“Novemba 1-7. Mafundisho na Maagano 125–128: ‘Sauti ya Furaha kwa Walio Hai na Wafu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Novemba 1–7. Mafundisho na Maagano 125–128,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021
Novemba 1–7
Mafundisho na Maagano 125–128
‘’Sauti ya furaha kwa walio Hai na Wafu’’
Fikiria maneno haya ya Mzee Ulisses Soares: “Mwalimu bora ni mfano ulio mwema. Kufundisha kitu tunachokiishi kwa dhati, kunaweza kuleta mabadiliko katika mioyo ya wale tunaowafundisha” (“Je, Ninawezaje Kuelewa?”. Ensign au Liahona, Mei 2019, 7).
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Washiriki wa darasa wanaweza kuandika ubaoni vifungu vya maneno kutoka Mafundisho na Maagano 125–28 ambavyo vinawavutia wao. Waache watoe mawazo yao kuhusu vifungu hivyo. Je, kujifunza vifungu hivi kuligusa vipi vitendo vyao wiki hii?
Fundisha Mafundisho
“Fanya huduma maalum kwa familia yako.”
-
Miito ambayo Brigham Young alipokea kuhudumu kanisani ilimhitaji yeye na familia yake kufanya dhabihu kubwa; maneno ya Bwana kwa Brigham katika sehemu ya 126 yangehamasisha mjadala wa darasa kuhusu ni kwa nini wakati mwingine Bwana huhitaji dhabihu katika huduma yetu. Ni jinsi gani Bwana ametusaidia kutimiliza majukumu yetu nyumbani, katika mito ya kanisani, na katika maeneo mengine ya maisha?
Tunaweza kumtegemea Bwana wakati wa nyakati ngumu.
-
Ni jinsi gani Mafundisho na Maagano 127:2–4 ingewasaidia washiriki wa darasa wanaohisi kuwa, kama vile Joseph Smith, wanaogelea katika “maji yenye kina kirefu”? Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma mistari hii na kuelezea jinsi ambavyo wangetoa muhtasari wa mtazamo wa Joseph juu ya changamoto zake. Ni kifungu gani cha maneno kutoka kwenye mistari hii kingemsaidia mtu ambaye anahangaika? Ni jinsi gani Joseph alimtegemea Bwana wakati wa majaribu yake? Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wake?
Mafundisho na Maagano128
Wokovu wa mababu zetu ni muhimu kwenye wokovu wetu.
-
Fikiria jinsi unavyoweza kuwahamasisha washiriki wa darasa kushiriki katika kazi ya hekaluni na historia ya familia. Mafundisho na Maagano 128:15–18 ingeweza kuwasaidia kuhisi uharaka wa kazi hii; ungeweza kuwaalika kupekua mistari hii kwa ajili ya kitu kinachoongeza hamu yao ya kufanya ubatizo wa mababu zao waliokufa. Maswali kama haya yanaweza kuwasaidia kutafakari mistari hii: kwa nini “sisi bila ya wafu wetu hatuwezi kukamilishwa”? (mstari wa 15). Je, ni kwa nini Joseph Smith anaita ubatizo kwa niaba ya waliokufa “mada tukufu zaidi kuliko mada zote zilizo kwenye injili ya milele”? (mstari wa 17; angalia pia nukuu katika “Nyenzo za Ziada”). Ni katika hali gani ulimwengu unaweza kulaaniwa kama hakuna “muunganiko … kati ya mababu na watoto”? (mstari wa 18). Ikiwa washiriki wa darasa wanahitaji msaada ili waanze kazi ya historia ya familia, unaweza kumwalika kiongozi wa kazi za hekalu na historia ya familia katika kata au tawi ili awatambulishe katika jukumu hili kwenye FamilySearch.org.
Pia ungewahamasisha kwa mistari inayoonesha shangwe ya kazi za hekaluni na historia ya familia, kama vile Mafundisho na Maagano 128:19–23. Washiriki wa darasa wanaweza kusoma mistari hii na kupata vifungu vya maneno vinavyoonesha jinsi Joseph Smith alivyoona kuhusu wokovu wa wafu. Halafu ungewaomba kuelezea uzoefu wao walipokuwa na hisia sawa na hizo kuhusu kazi hii. Kuonesha mojawapo ya video katika “ Nyenzo za Ziada” kunaweza pia kuwatia moyo.
-
Kwa sababu wokovu wa wafu ni jambo la kipekee kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunaweza kuwa na fursa ya kufafanua mafundisho haya kwa watu ambao hawajawahi kuyasikia kabla. Washiriki wa darasa wanaweza kupekua Mafundisho na Maagano 128 kwa ajili ya kitu ambacho wangekieleza katika mazungumzo na mtu anayeuliza kuhusu ubatizo kwa niaba ya watu waliokufa. Je, mafundisho haya ya imani yanatufundisha nini sisi kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo? Waruhusu washiriki wa darasa wafanyie mazoezi yale ambayo wangesema.
Nyenzo za Ziada
Video kuhusu kazi ya historia ya familia (ChurchofJesusChrist.org).
“Sikuweza Kuelezea Hisia hiyo”
“Ikiwa Tutamuweka Mungu Kwanza”
“Kuwakomboa Wafu Kulinikomboa Mimi”
“Kutembelewa na Baba”
“Umeunganishwa kwa Familia za Milele”
“Wakusanyaji katika Ufalme”
“Ikinijumuisha Mimi”
“Je, Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?”
“Utoaji Mtukufu na wa Ajabu.”
Rais Gordon B. Hinckley alisema:
“Upatanisho wa Yesu kwa niaba ya wote unawakilisha dhabihu kuu ya uwakilishi. “Upatanisho wa Yesu kwa niaba ya wote unawakilisha dhabihu kuu mbadala kwa ajili ya watu wote. Mpangilio huu ambapo ndani yake mtu mmoja anaweza kutenda kwa niaba ya mwingine unatimizwa katika ibada za nyumba ya Bwana. Hapa tunahudumu kwa niaba ya wale waliokufa bila ya ufahamu wa injili. Wao ni uchaguzi wa kukubali au kukataa ibada iliyofanywa. Wanawekwa katika njia iliyo sawa na wale wanaotembea duniani. Waliokufa wanapewa nafasi sawa kama wale wanaoishi. Tena, ni utoaji mtukufu na wa ajabu ulioje Mwenyezi Mungu amefanya kupitia Ufunuo Wake kwa Nabii Wake” (“Mambo Makuu Ambayo Mungu Ameyafunua,” Ensign au Liahona, Mei 2005, 82–83).