Agano la Kale 2022
Desemba 12–18. Malaki: “Nimewapenda Ninyi, Asema Bwana”


“Desemba 12–18. Malaki: ‘Nimewapenda Ninyi, Asema Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Desemba 12–18. Malaki,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Sanamu ya Christus

Desemba 12–18

Malaki

“Nimewapenda Ninyi, Asema Bwana”

Bwana anawapenda watoto unaowafundisha. Ni jinsi gani utawasaidia watoto wauone upendo Wake wakati unapofundisha mafundisho yanayopatikana katika kitabu cha Malaki?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Soma kifungu cha maneno kifuatacho kutoka Malaki 1:2: “Nimewapenda ninyi, asema Bwana” Mwalike kila mtoto ashiriki njia moja wanayojua kwamba Bwana anawapenda. Baada ya kila mtoto kushiriki, mshukuru na shiriki ushuhuda wako wa upendo wa Bwana kwa mtoto yule.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Malaki 3:10–12

Baba wa Mbinguni atanibariki ninapolipa zaka.

Hata kama watoto wadogo unaowafundisha bado hawana pesa, bado wanaweza kujifunza kuhusu baraka za kulipa zaka.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto wahesabu vitu vidogo vidogo10, kama vile sarafu zilizo kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Waalike watenge moja ya vitu kutoka kwenye vingine na eleza kwamba hiki ni kama zaka tunayompa Bwana. Tunampa moja ya kumi ya kile tunachopokea. Toa ushuhuda wako wa jinsi ambavyo Mwokozi anatubariki wakati tunapolipa zaka. Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu zaka, kama vile “I Want to Give the Lord My Tenth” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,150).

  • Chora dirisha ubaoni na usome Malaki 3:10 kwa watoto. Waalike waoneshe dirisha kwa kidole wakati unaposoma kifungu cha maneno “madirisha ya mbinguni.” Elezea kwamba hii inamaanisha kwamba Baba wa Mbinguni hutupatia baraka nyingi tunapolipa zaka. Wakati watoto wakipaka rangi ukurasa wa shughuli ya wiki hii, zungumza kuhusu baadhi ya sababu za kwa nini tunalipa zaka.

  • Shiriki hadithi kutoka gazeti la Rafiki au kutoka kwenye maisha yako mwenyewe kuhusu kulipa zaka. Waalike watoto wasikilize baraka ambazo zinaweza kuja kutokana na kulipa zaka.

Malaki 4:5–6

Tunaunganishwa kama familia ndani ya hekalu.

Kwa sababu ya funguo za ukuhani za kuunganisha ambazo Eliya alimpa Joseph Smith ndani ya Hekalu la Kirtland, familia zinaweza kuungana milele. Unapofundisha ukweli huu, kuwa makini na hisia za watoto ambao familia zao hazijaunganishwa hekaluni.

Shughuli Yamkini

  • Soma Malaki 4:5 kwa watoto. Kisha waambie kwamba ahadi hii ilitimizwa wakati Eliya alipomtokea Joseph Smith ndani ya Hekalu la Kirtland (ona “Sura ya 40: Maono ndani ya Hekalu la Kirtland,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano,157). Onesha picha ya tukio hili (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.95), na waalike watoto wawaoneshe kwa kidole Eliya na Joseph Smith. Eleza kwamba kwa sababu Eliya alikuja, tunaweza kuunganishwa kama familia hekaluni. Shiriki ushuhuda wako wa umuhimu wa kuunganishwa kama familia.

  • Waambie watoto kuhusu upendo wako kwa familia yako; onesha picha, kama inawezekana. Waalike baadhi ya watoto kueleza hisia zao juu ya familia zao. Imbeni pamoja wimbo kuhusu familia, kama vile “Families Can Be Together Forever” (Nyimbo za Kanisa, na.300), na shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni anataka familia ziunganishwe pamoja na kwamba hii ni moja ya sababu za sisi kuwa na mahekalu. Wasaidie watoto waelewe kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, tunaweza hata kuunganishwa na wanafamilia ambao hawakuweza kwenda hekaluni katika maisha haya. Waalike watoto wachore picha ya familia zao pamoja wakiwa mbinguni.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Malaki 3:8–12

Baba wa Mbinguni atanibariki ninapolipa zaka.

Kulipa zaka ni zaidi kuhusu kuwa na imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kuliko kuhusu pesa. Watoto unaowafundisha wanaelewa nini kuhusu zaka? Ni jinsi gani utawasaidia kuwa na imani ya kulipa zaka?

Shughuli Yamkini

  • Andika ubaoni maswali kuhusu zaka kama yafuatayo: Zaka ni nini? Ni jinsi gani ninalipa zaka? Zaka ni kwa ajili ya nini? Ni zipi baraka za kulipa zaka? Waalike watoto watafiti Malaki 3:8–12 na “Zaka, Kulipa Zaka” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org) na waandike majibu wanayopata. Waalike kushirikiana majibu yao wao kwa wao. Tunakuwa watu wa namna gani kwa kulipa zaka?

  • Onesha video “Jesus Teaches about the Widow’s Mite” (ChurchofJesusChrist.org), au someni pamoja Marko 12:41–44. Hadithi hii inatufundisha kuhusu jinsi Bwana anavyohisi kuhusu matoleo yetu?

  • Chora dirisha ubaoni na waalike watoto kuandika ndani ya dirisha baraka ambazo mtu anaweza kupokea kwa kulipa zaka (kwa mawazo, ona Malaki 3:10–12). Waalike watoto kushiriki mfano binafsi wa jinsi ambavyo wao au familia zao wamebarikiwa kutokana na kulipa zaka kwa uaminifu. Au unaweza kushiriki mfano kutoka kwenye maisha yako binafsi wa jinsi kulipa zaka kulivyoongeza imani yako katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Eliya akiwatokea Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Hekalu la Kirtland

Kielelezo cha Eliya akimtokea Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Hekalu la Kirtland, na RobertT. Barrett

Malaki 4:5–6

“Nitawapelekea Eliya nabii.”

Unabii wa Malaki kuhusu Eliya nabii ulitimizwa wakati Eliya alipomtokea Joseph Smith ndani ya Hekalu la Kirtland na kumpa funguo za ukuhani zinazoruhusu familia kuunganishwa pamoja milele. Unaweza kufikiria kumwalika mtu katika kata aliye na jukumu la kazi ya hekalu na historia ya familia (kama vile mshiriki wa urais wa akidi ya wazee au urais wa Muungano wa Usaidizi) ili akusaidie kufundisha mafundisho haya kwa watoto. Kumbuka kuwa makini kwenye hisia za watoto ambao familia zao hazijaunganishwa.

Shughuli Yamkini

  • Andika kila kifungu cha maneno kutoka Malaki 4:5–6 kwenye vipande tofauti vya karatasi. Wape watoto vipande vya karatasi na waombe waweke vifungu hivyo katika mpangilio sahihi. Someni mistari pamoja na mjadili maswali kama haya: Bwana aliahidi kumtuma nani? Yeye alisema mtu huyu angekuja lini? Bwana alisema kwamba mtu huyu angefanya nini? Kwa nini mtu huyu alihitajika kuja? Unabii huu ulitimizwa wapi? (ona Mafundisho na Maagano 110:13–16).

  • Andika ubaoni maswali kama Inamaanisha nini kwa mioyo ya watoto kuwageukia baba zao? (Ona Malaki 4:6). Waalike watoto watafakari swali hili wakati wakitazama video “Their Hearts Are Bound to You” (ChurchofJesusChrist.org). Kisha waalike watoto kushiriki mawazo yao kuhusu maswali ubaoni. Jadilini pamoja uzoefu ambao wewe au watoto mmekuwa nao kwa kujifunza kuhusu historia ya familia.

  • Onesha picha ya Eliya kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu tukio linaloelezewa na picha hii (ona pia Mafundisho na Maagano 110:13–16) Shuhudia kwamba nguvu ya kuunganisha iliyorejeshwa na Eliya inaruhusu familia kuwa pamoja milele—ikiwa ni pamoja na familia ambazo hazikupata fursa hiyo katika maisha ya duniani. Ikiwa umeshiriki kwenye ibada ya kuunganisha, iwe kwa ajili yako au kwa ajili ya mtu aliyekufa, zungumza kuhusu kile ulichojisikia wakati wa ibada hiyo. Waombe watoto kushiriki hisia zao kuhusu familia zao na kuhusu mpango wa Mungu kusaidia familia kuwa pamoja milele.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto wafikirie juu ya kitu kimoja walichojifunza wakati wa darasa leo na waombe watoto wachache waelezee. Wahimize watoto wote kushiriki na familia zao jambo walilojifunza kuhusu mafundisho ya Malaki.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Washirikishe watoto katika majadiliano ya injili. Unaweza kutaka kufikiria juu ya njia za ubunifu za kuwashirikisha watoto wadogo katika majadiliano ya injili. Kwa mfano, watoto wanaweza kupitisha mpira kwa mzunguko na kushiriki majibu yao kwa swali ulilouliza wakati wanapokuwa wameshikilia mpira.