Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 8–14. Mafundisho na Maagano 129–132: “Tukipokea Baraka Yoyote Kutoka kwa Mungu, Ni kwa Utiifu”


“Novemba 8–14. Mafundisho na Maagano 129–132: ‘Tukipokea Baraka Yo yote kutoka kwa Mungu, Ni kwa Utiifu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Novemba 8–14. Mafundisho na Maagano 129–132,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
Mafundisho ya Joseph Smith katika Nauvoo

Joseph Smith akiwa Nauvoo, 1840, na Theodore Gorka

Novemba 8–14

Mafundisho na Maagano 129–132

“Tukipokea Baraka Yoyote Kutoka kwa Mungu, Ni kwa Utiifu”

Wakati ikiwa ni muhimu kuwa na mpango wa kufundisha, ni muhimu pia kumwitikia Roho na mahitaji ya washiriki wa darasa. Pata kutoka kwa washiriki wa darasa ni kanuni zipi katika sehemu ya 129–32 zilikuwa na maana kwao.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki na wengine

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa huenda wamejifunza vitu kutoka kwenye kusoma kwao sehemu ya 129–32 vinavyohusiana na mada anuwai za injili. Ili kuwapatia nafasi ya kuelezea walichojifunza, unaweza kuandika baadhi ya mada hizo ubaoni, kama vile malaika, kuinuliwa, utiifu, asili ya Mungu, na ndoa ya milele (unaweza pia kuandika nyingine ubaoni ili kusimamia mada za ziada). Washiriki wa darasa wanaweza kutumia dakika chache kutafuta mstari katika sehemu hizi, unaohusiana na mojawapo ya mada hizi na kuandika marejeleo kwenye ubao. Kisha mnaweza kusoma mistari hii kama darasa na kuongea kuhusu kile ambacho kila mstari unafundisha kuhusu mada hiyo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 130:2, 18–23; 131:1–4; 132:20–25

Maisha haya yalikusudiwa kutuandaa sisi kwa ajili ya kuinuliwa.

  • Kuna vitu vingi ambavyo hatujui kuhusu kuinuliwa au maisha katika ufalme wa selestia—kiasi kikubwa yaweza kuwa ni zaidi ya uwezo wetu wa kufahamu kwa sasa. Lakini Mungu ameshafunua vidokezi vichache vyenye thamani, na vingi katika hivyo vinapatikana katika Mafundisho na Maagano 130–32. Washiriki wa darasa wanaweza kusoma rejeleo moja au zaidi yaliyoorodheshwa hapo juu na kushiriki na wengine maarifa yoyote watakayopata kuhusu kuinuliwa au ufalme wa selestia. Je, kujua taarifa hii kuhusu uzima wa milele hubariki vipi maisha yetu kwa sasa?

Mafundisho na Maagano 130:20–21; 132:5.

Baraka huja kwa kumtii Mungu.

  • Mafundisho na Maagano 130:20–21 na 132:5 hufundisha kanuni inayofanana. Wahimize washiriki wa darasa kusoma vipengele vyote viwili na kuelezea, kwa maneno yao wenyewe, kanuni hiyo ni kitu gani. Je, ni kwa namna gani kanuni hii imeoneshwa katika maisha yetu? Je, tunawezaje kupata matumaini na hakikisho katika Kristo wakati tukiwa watiifu lakini baraka tunazotarajia zisije moja kwa moja? Kwa zaidi juu ya mada hii, mnaweza kurejea pamoja utambuzi kutoka katika ujumbe wa Mzee Dale G. Renlund “Kujawa na Baraka” (Ensign au Liahona, Mei 2019, 70–73).

Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:3–25

Baba wa Mbinguni amefanya iwezekane kwa familia kuwa pamoja milele.

  • Tunaweza kumwambia nini rafiki ambaye huuliza, “Kwa nini ndoa na familia ni muhimu sana katika kanisa lenu?” Washiriki wa darasa wanaweza kufikiria wanavyoweza kujibu swali hilo wanaposoma Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:3–25; au maneno ya Mzee Dieter F. Uchtdorf’ katika “Nyenzo za Ziada.” Ni kwa jinsi gani ukweli huu unagusa namna tunavyoishi?

    Picha
    mwanamume na mwanamke nje ya Hekalu la Accra Ghana

    Mahusiano ya familia yanaweza kufanywa kuwa ya milele kupitia ibada za hekaluni.

Mafundisho na Maagano 132:1–2, 29–40

Ndoa ya wake wengi inakubalika kwa Mungu iwapo tu Yeye mwenyewe ameamuru.

  • Ikiwa washiriki wa darasa wana maswali kuhusu ndoa ya wake wengi, wasaidie kuona kwamba Joseph Smith na Watakatifu wengine wa awali walikuwa na maswali pia. Wahimize kutafuta swali ambalo Joseph alimuuliza Bwana katika Mafundisho na Maagano 132:1 na jibu alilopokea katika mistari 29–40 (ona pia Yakobo 2:27, 30). Kuwasaidia washirki wa darasa kujifunza kuhusu njia ambazo wanaweza kupata majibu kwa maswali yao ya injili, inaweza kusaidia kurejea pamoja “Answering Gospel Questions” katika topics.ChurchofJesusChrist.org. Pengine washiriki wa darasa wanaweza kuelezea jinsi walivyopata majibu ya maswali ya injili na wanavyobakia waaminifu hata kama baadhi ya maswali yalibaki bila kujibiwa.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Familia ndiyo “utaratibu wa mbinguni.”

Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha:

“Ninashukuru kwamba mimi ni wa kanisa ambalo linathamini ndoa na familia. Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanajulikana ulimwenguni kote kwa kuwa na baadhi ya ndoa na familia zilizo nzuri sana mnazoweza kuzipata duniani. Naamini hii ni kwa sababu, kwa kiasi fulani, kwa sababu ya ukweli wa thamani uliorejeshwa kupitia kwa Joseph Smith kwamba ndoa na familia zilikusudiwa kuwa za milele. Familia hazipo tu ili kufanya mambo yaende vizuri hapa duniani na kisha kutupwa tunapofika mbinguni. Bali, ni utaratibu wa mbinguni. Ni mwangwi wa mpangilio wa kiselestia na mfano wa familia ya milele ya Mungu.

“Lakini ndoa na uhusiano imara wa kifamilia havitokei tu kwa sababu sisi ni waumini wa Kanisa. Vinahitaji juhudi endelevu, za makusudi. Mafundisho ya familia za milele ni lazima yatutie moyo kuweka wakfu juhudi zetu za dhati katika kuokoa na kustawisha ndoa na familia zetu” (“Katika Kusifu Wale Ambao Huokoa,” Ensign au Liahona, Mei 2016, 77).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tengeneza mazingira salama. “Wahimize [washiriki wa darasa] wakusaidie kujenga mazingira yaliyo wazi, ya upendo, na heshima ili kwamba kila mmoja ajisikie yuko salama kuelezea uzoefu wao, maswali, na ushuhuda wao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,15).

Chapisha