Njoo, Unifuate
Septemba 30–Oktoba 13. Waefeso: ‘Kwa Kusudi la Kuwakamilisha Watakatifu’


“Septemba 30–Oktoba 13. Waefeso: ‘Kwa Kusudi la Kuwakamilisha Watakatifu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Septemba 30–Oktoba 13. Waefeso,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
familia ikitazama picha

Septemba 30–Oktoba 13

Waefeso

“Kwa Kusudi la Kuwakamilisha Watakatifu”

Unapojifunza waraka kwa Waefeso, fikiria kuhusu ni kanuni gani unaweza kusisitiza ili kuwabariki watoto unaowafundisha. Andika mawazo yoyote ambayo yanakuja kwenye fikra unaposoma.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kusimama kwenye mstari. Muombe mtu wa kwanza mstarini kuelezea kitu alichojifunza hivi karibuni wakati wa kujifunza maandiko katika familia, katika darasa la msingi, au po pote pale. Muombe mtoto anaefuatia msitarini kurudia kile mtoto aliyepita alichoelezea na kisha kuongeza kitu alichojifunza yeye. Rudia hivi mpaka kila mtoto amepata nafasi ya kushiriki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Waefeso 2:19

Waumini wa Kanisa wanapaswa kuwa marafiki na “wenyeji.”

Je, watoto katika darasa lako wapo zaidi kama “wageni” au “wenyeji” kwa kila mmoja na pamoja na waumini wengine wa kata? Wasaidie kuelewa kwamba ingawa tuna tofauti, Mwokozi anatusaidia kuwa wamoja na kupendana.

Shughuli Yamkini

  • Weka picha ya Mwokozi katikati ya darasa. Waalike watoto kusimama sehemu tofauti za chumba kuwakilisha “wageni” au “wageni kutoka nje ya nchi.” Unaposoma Waefeso 2:19, waalike kwenda mbele kuelekea picha ya Kristo ilipo mpaka watakaposimama wakiwa wamekaribiana. Waambie kwamba tunapokuja karibu zaidi kwa Mwokozi, tunaweza kuwa tumeunganika na wengine kama marafiki na “wenyeji.”

  • Tafuta picha za watoto kutoka sehemu tofauti za ulimwengu na zifiche kuzunguka chumba. Weka picha ya Mwokozi mbele ya chumba. Alika darasa lako kuwa katika majozi kama wamisionari na wafanye zamu kutafuta picha ya “mgeni” na kuiweka karibu na picha ya Mwokozi. Wasaidie kuelewa kwamba watu wanapobatizwa, wanakuwa sehemu ya familia yetu ya Kanisa, au “watu wa nyumbani mwake Mungu.” Je, tunawezaje kumsaidia mtu aliye mgeni ajisikie anakaribishwa?

Waefeso 6:1–3

Baba wa Mbinguni ananitaka niwatii wazazi wangu.

Unaposoma Waefeso 6:1–3, fikiria njia unazoweza kuwasaidia watoto kuelewa kwa nini ni muhimu kuwatii wazazi wao.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee Waefeso 6:1, au msaidie mmojawapo ya watoto kuisoma. Waambie waigize wakati ambapo waliwatii wazazi wao. Je, kingetokea nini kama wasingewatii?

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu utii, kama vile “Quickly I’ll Obey” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 197). Simama baada ya mstari wa kwanza, na muombe mtoto kutaja kitu ambacho mzazi anamtaka yeye kufanya; kisha malizia wimbo. Rudia mara kadhaa ili watoto wengine wapate zamu.

  • Elezea matukio ambayo wewe ulitii wazazi wako na ulibarikiwa. Au shiriki hadithi kuhusu Chloe kutoka mazungumzo ya Dada Carole M. Stephen “Kama Wanipenda, Shika Amri Zangu” (Ensign au Liahona, Nov. 2015, 118–20) Au onyesha video “Going to Grandma’s” (LDS.org).

Waefeso 6:10–18

Vazi la kivita la Mungu linaweza kunilinda mimi.

Je, utawasaidiaje watoto kuelewa kwamba kufanya mambo ya haki ni kama kuvaa vazi la kivita?

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya mtu aliyevaa vazi la kivita, kama vile yule aliye katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii au muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia. Unapofanya muhtasari Waefeso 6:10–18, waonyeshe watoto jinsi vipande tofauti vya vazi la vita vinavyolinda sehemu tofauti za mwili. (Ona “Silaha Zote za Mungu “ Friend, Juni 2016, 24–25)

  • Lete vitu kadha darasani ambavyo vinaweza kuwakilisha vipande vya vazi la vita lililotajwa katika Waefeso 6:14–17 (kwa mfano, kofia au aproni), au tengeneza vipande vya kawaida vya vazi la kivita kutokana na karatasi. Acha watoto wachuke zamu kulivaa “vazi la vita.” Jadilini inamaanisha nini kulindwa kutokana na uovu na jinsi ya kuvaa kila kipande cha vazi la vita kunaweza kuwalinda wao. Tunavaaje vazi la kivita la Mungu? (Kwa mfano, kwa kujifunza maandiko, kuhudumia wengine, kusali, kutii, na kadhalika).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Waefeso 2:13–19

Sisi ni watu wenyeji wa nyumbani mwake Mungu.

Watoto wanaimarishwa wanapokuwa na marafiki wazuri katika injili. Unawezaje kuwasaidia kujenga urafiki mzuri zaidi kati yao?

Picha
Shughuli ya Msingi

Sisi ni “wenyeji” pamoja na Watakatifu wa Mungu.

Shughuli Yamkini

  • Someni Waefeso 2:19 pamoja, na mjadiliane inamaanisha nini kuwa mgeni au mgeni kutoka nje ya inchi. Elezea tukio ambalo wewe ulijiona kama mgeni au mgeni kutoka nje ya nchi na mtu fulani akakusaidia kujisikia umekaribishwa na kukubalika. Waalike watoto kushiriki uzoefu kama huo. Tunaweza kufanya nini ili tuwe “wenyeji” badala ya kuwa wageni? Je, kuna watoto katika darasa lako wasiohudhuria kila mara, labda kwa sababu wanajiona kama wageni? Wasaidie watoto kuunda mpango wa kuwasaidia hao washiriki kujisikia wamekaribishwa na wanapendwa.

  • Kuwasaidia watoto unaowafundisha kukaribiana, andika maswali machache ubaoni ambayo yatawafanya mara moja washiriki kitu fulani kuhusu wao wenyewe, kama vile Lini uliweza kuona sala ikijibiwa? au kitu gani unachopenda kufanya na familia yako? Wagawe watoto katika majozi, na waombe kuulizana maswali. Walijifunza nini kuhusu wao kwa wao?

Waefeso 6:1–3

Baba wa Mbinguni ananitaka niwatii na kuwaheshimu wazazi wangu.

Fikiria kuhusu njia unazoweza kuwasaidia watoto kuelewa kwa nini ni muhimu kuwatii wazazi wao.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wasome Waefeso 6:1–3 binafsi na kutambua virai ambavyo vinawagusa. Waalike kushiriki virai hivi na kwa nini wanahisi virai hivi ni muhimu.

  • Waalike watoto kushiriki mifano ya watu katika maandiko waliowatii na kuwaheshimu wazazi wao, kama vile Mwokozi (ona Luka 2:42–52), Ruth (ona Ruth 1), au Nefi (ona 1 Nefi 3:1–8). Kwa nini ni muhimu kuwatii na kuwaheshimu wazazi wetu?

  • Mpe kila mtoto kipande cha karatasi chenye neno heshimu juu yake. Jadili neno hilo lina maana gani. Waalike watoto kuandika au kuchora kwenye karatasi zao kitu wanachoweza kufanya ili kuonyesha kwamba wanawaheshimu wazazi wao.

Waefeso 6:10–18

Vazi la vita la Mungu linaweza kunilinda dhidi ya uovu.

Unaposoma Waefeso 6:10–18, fikiria baadhi ya hatari za kiroho ambazo watoto wanakumbana nazo na jinsi unavyoweza kusaidia kuwaimarisha watoto dhidi ya hatari hizo.

Shughuli Yamkini

  • Wakati mtoto mmoja anasoma Waefeso 6:10–18, muombe mtoto mwingine kuorodhesha au kuchora ubaoni vipande vya vazi la vita vilivyotajwa. Kwa nini vazi la vita ni muhimu katika vita? Tunawezaje kuvaa vazi la vita la kiroho kila siku?

  • Mpangie kila mtoto achore na kuweka alama kipande cha vazi la vita lililosimuliwa katika Waefeso 6:14–17. Je, ni kwa jinsi gani vipande hivi vya vazi la vita vitatulinda dhidi ya uovu? Bwana anawaahidi nini hao wanaovaa vazi la vita la Mungu? (Ona Waefeso 6:13). Inamaanisha nini “kustahimili katika siku ya uovu”?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kumtafuta mtu fulani wiki hii anayeweza kujihisi kama ni mgeni. Wape changamoto ya kufanya kitu fulani ili kumsaidia mtu huyo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto wadogo kujifunza kutoka kwenye maandiko. Ili kuwasaidia watoto wadogo kujifunza kutoka kwenye maandiko, zingatia katika mstari mmoja wa maandiko au hata maneno muhimu tu. Unaweza kuwaalika watoto kusimama wakati wanaposikia neno maalumu au kirai. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25–26.)

Chapisha