“Julai 17–23. Matendo ya Mitume 10–15: ‘ Neno la Mungu Likakua na Kuongezeka’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)
“Julai 17–23. Matendo ya Mitume 10–15,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023
Julai 17–23
Matendo ya Mitume 10–15.
“Neno la Mungu Likakua na Kuongezeka”
Soma Matendo ya Mitume 10–15 kwa sala, ukifikiria kuhusu watoto wa darasani mwako. Unapata nini katika sura hizi ambacho unahisi mwongozo wa kukifundisha kwa watoto?
Alika Kushiriki
Ili kuwasaidia watoto kushiriki kile wanachojifunza na kukipitia, ungeweza kuwataka kushiriki vitu wanavyofanya ili kuonyesha kwamba wanamwamini Yesu Kristo.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Baba wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote.
Ukweli wa kimsingi kwamba hata watoto wadogo wanaweza kuelewa ni kwamba kila mmoja ni mtoto wa Mungu na kwamba Yeye anawapenda watoto Wake wote.
Shughuli Yamkini
-
Onyesha picha Kristo na Watoto kutoka Ulimwenguni kote (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.116) unaposoma Matendo ya Mitume 10:34–35. Elezea kwamba katika wakati wa Petro watu waliamini kwamba baraka za injili hazikuwa kwa ajili ya kila mtu. Lakini Petro alijifunza kwamba Mungu anawapenda watoto Wake wote na anataka wote wajifunze injili.
-
Waalike wanafunzi kuchora picha ya wao wenyewe. Wanaposhiriki picha zao, zungumza kuhusu kitu unachokipenda kuhusu kila mtoto. Shiriki ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni anampenda kila mmoja wao na watoto Wake wote, bila kujali wanaonekana vipi au wapi wanakotoka.
-
Imba na watoto wimbo kuhusu kuwapenda wengine, kama vile “I’ll Walk with You” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 140–41). Waalike watoto kushiriki njia zingine wanazoweza kuonyesha upendo kwa kila mmoja, kama Yesu alivyofanya.
-
Onyesha kidole kila mtoto mmoja baada ya mwingine na sema, “Baba wa Mbinguni anampenda [jina].” Waruhusu watoto wachukue zamu kuonyeshana wao kwa wao na kusema kirai hiki.
Mimi ni Mkristo kwa sababu ninamwamini na kumfuata Yesu Kristo.
Unawezaje kuwasaidia watoto kujifunza maana ya kuwa Mkristo?
Shughuli Yamkini
-
Soma Matendo ya Mitume 11:26 kwa watoto, na waalike kusimama wanaposikia wewe ukisema neno Mkristo. Waulize kile wao wanafikiri inamaanisha kuwa Mkristo. Eleza kwamba mtu anayeamini katika na kumfuata Yesu Kristo anaitwa Mkristo, kwa hiyo sisi ni Wakristo.
-
Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu kumfuata Yesu Kristo, kama vile “The Church of Jesus Christ” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77). Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha kwamba sisi ni wafuasi wa Yesu Kristo na ni wa Kanisa Lake? Wasaidie watoto kufikiria juu ya mambo wanayoweza kufanya ili kumfuata Yesu nyumbani, shuleni, na mahali pengine.
Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala.
Hadithi ya malaika akimfungua Petro kutoka gerezani inafundisha kwa nguvu kwamba Baba wa Mbinguni anajibu sala.
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto waigize hadithi ya Petro akiwekwa huru kutoka gerezani katika Matendo ya Mitume 12:1–17 unapofanya muhtasari wa hadithi hii. Je, ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni alijibu sala za wale waliokuwa wanasali kwa ajili ya Petro?
-
Imba wimbo kuhusu sala—kama vile, “We Bow Our Heads” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 25)—na pendekeza matendo yaambatane na maneno ambayo yanaweza kuwasaidia watoto kujifunza jinsi ya kusali. Waalike watoto kushiriki mifano ya vitu wanavyoweza kumshukuru Baba wa Mbinguni na kumwomba Yeye katika sala.
-
Onyesha picha za watu wakisali (ona, kwa mfano, Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.111–12) unaposhiriki uzoefu wako wa wakati Baba wa Mbinguni alipojibu sala zako.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Matendo ya Mitume 10:34–35; 15:6–11
“Mungu hana upendeleo.”
Watoto unaowafundisha wanahitaji kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote, bila kujali wanaonekanaje, wanatoka wapi, au ni chaguzi gani wanafanya.
Shughuli Yamkini
-
Waulize watoto kama wanaweza kusema mtu fulani yuko hivi kwa kuwaangalia tu au kubahatisha wapi wanakotoka. Kulingana na Matendo ya Mitume 10:35, ni kwa jinsi gani Mungu anaamua kama mtu fulani “anakubalika kwake”?
-
Soma Matendo ya Mitume 10:34–35; 15:6–11. pamoja na watoto. Eleza kwamba katika wakati wa Petro, Wayahudi waliamini kwamba Mungu hakuwakubali watu ambao hawakuwa Wayahudi (watu hawa waliitwa Wayunani). Lakini Mungu alimfundisha Petro kwamba Mungu anawapenda watoto Wake wote, Wayahudi na Wayunani. Imbeni pamoja “I Am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3). Waalike wanafunzi kubadili majina ya kila mmoja wao na maneno kama mie au mimi.
-
Waalike watoto kushiriki kitu cha kipekee kuhusu mtu mwingine katika darasa. Eleza kwamba maelezo “Mungu hana upendeleo” humaanisha kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote, na kwa sababu anawapenda, Yeye anataka watoto Wake wote kuisikia injili.
Mkristo ni mtu anayeamini na kumfuata Yesu Kristo.
Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kwamba maneno na matendo yao yanaonyesha kwamba wao ni Wakristo?
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto wasome Matendo ya Mitume11:26; 3 Nefi 27:3–8; na Mafundisho na Maagano 115:4. Andika Mkristo ubaoni na pigia mstari sehemu ambayo inasema “Kristo.” Waombe watoto kuelezea wanafikiri inamaanisha nini kuwa Mkristo.
-
Waombe watoto kutaja makundi tofauti ambayo wao wamo, kama vile familia zao au taifa. Waalike kushiriki sababu za kwa nini wao wanashukuru kuwa Wakristo na kuwa wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwaonyesha wengine kuwa sisi ni Wakristo?
-
Onyesha vitu kadhaa au picha ambazo zinawakilisha kweli za kipekee kwa Kanisa la Yesu Kristo, kama vile picha ya urejesho wa ukuhani (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 93–94). Muombe mtoto achague mojawapo ya vitu au picha na aeleze jinsi ilivyo baraka katika Kanisa letu. Eleza kwamba wakati Wakristo ulimwenguni kote wako kwenye Makanisa tofauti, sisi tupo katika Kanisa lile lile ambalo Yesu Kristo alilianzisha duniani.
-
Onyesha video “True Christianity” (ChurchofJesusChrist.org). Waalike watoto kuchora vitu wanavyoweza kufanya ili kuwa Wakristo wa kweli.
Wakati ninaposali kwa imani, Baba wa Mbinguni atajibu.
Tafakari nyakati ambapo Baba wa Mbinguni amejibu sala zako. Unawezaje kutumia uzoefu huu kuwafundisha watoto kwamba Baba wa Mbinguni atasikia na kujibu sala zao katika njia yake mwenyewe na kwa muda Wake?
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto waigize hadithi ya malaika akimwachilia huru Petro kutoka gerezani wakati mtoto mwingine anasoma hadithi katika Matendo ya Mitume 12:1–17.
-
Waulize watoto wanafikiri inamaanisha nini “likamwomba Mungu kwa juhudi” (Matendo ya Mitume 12:5). Je, ni kwa jinsi gani sala za watu zilijibiwa? Waalike watoto kushiriki uzoefu wao ambapo Baba wa Mbinguni alijibu sala binafsi au ya familia yao. Ungeweza pia kushiriki uzoefu ambapo Yeye alijibu sala zako. Unaweza kujumuisha matukio ambapo majibu yalikuja katika njia usiyotarajia. Shuhudia kwamba Mungu anatupenda, na atajibu sala zetu katika njia na ratiba ambayo ni mzuri sana kwetu sisi.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kufanya kitu ambacho kitawakumbusha wao juu ya kitu walichojifunza leo, kama vile kuwakumbusha kusali.