Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 15–21. Mafundisho na Maagano 133–134: “Jitayarisheni kwa Ajili ya Ujio wa Bwana Harusi”


“Novemba 15–21. Mafundisho na Maagano 133–134: ‘Jitayarisheni kwa ajili ya Ujio wa Bwana Harusi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Novemba 15–21. Mafundisho na Maagano 133–134,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
wanawali watano wenye hekima

Bwana Harusi Anakuja, na Elizabeth Gibbons

Novemba 15–21

Mafundisho na Maagano 133–134

“Jitayarisheni kwa ajili ya Ujio wa Bwana harusi’’

Ukweli gani katika Mafundisho na Maagano 133–34 unahisi kwamba utasaidia zaidi darasa lako? Kwa sala zingatia mahitaji yao mnaposoma wiki hii.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki na wengine

Alika Kushiriki

Unaweza kuandika neno kusikiliza ubaoni na waalike washiriki wa darasa waandike kando yake mistari kutoka Mafundisho na Maagano 133–34 ambayo wanaamini tunahitaji kuisikiliza katika siku yetu. Waombe kuelezea mawazo yao kuhusu mistari hiyo. (Wasaidie washiriki wa darasa wazingatie kanuni za mafundisho badala ya mitazamo ya kisiasa.)

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 133:1–19; 37–39

Bwana anatuhitaji tujiandae kwa ajili ya Ujio Wake wa Pili.

  • Ni vipi utasaidia darasa lako kufahamu umuhimu wa kujitakasa ili kuwasaidia wengine kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kufanyia marejeo Mafundisho na Maagano 133:1–19, 37–39 na kuandaa orodha mbili: orodha moja ni ya ushauri wa Bwana kuhusu jinsi ya kujitakasa na nyingine ni ya jinsi ya kuandaa dunia kwa ajili ya kurejea kwa Mwokozi. Je, ina maana gani, katika hali ya kiroho, “tokeni … katika Babilonia” (mstari wa 5) na “kimbilieni Sayuni”? (mstari wa 12). Kwa maelezo zaidi kuhusu maana ya utakaso, ona “Utakaso” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org).

Mafundisho na Maagano 133:19–53

Ujio wa Pili utakuwa furaha kwa wenye haki.

  • Katika kujifunza kwao nyumbani, washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa walipata vipengele vyenye maana katika sehemu hii ambavyo vinawasababisha wao kutazamia kwa hamu Ujio wa Pili wa Mwokozi. Waalike kuelezea vipengele hivyo. Pia unaweza kualika darasa kupekua mistari 19–53 katika jozi, wakitafuta sababu za kutazamia kwa hamu Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Huku washiriki wa darasa wakielezea walichopata, wahimize kuzungumza jinsi Mwokozi “alivyowakomboa, na [kuwasaidia], na kuwabeba” (mstari wa 53). Hii inaweza kuwa fursa nzuri ya kuimba pamoja wimbo wa kanisa unaohusu nguvu ya Mwokozi ya kukomboa, kama vile “Savior, Redeemer of My Soul” (Nyimbo za Kanisa, na. 112). Je, ni zipi zingine “nyimbo za shangwe isiyo na mwisho” (mstari wa 33) zinatusaidia sisi kuhisi “upendo mkarimu wa Bwana [wetu]”? (mstari wa 52).

Mafundisho na Maagano 134

“Serikali zimewekwa na Mungu kwa manufaa ya mwanadamu’’.

  • Ili kusaidia washiriki wa darasa kujifunza kutoka Mafundisho na Maagano 134, ungeweza kuweka maswali kama haya kwenye chombo au ubaoni: Je, ni kwa namna gani Mungu anataka serikali ziwanufaishe watoto Wake? Tunapaswa kufanya nini iwapo sheria za ulimwengu zinapingana na sheria za kimbingu? Je, kazi na majukumu yetu ni nini kama raia? Alika washiriki wa darasa ili wachague swali na watumie sehemu ya 134 kuunda jibu. Himiza washiriki wa darasa ili waepuke kuzungumza kuhusu masuala au mitazamo maalum ya kisiasa.

  • Uhuru wa “jinsi ya kuabudu, wapi au nini [sisi] tunataka” (Makala ya Imani 1:11) ni haki ambayo Bwana anataka kila mmoja awe nayo. Ikiwa unahisi kwamba itakuwa muhimu kwa darasa lako kuzungumza kuhusu kanuni za uhuru wa kidini, zingatia kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 134:4, 7, 9. Je, mistari hii inatufundisha nini kuhusu kazi ya serikali katika kulinda uhuru wa kidini? Je ni kwa namna gani tunaweza kuendeleza uhuru wa kidini kwa wengine na kwetu sisi? Washiriki wa darasa wanaweza kupata maarifa ya kuwasaidia kujibu swali hili katika “Nyenzo za Ziada”

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Nguzo za uhuru wa kidini.

Mzee Robert D. Hales alifundisha:

“Kuna nguzo nne za msingi wa uhuru wa kidini ambao sisi kama Watakatifu wa Siku za Mwisho lazima tuzitegemee na kuzilinda.

“Ya kwanza ni uhuru wa kuamini. Hakuna anayepaswa kushutumiwa, kuteswa, au kushambuliwa na watu binafsi au serikali kwa kile anachoamini kuhusu Mungu. …

“Nguzo ya pili ya msingi wa uhuru wa kidini ni uhuru wa kufundisha imani yetu na kusadiki kwetu kwa watu wengine. … Kama wazazi, wamisionari, na wamisionari waumini, tunategemea uhuru wa kidini ili kufundisha mafundisho ya Bwana katika familia zetu na duniani kote.

“Nguzo ya tatu ya msingi wa uhuru wa kidini ni uhuru wa kuunda taasisi ya kidini, kanisa, ili kuabudu kwa amani na watu wengine. Makala ya kumi na moja ya imani inasema, “Tunadai haki ya kumwabudu Mungu Mwenyezi kulingana na mwongozo wa dhamiri yetu sisi wenyewe, na tunawaruhusu watu wote haki hiyo, na waabudu namna, mahali, au chochote watakacho.’ …

“Nguzo ya nne ya msingi wa uhuru wa kidini ni uhuru wa kuishi imani yetu—utendaji huru wa imani si tu nyumbani na kanisani bali pia katika maeneo ya umma” (“Kutunza Haki ya Kujiamulia, Kulinda Uhuru wa Kidini,” Ensign au Liahona, Mei 2015, 112).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fundisha kipengele cha “kwa nini.” “Kama [washiriki wa darasa] wanaelewa mpango wa milele wa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya furaha ya watoto Wake, sababu za kanuni na amri za injili huwa wazi zaidi na hamasa ya kutii inaongezeka.” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 20).

Chapisha