Njoo, Unifuate
Januari 20–26. 1 Nefi 11–15: “Kujilinda kwa Utakatifu na kwa nguvu za Mungu”


“Januari 20–26. 1 Nefi 11–15: ‘Kujilinda kwa Utakatifu na kwa nguvu za Mungu” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Januari 20–26. 1 Nefi 11–15,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

watu wakila tunda la mti wa uzima

Tamu Zaidi Kuliko Utamu Wote, na Miguel Ángel González Romero

Januari 20–26

1 Nefi 11–15

“Kujilinda kwa Utakatifu na kwa nguvu za Mungu”

Anza maandalizi yako ya kufundisha kwa kusoma 1 Nefi 11–15. Andika mawazo yako na misukumo kuhusu vifungu na kanuni utakazowatia moyo washiriki wa darasa kujadili. Mawazo yaliyopo hapo chini yanaweza kusaidia.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Sura hizi zina kanuni ambazo washiriki wa darasa wanaweza kutaka kuzingatia wakati wanaposhiriki injili na wengine. Fikiria kuandika maswali kama yafuatayo ubaoni na kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki vitu walivyovipata katika kusoma kwao wiki hii ambavyo vinaweza kusaidia kujibu maswali haya:

  • Nini maana ya Ukengeufu na Urejesho?

  • Kwa nini Kitabu cha Mormoni ni muhimu?

  • Ninawezaje kujua kweli za Mungu kwa ajili yangu mwenyewe?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

1 Nefi 11:1–5, 13–33

Mungu alimtuma Yesu Kristo kama dhihirisho la upendo Wake.

  • Malaika alimwonyesha Nefi ishara na matukio kutoka kwenye maisha ya Mwokozi ambayo yalidhihirisha upendo wa Mungu. Yaweza kuwa yenye msaada kuchunguza ishara hizi na matukio kama darasa na kujadili jinsi yanavyodhihirisha upendo wa Mungu kwetu. Je, kuna picha zozote, video, au vielelezo vingine ungeweza kuonesha ambavyo vinaelezea kwa michoro baadhi ya matukio katika mistari hii? (ona, kwa mfano, biblevideos.ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa jinsi gani maisha ya Mwokozi na Upatanisho Wake vinakusaidia kuelewa upendo wa Mungu kwa ajili yako?

1 Nefi 12–15

Mungu atatusaidia kupinga ushawishi wa Shetani.

  • Washiriki wa darasa lako wakati mwingine wanaweza kuhisi kama watu katika ono la Nefi ambao walikuwa wanatangatanga katika ukungu wa giza au kukabiliana na dhihaka ya wale walio katika jengo kubwa na pana. Ungeweza kuuliza darasa kwa nini ukungu wa giza ni ishara nzuri kwa majaribu (ona 1 Nefi 12:17) na kwa nini jengo kubwa na pana ni ishara nzuri kwa mawazo yasiyofaa na kiburi cha ulimwengu (ona 1 Nefi 12:18). Kisha ungeweza kugawa sura ya 12–15 miongoni mwa washiriki wa darasa na waalike kutafuta mistari ambayo inafundisha jinsi Mungu atakavyotusaidia kushinda majaribu, majivuno, na kiburi (ona, kwa mfano, 1 Nefi 13:34–40; 14:14).

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa vyema nguvu ambayo inakuja kutokana na neno la Mungu? (ona 1 Nefi 15:24). Ungeweza kuwaalika kujadili maswali kama yafuatayo: Nefi alijifunza nini kuhusu nguvu ya neno la Mungu? Ni kwa jinsi gani Shetani anajaribu kudhoofisha neno la Mungu ? (ona 1 Nefi 13:26–29). Bwana na manabii Wake walifanya nini ili kulihifadhi neno Lake? Kama sehemu ya majadiliano yenu, ungeweza kuwaomba washiriki wachache wa darasa kushiriki jinsi wanavyojifunza maandiko na nini wanafanya kulifanya neno la Mungu sehemu ya maisha yao ya kila siku.

1 Nefi 13

Bwana alitayarisha njia kwa ajili ya Urejesho wa Kanisa Lake.

  • Labda mpangilio wa muda ungeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa ono la Nefi la matukio ya Urejesho. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kutengeneza mmoja ubaoni, unaojumuisha matukio wanayoyapata yaliyoelezwa katika 1 Nefi 13. Yapi kati ya matukio haya tayari yamekwishatokea? Yapi yanatokea sasa? Fikiria kushiriki dondoo katika “Nyenzo za Ziada” na George Washington, rais wa kwanza wa Marekani, ambayo inaonesha kwamba alitambua ushawishi wa Mungu katika Mapinduzi ya Marekani, tukio ambalo lilitayarisha njia kwa ajili ya Urejesho.

  • Ni kwa jinsi gani washiriki wa darasa wangetumia 1 Nefi 13 kumwelezea mtu fulani wa imani nyingine kwa nini Urejesho ulikuwa muhimu? (Kwa mfano, ona 1 Nefi 13:26–29, 35–42). Ni maandiko gani mengine washiriki wa darasa wangeweza kutumia kuwasaidia wengine kuelewa kwa nini Urejesho ulikuwa muhimu? (Kwa baadhi ya mifano, ona Mwongozo wa Mada, “Urejesho wa Injili”). Washiriki wa darasa wangeweza kunufaika kutokana na kuigiza jinsi watakavyoelezea kwa mtu fulani haja ya Urejesho na jinsi ulivyowabariki.

1 Nefi 13:20–41

Kitabu cha Mormoni kinafundisha kweli za wazi na zenye thamani kubwa.

  • Inaweza kusaidia kutumia 1 Nefi 13:20–41 kuanza majadiliano kuhusu kwa nini tunahitaji Kitabu cha Mormoni. Washiriki wa darasa wangeweza kuorodhesha baadhi ya “vitu vilivyo wazi na vyenye thamani” ambavyo vilipotea kutoka kwenye Biblia na kurejeshwa kupitia Kitabu cha Mormoni (kwa baadhi ya mifano, ona mistari 26 na 39 au orodha katika “Nyenzo za Ziada”). Ungeweza pia kutaka kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki jinsi hivi “vitu vilivyo wazi na vyenye thamani” vilivyorejeshwa vilivyowasaidia kuwa karibu zaidi na Mungu.

    familia ikisoma maandiko

    Roho anaweza kutusaidia kugundua “kweli za wazi na zenye thamani” kwa ajili yetu wenyewe.

  • Fikiria kuonesha video “Kitabu cha Mormoni—Kitabu kutoka kwa Mungu” (ChurchofJesusChrist.org), na waalike washiriki wa darasa kushiriki kile video hii inachofundisha kuhusu kwa nini tunahitaji Kitabu cha Mormoni. Au ungeweza kumwalika mshiriki wa darasa kuchora ubaoni kielelezo kilichoelezwa katika dondoo ya Mzee Tad R. Callister katika “Nyenzo za Ziada.” Washiriki wa darasa kisha wangeweza kushiriki jinsi Kitabu cha Mormoni kilivyowasaidia kuelewa vyema injili ya Yesu Kristo.

    2:3
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma 1 Nefi 16–22 wakati wa wiki ijayo, ungeweza kutaja kwamba ina maelezo ambayo yanaweza kuwavutia na kuwasaidia wakati wanapotakiwa kufanya kitu fulani ambacho kinaonekana hakiwezekani.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Video za Kitabu cha Mormoni.

Tafuta video ambazo zinaonesha kwa michoro matukio kutoka 1 Nefi 11–15 Katika mkusanyiko wa video za Kitabu cha Mormoni kwenye ChurchofJesusChrist.org au Gospel Library app.

Mkono wa Mungu katika Mapinduzi ya Marekani.

George Washington alisema: “Mtu ni lazima awe mbaya kweli kweli ikiwa anaweza kuangalia matukio ya Mapinduzi ya Merekani bila ya kuhisi shukrani za dhati juu ya Muumbaji Mkuu wa Ulimwengu ambaye uamuzi Wake mtakatifu ulidhihirika mara kwa mara kwa niaba yetu” (Barua kwa Samuel Langdon, Sept. 28, 1789, founders.archives.gov/Washington/05-04-02-0070).

Orodha ya Rais Russell M. Nelson ya kitabu cha Mormoni.

Kutoka “Kitabu cha Mormoni: Maisha Yako Yangekuwaje Bila Hicho?” (Ensign au Liahona, Nov. 2017, 60–63).

Kitabu cha Mormoni kinakanusha dhana za kwamba:

  • Ufunuo uliishia kwenye Biblia.

  • Watoto wachanga wanahitaji kubatizwa.

  • Furaha inaweza kupatikana katika uovu.

  • Wema wa mtu binafsi unatosha kwa ajili ya kuinuliwa (ibada na maagano vinahitajika).

  • Kuanguka kwa Adamu kuliwatia doa wanadamu kwa “dhambi ya asili.”

Kitabu cha Mormoni kinafafanua uelewa kuhusu:

  • Maisha yetu kabla ya kuzaliwa.

  • Kifo. Ni sehemu muhimu ya mpango mkuu wa furaha wa Mungu.

  • Maisha baada ya kifo, yanayoanzia paradiso.

  • Jinsi kufufuka kwa mwili, kuunganika tena na roho yake, kunakuwa nafsi isiyokufa.

  • Jinsi hukumu yetu itakayotolewa na Bwana itakavyokuwa kulingana na matendo yetu na matamanio ya mioyo yetu.

  • Jinsi gani ibada zinafanywa kwa usahihi: kwa mfano, ubatizo, sakramenti, kutunuku kipawa cha Roho Mtakatifu.

  • Upatanisho wa Yesu Kristo

  • Ufufuo.

  • Jukumu muhimu la malaika.

  • Asili ya milele ya ukuhani.

  • Jinsi tabia ya mwanadamu inavyoshawishiwa zaidi na nguvu ya neno kuliko nguvu ya upanga.

Tunahitaji Kitabu cha Mormoni.

Mzee Tad R. Callister alifundisha:

“Biblia ni shahidi mmoja wa Yesu Kristo, Kitabu cha Mormoni ni mwingine. Kwa nini huyu shahidi wa pili ni muhimu hivyo? Mchoro ufuatao unaweza kusaidia: Unaweza kuchora mistari mingapi iliyonyooka kupitia kituo kimoja kwenye kipande cha karatasi? Jibu ni bila kikomo. Kwa muda, tuseme kituo hicho kimoja kinawakilisha Biblia na kwamba mamia ya mistari hiyo iliyonyooka iliyochorwa kupitia kituo hicho inawakilisha tafsiri tofauti za Biblia na kwamba kila moja ya tafsiri hizo inawakilisha kanisa tofauti.

“Nini kinatokea, kwa upande mwingine, kama kwenye kipande hicho cha karatasi kuna kituo kingine kinachowakilisha Kitabu cha Mormoni? Mistari mingapi iliyonyooka ungeweza kuchora kati ya pointi hizi mbili za rejeleo: Biblia na Kitabu cha Mormoni? Mmoja tu. Tafsiri moja tu ya mafundisho ya Kristo inaupa uhai ushuhuda wa mashahidi hawa wawili” (“Kitabu cha Mormoni—Kitabu kutoka kwa Mungu,” Ensign au Liahona, Nov. 2011, 75).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ongoza Majadiliano Yenye Maongozi. Kila mtu ana jambo la kuchangia kwenye majadiliano ya darasa, lakini mara nyingi si kila mtu anapata nafasi. Tafuta njia za kuongeza nafasi za washiriki wa darasa kuweza kushiriki shuhuda zao. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 33.)