katika aya hizi na kusimulia kuhusu muda alipopata uzoefu wa tunda la Roho. Waalike wanafunzi kuchora picha za kawaida za uzoefu wao.
Yesu Kristo ananitaka niwasaidie wale wenye shida.
Maelekezo katika Wagalatia 6:2 yanafanana na mafundisho ya Alma katika Mosia 18:8 kwa watu waliokuwa karibu kubatizwa. Chukua nafasi hii kuwasaidia watoto kujitayarisha kwa ajili ya maagano ya ubatizo.
Shughuli Yamkini
-
Onyesha picha ya mtoto akibatizwa (kama vile Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 104). Waulize watoto, mtoto anafanya nini. Eleza kwamba tunapobatizwa, tunafanya maagano, au ahadi. Soma Wagalatia 6:2 au Mosia 18:8 kuwasaidia watoto kujifunza mojawapo ya vitu tulivyoahidi kufanya: kubebeana mizigo. Waalike watoto kuchora picha za njia wanazoweza kuwasaidia wengine wanaobeba mizigo.
-
Wasomee watoto kirai hiki kutoka Wagalatia 6:2: “Mchukuliane mizigo.” Ili kuelezea hii inamaanisha nini, mpe mmojawapo wa watoto kitu fulani kizito akibebe. Kisha omba mtu ajitolee kumsaidia mtoto kubeba mzigo huo. Eleza kwa watoto kwamba vitu vingi vinaweza kuwa kama mzigo, kama kuwa mgonjwa au kuhuzunika au kuwa mpweke. Tufanye nini kumsaidia mtu na aina hii ya mzigo?
Matendo yetu, yote mazuri na mabaya, yana matokeo yake.
Ni muhimu kwa watoto kuelewa kwamba chaguzi zetu zina matokeo. Unaweza kutumia Wagalatia 6:7–9 kuonyesha kielelezo cha ukweli huu.
Shughuli Yamkini
-
Onyesha mbegu na mboga. Wasomee watoto Wagalatia 6:7–9. Waalike watoto wajifanye wanapanda mbegu wanaposikia neno “panda.” Waombe wajifanye wanachuna mboga kutoka kwenye mmea wanaposikia neno “vuna.”
-
Waonyeshe watoto mboga aina kadhaa, na wasaidie kupata mbegu katika kila mboga. Weka mbegu katika chombo, na waache watoto wachukue zamu kuchagua moja na kusimulia ni mboga gani itaota kama wanaipanda. Wasaidie waone kwamba kama mbegu tunazopanda zinaamua mboga tunayopata, maamuzi tunayofanya yanaamua matokeo na baraka hatimaye tunazopata.
-
Fanya msitari sakafuni kwa utepe. Weka sura yenye furaha na sura ya huzuni mkabala na miisho ya mstari. Mwalike mtoto kusimama katikati ya mstari, na mwache mtoto mwingine ataje chaguzi ambazo zitaelekeza kwenye furaha au huzuni (unaweza kutaka kutoa mifano michache). Kwa kila uchaguzi, muombe mtoto aliyepo katikati apige hatua kuelekea upande wa furaha au upande wa huzuni. Rudia shughuli hii mara kadhaa, na waache watoto wengine wachukue zamu kusimama juu ya utepe.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Yesu Kristo anatuweka huru.
Baadhi ya watu wanafikiria injili ya Yesu Kristo inawekea kuzuizi uhuru wao. Tafakari jinsi utakavyowasaidia watoto kuona kwamba kwa kweli inatuletea uhuru kutokana na dhambi na kifo.
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto wasome Mathayo 5:1. Katika njia zipi Yesu Kristo anatufanya huru ili tuweze kurudi kwa Baba wa Mbinguni? Onyesha picha za mateso ya Yesu katika Gethsemane na Ufufuko Wake kuwasaidia watoto kuelewa jinsi Yesu alivyotuweka huru kutokana na dhambi na kifo (ona Kitabu cha sanaa za Injili, na. 56, 59).
-
Imbeni pamoja na rejea maneno ya wimbo kuhusu Mwokozi, kama vile “Najua Mkombozi Wangu Anasihi” (Nyimbo, na. 136). Waombe watoto kutafuta maneno katika wimbo huu ambayo yanaelezea njia ambazo Yesu Kristo anaweza kutuweka huru kutokana na utumwa wa kiroho.
Kama “nitaenenda katika Roho,” naweza kufurahia “tunda la Roho.”
Utawasaidia vipi watoto kutambua wakati wanapomhisi Roho Mtakatifu?
Shughuli Yamkini
-
Mpe kila mtoto kipande cha karatasi kilichoumbwa kama tunda, na waombe watoto kutafuta “tunda la Roho” lililoorodheshwa katika Wagalatia 5:22–23. Waalike kuandika mojawapo ya matunda upande mmoja wa karatasi yao na neno ambalo lina maana ya kinyume chake upande mwingine. (Wasaidie kuelewa maneno ambayo hawana uzoefu nayo.) Waalike washiriki matunda yao na darasa.
-
Waalike watoto wasome kuhusu tunda la Roho katika Wagalatia 5:22–23 na andika kuhusu au chora picha ya wakati Roho Mtakatifu alipowasaidia kuona mojawapo ya matunda hayo. Waombe wasimulie hadithi zao au picha na mtu mwingine katika darasa. Je, ni kwa nini tunda ni njia nzuri ya kutusaidia kuelewa jinsi Roho anavyotushawishi?
Matendo yetu, yote mazuri na mabaya, yana matokeo yake.
Wasaidie watoto kuelewa kwamba matokeo ya tabia zetu wakati mwingine yanakuja mara moja na wakati mwingine yanaweza kuja “katika kipindi kijacho” (aya 9).
Shughuli Yamkini
-
Someni pamoja Wagalatia 6:7–9. Waalike watoto kuchora picha ya kawaida ambapo mtu fulani anapanda mbegu ya tunda moja na anavuna tunda tofauti. Je, ni kwa nini hii itakuwa haiwezekani? Je, ni kwa jinsi gani kufanya chaguzi zisizo sahihi na kupata uzoefu wa matokeo chanya haiwezekani tu?
-
Kama darasa, fanya mzingile kama ule kwenye ukurasa wa shughuli wa wiki hii. Waalike watoto kufikiria maneno mengine kuliko hayo katika mzingile ambayo yanawakilisha hisia nzuri kutoka kwa Roho Mtakatifu au chaguzi mbaya ambazo zinaweza kumfukuza mbali. Jadilini matokeo ya chaguzi walizozifikiria.
-
Waalike watoto kuorodhesha baadhi ya baraka wanazotegemea kuzipata kutoka kwa Baba wa Mbinguni. Wasaidie kufikiri juu ya “mbegu” wao lazima wapande ili “wavune” baraka hizi.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kutazamia matokeo mazuri, au “tunda”, ambalo linakuja kwa sababu ya maamuzi mazuri wanayofanya wiki hii. Waambie kwamba wiki ijayo wanaweza kuelezea uzoefu wao.