“Nyenzo za Ziada za Kufundisha Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Nyenzo za Ziada za Kufundisha Watoto” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Nyenzo za Ziada za Kufundisha Watoto
Nyenzo hizi zote zinaweza kupatikana katika LDS.org na katika Gospel Library app.
Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia
Unaweza kutohoa shughuli zozote kutoka kwenye nyenzo hizi kwa kutumia katika darasa lako la Msingi. Hata kama wazazi wanatumia shughuli hizi na watoto wao nyumbani, marudio yanaweza kuwa njia muhimu kuwasaidia watoto kujifunza. Watoto wanaweza kuhitaji kukuambia jinsi walivyofanya shughuli pamoja na familia zao na kile walichojifunza.
Tazama Watoto Wako: Kitabu cha Kiada cha Chekechea
Mada nyingi zinazofundishwa katika kitabu cha kiada cha chekechea zinafanana na zile utafundishia katika Msingi. Hususani kama utafundisha watoto wadogo, fikiria kuangalia katika kitabu cha kiada cha chekechea kwa nyimbo za ziada, hadithi, shughuli, na ufundi.
Magazeti ya Friend na Liahona
Magazeti ya Friend na Liahona hutoa hadithi na shughuli ambazo zinaweza kuongezea kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.
Nyimbo na Kitabu cha Nyimbo za Watoto
Muziki mtakatifu hualika Roho na kufundisha mafundisho katika njia ya kukumbukwa. Kwa nyongeza katika matoleo ya uchapishaji wa Nyimbo na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi ya sauti na video za nyimbo nyingi na nyimbo za watoto katika music.lds.org au katika LDS Music App.
Hadithi za Agano Jipya
Hadithi za Agano Jipya (2005) zinaweza kuwasaidia watoto kujifunza mafundisho na hadithi zilizopatikana katika Agano Jipya. Unaweza pia kuzipata video za hadithi hizi katika medialibrary.lds.org.
Maktaba ya Vyombo vya Habari
Sanaa, video, na vyombo vya habari vingine vinaweza kukusaidia wewe na watoto kutazama mafundisho na hadithi zinazopatikana katika Agano Jipya. Tembelea medialibrary.lds.org kuvinjari orodha ya Kanisa ya nyenzo za vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na mfululizo wa video za Biblia, ambao unaonyesha matukio katika Agano Jipya.
Sanaa ya Injili
Sanaa inaweza kuwasaidia watoto kutafakari mafundisho na hadithi zinazopatikana katika Agano Jipya. Picha nyingi ambazo unaweza kutumia katika darasa zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili na katika medialibrary.lds.org.
Misaada ya Somo kwa Kufundisha Watoto
Katika lds.org/children/resources unaweza kupata orodha ya makala za gazeti, shughuli, na vyombo vya habari juu ya mada mbalimbali za injili.
Kweli kwa Imani
Ikiwa unahitaji msaada wa ziada kuelewa kanuni za msingi utakazowafundisha watoto, fikiria kuangalia katika Kweli kwa Imani (2004). Kitabu hiki kinatoa maelezo rahisi ya mada za injili, yaliyoorodheshwa kwa utaratibu wa alfabeti.
Kufundisha katika Njia ya Mwokozi
Nyenzo hii inaweza kukusaidia kujifunza na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo. Kanuni hizi zinajadiliwa na hufanyika katika mikutano ya baraza la walimu