Agano Jipya 2023
Agosti 28–Septemba 3. 1 Wakorintho 8–13: “Ninyi ni Mwili wa Kristo”


“Agosti 28–Septemba 3. 1 Wakorintho 8–13: ‘ Ninyi ni Mwili wa Kristo’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Agosti 28–Septemba 3. 1 Wakorintho 8–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
mkutano wa sakramenti

Agosti 28–Septemba 3

1 Wakorintho 8–13

“Ninyi ni Mwili wa Kristo”

Unaposoma 1 Wakorintho 8–13, sikiliza ushawishi kutoka kwa Roho kuhusu jinsi ya kufundisha kanuni zilizopo katika sura hizi. Kumbuka kwamba wazo la shughuli yoyote linaweza kutoholewa kwa watoto wote wakubwa na wadogo.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto washiriki kitu fulani walichofanya wakati wa mkutano wa sakramenti leo ili kufikiria kuhusu Yesu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

1 Wakorintho 10:13

Baba wa Mbinguni atanisaidia mimi kufanya maamuzi ya haki.

Siyo rahisi kila mara kuchagua yaliyo mema, na Baba wa Mbinguni anajua hilo. Tukimwomba, Yeye atatusaidia kwa sababu Yeye anataka sisi tufanikiwe.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee 1 Wakorintho 10:13 watoto, ukiwaalika kutikisa vichwa vyao wanaposikia maneno “alijaribiwa” au ”majaribu.” Elezea mstari huu unamaanisha nini kwako wewe?

  • Simulia baadhi ya hadithi kwa ufupi za watu ambao wanakaribia kufanya uchaguzi usio sahihi. Wakati watoto wanasikiliza, waalike kuinua juu mikono yao au alama ya karatasi isemayo sitisha wakati mtu katika hadithi hiyo anafanya uchaguzi usio sahihi. Je, uchaguzi sahihi ungekuwa upi? Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni atatusaidia kuchagua yaliyo sahihi.

  • Onyesha picha ya Yesu, na imba pamoja na watoto wimbo kuhusu Yeye, kama vile “I’m Trying to Be Like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79). Zungumza kuhusu kumkumbuka Yesu kunakusaidiaje wewe kufanya uchaguzi sahihi. Onyesha picha za vitu vingine ambavyo vinatusaidia kufanya chaguzi sahihi, kama vile wazazi au maandiko. Waulize watoto ni nini kinachowasaidia kufanya chaguzi sahihi.

1 Wakorintho 12:4, 7–12

Baba wa Mbinguni amenibariki na karama za kiroho.

Baba wa Mbinguni amewapa watoto wake wote karama za kiroho. Ni karama gani za kiroho unazoziona katika watoto unaowafundisha?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wachore picha ya karama waipendayo waliyopokea. Eleza kwamba Baba wa Mbinguni anatupa karama za kiroho ili kuimarisha imani yetu na kutusaidia kuwabariki wengine. Shiriki pamoja na watoto maelezo yanayopatikana katika 1 Wakorintho 12:7–11.

  • Andika barua kwa kila mtoto, ukieleza karama ya kiroho uliyoiona kwake (au unaweza kuwataka wazazi waandike barua hizi). Weka barua hizo katika bahasha. Waruhusu watoto wafungue bahasha zao, na wasaidie kusoma kuhusu karama zao za kiroho.

Picha
maboksi ya zawadi

Baba wa Mbinguni amewapa watoto Wake wote karama za kiroho.

1 Wakorintho 13

Naweza kuwapenda wengine

Maandiko yanafundisha kwamba hisani ni “upendo safi wa Kristo” (Moroni 7:47). Unawezaje kuwasaidia watoto kukuza na kuonyesha upendo kama wa Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Soma 1 Wakorintho 13:13 na Moroni 7:47, na wasaidie watoto kurudia kirai “Hisani ni upendo msafi wa Kristo.” Onyesha picha za Yesu akiwa mwenye upendo na mkarimu, na waulize watoto jinsi gani alionesha upendo kwa wengine (ona Kitabu cha Sanaa cha Injili kwa ushauri).

  • Imbeni wimbo kuhusu kuwapenda wengine, kama vile “Jesus Said Love Everyone” au “Love One Another” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61, 136), pamoja na watoto. Onyesha picha za watu tofauti (kama vile mzazi, ndugu, mwalimu, au rafiki), na waombe watoto kushiriki jinsi gani wanaweza kumhudumia mtu yule. Waombe watoto kufikiria juu ya mtu fulani ambaye wanaweza kumhudumia na kisha kuandika barua au kuchora picha ya kumpa mtu yule. Kama wanataka mawazo mengine, onyesha video “Pass It On” (ChurchofJesusChrist.org).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

1 Wakorintho 10:13

Baba wa Mbinguni atanisaidia mimi kupinga majaribu.

Ahadi katika mstari huu zinaweza kuwapa watoto kujiamini kwamba wanaweza kuyapinga majaribu kwa msaada wa Baba wa Mbinguni.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wasome 1 Wakorintho 10:13 wawili wawili na kufanya muhtasari wa mstari huu katika maneno yao. Waombe watoto kushiriki uzoefu ambapo Baba wa Mbinguni aliwasaidia kuepuka au kupinga majaribu. Je, tunaweza kufanya nini ili kumtegemea Baba wa Mbinguni wakati tunapojaribiwa?

  • Andika katika vipande vya karatasi majaribu ambayo watoto wanaweza kukabiliana nayo leo. Waalike watoto kila mmoja kuchagua karatasi na kushiriki kile Baba wa Mbinguni alichotupa ili kutusaidia kuepuka au kuyapinga majaribu haya. Kwa baadhi ya mawazo; someni pamoja Alma 13:28–29.

1 Wakorintho 11:23–29

Wakati wa Sakramenti, naweza kufikiria kuhusu jinsi ninavyomfuata Mwokozi.

Wasaidie watoto unaowafundisha kuona kwamba sakramenti ni fursa ya “kujihoji” wenyewe na kufanya upya maagano yao ya ubatizo ya kumtumikia Bwana na kushika amri zake (1Wakorintho 11:28).

Shughuli Yamkini

  • Muombe mtoto asome 1 Wakorintho 11:28. Ina maana gani “kujihoji” wenyewe kabla ya kupokea sakramenti? Waombe watoto kufikiria juu ya watu wengine ambao wanapima vitu, kama madaktari, wapelelezi, au wanasayansi (kwa mfano, madaktari hutupima miili yetu ili kuhakikisha kwamba tuna afya njema). Tunapopokea sakramenti, tunaweza kufanya nini ili kujihoji tunayaishije maagano yetu ya ubatizo?

  • Waombe watoto kutengeneza orodha ya vitu wanavyoweza kufikiria juu yake wakati wanapopokea sakramenti. Waalike watumie orodha zao kama ukumbusho wa kujihoji wenyewe wakati wa sakramenti.

1 Wakorintho 12:4, 7–12,31; 13:1–8

Ninazo karama za kiroho.

Paulo alifundisha kwamba karama za kiroho “zinatolewa kwa kila mtu” (1 Wakorintho 12:7). Kanuni hii inaweza kuwasaidia watoto kujenga hisia za kujithamini, hususani wanapotumia karama zao kubariki wengine.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kuandika ubaoni karama za kiroho wanazopata katika 1 Wakorintho 12:7–11; 13:2. Waalike watafute karama yoyote ya nyongeza iliyotajwa katika Moroni 10:8–18 na Mafundisho na Maagano 46:13–26. Shiriki pamoja nao baadhi ya karama za kiroho za ziada zilizotajwa na Mzee Marvin J. Ashton: “Karama ya kuomba; karama ya kusikiliza; … karama ya kuepuka mabishano; … karama ya kutafuta kile kilicho cha haki; karama ya kutohukumu; karama ya kumtegemea Mungu kwa ajili ya mwongozo; … karama ya kuwajali wengine; … karama ya kutoa sala; karama ya kutoa ushuhuda wenye nguvu” (“There Are Many Gifts,” Ensign, Nov. 1987, 20). Waalike watoto kuzungumzia kuhusu karama za kiroho wanazoziona katika kila mmoja.

  • Kabla ya darasa, waulize wazazi wa watoto wa darasa lako kuhusu karama wanazoziona kwa watoto wao, au fikiria kuhusu karama za watoto wewe mwenyewe. Waambie watoto kuhusu karama hizi. Waombe watoto kuandika njia moja watakayotumia karama zao kumbariki mtu fulani wiki hii.

  • Shiriki hali tofauti ambazo watu wanaweza kutumia karama ya kiroho kutoka 1 Wakorintho 12:7–10. Waalike watoto kutambua karama za kiroho ambazo zinaweza kutumika katika kila hali.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Pendekeza kwamba watoto wajadili kitu fulani ulichokizungumza darasani wakijadili na familia zao. Kwa mfano, ungeweza kuwaalika watoto kushiriki karama zao za kiroho pamoja na familia zao na waulize washiriki wa wanafamilia wao vipawa vyao ni vipi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa mialiko ambayo inaheshimu haki ya kujiamulia. Unapowaalika watoto kufanya juu ya kile wanachojifunza, fikiria njia ya kuheshimu haki yao ya kujiamulia. Badala kutoa mwaliko maalulmu, fikiria kuwataka wawazie njia zao wenyewe za kutumia kile walichojifunza.

Chapisha