“Wewe ni Mwalimu wa Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Wewe ni Mwalimu wa Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Wewe ni Mwalimu wa Watoto
Umeitwa na Mungu kufundisha watoto Wake katika njia ya Mwokozi. Umesimikwa katika wito huu kwa mamlaka ya ukuhani Wake mtakatifu. Hata kama wewe si mwalimu mwenye uzoefu, unapoishi kwa usahili, kuomba kila siku, na kujifunza maandiko, Mungu atakupa ushawishi na uwezo wa Roho Mtakatifu (ona 2 Nefi 33:1).
Wale waliowekwa chini ya uangalizi wako ni watoto wa Baba wa mbinguni, na Yeye anajua kile wanachohitaji na jinsi ya kuwafikia. Kupitia kwa Roho Mtakatifu, Mungu atakuongoza wakati wa maandalizi yako na wakati unapofundisha. Atakufunulia kile unachopaswa kusema na unachopaswa kufanya.
Katika nyanja zote za maisha yao, watoto hawa wa thamani wanaendelea kupata habari, kutengeneza na kusafisha mawazo yao, na kufanya na kushiriki uvumbuzi. Hii ni kweli hasa kwa injili, kwani watoto wapo tayari na wana nia ya kujifunza ukweli wake rahisi. Imani yao katika mambo ya kiroho ni imara na safi, na wanaona kila wakati kama wakati wa kujifunza. Wanatenda kwa hiari juu ya yale waliyojifunza, hata kama ufahamu wao bado haujakamilika. Hivi ndivyo jinsi sote tunavyopaswa kupokea injili. Kama Mwokozi Alivyofundisha, “Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe” (Luka 18:17).
Wito wa kufundisha watoto ni aminisho takatifu. Ni kawaida kuhisi kuzidiwa nyakati fulani. Lakini kumbuka kwamba Baba yako wa Mbinguni alikuita, na Yeye hatakuacha kamwe Hii ni kazi ya Bwana, na unapotumikia “kwa moyo wako wote, uwezo, akili na nguvu” (M&M 4:2), Atakuza uwezo wako, zawadi, na vipaji, na huduma yako itabariki maisha ya watoto unaowafundisha.