“Septemba 18–24. 2 Wakorintho 8–13: ‘Mungu Humpenda Yeye Atoaye kwa Moyo wa Ukunjufu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2022)
“Septemba 18–24. 2 Wakorintho 8–13” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023
Septemba 18–24
2 Wakorintho 8–13
“Mungu Humpenda Yeye Atoaye kwa Moyo wa Ukunjufu”
Mawazo yako bora kwa ajili ya kuwafundisha watoto katika darasa lako yatakuja unapojifunza kwa maombi 2 Wakorintho 8–13 na wao wakiwa akilini mwako. Mawazo ya ziada ya kufundisha yanaweza kupatikana katika muhtasari huu.
Alika Kushiriki
Njia moja mzuri ya kualika kushiriki miongoni mwa watoto ni kuwakumbusha juu ya kitu fulani ulichowataka wafanye wakati wa somo lililopita. Waombe washiriki uzoefu wao.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Ninaweza kutoa kwa moyo wa ukunjufu kwa watu wenye shida.
Daima ni vizuri kuwahudumia wengine, lakini ni bora zaidi kuhudumia kwa moyo wa ukunjufu. Fikiria nini kitamvutia kila mtoto kuwa “atoaye kwa moyo wa ukunjufu.”
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto kurudia kirai “Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” (2 Wakorintho 9:7). Inamaanisha nini kuwa “atoaye kwa moyo wa ukunjufu”? Onyesha picha ya uso wenye furaha na uso wenye huzuni, na waulize watoto upi unaonekana kama atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
-
Imbeni pamoja wimbo kuhusu huduma, kama vile “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198), mara kadhaa. Mara ya kwanza, waombe watoto waimbe kwa furaha; kisha waombe waimbe wimbo kwa mihemko au mitazamo, kama vile huzuni, kuchoka, hasira, au hofu. Wakumbushe watoto kwamba Baba wa Mbinguni anatutaka kusaidia wengine kwa furaha. Kisha imba wimbo huo tena kwa furaha.
-
Wasaidie watoto kutengeneza nyuso zenye kutabasamu na nyuso zilizonuna. Waombe waziinue juu picha zao wakati wanaposikia maneno tabasamu au kutabasamu wanapoimba “Smiles” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 267). Wanaweza kufanya kitu kile kile na picha za sura zilizonuna na maneno nuna na kununa. Wasaidie watoto kutambua sura ipi imefurahi na ipi imenuna. Waambie watoto kwamba njia mojawapo ya kuwa mwenye ukunjufu na kuhudumia wengine ni kutabasamu na kuwasaidia wengine nao watabasamu.
-
Panga shughuli ya darasa ili kumhudumia mtu fulani, kama vile mtoto asiyehudhuria darasa la msingi au mshiriki wa kata au jirani mwenye shida. Mnaweza kupanga kutembelea nyumbani kwa mtu huyu, kuandika barua za ukarimu au kuchora picha, au kutengeneza kitafunwa cha kushiriki naye.
-
Mwalike kila mtoto kupanga tendo la huduma ya furaha kwa mmoja wa washiriki wa familia yake. Wakati wa somo la wiki ijayo, waombe waelezee kile walichofanya.
Baba wa Mbinguni daima anajibu sala, lakini sio daima katika njia tunayotarajia.
Uzoefu wa Paulo wa kusali kwa ajili ya “mwiba katika mwili” uondolewe inatufundisha kwamba Mungu wakati mwingine anatuimarisha katika majaribu kuliko kuyaondoa.
Shughuli Yamkini
-
Onyesha watoto mmea wenye miiba (au picha yake). Wasaidie kufikiria jinsi watakavyohisi kuwa na mwiba uliokwama katika miili yao kwa muda mrefu. Fanya muhtasari wa 2 Wakorintho 12:7–10 kwa ajili ya watoto, ukielezea kwamba “mwiba katika mwili” wa Paulo ulikuwa ni majaribu, kitu fulani kigumu katika maisha yake. Hata kama Paulo alipomwomba Mungu kuondoa jaribu hilo, Mungu hakufanya hivyo. Badala yake, Mungu alimfundisha Paulo kwamba changamoto zinaweza kutusaidia kujifunza kuwa wanyenyekevu na kumtumaini Yeye. Ndipo Mungu anaweza kutufanya kuwa imara.
-
Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni anajua kitu kilicho bora kwetu sisi, Naye atatupa kile tunachohitaji, hata kama ni tofauti na kile tunachodhani tunakihitaji. Unaweza pia kushiriki uzoefu wakati sala zako zilipojibiwa katika njia au wakati ambao ulikuwa tofauti na ule uliotegemea. Hadithi kama “Mtanzuko wa Ugonjwa wa Kisukari” (Rafiki, Sept. 2019, 4–5) au “Tafadhali Mbariki Ace” (Rafiki, Nov. 2019, 32–33) zinaweza pia kusaidia.
-
Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu Upendo wa Baba wa Mbinguni, kama vile “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13). Waulize watoto kile watakachosema kwa mtu fulani anayeshangaa kama Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala. Imbeni wimbo tena, na onyesha mistari ambayo inaeleza jinsi Baba wa Mbinguni anavyojisikia kuhusu sisi.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Ninaweza kutoa kwa moyo wa ukunjufu kwa watu wenye shida.
Paulo alitaka kuwapa mwongozo wa kiungu Watakatifu wa kutoa ziada yao ili kuwasaidia maskini. Je, ni kwa jinsi gani wewe utatumia maneno yake kuwapa mwongozo wa kiungu watoto ili kuwahudumia wengine?
Shughuli Yamkini
-
Andika maneno ya 2 Wakorintho 9:7 ubaoni, na huku ukiacha mapengo ya maneno muhimu. Waalike watoto kubahatisha ni maneno gani yanayokosekana. Kisha waache wasome mstari katika maandiko ili kujaza mapengo. Inamaanisha nini kutoa “kwa kunung’una, au kwa kulazimaka”? Inamaanisha nini kuwa “atoaye kwa moyo wa ukunjufu”?
-
Waalike watoto wakusaidie kutafuta picha za Mwokozi akiwahudumia watu wengine (zipo kadhaa katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waulize wanaona nini katika picha hizi ambacho kinawasaidia kujua kwamba Yesu aliwahudumia wengine kwa upendo. Wekeni lengo kama darasa kusema ndiyo wakati wanafamilia au wengine wanapotuomba kuhudumia katika wiki ijayo, kama vile kwa kusaidia nyumbani au kushughulikia wengine.
-
Wasaidie watoto kupamba mawe madogo. Eleza kwamba haya ni “mawe ya huduma“ ambayo wanaweza kuyabeba mifukoni mwao wiki hii ili kuwasaidia kukumbuka kuwahudumia wengine kwa moyo wa ukunjufu.
-
Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu huduma, kama vile “Fun to Do” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 253). Wasaidie watoto wafikirie juu ya mistari mipya ya wimbo ambao unaelezea njia tofauti za kuwahudumia wengine.
Baba wa Mbinguni daima anajibu sala, lakini sio siku zote atanipa kila ninachoomba.
Paulo alimwomba Mungu kuondoa udhaifu wake, lakini Mungu alijua kwamba udhaifu wa Paulo utamfanya awe myenyekevu na Mungu angemfanya kuwa imara.
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto kufananisha 2 Wakorintho 12:9–12 na Etheri 12:27. Je, ni maneno gani au virai gani vilivyorudiwa? Je, mistari hii inafundisha nini? (Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba Paulo alikuwa anafananisha changamoto yake na mwiba katika ngozi yake.) Mungu alimfundisha nini Paulo kuhusu majaribu?
-
Waalike watoto kuorodhesha baadhi ya majaribu ambayo watu huwa nayo katika maisha. Wasaidie wao kufikiria jinsi mtu fulani anavyoweza kujifunza kutokana na majaribu haya na kubarikiwa nayo.
-
Soma pamoja na watoto “Mtanziko wa Ugonjwa wa Kisukari” (Rafiki, Sept. 2019, 4–5). Waombe watoto kushiriki uzoefu wakati walipoomba kwa ajili ya kitu fulani na hawakukipata. Waombe washiriki kile walichojifunza kutokana na uzoefu wao. Unaweza kuwa na uzoefu wako binafsi wa kushiriki pia. Toa ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni siku zote anajibu sala zetu katika njia na katika wakati ambao utatubariki zaidi.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kuwa watoaji kwa moyo wa ukunjufu katika nyumba zao wiki hii na kuja darasani wiki ijayo wakiwa wamejiandaa kutoa taarifa juu ya jinsi walivyomhudumia mtu mwenye shida.