Agano la Kale 2022
Desemba 19–25. Krismasi: “Tumemngojea Yeye, na Atatuokoa”


“Desemba 19–25. Krismasi: ‘Tumemngojea Yeye, na Atatuokoa’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Desemba 19–25. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Mtoto Yesu amefunikwa na nguo nyeupe na amelala katika majani makavu

Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, na Simon Dewey

Desemba 19–25

Krismasi

“Tumemngojea Yeye, na Atatuokoa”

Manabii wa Agano la Kale walitazamia kwa shangwe kuu kuzaliwa kwa Masiya (ona Isaya 25:9). Unapojiandaa kufundisha kipindi cha msimu wa Krismasi, fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto wapate shangwe katika kuzaliwa kwa Mwokozi Yesu Kristo.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kuelezea kitu wanachojua kuhusiana na kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Wanapotaja mtu au kitu kutoka kwenye hadithi, waalike wakichore ubaoni. Waulize watoto ni kitu gani wanakipenda kuhusu hadithi hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Agano la Kale hunifundisha kuhusu Yesu.

Wasaidie watoto wafokasi kwa Mwokozi Yesu Kristo kama sababu ya kusherehekea Krismasi. Unaweza kufanya hili kwa kutumia maandiko kutoka Agano la Kale ambayo yanamshuhudia Yeye.

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya kuzaliwa kwa Yesu (kama vile Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.30, au moja ya picha katika muhtasari wa wiki hii kwenye Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Soma Isaya 9:6, ukimpa kila mtoto zamu ya kumwonesha kwa kidole mtoto Yesu pale wanaposikia kifungu cha maneno “mtoto amezaliwa.” Shiriki ushuhuda wako kwamba manabii katika Agano la Kale walijua kwamba Yesu angezaliwa.

  • Mwalike kila mtoto ataje jina lake na dokeza kwamba kwenye nyongeza ya majina yetu, tunaweza kuitwa vitu vingine, kama dada au kaka au rafiki. Waalike watoto wafikirie mifano mingine. Wasomee watoto Isaya 9:6, ukisisitiza majina yanayomrejelea Yesu Kristo: “wa Ajabu, Mshauri, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani.” Wasaidie watoto waelewe majina haya yanatuambia nini kuhusu Yesu.

  • Mpe kila mtoto nyota ya karatasi na waalike watoto wanyanyue nyota zao juu wakati ukisoma kifungu cha maneno kifuatacho kutoka Hesabu 24:17: “nyota itatokea katika Yakobo.” Waalike watoto kushiriki jinsi ambavyo Yesu ni kama nyota angavu ambayo huangaza kwa ulimwengu wote. Imbeni pamoja wimbo kuhusu nyota iliyotokea wakati Yesu alipozaliwa, kama vile “Stars Were Gleaming” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,37) au “The First Noel” (Nyimbo za Kanisa, na.213).

Yesu Kristo ni Mwokozi wangu.

Krismasi ni wakati wa kusherehekea si tu kuzaliwa kwa Yesu bali pia maisha na misheni Yake kama Mwokozi wa ulimwengu. Ni jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuhisi shangwe na shukrani kwa ajili ya Upatanisho wa Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wafikirie kitu wanachotazamia. Eleza kwamba watu waaminifu katika Agano la Kale walitazamia kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Wasomee watoto Isaya 25:9 na watake warudie kifungu cha maneno “Tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.” Waeleze kwa nini wewe unafurahi na kushangilia kwamba Kristo alizaliwa. Waalike watoto kushiriki hisia zao kuhusu Mwokozi.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu kuzaliwa kwa Yesu, kama vile “Away in a Manger” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 42–43) au “Hark! The Herald Angels Sing” (Nyimbo za Kanisa, na.209). Wasaidie watoto wagundue virai katika nyimbo hizi ambavyo vinatufundisha kuhusu Mwokozi wetu na baraka tulizonazo kwa sababu Yake.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Agano la Kale hunifundisha kuhusu Yesu Kristo, Masiya aliyeahidiwa.

Agano la Kale ni zaidi tu ya mkusanyiko wa hadithi na maandishi ya kuvutia; lengo lake, kama vile maandiko yote, ni kushuhudia juu ya Yesu Kristo. Wasaidie watoto wajifunze jinsi ya kumtafuta Yeye katika Agano la Kale.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto watengeneze orodha ya majina na vichwa vya habari vyote vya Yesu Kristo wanavyoweza kupata katika Musa 7:53; Zaburi 23:1; Ayubu 19:25; Isaya 7:14; 9:6; 12:2; Amosi 4:13; na Zekaria 14:16. Waruhusu wafanye kazi katika jozi ikiwa watapenda. Waalike kushiriki orodha yao wao kwa wao. Je, tunajifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwenye kila moja ya majina na vichwa hivi vya habari?

  • Waoneshe watoto baadhi ya mapambo ya Krismasi (au picha za mapambo), kama vile nyota, mianga au zawadi. Waulize watoto jinsi kila moja ya vitu hivi kinavyoweza kutukumbusha juu ya Mwokozi. Eleza kwamba maandiko daima hutumia ishara kutufundisha kuhusu Yesu Kristo. Waalike watoto watazame moja au zaidi ya mistari ifuatayo ili kupata kitu ambacho kinaweza kuwa ishara ya Yesu Kristo: Mwanzo 22:8; Kutoka 17:6; Zaburi 18:2; 27:1 (ona muhtasari wa wiki hii kwenye Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa mifano zaidi). Ni jinsi gani Yesu ni kama mwana kondoo, maji, mwamba, ngome au nuru?

  • Mwisho wa kujifunza Agano la Kale mwaka huu, waalike watoto kushiriki hadithi au maandiko yao pendwa kutoka Agano la Kale. Je, hadithi au maandiko haya hutufundisha nini kuhusu Yesu Kristo? Kwa nini sisi ni wenye shukrani kwa kuwa na Agano la Kale?

Yesu Kristo ni Mwokozi na Mkombozi wangu.

Tunaposherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo, tunaweza pia kusherehekea katika maisha na dhabihu Yake ya kulipia dhambi. Ni jinsi gani unaweza kutumia maandiko kutoka Agano la Kale kuwasaidia watoto kujenga imani yao katika Mwokozi na Mkombozi wao?

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Isaya 7:14; kisha waalike watoto kushiriki kile wanachofahamu kuhusu kuzaliwa kwa Kristo. Au onesha video “The Nativity” (ChurchofJesusChrist.org), na mwalike kila mtoto achague mtu kutoka kwenye video na ashiriki jinsi ambavyo yawezekana mtu huyo alihisi. Shiriki ushuhuda wako kuhusu Mwokozi na waalike watoto wafanye hivyo pia.

  • Ili kuwasaidia watoto waelewe vyema zaidi jukumu la Yesu Kristo kama Mwokozi wetu, waalike wasome Isaya 25:8–9; 53:3–5; na Hosea 13:14. Je, maandiko haya yanatufunza nini kuhusu jinsi Bwana anavyotuokoa? Ni jinsi gani sisi “tunashangilia wokovu wake”? (Isaya 25:9).

  • Imbeni wimbo pamoja kuhusu upendo wa Yesu Kristo kwetu sisi, kama vile “Away in a Manger” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 42–43) au “I Stand All Amazed” (Kitabu cha Nyimbo za Kanisa, na.193). Waalike watoto kushiriki vifungu vya maneno ambavyo vinawasaidia wao kuhisi upendo wa Mwokozi.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki na familia zao au rafiki jambo walilojifunza kuhusu Yesu Kristo kutoka katika Agano la Kale. Wahimize waanze kusoma Agano Jipya wiki hii.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tengeneza mazingira ambayo yanamwalika Roho. Kuna njia nyingi unaweza kumwalika Roho katika darasa lako. Muziki unaweza kuhimiza unyenyekevu. Kuelezea upendo na ushuhuda kunaweza kutengeneza mazingira mazuri ya kiroho. Kwa sala fikiria jambo unaloweza kufanya ili kutengeneza mazingira ya kiroho katika darasa lako. (Ona Kufundisha katika njia ya Mwokozi,15.)

Chapisha