“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019) (2019)
“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi
Kuandaa Kufundisha katika Msingi
Nyumbani panapaswa kuwa kitovu cha kujifunza injili. Hii ni kweli kwako na kwa watoto unaowafundisha. Unapojiandaa kufundisha, anza kwa kuwa na uzoefu wako mwenyewe katika maandiko. Maandalizi yako muhimu zaidi yatatokea wakati unatafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu.
Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia pia ni sehemu muhimu ya maandalizi yako. Itakusaidia kupata ufahamu zaidi wa kanuni za mafundisho zinazopatikana katika maandiko.
Wakati wa maandalizi yako, mawazo na misukumo itakujia kuhusu watoto unaowafundisha. Utapokea umaizi juu ya jinsi kanuni katika maandiko zitakavyobariki maisha yao. Utaongozwa ili uwahamasishe kugundua kanuni hizi wanapojifunza kutoka katika maandiko wao wenyewe na pamoja na familia zao. Kumbuka kuwa na uangalifu kwa watoto ambao hali zao za familia haziwezi kumudu kujifunza maandiko kama familia kila mara.
Mawazo ya Kufundisha
Unapojiandaa kufundisha, unaweza kupata mwongozo wa ziada kwa kuchunguza miuhtasari ya nyenzo hizi. Usifikirie juu ya mawazo haya kama maelekezo ya hatua kwa hatua lakini badala yake ni kama mapendekezo ya kuchochea mwongozo wako mwenyewe. Unawajua watoto hawa, na Bwana anawajua pia—ikiwa ni pamoja na kile wanachohitaji na kile wanachoweza kuelewa. Atakuongoza kwa njia bora za kufundisha na kuwabariki watoto.
Una nyenzo zingine nyingi zinazopatikana wakati unapojiandaa, ikiwa ni pamoja na mawazo katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na magazeti ya Kanisa. Kwa habari zaidi kuhusu nyenzo hizi na zingine, ona “Nyenzo za Ziada za Kufundisha Watoto.”
Vitu Vingine vya Kukumbuka
-
Wazazi wana jukumu kuu la kufundisha watoto wao. Kama mwalimu, una jukumu muhimu la kuhimili, kuhimiza, na kujenga juu ya kujifunza injili nyumbani. Kuwa na usikivu kwa watoto ambao wazazi wao hawafundishi injili nyumbani mwao. Jumuisha watoto wote katika majadiliano ya injili bila kujali mazingira yao ya nyumbani.
-
Kurudiarudia ni vizuri. Watoto hujifunza kweli za injili kwa ufanisi zaidi wakati ukweli huu unapofundishwa kupitia kwa shughuli mbalimbali. Ikiwa unaona kuwa shughuli ya kujifunza inafaa kwa watoto, fikiria kuirudia, hasa ikiwa unafundisha watoto wadogo. Unaweza pia kupitia shughuli kutoka kwa somo la awali.
-
Baba wa Mbinguni anakutaka wewe ufanikiwe kama mwalimu. Ametoa nyenzo nyingi kukusaidia ufanikiwe, ikiwa ni pamoja na mikutano ya baraza la walimu. Katika mikutano hii unaweza kushauriana na walimu wengine kuhusu changamoto zozote mnazoweza kuwa mnakabiliana nazo. Unaweza pia kujadili na kutekeleza kanuni za kufundisha kama Kristo.
-
Ikiwa unafundisha watoto wadogo na unahitaji msaada wa ziada, tazama “Kukidhi Mahitaji ya Watoto Wadogo” katika hii nyenzo.
-
Nyenzo hii inajumuisha muhtasari kwa ajili ya kila wiki ya mwaka isipokuwa kwa Jumapili mbili wakati mkutano mkuu unafanyika. Siku ya Jumapili wakati Msingi haufanyiki kwa sababu ya mkutano wa kigingi au sababu nyingine yoyote, familia zinaweza kuendelea kusoma Agano Jipya nyumbani kulingana na ratiba iliyotajwa. Ili kuweka darasa lako la Msingi katika ratiba, unaweza kuchagua kuruka somo au kuchanganya masomo mawili. Ili kuepuka kuchanganyikiwa, Marais wa Msingi wanaweza kuwashauri walimu kuhusu marekebisho haya mapema.