Agano la Kale 2022
Desemba 5–11. Hagai; Zekaria 1–3; 7–14: “Utakatifu kwa Bwana”


“Desemba 5–11. Hagai; Zekaria 1–3; 7–14: ‘Utakatifu kwa Bwana’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Desemba 5–11. Hagai; Zekaria 1–3; 7–14,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Hekalu la Laie Hawaii

Desemba 5–11

Hagai; Zekaria 1–3; 7–14

“Utakatifu kwa Bwana”

Kwa sala soma Hagai na Zekaria, ukitafakari misukumo unayopokea. Ni jinsi gani ukweli katika vitabu hivi husaidia kukidhi mahitaji ya watoto?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Chora uso wa furaha kwenye kipande cha karatasi, na waruhusu watoto wafanye zamu kukishikilia. Wakati wa zamu yao, waalike kushiriki jambo wanalojifunza kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ambalo huwapa furaha.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Hagai 1:6–8

Ninaweza kumweka Mungu kwanza katika maisha yangu.

Kujifunza kuhusu ushauri wa Bwana “zitafakarini njia zenu” ni fursa kwa watoto kuhakikisha wanafanya mambo muhimu ambayo Mungu ametutaka tufanye.

Shughuli Yamkini

  • Waeleze watoto kwamba Bwana aliwataka Waisraeli wajenge hekalu, lakini badala yake walikuwa wakifanya mambo mengine. Soma kwa sauti Hagai 1:7, na eleza kwamba “zitafakarini njia zenu” ina maana kwamba Bwana aliwataka Waisraeli kufikiria kuhusu ikiwa walikuwa wanafanya mambo muhimu zaidi. Soma mstari wa 8 kwa watoto, na waalike wajifanye “kupanda mlimani,” “kuleta kuni,” na “kuijenga nyumba [ya Bwana].” Ni mambo gani muhimu ambayo Mungu anatutaka tufanye?

  • Weka picha juu ya meza zikiwa zinaangalia chini ambazo huwakilisha mambo ambayo ni muhimu kwa Mungu, kama vile maandiko, sala na hekalu. Waruhusu watoto wafanye zamu kuchagua picha na kuionesha kwa darasa. Wasaidie waelewe kwa nini ni muhimu kuhakikisha kwamba tunatenga muda kwa ajili ya kila moja ya kitu kilichoko katika picha.

Zekaria 3:1–7

Yesu Kristo anaweza kuifanya roho yangu kuwa safi.

Nguo chafu za kuhani mkuu Yoshua, zilizoelezewa katika Zekaria 3:1–7, zinawakilisha kile kinachotokea wakati tunapofanya dhambi. Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kufanywa safi, kama Yoshua alivyofanywa safi wakati alipopokea nguo mpya.

Shughuli Yamkini

  • Waruhusu watoto wapitishe kwa mzunguko shati chafu, na wasome Zekaria 3:3. Kisha wapitishe shati safi na wasome mstari wa 4. Zungumza na watoto kuhusu jinsi kufanya chaguzi mbaya ni kama kuwa mchafu kiroho, lakini Mwokozi anaweza kutufanya wasafi tena. Tunahisi vipi tunapokuwa wasafi? Shiriki ushuhuda wako kwamba kwa sababu Yesu Kristo aliteseka na kufa kwa ajili yetu, tutakuwa wasafi kutokana na dhambi pale tunapotubu.

  • Ikiwa inawezekana, waoneshe watoto picha ya mtu wanayemfahamu akiwa amevalia nguo nyeupe kwenye ubatizo wake (au ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 103, 104). Kwa nini tunavaa nguo nyeupe kwenye ubatizo wetu? Imbeni wimbo kuhusu ubatizo, kama vile “When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,103). Waalike watoto wajichore wao wenyewe wakibatizwa na kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu kubatizwa siku za mbeleni.

Zekaria 2:10; 9:9; 14:3–9

Manabii hutufundisha sisi kuhusu Yesu Kristo.

Kama vile manabii wengine wa Agano la Kale, Zekaria alitoa unabii juu ya Yesu Kristo. Unabii katika Zekaria 2:10; 9:9; 14:3–9 unawafundisha nini watoto kuhusu Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya Yesu Kristo akiingia Yerusalemu juu ya mwana punda (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.50). Waambie watoto kwamba miaka mingi kabla ya Yesu kuja duniani, Zekaria alitoa unabii kwamba Yesu Kristo angepanda mwana punda kwenda Yerusalemu kabla ya kufa kwa ajili yetu. Unaposoma Zekaria 9:9, waombe watoto waoneshe kwa kidole watu katika picha ambao “walifurahi sana” na pia wamuoneshe “Mfalme.” Mfalme ni nani? Waombe watoto kushiriki kwa nini wana shukrani kwa ajili ya Yesu.

  • Wasomee watoto baadhi ya unabii aliotoa Zekaria kuhusu Ujio wa Pili wa Mwokozi, kama vile ule ulio katika Zekaria 2:10; 14:9. Waombe watoto wachore picha ya vile wanavyodhani itakuwa wakati Yesu atakaporudi tena, au imbeni pamoja wimbo kuhusu Ujio wa Pili, kama vile “When He Comes Again” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Hagai 1:2–8

“Zitafakarini njia zenu.”

Ni muhimu kwetu sote tuwe makini na vipaumbele vyetu na kutenga muda “kuzitafakari njia [zetu].” Ni jinsi gani unaweza kuwashawishi watoto watenge muda katika maisha yao kwa ajili ya manbo ya Mungu?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wasome Hagai 1:2–5 kutafuta kwa nini Bwana hakupendezwa na Waisraeli. Waombe watoto kuchagua kifungu cha maneno kutoka mstari wa 6 na kuchora picha yake. Ruhusu darasa libahatishe ni kifungu gani cha maneno kila mchoro unawakilisha. Zungumza kuhusu jinsi kutumia muda kwenye vitu tofauti na vile Bwana anavyotaka ni sawa na kula bila kushiba, kuvaa bila kupata joto na kadhalika. Kwa nini ni muhimu kutenga muda kwa ajili ya vitu ambavyo ni muhimu kwa Bwana?

  • Andika “Zitafakarini njia zenu” ubaoni (mstari wa 7). Mwalike kila mtoto atengeneze orodha ya mambo anayoweza kufanya katika siku ya kawaida, ikiwa ni pamoja na mambo ambayo Bwana ametuomba tufanye. Waombe watoto “wazitafakari njia [zao]” kwa kufikiria kile ambacho Bwana angeweza kusema ni mambo muhimu kwenye orodha yao. Ni jinsi gani tunahakikisha kwamba tunatenga muda kila siku kwa ajili ya mambo ambayo Bwana anataka tufanye?

Picha
msichana akibatizwa na mwanamume

Tunavaa nguo nyeupe kwenye ubatizo wetu kuonesha kwamba Yesu Kristo anaweza kutufanya kuwa safi pale tunapotubu dhambi zetu (ona Zekaria 3:3–4).

Zekaria 3:1–7

Kufanya na kushika maagano kunaweza kunisaidia kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Katika ono, Zekaria alimwona kuhani mkuu aliyeitwa Yoshua, ambaye alikuwa “amevaa nguo chafu sana” (Zekaria 3:3). Malaika alimpa nguo safi na kueleza kwamba hii ilikuwa ishara ya kusafishwa kutokana na maovu yake. Ungeweza kutumia ono hili kuwasaidia watoto waelewe maagano na baraka zinazohusiana na ubatizo.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Zekaria 3:1–7 na jadilini maswali kama haya: “nguo chafu” za Yoshua ziliwakilisha nini? Ni jinsi gani tunakuwa wasafi kutokana na dhambi zetu? Ni jinsi gani maagano yetu ya ubatizo hutusaidia “kwenda katika njia za [Bwana]”?

  • Siku chache kabla ya darasa, mwalike mtoto aje akiwa amejiandaa kuzungumza kuhusu ubatizo wake. Rejeeni pamoja agano tunalofanya kwenye ubatizo (ona Mafundisho na Maagano 20:37). Ni jinsi gani kutunza ahadi zetu hutusaidia kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo? Ni jinsi gani kupokea sakramenti kila wiki kunatusaidia kuyashika maagano yetu ya ubatizo?

Zekaria 9:9–11; 11:12; 13:6–7

Yesu Kristo ndiye Masiya aliyeahidiwa.

Watoto wanaweza kujifunza nini kutokana na unabii wa Zekaria kuhusu Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto waandike ukweli waliojifunza darasani. Waalike wajadili na familia zao jinsi wanavyoweza kupata ushuhuda imara wa ukweli huo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia ubunifu wako. Ruhusu mawazo katika muhtasari huu yachochee ubunifu wako mwenyewe. Fikiria kuhusu kitu ambacho watoto katika darasa lako watafurahia na kile kitakachowasaidia kupata muunganiko kati ya maandiko na maisha yao.

Chapisha