Njoo, Unifuate
Agosti 12–18. Warumi 7–16: ‘Shinda Uovu kwa Wema’


Agosti 12–18. Warumi 7–16 ‘Shinda Uovu kwa Wema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019.)

Agosti 12–18. Warumi 7–16” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Rumi

Agosti 12–18

Warumi 7–16

“Shinda Uovu kwa Wema”

Soma Warumi 7–16, na andika mawazo unayopata kuhusu jinsi ya kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutoka kwenye maandiko. Mwanzoni misukumo yako inaweza kuonekana kama mawazo rahisi, lakini unapoyatafakari, yanaweza kuwa shughuli muhimu za kujifunza.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa lazima wajisikie huru kuelezea kitu chochote ambacho kimewapa mwongozo wa kiungu katika kujifunza kwao binafsi au kama familia, lakini wakati mwingine inasaidia kuomba mawazo juu ya kitu fulani mahususi. Kwa mfano, unaweza kusoma Warumi 10:17 na 15:4 na kuwaomba kushiriki maandiko ambayo yanajenga imani yao au kuwapa tumaini.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Warumi 8:14–18

Kupitia Yesu Kristo, sisi tunaweza kurithi vitu vyote ambavyo Baba wa Mbinguni anavyo.

  • Kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunaamini kuwa virai kama “warithi wa Mungu” na “warithi pamoja na Kristo” vinamaanisha kwamba kwa msaada wa Yesu Kristo, tunaweza kuwa kama Baba wa Mbinguni na kupokea vyote alivyo navyo (Warumi 8:17; ona pia M&M 132:19–20). Kuwasaidia washiriki wa darasa kuona jinsi gani fundisho hili linafundishwa katika maandiko, ungeweza kualika nusu ya darasa kujifunza baadhi ya mistari ya Biblia iliyoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada” na nusu nyingine kujifunza mistari kutoka maandiko ya siku za mwisho, pia katika “Nyenzo za ziada.” Kisha washiriki wa darasa wanaweza kufundishana kile walichojifunza. Wape muda wa kujadiliana kwa nini fundisho hili ni la muhimu sana. Kwa mfano, ni tofauti gani inaweza kutokea kwenye maisha yetu kama tukijua kuwa sisi tunaweza kuwa “warithi wa mungu” na “warithi pamoja na Kristo”? (Warumi 8:17).

  • Kukumbuka kuwa baraka za milele zinawangoja waaminifu kunaweza kutusaidia wakati tunapopata majaribu na taabu (ona Warumi 8:18). Njia rahisi ya kuieleza kanuni hii ingeweza kuwa kwa kuchora mizani kwenye ubao; waombe washiriki wa darasa kuorodhesha upande mmoja baadhi ya majaribu ambayo watu wanaweza kupata. Kisha wanaweza kutafuta baadhi ya maandiko katika “Nyenzo za Ziada” na kuyaorodhesha kwenye upande mwingine wa mizani wa maelezo ya baraka za milele ambazo huja kwa wale ambao hukabiliana na majaribu yao kwa imani. Ni kwa namna gani majaribu yanalinganishwa na baraka zilizoahidiwa? Je, ni nini tungeweza kusema kwa mtu ambaye alituuliza kama kuna faida kuwa waaminifu katika amri za Bwana?

  • Analojia iliyotolewa na Mzee Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada” ingeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili ni kwa namna gani tunaweza kujiandaa kuwa “Warithi wa Mungu” (Warumi 8:17). Ni zipi baadhi ya “sheria na kanuni” Mzee Oaks anazungumzia?

Warumi 8:18, 28, 31–39

“Ni nani atakayetutenganisha na upendo wa Kristo?”

  • Kujadili Warumi 8 kwa pamoja kungeweza kuleta nafasi ya kuwasaidia washiriki wa darasa kuhisi upendo wa Mwokozi. Fikiria kuonyesha picha ya ukurasa mzima katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia au picha nyingine ya Yesu Kristo wakati mnasoma Warumi 8:18, 28, 31–39 kama darasa. Je, ni mawazo gani au hisia zipi washiriki wa darasa wanazo baada ya kusoma mistari hii? Unaweza kuwaalika washiriki wachache wa darasa kueleza ni kwa namna gani wamepata ushuhuda wa ukweli unaopatikana kwenye mistari hii. Mnaweza pia kuimba wimbo kama darasa (au kumuomba mtu mmoja kuimba wimbo) kuhusu upendo wa Mungu na Yesu Kristo, kama vile “Mungu Alitupenda, Hivyo akamtuma Mwanaye” au “Ninashangaa Sana” (Wimbo, namba. 187, 193). Ni maneno gani au kirai kipi katika nyimbo hizi huwasaidia washiriki wa darasa kuuona upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Warumi 13:8–10

Amri zote za Mungu hutimizwa katika amri ya upendo.

  • Kuwasaidia washiriki wa darasa kuona ni kwa jinsi gani amri zote kwa “kifupi zimejumuishwa” katika amri ya kumpenda jirani yako (Warumi 13:9), waalike kutengeneza orodha kwenye ubao ya amri zote ambazo wanaweza kufikiria. Someni kwa pamoja Warumi 13:8–10 na Mathayo 22:36–40, na jadilini kama darasa uhusiano uliopo kati ya kumpenda Mungu na jirani na kutii kila amri iliyoorodheshwa kwenye ubao. Ni kwa namna gani ukweli huu unabadilisha namna tunavyofikiri kuhusu amri na utiifu?

Warumi 14

Lazima tujiepushe na kuhukumu maamuzi ya wengine na kuwa vizuizi vya kiroho.

  • Kutoa muktadha wa Warumi 14, ungeweza kuonyesha kuwa baadhi ya watakatifu wa Rumi walibishana wao kwa wao kuhusu tabia tofauti wakati wa kula, kuadhimisha sikukuu na mambo mengine ya kitamaduni. Ni hali gani kama hiyo ambayo tunakumbana nayo kwa sasa? Labda washiriki wa darasa wangepitia kwa haraka Warumi 14 na kutoa ufupisho kwa sentensi moja kuhusu ushauri wa Paulo. Ni ushauri gani tunaweza kushiriki na wengine kuhusu namna ya kuepuka kuwa wenye kuhukumu? Kauli toka kwa Rais Dieter F. Uchtdorf katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kusaidia.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwahamasisha washiriki wa darasa kusoma 1 Wakorintho 1–7, unaweza kuwaambia kwamba inajumuisha ushauri wa Paulo kwa waumini wanaokaa katika sehemu iliyojulikana kama ulimwengu wa kale uliokosa maadili na miji ya waabudu sanamu.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Warumi 7–16

Kupokea “yote ambayo Baba anayo” (Mafundisho na Maagano 84:38).

Kutoka kwenye Biblia

Kutoka maandiko ya siku za mwisho

Mzee Dallin H. Oaks alisimulia hadithi ifuatayo:

“Baba tajiri alijua kwamba kama angemrithisha utajiri mtoto wake ambaye alikuwa bado hajakua vya kutosha na hajapata busara inayohitajika, urithi labda ungetumika vibaya. Baba alimwambia mtoto wake:

Kila kitu nilichonacho ninatamani kukupa—si tu utajiri wangu, lakini pia cheo changu na sifa yangu miongoni mwa watu. “‘Kile ambacho ninacho ninaweza kukupa kiurahisi, lakini ule utu wangu lazima uupate wewe mwenyewe. Utastahili urithi wako kwa kujifunza kile nilichojifunza na kwa kuishi vile nilivyoishi. Nitakupa sheria na kanuni ambazo kwazo nimepata busara yangu na akili. Fuata mfano wangu, pata ujuzi kama nilivyopata, na utakuwa kama nilivyo, na vyote nilivyonavyo vitakuwa vyako’” (“Changamoto ya Kuwa,” Ensign, Nov. 2000, 32).

Warithi pamoja na Kristo.

“Watakatifu wa Siku za Mwisho wanawaona watu wote kama watoto wa Mungu katika hali na ukamilifu wote; wanamchukulia kila mtu kuwa na uungu katika asili, uhalisi, na uwezekano wa kuwa. … Kama vile mtoto anavyoweza kukuza tabia kama ya wazazi wake kadiri ya muda, asili takatifu ambayo wanadamu hurithi inaweza kuendelezwa kwenye kuwa kama Baba yao wa Mbinguni. … Wanaume na wanawake wana uwezekano wa kuinuliwa mpaka katika hali ya uungu” (“Kuwa Kama Mungu,” Mada za Injili, topics.lds.org).

Kuhukumu wengine.

Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha:

“Mada hii ya kuhukumu wengine ingeweza hasa kufundishwa katika mahubiri ya maneno mawili. Inapokuja kwenye kuchukia, kusengenya, kudharau, kudhihaki, kuwa na kinyongo au kutaka kudhuru, tafadhali fanya ifuatavyo:

“Acha!

“Ni rahisi hivyo. Tunatakiwa kuacha kuhukumu wengine na kubadili mawazo na hisia za kuhukumu kwa moyo uliojaa upendo kwa Mungu na watoto Wake. Mungu ni Baba yetu. Sisi ni watoto Wake. Sisi wote ni kaka na dada. … Karatasi niliyoiona hivi karibuni … ilikuwa imebandikwa nyuma ya gari ambalo dereva wake alionekana kutokuwa makini sana kandokando ya kingo, lakini maneno katika karatasi yalifundisha somo lenye umuhimu mkubwa. Ilisomeka, ‘Usinihukumu kwa kuwa natenda dhambi tofauti na wewe’” (“Wenye Rehema watapata Rehema,” Ensign au Liahona, Mei 2012, 75).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tafuta Nyenzo ambazo zinaunga mkono kanuni. Kwa kuongezea katika mawazo ya kufundisha katika muhtasari huu, ungeweza kuboresha shughuli kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia kutumia katika darasa lako. (Ona pia Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 17-18.)

Chapisha