Njoo, Unifuate
Agosti 19–25. 1 Wakorintho 1–7: ‘Muunganishwe Pamoja kwa Ukamilifu’


“Agosti 19–25. 1 Wakorintho 1–7: ‘Muunganishe Pamoja kwa Ukamilifu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Agosti 19–25. 1 Wakorintho 1–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Korintho

Korintho, Ugiriki ya Kusini, Baraza na Kitovu cha Jiji, mchoro na Balage Balogh

Agosti 19–25

1 Wakorintho 1–7

“Muunganishwe Pamoja kwa Ukamilifu”

Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha kwamba watu wengi “huja [Kanisani] wakitafuta uzoefu wa kiroho” (“Mwalimu Hutoka kwa Mungu,” Ensign, Mei 1998, 26). Unaposoma 1 Wakorintho 1–7, kwa maombi fikiria unaweza kufanya nini ili uweze kusaidia kutengeneza uzoefu wa kiroho katika darasa lako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuandika ni kwa namna gani wamefanyia kazi kile wanachojifunza kutoka kwenye maandiko. Waombe washiriki wachache wa darasa kuelezea walichoandika.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

1 Wakorintho 1:10–173

Waumini wa Kanisa la Kristo lazima wawe na umoja.

  • Kujadili sura chache za mwanzo za 1 Wakorintho kunaweza kuwa ni nafasi ya kujenga umoja mkubwa miongoni mwa waumini wa kata. Unaweza kuanza kwa kuwauliza washiriki wa darasa kuongelea kuhusu klabu, kundi au timu waliyowahi kujiunga nayo ambayo ilikuwa na umoja mkubwa. Kwa nini kundi hili lilihisi kuwa na umoja sana? Kisha ungeweza kuchunguza baadhi ya mafundisho ya Paulo kuhusu umoja katika 1 Wakorintho 1:10–13; 3:1–11. Je, mistari hii, pamoja na uzoefu wetu, hufundisha nini kuhusu nini husaidia kutengeneza umoja na nini hutishia umoja huo? Ni baraka gani huja kwa wale walio na umoja? Hadithi zilizosimuliwa na Rais Henry B. Eyring katika “Nyenzo za Ziada” zingeweza pia kusaidia katika mjadala huu.

  • Paulo anatumia taswira ya jengo ili kuhimiza umoja 1 Wakorintho 3:9–17. Ni kwa namna gani analojia hii inaweza kulisaidia darasa lako kuelewa zaidi kuhusu umoja? Kwa mfano, baada ya kusoma mistari hii pamoja, ungeweza kumpa kila mshiriki wa darasa kitofali na mfanye kazi kwa pamoja ili kujenga kitu fulani. Ni kwa namna gani sisi ni “jengo la Mungu”? (1 Wakorintho 3:9). Ni kwa namna gani Mungu anamjenga kila mtu binafsi? Ni kipi tunakijenga pamoja kama Watakatifu? Ni kipi tunaweza kufanya kwa pamoja kama kata yenye umoja ambacho tusingeweza kufanya kila mtu binafsi?

1 Wakorintho 1:17–31; 2; 3:18–20

Ili kutimiza kazi ya Mungu, tunahitaji busara ya Mungu.

  • Baadhi ya watu hujiona hawastahili kutumikia katika Kanisa kwa sababu hawana elimu au mafunzo ya kitaaluma. Wengine hujiona wanastahili kabisa kwa sababu wana elimu au mafunzo ya kitaaluma. Haya yote hutoa taswira isiyo sahihi ya kipi hasa kinatufanya tustahili kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hapa kuna wazo la kulisaidia darasa lako kumtegemea Mungu: Gawa washiriki wa darasa lako katika makundi na waombe kupitia 1 Wakorintho 1:17–31; 2; au 3:18–20 wakitafuta maneno kama busara na upumbavu. Kisha wangeweza kushiriki katika makundi yao ni nini mistari hii hufundisha kuhusu kuwa na busara katika kazi ya Bwana. Ni mambo gani kuhusu injili yanaweza kuonekana ya kipumbavu kwa baadhi ya watu? Ni kwa namna gani mambo haya yanaonyesha hekima ya Mungu? Labda washiriki wa darasa wangeweza pia kushiriki uzoefu ambapo walitegemea hekima ya Mungu, kuliko yao wenyewe ili kutimiza kazi Yake.

1 Wakorintho 6:9–20

Miili yetu ni mitakatifu.

  • Kwa kuanza majadiliano juu ya mistari hii, ungeweza kuandika kwenye ubao maswali kama yafuatayo: Je, Bwana huitazamaje miili yetu? Ni kwa namna gani hii ni tofauti na vile shetani hututaka sisi tuifikirie miili yetu? Inamaanisha nini kwamba miili yetu ni mahekalu ya Roho Mtakatifu? Waalike washiriki wa darasa kutafuta majibu ya maswali haya katika 1 Wakorintho 6:9–20 (ona pia Mafundisho na Maagano 88:15; Musa 6:8–9).

  • Mjadala wenu kuhusu utakatifu wa miili yetu ungeweza kujumuisha maongezi kuhusu sheria ya usafi wa kimwili. Hii hususan ingeweza kusaidia kwa sababu kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, mara nyingi tunakuwa na nafasi ya kuelezea imani yetu kuhusu usafi wa kimwili kwa wale ambao si washiriki wa imani hizo. Labda ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa nini wanajifunza kutoka kwa Paulo—pia kutoka kwenye nyenzo zingine za Kanisa—ambazo zingeweza kuwasaidia kuelezea kwa wengine kwa nini usafi wa kimwili ni muhimu. Baadhi ya nyenzo hizi zinaweza kuwa zile zilizoorodheshwa kwenye “Nyenzo za Ziada.”

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waambie washiriki wa darasa lako kuwa kama wangetaka mawazo ya ziada juu ya ya jinsi ya kuwa na umoja zaidi na wenzi wao, familia, au kata, dhima ya umoja inaendelea katika 1 Wakorintho 8–11.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

1 Wakorintho 1–7

Mifano ya umoja

Rais Henry  B. Eyring alifundisha:

“Nilialikwa kupiga magoti pembeni ya kitanda pamoja na familia wakati nilipokuwa mgeni nyumbani mwao. Mtoto mdogo aliombwa kuwa msemaji wa sala. Aliomba kama patriaki kwa ajili ya kila mtu katika familia, kwa jina. Nilifungua macho yangu mara moja kuona nyuso za watoto wengine na wazazi wao. Niliweza kuona walikuwa wakiungana katika imani na mioyo katika sala ya yule mtoto mdogo wa kiume.

“Baadhi ya akina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama hivi karibuni walisali kwa pamoja walipokuwa wakijiandaa kumtembelea kwa mara ya kwanza mjane kijana ambaye mume wake alifariki ghafla. Walitaka kujua nini cha kufanya na jinsi ya kufanya kazi pamoja kusaidia kuandaa nyumba na familia na marafiki ambao wangekuja wakati wa msiba. Jibu la sala yao lilikuja. Walipofika kwenye nyumba, kila dada alienda kutekeleza kazi fulani. Nyumba ilikuwa tayari kwa haraka sana mpaka baadhi ya akina dada walijutia kutoweza kufanya zaidi. Maneno ya kufariji yalizungumzwa ambayo kwa pamoja yalifaa kikamilifu. Walitoa huduma ya Bwana kama wamoja, mioyo ikiwa imeunganishwa pamoja” (“Mioyo Yetu Imeungana kama Mmoja,” Ensign au Liahona, Nov. 2008, 68–69).

Baraka za usafi wa kimwili

Katika Ibada ya Ulimwengu Wote kwa Vijana Wakubwa, dada Wendy W. Nelson alisema:

Usafi binafsi ni muhimu kwenye upendo wa kweli. Kadiri mawazo na hisia zako, maneno yako na vitendo, vinapokuwa safi ndivyo utakavyokuwa mkubwa uwezo wako wa kutoa na kupokea upendo wa kweli. …

Kama sehemu muhimu ya kuelezea upendo wao, Bwana anataka mume na mke wapate uzuri na shangwe ya uhusiano wa ndoa. …

“… Chochote kile kinachomwalika Roho katika maisha yako, na katika maisha ya mwenzi wako na ndoa yako, kitaongeza uwezo wako wa kupata uzoefu wa uhusiano wa ndoa. … Kwa upande mwingine, chochote ambacho humuhuzunisha Roho kitapunguza uwezo wako wa kuwa wamoja na mwenzi wako. …

“Uhusiano wa kindoa ulioidhinishwa na Roho umebarikiwa na Bwana na unatakasa” (“Mapenzi na Ndoa,” Ibada ya Ulimwengu wote kwa Vijana Wakubwa, Jan. 8, 2017, broadcasts.lds.org).

Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Acha nisisitize kwamba uhusiano wa kimapenzi utunzwe kwa ajili ya wanandoa kwa sababu ni alama kuu ya muungano kamili, muungano uliotawazwa na kufafanuliwa na Mungu. …

“Lakini muungano kamili wa jinsi hiyo, wenye ahadi isiyotetereka kati ya mume na mke, unaweza tu kuja kwa urafiki na kudumu kunakowezekana katika agano la ndoa, kwa ahadi za dhati na kujitolea kwa kila kitu walichonacho—mioyo yao yote na mawazo, siku zote na ndoto zao zote” (“Personal Purity,” Ensign, Nov. 1998, 76).

Mzee David A. Bednar alifafanua: “mahusiano ya [kimapenzi] si udadisi tu ambao unahitaji uchunguzi, tamaa ambayo inahitaji kuridhishwa au aina ya shughuli au burudani ya kutafutwa kwa ubinafsi. Si tu ushindi ambao unatakiwa kufikiwa au kitendo cha kufanywa kiurahisi tu. Badala yake, ni moja kati ya vielelezo vikuu duniani vya asili ya uungu wetu na uwezo wetu na njia ya kuimarisha hisia na unganiko la kiroho kati ya mume na mke. Sisi ni mawakala tuliobarikiwa kuwa na haki ya kujiamulia na tunatambulika kwa urithi wetu mtakatifu kama watoto wa Mungu—na si kwa tabia za kimapenzi, mitazamo ya kisasa au falsafa za kidunia” (“Tunaamini katika Kuwa Wasafi,” Ensign au Liahona, Mei 2013, 42).

Namna ya kubaki msafi kimwili.

  • “Usafi wa kimwili: Mipaka Yake ni Ipi?” “Nilichagua kuwa msafi” (video), LDS.org

  • “Ubikira,” Kwa Nguvu ya Vijana, 35–37

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Shuhudia kuhusu Yesu Kristo. Unapofundisha, kumbuka mfano wa Paulo: Yeye “hakuja na uwezo wa juu wa kuongea au hekima, kutangaza … ushuhuda wa Mungu” (1 Wakorintho 2:1). Ushuhuda wako rahisi juu ya Mwokozi unaweza kuwa na ushawishi kwa kiasi kikubwa sana.

Chapisha