“Novemba 28–Desemba4. Nahumu; Habakuki; Sefania: ‘Miendo Yake Ilikuwa Kama Siku za Kale’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)
“Novemba 28–Desemba4. Nahumu; Habakuki; Sefania,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022
Novemba 28–Desemba4
Nahumu; Habakuki; Sefania
“Miendo Yake Ilikuwa Kama Siku za Kale”
Upendo wako wa maandiko unaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa watoto unaowafundisha. Waruhusu waone jinsi ulivyo na shukrani kwa ajili ya neno la Mungu.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waruhusu watoto wafanye zamu kusimama na kujifanya kuwa nabii wa Agano la Kale aliyesimama “juu ya mnara” kama Habakuki (Habakuki 2:1). Waombe wawaambie watoto wengine jambo wanalojifunza kuhusu Yesu Kristo na injili Yake.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Bwana daima atatimiza ahadi Zake.
Nabii Habakuki alihuzunishwa na uovu aliouona miongoni mwa watu wa Yuda (ona Habakuki 1:2–4). Bwana alimhakikishia kwamba ahadi Zake zingetimizwa katika wakati Wake (ona Habakuki 2:3).
Shughuli Yamkini
-
Shiriki baadhi ya mifano ya mambo ambayo ni mazuri lakini ni mpaka pale tu tunapokuwa tumesubiri—kama tunda linalohitaji kuiva au kinyunya kinachohitaji kuokwa. Ni nini kitatokea ikiwa tutajaribu kula tunda au kinyunya kabla havijawa tayari? Zungumza kuhusu nabii Habakuki, ambaye alitaka kujua ni lini Bwana angezuia uovu aliouona ukimzunguka. Wasomee watoto jibu la Bwana, linalopatikana katika Habakuki 2:3. Sisitiza kwamba Habakuki alipaswa kusubiri ahadi za Bwana zitimizwe, kama ambavyo sisi wakati mwingine tunapaswa kufanya. Shiriki wakati ambapo ulipaswa kusubiri baraka.
-
Wasaidie watoto wafikirie mambo ambayo Mungu ameahidi—kwa mfano, kwamba Yesu Kristo atarudi duniani au kwamba tunaweza kuishi na Mungu tena. Kwa kila mfano, waalike watoto warudie kirai “ingojee; kwa kuwa hakika itakuja.”
Ninaweza kuijaza dunia kwa ufahamu wa Yesu Kristo.
Habakuki alitoa unabii wa siku ambapo ulimwengu wote utajua kuhusu Yesu Kristo. Unabii huo unaanza kutimizwa katika siku yetu. Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuwa sehemu ya utimizwaji wake.
Shughuli Yamkini
-
Weka jagi tupu na mpe kila mtoto kitu kidogo. Muombe kila mtoto ashiriki jambo ambalo Yesu alifanya au kufundisha na kisha waweke kitu chao ndani ya jagi. Soma kwa sauti Habakuki 2:14, na eleza kwamba kama vile watoto walivyojaza jagi kwa ufahamu wao juu ya Bwana, sisi pia tunaweza kuujaza ulimwengu kwa ufahamu Wake.
-
Waoneshe watoto ramani ya ulimwengu (ona Ramani za Historia ya Kanisa, na.7, “Ramani ya Ulimwengu”). Wasaidie watafute mahali ambapo wanaishi na mahali ambapo wamisionari wanaowafahamu wamehudumu. Toa ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni anataka watu wote kote duniani kumjua Yesu Kristo. Ni jinsi gani tunaweza kusaidia kuwafundisha watu wengine kuhusu Yesu? Waambie watoto kuhusu mambo ambayo umewaona wakifanya ambayo yanakufundisha kuhusu Yesu Kristo. Wasaidie wafikirie juu ya mambo mengine wanayoweza kufanya.
-
Imbeni pamoja wimbo kuhusu kushiriki injili, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,168). Ni kipi tunaweza kuwaambia wengine kuhusu Yesu Kristo? Kwa baadhi ya mawazo, ona Makala za Imani.
“Mtafuteni Bwana.”
Sefania alifundisha kwamba tunapaswa kumtafuta Bwana wakati wa kipindi cha maovu mengi, kama vile katika siku hizi za mwisho. Tafakari jinsi utakavyowashawishi watoto kumtafuta Yeye.
Shughuli Yamkini
-
Onesha picha ya Yesu na wasomee watoto Sefania 2:3. Waalike wakunje mikono yao kuzunguka jicho kama vile miwani na kutazama picha kila mara unaposoma neno “tafuta.” Eleza kwamba nabii Sefania aliwataka watu wamtafute Bwana. Ni jinsi gani tunamtafuta Bwana? Ni wapi tunaweza kumpata?
-
Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii, au fikiria mchezo mwingine ambao unawahimiza watoto kumtafuta Bwana. Chezeni au imbeni pamoja wimbo unaohusiana na mada hii, kama vile “Seek the Lord Early” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,108). Jadilini wimbo unafundisha nini kuhusu jinsi tunavyoweza kumtafuta Yesu Kristo katika maisha yetu.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
“Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu.”
Kila mmoja wetu anakabiliana na “siku yake ya taabu yeye mwenyewe.” Ni jinsi gani utawasaidia watoto kumgeukia Bwana, “kumtumaini Yeye,” na kupata usalama wa kiroho katika siku zao za taabu?
Shughuli Yamkini
-
Waoneshe watoto picha ya ngome. Ni zipi baadhi ya sababu za watu kuhitaji ngome? Waalike watoto wasome Nahumu 1:7 ili kutafuta kile nabii Nahumu alichosema kuwa ni kama ngome kwa ajili yetu. Mwokozi anaweza kutulinda sisi kutokana na nini?
-
Waalike watoto wajichore picha zao wenyewe na familia zao ndani ya ngome. Waalike waandike maneno kuzunguka ngome ambayo yanafafanua baadhi ya ushawishi mwovu katika ulimwengu. Waalike waandike maneno ndani ya ngome ambayo yanamwelezea Yesu Kristo. Yeye anatuomba tufanye nini ili kupokea nguvu na ulinzi Wake? (ona Mafundisho na Maagano 35:24).
Ninaweza kuwa na shangwe katika Yesu Kristo, hata kama mambo hayaendi vizuri.
Habakuki alielezea baadhi ya majaribu ambayo yangeweza kutokea kwa watu wake, ikiwa ni pamoja na miti au mizabibu ambayo haikuzaa matunda. Kisha alisema kwamba hata ikiwa mambo haya yangetukia, “walakini nitamfurahia Bwana.”
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto wasome Habakuki 3:17 na bainisha majaribu yaliyoelezwa katika mstari huu. Yawezekana mtu angehisi vipi kama mambo haya yangetokea? Wasaidie watoto wafikirie majaribu ambayo yangeweza kutokea kwao. Kisha someni pamoja mistari 18–19 ili kujifunza jinsi Habakuki alivyosema angehisi hata ikiwa mambo haya yangetokea kwake.
-
Wasaidie watoto watafute mifano mingine ya watu katika maandiko ambao walipata shangwe kwa Bwana hata katika nyakati ngumu. Wanaweza kupata mifano katika Matendo ya Mitume 16:19–25; Mosia 24:10–15; na ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Kushukuru kwa Kila Hali” (Liahona, Mei 2014, 70–77), hususan kipengele cha “Kushukuru kwa Hali Zetu.” Kwa nini watu hawa waliweza kuwa na shangwe katika nyakati ngumu? Ni jinsi gani tunaweza kufuata mifano yao?
Wale wanaomfuata Yesu Kristo watapata amani na shangwe.
Sefania 3:14–20 inaelezea siku ya shangwe wakati Yesu Kristo, “mfalme wa Israeli,” atakapotawala miongoni mwa watu Wake na “kutushangilia [sisi] kwa kuimba” (mistari 15,17).
Shughuli Yamkini
-
Someni pamoja Sefania 3:14. Kisha mwalike kila mtoto achague moja ya mistari katika Sefania 3:15–20 na wausome, wakitafuta jambo linaloweza kutusaidia “kushangilia kwa furaha.” Waalike kushiriki kile wanachopata.
-
Wasaidie watoto kupata nyimbo za kanisa au nyimbo za watoto zinazowasaidia “kufurahi na kushangilia kwa moyo wote” (Sefania 3:14). Imbeni nyimbo kadhaa kwa pamoja na wahimize watoto wazungumzie shangwe wanayopata katika injili ya Yesu Kristo.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waombe watoto waandike rejeleo kwenye maandiko ambayo wanataka kuyashiriki na familia zao (au waandikie rejeleo hilo).