Njoo, Unifuate
Desemba 30–Januari 5. Kurasa za utambulisho wa Kitabu cha Mormoni: “Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo”


Desemba 30–Januari 5. Kurasa za utangulizi wa Kitabu cha Mormoni: ‘Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo”. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)

Desemba 30–Januari 5. Kurasa za utangulizi wa Kitabu cha Mormoni,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
mabamba ya dhahabu.

Desemba 30–Januari 5

Kurasa za utangulizi wa Kitabu cha Mormoni

“Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo”

Jifunze ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni na utambulisho; shuhuda za Mashahidi Watatu, Mashahidi Wanane, na Nabii Joseph Smith; na “Muhtasari wa maelezo kuhusu Kitabu cha Mormoni.” Unapofanya hivi, tafuta ushawishi kutoka kwa Roho Mtakatifu kuhusu jinsi unavyoweza kuwatia moyo washiriki wa darasa lako kuanza mafunzo ya maana ya kitabu cha Mormoni.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Kwa kuanza, unaweza kualika watu wachache kushiriki kitu fulani walichojifunza kutoka kurasa za utangulizi za Kitabu cha Mormoni ambacho kiliongeza ushuhuda wao wa kitabu hiki kitakatifu.

Picha
ikoni ya kufundishia

Fundisha Mafundisho

Ukurasa wa Jina wa Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni kinaweza kuimarisha imani yetu katika Yesu Kristo.

  • Kusoma ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni, ulioandikwa na Moroni, kunaweza kuwaandaa washiriki wa darasa lako kujifunza Kitabu cha Mormoni mwaka huu. Jumbe kwenye ukurasa wa jina zinawezaje zikaboresha kijufunza kwao? Labda unaweza kuandika swali moja au zaidi ubaoni—kama vile Kwa nini tuna Kitabu cha Mormoni? Au Jinsi gani Kitabu cha Mormoni ni tofauti na vitabu vingine?—na waalike washiriki wa darasa watafute majibu wanaporudia upya ukurasa wa jina binafsi au wawili wawili. Kisha wanaweza kushiriki misukumo ambayo inawajia. Unaweza pia kuwahimiza washiriki wa darasa kujadili mipango yao kwa ajili ya kujifunza Kitabu cha Mormoni mwaka huu. Kwa mfano, watakuwa wanatafuta nini? Watajifunza vipi kutoka kwa Roho Mtakatifu wanapojifunza?

  • “Mojawapo ya madhumuni makuu ya Kitabu cha Mormoni, kama ilivyoandikwa katika ukurasa wake wa jina, kuwathibitishia “Myahudi na Myunani kwamba Yesu ndiye Kristo,” Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki vifungu kutoka Kitabu cha Mormoni ambavyo vimeimarisha imani yao katika Yesu Kristo (wanaweza pia kusoma vifungu vichache vilivyoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada”). Washiriki wa darasa wanaweza kusoma baadhi ya aya hizi pamoja na mtu aliyekaa karibu nao na kushiriki jinsi Kitabu cha Mormoni kilivyoshawishi ushuhuda wao wa Mwokozi.

Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni kinaweza kutusaidia “kumkaribia zaidi Mungu.”

  • Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni unatoa taarifa ambayo ni muhimu kwa wasomaji kuelewa. Washiriki wa darasa lako wanaweza kunufaika kutokana na kuchunguza utangulizi na kuyatambua mambo matatu hata matano ambayo yataweza kusaidia kushiriki pamoja na mtu fulani anayesoma Kitabu cha Mormoni kwa mara ya kwanza. Washiriki wa darasa kisha wanaweza kushiriki kile wanachokipata. Wanaweza hata kutaka kuigiza kukitambulisha Kitabu cha Mormoni kwa mtu fulani. Video zilizopendekezwa katika “Nyenzo za ziada” zinaweza pia kusaidia.

  • Baadhi ya washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa walikuwa na uzoefu ambao ulithibitisha ukweli wa maneno ya Joseph Smith: “Mtu angeweza kumkaribia zaidi Mungu kwa kuzingatia mwongozo wa [Kitabu cha Mormoni], kuliko kitabu kingine chochote.” Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki jinsi kuishi kweli walizojifunza katika Kitabu cha Mormoni kumewasaidia kumkaribia zaidi Mungu. Unaweza pia kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki majibu kwa maswali haya matatu yaliyopendekezwa na Rais Russell M. Nelson: “Kwanza, maisha yako yangekuwaje bila Kitabu cha Mormoni? Pili, nini ungeweza kutokujua? Na tatu, nini ungeweza kuto kuwa nacho?” (“Kitabu cha Mormoni: Maisha Yako Yangekuwaje Bila hicho?” (Ensign au Liahona, Nov. 2017, 61).

  • Kuna yeyote katika darasa lako aliyesoma vifungu katika Kitabu cha Mormoni ambavyo vina majina tofauti kwa ajili ya mpango wa wokovu, kama ilivyopendekezwa katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia? Kama ndivyo, waalike washiriki kile walichojifunza.

Ushuhuda wa Mashahidi Watatu”; “Ushuhuda wa Mashahidi Wanane

Tunaweza sote kuwa mashahidi wa Kitabu cha Mormoni.

  • Kujifunza Ushuhuda wa Mashahidi Watatu na Wanane kunaweza kuimarisha shuhuda za washiriki wa darasa lako na kuwasaidia kutafakari jinsi wanavyoweza kushiriki ushahidi wao wenyewe. Unaweza kuwataka nusu ya darasa wasome “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” na nusu ingine kusoma “Ushuhuda wa Mashahidi Wanane” na kushiriki misukumo au undani ambao unaonekana wazi kwao. Shuhuda hizi mbili ni tofauti kwa jinsi gani? Zinafanana vipi? Tunajifunza nini kutoka kwa mashahidi hawa kuhusu kushiriki shuhuda zetu? Kuanza majadiliano kuhusu kwa nini Mashahidi Watatu ni muhimu, unaweza kushiriki kauli ya Rais Dallin H. Oaks au ushuhuda wa John Whitmer katika “Nyenzo za Ziada,” au unaweza kuonesha video “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” (ChurchofJesusChrist.org).

Picha
Joseph Smith na Mashahidi Watatu wakisali pamoja

Mashahidi Watatu walitoa ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni.

Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith

Joseph Smith alikuwa ni chombo katika mikono ya Mungu kukileta Kitabu cha Mormoni.

  • Washiriki wa darasa tayari wanaweza kuwa na uzoefu na matukio yaliyoelezwa katika “Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith,” lakini pengine unaweza kuwasaidia kupata undani mpya. Kwa mfano, unaweza kuwataka kuorodhesha matukio muhimu katika maelezo ya Joseph Smith. Tunaweza kuhitimisha nini kutoka uzoefu wake kuhusu umuhimu Bwana ameuweka juu ya Kitabu cha Mormoni?

  • Wimbo “An Angel from on high” (Nyimbo, na. 13) unaelezea juu ya kujitokeza kwa Kitabu cha Mormoni. Baada ya kuimba au kusikiliza wimbo huu, washiriki wa darasa wanaweza kupata maelezo katika “Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith” ambao unafanana au kuongeza nguvu misemo katika wimbo.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwatia moyo washiriki wa darasa kusoma 1 Nefi 1–7, waalike watafute mawazo au kweli ambazo zinawasaidia na hali yao ya maisha ya sasa—kwa mfano, changamoto ya familia au wito wa Kanisa.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mafungu ya maneno ya Kitabu cha Mormoni ambayo yanamshuhudia Yesu Kristo.

Video kuhusu Kitabu cha Mormoni kwenye ChurchofJesusChrist.org.

  • “Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni”

  • “Kitabu cha Mormoni ni nini? Sekunde 60 za maelezo ya jumla”

  • “Hadithi ya Kitabu cha Mormoni”

Kwa zaidi, ona lundo la video za Kitabu cha Mormoni kwenye ChurchofJesusChrist.org au Gospel Library app.

Umuhimu wa Mashahidi Watatu.

Rais Dallin H. Oaks alieleza kwa nini ushuhuda wa Mashahidi Watatu unavutia sana:

Ushuhuda wa Mashahidi Watatu kwa Kitabu cha Mormoni unasimama mbele kwa nguvu kubwa. Kila mmoja kati ya hao watatu alikuwa na sababu kubwa na nafasi ya kukanusha ushuhuda wake kama ungekuwa wa uongo, au kutatiza maneno juu ya undani kama chochote kingekuwa si cha kweli. Kama inavyojulikana vizuri, kwa sababu ya kutokubaliana au wivu kuhusiana na viongozi wengine wa Kanisa, kila mmojawapo wa hawa mashashidi watatu alitengwa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho karibu na takribani miaka minane baada ya chapisho la ushuhuda wao. Wote watatu walikwenda njia zao tofauti, bila masilahi ya pamoja kusaidia juhudi za kushirikiana. Hata , mwishoni mwa maisha yao—vipindi kadiri ya miaka 12 mpaka 50 baada ya kutengwa kwao—hakuna kati ya mashahidi hawa aliekengeuka kutoka ushuhuda wake uliochapishwa au aliyesema chochote ambacho kina mashaka yoyote juu ya ukweli wake” (“Shahdi: Martin Harris,” Ensign, Mei 1999 36).

Ushuhuda wa John Whitmer.

John Whitmer, mmoja wa mashahidi Wanane wa Kitabu cha Mormoni, alitangaza: “Mimi kamwe sijawahi kusikia kwamba shahidi yoyote kati ya watatu au wanane wakati wowote ameukana ushuhuda ambao wameutoa. … Majina yetu yamekwenda mbele ya mataifa yote, ndimi na watu kama ufunuo mtakatifu kutoka kwa Mungu. Na utaleta makusudio ya Mungu kulingana na azimio lililopo ndani yake” (katika Noel B. Reynolds,ed., Book of Mormon Authorship revisited: The Evidence for Ancient Origins [1997],55–56.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tafuta mwongozo wako mwenyewe. Badala ya kuichukulia mihutasari hii kama maelekezo ambayo ni lazima uyafuate, itumie kama chanzo cha mawazo kuanzisha mwongozo wako wa kiungu unapotafakari mahitaji ya wale unaowafundisha.

Chapisha