Agano Jipya 2023
Wewe ni Mwalimu wa Watoto


“Wewe ni Mwalimu wa Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2023)

“Wewe ni Mwalimu wa Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Yesu amembeba mtoto

Wewe ni Mwalimu wa Watoto

Umeitwa na Mungu kufundisha watoto Wake katika njia ya Mwokozi. Umesimikwa katika wito huu kwa mamlaka ya ukuhani Wake mtakatifu. Hata kama wewe sio mwalimu mwenye uzoefu, unapoishi kwa kustahili, kusali kila siku, na kujifunza maandiko, Baba wa Mbinguni atakuzawadia ushawishi na nguvu za Roho Mtakatifu ili kukusaidia ufanikiwe (ona 2 Nefi 33:1).

Wale waliowekwa chini ya uangalizi wako ni watoto wa Baba wa Mbinguni, na Yeye anajua kile wanachohitaji na jinsi ya kuwafikia vyema. Kwa sala unapotafuta ushawishi wa Roho Mtakatifu, Yeye atakuongoza wakati wa maandalizi yako na wakati unapofundisha. Atakufunulia kile unachopaswa kusema na kile unachopaswa kufanya (ona 2 Nefi 32:5).

Kamwe usidharau uwezo wa mtoto wa kuelewa injili. Katika nyanja zote za maisha yao, watoto hawa wa thamani wanaendelea kufyonza habari, wakiunda na kusafisha mawazo yao, na kufanya na kushiriki uvumbuzi. Hii ni kweli hasa kwa injili, kwani watoto wapo tayari na wana nia ya kujifunza ukweli wake rahisi. Imani yao katika mambo ya kiroho ni imara na safi, na kila wakati ni fursa ya kujifunza. Kwa hiyari wako tayari kutenda juu ya yale waliyojifunza, hata kama ufahamu wao bado haujakamilika. Hivi ndivyo jinsi sote tunavyopaswa kupokea injili. Kama Mwokozi alivyofundisha, “Mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe” (Luka 18:17).

Wito wa kufundisha watoto ni wajibu mtakatifu, na ni kawaida kuhisi kuzidiwa wakati mwingine. Lakini kumbuka kwamba Baba yako wa Mbinguni alikuita, na Yeye atakusaidia. Hii ni kazi ya Bwana, na unapohudumu “kwa moyo wako wote, uwezo, akili na nguvu” (Mafundisho na Maagano 4:2), Yeye atapanua uwezo wako, vipawa, na vipaji, na huduma yako itabariki maisha ya watoto unaowafundisha.

Chapisha