Agano Jipya 2023
Septemba 4–10 1 Wakorintho 14–16: “Mungu si Mungu wa Machafuko, bali wa Amani”


“Septemba 4–10. 1 Wakorintho 14–16: ‘Mungu Si Mungu wa Machafuko, bali wa Amani’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)

“Septemba 4–10. 1 Wakorintho 14–16,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
kisima cha maji ya ubatizo cha hekaluni

Septemba 4–10

1 Wakorintho 14–16

“Mungu si Mungu wa Machafuko, bali wa Amani”

Unaposoma 1 Wakorintho 14–16, Roho Mtakatifu atakusaidia kujua nini cha kuwafundisha watoto katika darasa lako. Pitia upya muhtasari huu kwa ajili ya mawazo ya ziada.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Unaweza kuanza somo la wiki hii kwa kusoma 1 Wakorintho 14:26 kwa sauti. Weka angalizo kwamba tunapokuja pamoja kanisani, tunaweza kuwainua (au kuwajenga na kuwasaidia) wengine wakati tunaposhiriki kile tunachojifunza. Waulize watoto kile wanachoweza kushiriki ili kumjenga mtu katika darasa leo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

1 Wakorintho 3:12–22

Ninaweza kuishi na Baba wa Mbinguni baada ya mimi kufa kwa sababu Yesu Kristo alifufuka.

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwafundisha watoto katika darasa lako kwamba kwa sababu Yesu Kristo alifufuka sisi tunaweza kuishi tena?

Shughuli Yamkini

  • Rudia kirai kifuatacho mara kadhaa pamoja na watoto: “Katika Kristo wote watahuishwa” (1 Wakorintho 15:22). Onyesha picha ya Mwokozi mfufuka (ona muhutasari wa wiki hii katka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Bnafsi na Familia) au onyesha video “Jesus Is Resurrected” (ChurchofJesusChrist.org). Elezea kwamba sisi wote tutakufa siku moja, lakini kwa sababu Yesu alifufuka, sisi pia tutaishi tena baada ya kufa.

  • Waoneshe watoto koti, ambalo linawakilisha miili yetu ya nyama na mifupa. Tunapokuwa hai, roho zetu zinakuwa ndani ya miili yetu, na miili yetu inaweza kutembea (vaa koti). Tunapokufa, roho zetu zinaiacha miili yetu ya nyama na mifupa, na miili yetu haiwezi kutembea (vua koti na liweke juu ya meza au kiti kuwakilisha mwili bila roho yake). Tutakapofufuka, roho zetu zinarudi ndani ya miili yetu (vaa koti tena), na kamwe havitengani tena. Waache watoto wachukuwe zamu kulivaa koti na kulivua wakati mtoto mwingine anaelezea nini kinatokea wakati tutakapofufuka.

1 Wakorintho 15:29

Ninaweza kubatizwa kwa ajili ya watu walio kufa.

Watoto wanapojiandaa kwa ajili ya ubatizo wao fikiria jinsi ya kuwasaidia kuitazamia fursa ya kubatizwa kwa niaba ya waliokufa.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya mambo wasiyoweza kujifanyia wenyewe. Ni nani anayewasaidia kufanya mambo haya? Onyesha picha ya mmoja wa mababu zako aliyekufa bila kubatizwa. Waambie watoto kuhusu mtu huyu, na eleza kwamba mtu huyu anahitaji msaada wetu kubatizwa.

  • Waulize watoto kama wana mwanafamilia yo yote ambaye amewahi kuwa hekaluni kwa ajili ya kufanya ubatizo kwa ajili ya wafu. Onyesha picha za birika ya ubatizo ya hekaluni. Waulize watoto kama wanajua kile hufanyika hapa. Elezea kwamba ndani ya hekalu tunaweza kubatizwa kwa niaba ya watu waliokufa bila kubatizwa. Kisha watu hao wanaweza kuchagua kama watakubali ubatizo huo.

1 Wakorintho 15:40–41

Baba wa Mbinguni ananitaka mimi kuishi pamoja Naye katika ufalme wa selestia.

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwafundisha watoto kuhusu falme za selestia, terestria, na telestia? Shughuli hizi zinaweza kukusaidia.

Shughuli Yamkini

  • Andika ubaoni selestia, terestria, na telestia. Wasaidie watoto kujifunza kusema maneno haya.

  • Onyesha picha ya jua, mwezi, na nyota. Waalike watoto kuviweka katika mpangilio sahihi kuanzia na angavu zaidi hadi angavu. Soma 1 Corinthians 15:40–41 kwa watoto (ona pia Tafsiri ya Joseph Smith katika mstari wa 40, tanbihi a). Eleza kwamba jua, mwezi, na nyota vinawakilisha falme tunazoweza kuishi baada ya kufufuliwa. Katika ufalme wa selestia, tunaweza kuishi na Baba wa Mbinguni.

  • Wape watoto nakala za ukurasa wa shughuli ya wiki hii wapake rangi. Wakati wakipaka rangi, shiriki nao hisia zako kuhusu Mwokozi na kile Yeye alichofanya ili kutuwezesha sisi kuishi na Baba wa Mbinguni tena.

Picha
mawio

“Kuna fahari moja ya jua” (1 Wakorintho 15:41).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

1 Wakorintho 15:12–22

Kwa sababu ya Yesu Kristo na Ufufuko Wake, nami nitafufuliwa.

Je, watoto unaowafundisha wanaelewa umuhimu wa kufufuka kwa Yesu Kristo? Mawazo haya yanaweza kukusaidia.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kuchukua zamu kusoma mistari katika 1 Wakorintho 15:12–22, wakitafuta majibu kwa swali “kingetokea nini kama kusingekuwa na ufufuko?”

  • Waalike watoto kuigiza jinsi ya kuelezea ufufuko kwa mtu mwingine. Kwa ajili ya mawazo, wangeweza kurejelea wimbo kuhusu Ufufuko wa Mwokozi, kama vile “Did Jesus Really Live Again?” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64). Ona pia video ya “Until We Meet Again” (ChurchofJesusChrist.org). Toa ushuhuda wako juu ya Ufufuko wa Kristo.

1 Wakorintho 15:12–13, 20–22, 29

Ninaweza kujiandaa kwenda hekaluni kubatizwa kwa niaba ya wafu.

Ubatizo kwa niaba ya wafu ni kazi yenye shangwe ya upendo kwa niaba ya mababu zetu. Ni kwa jinsi gani utawasaidia watoto hawa kujiandaa kushiriki katika kazi hii?

Shughuli Yamkini

  • Soma 1 Wakorintho 15:29. Je, Watakatifu katika siku ya Paulo walikuwa wakifanya nini ambacho sisi pia tunafanya leo? Waulize watoto kwa nini tunabatizwa kwa niaba ya wafu. Kama ni muhimu, eleza kwamba mababu zetu wengi hawakuwa na nafasi ya kubatizwa na kuthibitishwa wakati wa maisha haya. Katika hekalu tunaweza kubatizwa na kuthibitishwa kwa ajili yao.

  • Siku chache kabla ya darasa, muombe mzazi wa mmoja wa watoto kumsaidia mtoto wake kushiriki mti wa familia yake au kusimulia hadithi kuhusu babu yake. Unaweza pia kushiriki kuhusu mababu zako.

  • Mwalike mshiriki wa uaskofu au vijana katika kata yako ili waelezee baadhi ya vitu ambavyo watoto wanaweza kufanya ili kujiandaa kuingia hekaluni. Waombe watoto kuongezea mawazo yao. Waalike kuweka lengo la kwenda hekaluni siku moja.

1 Wakorintho 15:40–41

Baada ya kufufuka, ninaweza kuishi katika ufalme wa selestia.

Ili kuwafundisha Wakorintho kuhusu miili tutakayopokea katika Ufufuko, Paulo alitaja madaraja matatu ya utukufu: selestia, terestria, na telestia.

Shughuli Yamkini

  • Soma 1 Wakorintho 15:40–41 na mwalike mtoto kuchora jua, mwezi, na nyota ubaoni. Waombe washiriki wa darasa kutambua aina gani ya mwili uliofufuka unawakilishwa na kila mchoro.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu mahekalu, kama vile “The Lord Gave Me a Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 153). Au onyesha video “Our Eternal Life” (ChurchofJesusChrist.org). Wimbo huu au video hii inatufundisha nini sisi kuhusu kujiandaa kuishi katika utukufu wa selestia?

  • Eleza kwamba Joseph Smith alipata ono ambamo ndani yake aliona falme tatu ambazo zinafanana na aina ya miili Paulo anayoelezea. Wasaidie watoto kupata virai kutoka Mafundisho na Maagano 76:50–53, 70; 76:71–79; 76:81–82 ambavyo vinaelezea falme hizi tatu.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuwaomba wazazi wao kuwasimulia hadithi kuhusu mmoja wa mababu zao. Wanaweza kushiriki hadithi hiyo pamoja na darasa wiki ijayo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wahimize watoto kuuliza maswali “Jitahidi kuona maswali ya [watoto] kama fursa, siyo kama usumbufu au vizuizi kwenye somo lako. … Maswali kama haya yanakupa umaizi muhimu wa kujua kile watoto wanachofikiria, wasiwasi walio nao, na jinsi wanavyoitikia mambo wanayojifunza. Wasaidie kuona kwamba majibu ya maswali yao yanaweza kupatikana katika maandiko na maneno ya manabii walio hai” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25–26).

Chapisha