Agano Jipya 2023
Juni 26–Julai 2. Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21: “Amefufuka”


“Juni 26–Julai 2. Mathayo 28; Marko 16: Luka 24; Yohana 20–21: ‘Amefufuka,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Juni 26–Julai 2. Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Yesu Akiongea na Petro ufukweni mwa bahari

Walishe Kondoo Wangu, na Kamille Corry

Juni 26–Julai 2

Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21

“Amefufuka”

Watoto wenye ushuhuda juu ya kweli katika sura hizi wana msingi imara ambamo juu yake wanajenga imani yao. Ni kwa jinsi gani utamwalika Roho ashuhudie juu ya kweli hizi?

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kuona picha kunaweza kusaidia watoto kukumbuka vitu walivyojifunza nyumbani au katika mazingira mengine. Labda unaweza kuonyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. na waombe watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu hadithi iliyoonyeshwa katika picha.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20:1–23

Nitaishi tena baada ya kufa, kama vile Yesu alivyofanya.

Upatanisho wa Yesu Kristo, ikiwa ni pamoja na Ufufuko Wake, ni tukio muhimu zaidi katika historia, na ni msingi wa imani ya Kikristo. Unaposoma kuhusu Ufufuko, tafakari jinsi unavyoweza kusaidia watoto kujenga imani yao katika Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Simulia hadithi juu ya Ufufuko wa Yesu Kristo kwa maneno yako mwenyewe. (Kama inahitajika, tumia “Sura ya 54: Yesu Amefufuka,” katika Hadithi za Agano Jipya, 139–44, au video zinazoambatana katika ChurchofJesusChrist.org.) Elezea kwamba Yesu Alipokufa, Roho Yake iliuacha mwili Wake. Alipofufuka, Roho Yake na mwili Wake viliungana tena. Waombe watoto kuchukua zamu kurudia kukusimulia wewe hadithi hiyo. Waombe watoto kuelezea jinsi ambavyo wangejisikia kama wangelimwona akiwa hai tena.

  • Onyesha video “What Happens after We Die?” (ChurchofJesusChrist.org), na simulia kuhusu mtu fulani unayemjua kuwa amefariki. Toa ushuhuda wako kwamba kila mtu atafufuka siku moja. Waalike watoto kushiriki shuhuda zao.

  • Imbeni wimbo kuhusu Ufufuko wa Mwokozi, kama vile “Did Jesus Really Live Again?” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64). Waombe watoto wafikirie jinsi itakavyokuwa kumuona Yesu. Waache washiriki mawazo yao na darasa.

Yohana 20:24–29

Ninaweza kuwa na imani katika Yesu Kristo ijapokuwa siwezi kumuona.

Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa imani ni nini na jinsi wanavyoweza kuonyesha imani katika Mwokozi.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha Yesu Akimsogelea Tomaso (ChurchofJesusChrist.org) unaposimulia kuhusu tukio la Tomaso katika Yohana 20:24–29. Rudia hiyo hadithi, lakini sasa waombe watoto watoe baadhi ya maelezo.

  • Onyesha sanduku likiwa na kitu ndani ambacho watoto hawawezi kuona, na ukielezee kitu hicho kwa watoto. Waulize kama wanaamini kitu hicho kipo kweli ndani ya sanduku na kwa nini. Kisha waonyeshe kitu hicho, na kueleza kwamba imani ni kusadiki katika vitu tusivyoweza kuviona. Imani muhimu zaidi tunayoweza kuwa nayo ni imani katika Yesu Kristo.

Yesu akionyesha mikono kwa Mitume

Tazameni Mikono Yangu, na Jeff Ward

Yohana 21:15–17

Ninaweza kuonyesha upendo wangu kwa Yesu kwa kuwatumikia wengine.

Ni kwa jinsi kwa gani unaweza kuwashawishi watoto kuwapenda na kuwasaidia wale wanaowazunguka?

Shughuli Yamkini

  • Soma Yohana 21:15–17, au Onyesha video “Feed My Sheep” (ChurchofJesusChrist.org). Wasaidie watoto kuelewa kile Yesu alichotaka Petro afanye: shiriki injili na kumwalika kila mtu kuamini katika Yesu. Mpe kila mtoto kondoo wa karatasi, na waombe kuiandika au kuchora juu yake kitu anachoweza kufanya ili kumsaidia mtu wanayemjua kuja karibu zaidi na Yesu.

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya vitu wanavyofanya katika kuwapenda na kuwatumikia wengine. Tunaweza kufanya nini kingine ili kuonyesha upendo wetu?

  • Andika jina la kila mtoto katika darasa lako katika kipande cha karatasi kilichokatwa katika umbo la kondoo, na kusambaza kondoo hawa kote chumbani. (Jumuisha majina ya watoto wasiohudhuria kila mara.) Waalike watoto kukusanya kondoo kwa kumtafuta mmoja mwenye jina lake juu yake. Wasaidie watoto wafikirie njia ambazo wanaweza kuwafikia wale wasiokuja kanisani.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20:1–23

Kwa sababu Yesu alifufuka, watu wote watafufuliwa.

Ni kawaida kwa watoto kujiuliza kinachotokea baada ya kufa. Fikiria jinsi unavyoweza kufundisha juu ya Ufufuko kwa njia ambayo itajenga imani yao.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kufumba macho yao na kufikiri kwamba wameketi kando ya kaburi la Yesu wakati unaposoma Yohana 20:1–17 au fupisha hadithi ya Ufufuko Wake (ona pia “Sura ya 54: Yesu Amefufuka,” katika Hadithi za Agano Jipya, 139–44, au video inayoambatana katika ChurchofJesusChrist.org). Inamaanisha nini kufufuka? Ingekuwaje kumuona Mwokozi aliyefufuka?

  • Muombe kila mtoto kujifunza uzoefu wa mtu fulani aliyemuona Mwokozi aliyefufuka na shiriki na wana darasa wengine wote kile ambacho mtu huyo alijifunza.

  • Tazama moja au zaidi ya video hizi pamoja na watoto: “Jesus Is Laid in a Tomb,” “Jesus Is Resurrected,” “Christ Appears on the Road to Emmaus,” na “The Risen Lord Appears to the Apostles” (ChurchofJesusChrist.org). Waalike watoto washiriki kwa nini Ufufuko wa Mwokozi ni muhimu kwao.

Yohana 20:24–29

Ninaweza kuwa na imani katika Yesu Kristo licha ya kuwa siwezi kumuona.

Ni kwa jinsi gani utawasaidia watoto kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kusoma Yohana 20: 24–29. (Ona pia video “Blessed Are They That Have Not Seen, and Yet Have Believed” kwenye ChurchofJesusChrist.org.) Je, tunawezaje kujua kwamba Yesu yu hai, hata kama hatuwezi kumwona?

  • Andika kila neno katika kirai “Heri wale wasioona, na wakaamini” katika vipande tofauti vya karatasi. Waalike watoto wayapange maneno katika utaratibu. Waalike wao washiriki uzoefu ambao walihisi upendo wa Mwokozi hata kama hawakuwa wamemuona Yeye.

  • Waalike watoto wachore picha za vitu wanavyoweza kufanya ili kuimarisha imani yao. Waombe kushiriki kile walichochora, na shiriki kile ulichokifanya ili kuimarisha imani yako katika Yesu Kristo.

Yohana 21:1–17

Ninaweza kuonyesha upendo wangu kwa Yesu kwa kulisha kondoo Wake.

Watoto wanaweza kuwashawishi kwa kiasi kikubwa wale wanaowazunguka. Unawezaje kuwatia moyo wao ili kuwaimarisha wengine katika injili?

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Yohana 21:1–17. Unaposoma mstari wa 9–13, waombe watoto kufikiria kuhusu wakati mtu fulani alipotengeneza chakula maalumu kwa ajili yao, na waalike kufikiria njia ambazo Yesu anatulisha sisi kiroho. Unaposoma mstari wa 15–17, badilisha jina la Simioni na weka majina ya watoto badala yake. Kondoo wa Yesu ni wakina nani? Tunawezaje kumsaidia Yeye kuwalisha?

  • Shiriki vitafunwa rahisi na watoto. Wanapokuwa wanakula, waulize ni kwa namna gani kushiriki injili na watu ni kama kuwalisha wao.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii ili kufundisha familia zao kuhusu Ufufuko wa Mwokozi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fuatilia Mialiko ya Kutenda. Unapowaalika watoto kutenda katika kile wanachojifunza, fuatilia katika mwaliko wako wakati wa darasa lijalo. Hii inawaonyesha watoto kuwa unajali kuhusu jinsi gani injili inabariki maisha yao. Wanaposhiriki uzoefu wao, wataimarishwa na watasaidiana kuishi injili.