Agano Jipya 2023
Julai 3–9. Matendo ya Mitume 1–5: “Mtakuwa Mashahidi Wangu”


“Julai 3–9. Matendo ya Mitume 1–5: ‘Nanyi Mtakuwa Mashahidi Wangu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Julai 3–9. Matendo ya Mitume 1-5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
umati wa watu kwenye kingo za mto na wakibatizwa mtoni

Siku ya Pentekoste, na Sidney King

Julai 3–9

Matendo ya Mitume 1–5

“Nanyi Mtakuwa Mashahidi Wangu”

Anza maandalizi yako kwa kusoma Matendo ya Mitume 1–5. Kwa maombi tafuta kuelewa mahitaji ya watoto unaowafundisha Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu unaweza pia kukusaidia.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Andika Mimi ni Nani? ubaoni. Toa kauli kadha kuhusu Petro na waulize watoto kauli hizo zinamhusu nani. Kitu gani kingine wanachokijua kuhusu Petro?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Matendo ya Mitume 1:1–11

Yesu Kristo huongoza Kanisa Lake kupitia manabii na mitume.

Kujifunza kuhusu jinsi Mwokozi alivyoliongoza Kanisa Lake la kale kupitia Mitume kunaweza kuwasaidia watoto kupata shuhuda juu ya manabii na mitume wa leo.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha iliyojaa ukurasa mzima kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waulize watoto kwa nini wanafikiri watu wanaangalia angani. Fanya muhtasari wa maelezo kutoka Matendo ya Mitume 1:1–11. (Ona pia “Sura ya 55: Mitume Wanaongoza Kanisa,” katika Hadithi za Agano Jipya, 145-47, au video zinazofanana katika ChurchofJesusChrist.org.) Mualike mtoto kunyanyua juu picha ya Mitume wa sasa. Nani anamsaidia Yesu Kristo kuliongoza Kanisa wakati Yeye hayupo duniani?

  • Cheza mchezo wa kuoanisha na seti mbili za picha za Urais wa kwanza na Mitume Kumi na Wawili walio hai. Wakati mchezo unafanywa, taja jina la Mtume au Rais na kitu fulani kuhusu yeye.

  • Nyuma ya picha ya Rais wa Kanisa, bandika picha ndogo ndogo za vitu anavyofundisha kuhusu, kama Mwokozi, ubatizo, au hekalu. Acha kila mtoto kuchukua zamu kuangalia mojawapo ya picha na kuwaambia darasa zima, “Nabii anatufundisha kuhusu [mada kwenye picha].” Shuhudia kwamba manabii na mitume wanatufundisha kile ambacho Yesu anataka sisi tujue na kufanya.

Matendo ya Mitume 3:1–10

Baba wa Mbinguni anaweza kuwabariki wengine kupitia kwangu.

Unaweza kufanya nini ili kuwasaidia watoto kutambua njia wanazoweza kubariki wale wanaowazunguka? Wasaidie kujifunza kutokana na mfano wa Petro na Yohana wakimponya mtu dhaifu.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kufanya matendo ambayo yanaendana na hadithi katika Matendo ya Mitume 3:1–10, kama vile kunyoosha mikono yao kwa ajili ya pesa na kuruka kwa furaha. Ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni alimbariki mtu ambaye hakuweza kutembea?

  • Leta mfuko wenye picha ambazo zinaelezea njia ambazo tunaweza kuwabariki na kuwahudumia wengine. Waache watoto wachukue zamu kuchagua picha kutoka kwenye mfuko na kushiriki jinsi wanavyoweza kuwabariki wengine katika njia hiyo.

  • Waalike watoto kushiriki wakati walipomsaidia mtu fulani.

Matendo ya Mitume 5:1–11

Naweza kuwa mwaminifu

Wakristo wa awali walishiriki kile walichokuwa nacho ili kusaidia kutunzana. Wale waliomiliki ardhi waliiuza na kutoa pesa hiyo kwa mitume igawanywe miongoni mwa Watakatifu kulingana na mahitaji yao. Anania na Safira hawakuwa waaminifu kuhusu mchango wao, wakifikiri wangeweza kuwadanganya watumishi wa Bwana.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kuigiza hadithi ya Anania na Safira. Eleza kwamba ingawa hatutakufa tutakaposema uongo, hadithi hii inaonyesha jinsi gani ilivyo muhimu kuwa mwaminifu kwa Baba wa Mbinguni.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu uaminifu, kama vile “I Believe in Being Honest” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 149). Wasaidie watoto kuelewa kwamba kuwa mwaminifu ina maana siku zote kusema ukweli na sio kuchukuwa vitu ambavyo ni mali ya mtu mwingine.

  • Tumia vikaragosi vya mfuko wa karatasi kuigiza hali rahisi ambapo mtu anakuwa mwaminifu au sio mwaminifu. Waombe watoto kusimama kama mtu alikuwa mwaminifu au kukaa sakafuni kama mtu alikuwa sio mwaminifu. Wasaidie watoto kuelewa kwa nini ni muhimu kuwa mwaminifu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Matendo ya Mitume 1:8, 22–26

Yesu Kristo huongoza Kanisa Lake kupitia manabii na mitume.

Utawasaidiaje watoto kuelewa kwamba Kanisa la Mwokozi linaongozwa na manabii na mitume, kama ilivyokuwa nyakati za kale?

Shughuli Yamkini

  • Andika ubaoni Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo anaongoza Kanisa wakati Yeye hayupo duniani? Waalike watoto kusikiliza majibu ya swali unaposoma maneno ya Mwokozi kwa Mitume katika Matendo ya Mitume 1:8. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Yesu amewachagua manabii na mitume ili kuliongoza Kanisa leo, kama vile tu alivyofanya hapo zamani.

  • Someni pamoja Matendo ya Mitume 1:22–26. Kama darasa, tambueni jinsi Mitume walivyomwita Mtume mpya.

  • Kabla ya wakati mwombe mtoto mmoja na wazazi wake kujifunza kuhusu Mtume aliyeitwa hivi karibuni (wanaweza kupata taarifa kuhusu Mtume huyo kwenye “Akidi ya Mitume Kumi na Wawili,” ChurchofJesusChrist.org). Mwalike mtoto huyo kushiriki kile ambacho yeye alijifunza pamoja na darasa na, kama inawezekana, kile ambacho Mtume alisema kuhusu wito wake katika ujumbe wake kwenye mkutano wake mkuu wa kwanza.

Picha
Mitume wamekaa pamoja na wakizungumza

Mitume waliliongoza Kanisa baada ya Kristo kupaa mbinguni.

Matendo 2:36–47

Roho Mtakatifu hushuhudia kwenye moyo wangu juu ya ukweli wa injili.

Wakati watoto wanapojifunza kutambua jinsi Roho Mtakatifu anavyozungumza na wao, watavutiwa kumsikiliza na kutenda kazi juu ya mwongozo wa kiungu wanaopokea.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Matendo ya Mitume 2:36–37. Inasikikaje wakati Roho Mtakatifu anapotuambia kitu katika mioyo yetu?

  • Kama darasa, tengeneza bango lenye maneno Tutafanya nini? juu yake. Onyesha bango hilo kila wiki, na ongeza njia watoto wanazoweza kufanyia kazi kile wanachojifunza katika kila somo la wiki.

  • Waalike watoto kusoma Matendo ya Mitume 2:41–47 na kutafuta mambo mazuri watu waliyofanya baada ya kubatizwa. Je, ni vitu gani vizuri tunaweza kufanya ili kuonyesha tunashukuru kwa kipawa cha Roho Mtakatifu tulichopokea wakati tulipobatizwa?

Matendo ya Mitume 3:1–10

Baba wa Mbinguni anaweza kuwabariki wengine kupitia kwangu.

Unawezaje kuwafundisha watoto kwamba wanaweza kuwabariki wengine, hata kama hawana “fedha na dhahabu”? (Matendo ya Mitume 3:6). Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto waone fursa za kumhudumia Mungu kwa kuwahudumia wengine? (ona Mosia 2:17).

Shughuli Yamkini

  • Muombe mtoto asome Matendo ya Mitume 3:1–10 wakati watoto wengine wanaigiza hadithi nzima. (Kwa msaada, ona pia “Sura ya 56: Petro Anamponya Mtu,” katika Hadithi za Agano Jipya, 148–49, au video zinazofanana nayo katika ChurchofJesusChrist.org.) Unaweza pia kuonyesha video “Peter and John Heal a Man Crippled Since Birth” (ChurchofJesusChrist.org). Kwa jinsi gani baraka aliyopokea mtu huyu ilikuwa kubwa zaidi kuliko pesa alizoomba?

  • Pitisha mfuko wa sarafu. Watoto wanaposhikilia mfuko, waulize wanaweza kununua nini na hizo pesa. Waulize watoto ni kitu gani tunachopaswa kuwapa wengine ambacho hakigharimu pesa. Waalike kushiriki jinsi wanavyoweza kuwasaidia wengine kuja karibu zaidi na Mwokozi—zawadi ambayo haihitaji pesa (Matendo ya Mitume 3:6).

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Watie moyo watoto kupanga njia moja wanayoweza kumhudumia Baba wa Mbinguni kwa kumsaidia mwanafamilia wao wiki hii.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kariri andiko. Chagua kipengele cha maandiko ambacho unafikiri kingeweza kuwasaidia watoto katika darasa lako, kama vile Matendo ya Mitume 2:38 au Matendo ya Mitume 3:19, na wasaidie kukariri kirai hicho kutoka katika maandiko. Vielelezo au matendo vinaweza pia kuwasaidia watoto kuweka maandiko katika kumbukumbu.

Chapisha