Agano Jipya 2023
Nyenzo za Ziada kwa ajili ya Kufundishia Watoto


“Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2023)

“Nyenzo za Ziada kwa ajili ya Kufundishia Watoto” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
walimu wanawake wakiwafundisha watoto wadogo katika darasa la kanisa

Nyenzo za Ziada kwa ajili ya Kufundishia Watoto

Nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika programu ya Maktaba ya Injili na kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia

Unaweza kutohoa shughuli kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa ajili ya matumizi katika darasa lako la Msingi. Usihofu kama watoto tayari wamekwishafanya shughuli hizi pamoja na familia zao nyumbani; marudio husaidia watoto kujifunza. Watoto wanaweza kuhitaji kukuambia jinsi walivyofanya shughuli pamoja na familia zao na kile walichojifunza.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho na hutusaidia sisi kuhisi upendo wa Mungu, na zinafundisha mafundisho katika njia ya kukumbukwa. Katika kuongezea kwenye matoleo yalilochapishwa ya Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi za sauti na video za nyimbo nyingi za kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika programu takatifu za Muziki na Injili.

Kwa ajili ya mawazo, angalia “Kutumia Muziki ili Kufundisha Mafundisho” na “Kuwasaidia Watoto Kujifunza na Kukumbuka Nyimbo za Msingi pamoja na Nyimbo za Kanisa” katika “kiambatisho cha kitabu hiki cha kiada.

Tazama Wachanga Wenu

Nyingi kati ya mada zilizotajwa katika kitabu cha kiada cha Behold Your Little Ones: Nursery Manual ni sawa na zile utakazofundisha katika Msingi. Hususani kama unafundisha watoto wadogo, fikiria kuangalia katika kitabu cha kiada cha chekechea kwa ajili ya nyimbo za ziada, hadithi, shughuli, na sanaa na kazi za mikono.

Rafiki

Gazeti la Rafiki hutoa hadithi na shughuli ambazo zinaweza kuwa nyongeza ya kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Hadithi za Agano Jipya

Hadithi za Agano Jipya zinaweza kuwasaidia watoto kujifunza mafundisho na hadithi zilizopatikana katika Agano Jipya. Unaweza pia kupata video za hadithi hizi katika programu ya Maktaba ya Injili na kwenye MediaLibrary.ChurchofJesusChrist.org.

Kitabu cha Kupaka Rangi—Agano Jipya

Nyenzo hii ina kurasa za shughuli zilizokusudiwa kuongeza kujifunza kwa watoto kutoka kwenye Agano Jipya.

Video na Sanaa

Sanaa za kuchora, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa mafundisho na kupata taswira ya hadithi zinazohusiana na maandiko. Tembelea Gospel Media kwenye GospelMedia.ChurchofJesusChrist.org ili kuperuzi mkusanyiko wa nyenzo za habari za Kanisa. Gospel Media pia inapatikana kama app ya simu ya mkononi. Picha nyingi ambazo unaweza kutumia katika darasa zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili.

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi inaweza kukusaida wewe kujifunza kuhusu, na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo. Kanuni hizi zinajadiliwa na kufanyiwa mazoezi katika mikutano ya baraza la mwalimu.

Chapisha