Agano Jipya 2023
Julai 10–16. Matendo ya Mitume 6–9: “Ungetaka Nifanye Nini?”


“Julai 10–16. Matendo ya Mitume 6-9: ‘Ungetaka Nifanye Nini’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Julai 10–16. Matendo ya Mitume 6-9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Paulo ameanguka chini

Maongezi Njiani kwenda Dameski, na Michelangelo Merisi da Caravaggio

Julai 10–16

Matendo ya Mitume 6–9

“Ungetaka Mimi Nifanye Nini?”

Anza kwa kusoma Matendo ya Mitume 6–9. Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unaweza kukusaidia kujifunza sura hizi. Shughuli kwa ajili ya watoto wadogo katika muhtasari huu zinaweza kutoholewa kwa ajili ya watoto wakubwa, na kinyume chake.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Andika ubaoni majina ya baadhi ya watu kutoka Matendo ya Mitume 6–9, kama vile Sauli, Stefano, na Tabitha. Waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu watu hawa.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Matendo ya Mitume 6–7

Ninaweza kumfuata Yesu Kristo kwa kusimamia haki.

Watoto wanaweza kujifunza nini kutoka kwa Stefano kuhusu kuwa mfuasi wa Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kufanya matendo yanayoendana na wimbo kuhusu kuchagua yaliyo mema, kama vile “Stand for the Right” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 159). Tumia Matendo ya Mitume 7:51–60 ili kuwafundisha kwamba Stefano alifundisha kuhusu Yesu Kristo, ingawa iliwafanya viongozi wa Kiyahudi wakasirike sana (ona pia “Sura ya 57: Watu Waovu Wamuua Stefano,” katika Hadithi za Agano Jipya, 150–51, au video inayofanana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Je, ni kwa jinsi gani Stefano alisimamia haki?

  • Wape watoto matukio kadhaa ya watoto ambao wanatakiwa kufanya uchaguzi kati ya jema na ovu. Uliza watoto je wangelifanya nini ili kusimama kwa ajili ya haki.

Matendo ya Mitume8:26–39

Roho Mtakatifu ananipa mwongozo wa kushiriki injili na wengine.

Filipo alifuata ushawishi wa Roho na kumsaidia Muethiopia ambaye alikuwa akijitahidi sana kuelewa maandiko. Ni masomo gani katika hadithi hii yana msisimko kwa watoto unaowafundisha?

Filipo anamfundisha Muethiopia

Filipo anamfundisha Muethiopia, na Robert T. Barrett

Shughuli Yamkini

  • Weka viti viwili pamoja ili kuumba kibandawazi. Waalike watoto wawili kukaa katika kibandawazi, mmoja kumwakilisha Filipo na mwingine mtu wa Ethiopia. Kisha simulia hadithi ya jinsi Filipo alivyofundisha injili kwa mtu kutoka Ethiopia.

  • Shiriki uzoefu ambapo wewe ulimsikia Roho Mtakatifu akikuambia shiriki injili na mtu mwingine. Shuhudia kwamba Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia sisi kuwaambia wengine kuhusu Yesu.

Matendo ya Mitume 9:1–20

Baba wa Mbinguni ananialika nitubu na nifanye mabadiliko.

Wakati Yesu alipomwambia Sauli kuacha kutesa Kanisa la Bwana, Sauli mara moja alitubu na kubadilika. Ni kwa jinsi gani maelezo haya yanaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kutamani kubadilika kwa haraka wakati wanapofanya kosa?

Shughuli Yamkini

  • Fanya muhtasari wa hadithi ya kuongoka kwa Sauli inayopatikana katika Matendo ya Mitume 9:1–20 (ona pia “Sura ya 59: Sauli Anajifunza kuhusu Yesu,” katika Hadithi za Agano Jipya, 154–55. au video inayofanana katika ChurchofJesusChristLDS.org).

  • Ongea na watoto kuhusu mambo ambayo yanabadilika, kama vile kiluwiluwi, ambacho kinabadilika na kuwa chura, au kiwavi, ambacho hubadilika na kuwa kipepeo. Onesha picha, ikiwezekana. Ni kwa jinsi gani Sauli alibadilika wakati Yesu Kristo alipomtembelea?

  • Chora barabara yenye njia panda ubaoni. Waalike watoto kutaja sehemu ambazo wangependa kutembelea na ziandike juu ya barabara moja. Je, nini kingetokea kama tungeshika barabara isiyo sahihi? Je, ni kwa jinsi gani toba ni kama kurudi kwenye barabara sahihi?

  • Waombe watoto kurudia kile Sauli alichosema kwa Bwana: “Nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.?” (Matendo ya Mitume 9:6). Je, Bwana anatutaka sisi tufanye nini?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Matendo ya Mitume 6–7

Nitakuwa shahidi wa Yesu Kristo.

Unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kujifunza kutokana na mfano wa Stefano wa kusimama kama shahidi wa Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Soma Matendo ya Mitume 6:5–15 na 7:51–60 pamoja na watoto. Ni kitu gani kilimfanya Stefano kuwa shahidi mwenye nguvu wa Yesu Kristo. Alika mtoto mmoja au zaidi wajifanye kuwa Stefano na kushiriki kwa nini wao waliamini katika Yesu Kristo.

  • Waalike watoto kuchukua zamu kusoma Matendo ya Mitume 6:3–10, wakitafuta sifa Stefano alizokuwa nazo ambazo zilimsaidia kukua.

  • Waombe watoto kukusaidia kufikiria juu ya hali ambazo wanaweza kusimama kama mashahidi wa Yesu Kristo na injili Yake. Wasaidie kuigiza baadhi ya hali hizi. Waombe watoto kusoma Mosia 18:9. Toa angalizo kwamba kuwa shahidi wa Yesu Kristo ni pamoja na ahadi tunazofanya wakati wa ubatizo.

Matendo ya Mitume 8:9–24

Ukuhani ni zawadi ya thamani kuu kutoka kwa Mungu.

Shetani anajenga ujumbe kwamba vitu vya dunia vinatuletea furaha. Unawezaje kutumia hadithi ya Simoni kuwasaidia watoto kuthamini mambo ya kiroho kama vile ukuhani na baraka zake?

Shughuli Yamkini

  • Fanya muhtasari wa hadithi ya Simoni, inayopatikana katika Matendo ya Mitume 8:9-24 (ona pia “Sura ya 58: Simoni na Ukuhani,” Hadithi za Agano Jipya, 152–53, au video inayofanana katika ChurchofJesusChrist.org). Kwa nini hatuwezi kuupokea ukuhani kwa kuununua? Je, mtu anapokeaje hasa mamlaka ya ukuhani? (ona Makala ya Imani 1:5).

  • Onyesha picha za sakramenti, hekalu (ikiwakilisha baraka za hekalu), ubatizo, na baraka zingine tunazopokea kupitia ukuhani. Eleza kwamba vipawa hivi kutoka kwa Mungu ni vya thamani kuu na haviwezi kununuliwa na pesa. Kwa nini vina thamani kubwa kuliko kitu kingine cho chote tunachoweza kununua? Je, sisi tupokeaje baraka hizi?

Matendo ya Mitume 9:1–20

Baba wa Mbinguni ananialika nitubu na nibadilike.

Wakati Yesu alipomwambia Sauli kuacha kutesa Kanisa la Bwana, Sauli mara moja alitubu na kubadilika. Ni kwa jinsi gani maelezo haya yanaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kutamani kubadilika kwa haraka wakati wanapofanya kosa?

Shughuli Yamkini

  • Waalike wanafunzi kukunja kipande cha karatasi kiwe nusu. Waombe waandike Kabla kwenye nusu moja na Baada kwenye nusu nyingine. Soma pamoja na watoto Matendo ya Mitume 8:1–3; 9:1–2; na 9:17–22, na waombe waandike chini maneno au virai ambavyo vinamwelezea Sauli kabla na baada ya kumwona Bwana.

  • Mwalike mshiriki wa kata kushiriki hadithi yake ya kuongolewa na jinsi kuwa muumini wa Kanisa kumebadilisha maisha yake, kama maisha ya Sauli yalivyobadilika.

  • Chora “barabara kwenda Dameski” ubaoni. Waalike watoto kusoma Matendo ya Mitume 9:6, 11, 18, 20–22, wakitafuta kile Sauli alichofanya ili kutubu na kumgeukia Kristo, na andika vitendo hivi kwa kuambaa na barabara. Tunajifunza nini kutoka kwa Sauli kuhusu jinsi tunavyoweza kuwa zaidi kama Kristo?

  • Waalike watoto kuchora sehemu waliyoipenda ya hadithi ya kuongoka kwa Sauli na kushiriki mchoro wao pamoja na washiriki wa darasa.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Watie moyo watoto waelezee familia zao shughuli waliyoipenda kutoka darasani leo na iliwafundisha nini wao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kujifunza kutoka kwenye maandiko. Watoto wadogo wanaweza kushindwa kusoma sana, lakini bado unaweza kuwahusisha katika kujifunza kutoka kwenye maandiko. Wakati mwingine unaweza kusoma kifungu na kuwaalika watoto kusimama au kuinua mikono yao juu wakati wanaposikia neno fulani au kirai unachotaka kukizingatia.