Njoo, Unifuate
Agosti 12–18. Warumi 7–16: ‘Ushinde Ubaya kwa Wema’


“Agosti 12–18. Warumi 7–16: ‘Ushinde Ubaya kwa Wema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Agosti 12–18. Warumi 7–16,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
Roma

Agosti 12–18.

Warumi 7–16

“Ushinde Ubaya kwa Wema”

Ni kanuni chache tu za injili katika Warumi 7–16 zinaweza kujumuishwa kwenye muhtasari huu, kwa hiyo usijiwekee mipaka kwenye kile kilichoongelewa hapa. Zingatia mwongozo wa kiungu unaopokea pale unapojifunza.

Andika Misukumo Yako

Alipofungua waraka wake kwa Warumi, Paulo aliwasalimu waumini wa Kanisa katika Rumi kwa kuwaita “wapendwao na Mungu” “walioitwa kuwa watakatifu.” Alisema kwamba” imani yao [ilikuwa] inahubiriwa katika dunia nzima” (Warumi 1:7–8). Japokuwa Paulo alitumia sehemu kubwa ya waraka wake kusahihisha mawazo ya uongo na tabia zenye dosari, inaonekana alitaka pia kuwahakikishia waongofu hawa wapya wa Kikristo kwamba walikuwa Watakatifu kweli wapendwao na Mungu. Kwa unyenyekevu wa kuonyesha maono kwa ajili yao, Paulo alikiri kwamba amejisikia kama “masikini” wakati fulani (Warumi 7:24), lakini injili ya Yesu Kristo ilimpa nguvu ya kushinda dhambi (ona Tafsiri ya Joseph Smith, Warumi 7:22–27 [katika kiambatisho cha Biblia]). Aliendelea kuelezea ushauri nyeti kwa ajili yetu sote ambao tunahangaika kujiona tunapendwa na kwa ajili ya wale ambao kwao utakatifu unaweza kuonekana usiofikika. “Usishindwe na ubaya,” alisema—wote ubaya katika ulimwengu na ubaya ndani yetu—”bali ushinde ubaya kwa wema” (Warumi 12:21).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Warumi 7–8

Nikimfuata Roho, ninaweza kushinda dhambi na kujiandaa kwa urithi na Mungu.

Hata baada ya kuingia katika “upya wa uzima” kupitia agano la ubatizo (Warumi 6:4), pengine umehisi baadhi ya vita vya ndani Paulo alivyovielezea katika Warumi 7—“kupiga vita” kati ya mwanadamu wa tabia ya asili na matamanio yetu ya haki (Warumi 7:23). Lakini Paulo pia alizungumza juu ya tumaini katika Warumi 8:23–25. Ni nini sababu ya tumaini hili unazipata katika sura ya 8? Unaweza pia kutafuta baraka zinazokuja kutokana na “Roho wa Mungu kukaa ndani yako” (Warumi 8:9). Ni kwa jinsi gani unaweza kutafuta wenza wa Roho Mtakatifu kwa utimilifu zaidi katika maisha yako?

Warumi 8:17–39

Utukufu wa milele unaowasubiri waaminifu unayazidi kwa mbali sana majaribu ya maisha haya.

Kama miaka michache tu baada ya Paulo kuandika waraka huu, Watakatifu katika Rumi walipata mateso ya kutisha. Je, unapata katika Warumi 8:17–39 kile ambacho kiliweza kuwasaidia Watakatifu hawa mateso yalipokuja? Ni kwa jinsi gani maneno haya yanaweza kutumika kwako na majaribu yanayokupata sasa?

Tafuta uhusiano kati ya maneno haya na ushauri huu kutoka kwa Dada Linda S. Reeves: “Sijui ni kwa nini tuna majaribu haya mengi tuliyonayo, lakini ni hisia yangu binafsi kwamba thawabu ni kubwa sana, ambayo ni ya milele na ya kudumu milele, ya furaha na ya kupita uelewa wetu kwamba katika siku ile ya thawabu, tuweze kujisikia kusema kwa Baba yetu mpendwa, mwenye rehema, ‘Je hiyo ndiyo yote iliyohitajika? Ninaamini kwamba kama kila siku tutakumbuka na kutambua kina cha upendo ule Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu walio nao kwetu, tutakuwa radhi kufanya chochote ili kurudi katika uwepo Wao tena, tukizungukwa na upendo Wao milele. Hatutajali … kile tulichoteseka hapa kama, mwishoni, majaribu hayo ndicho kitu hasa kinachotupasisha sisi kwa ajili ya uzima wa milele na kuinuliwa katika ufalme wa Mungu tukiwa na Baba yetu na Mwokozi wetu?” (“Kustahili Baraka Zetu Tulizoahidiwa,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 11).

Amua nini utafanya kila siku “kukumbuka na kutambua” upendo wa Mungu kwako.

Warumi 8:29–30; 9–11

Je, Paulo alimaanisha nini kwa “kuamuliwa kabla,” “kuteuliwa,” na “kujulikana kabla”?

Paulo alitumia maneno haya kufundisha kwamba baadhi ya watoto wa Mungu walichaguliwa kabla au waliteuliwa kabla ya kuzaliwa, kupokea baraka na majukumu maalumu ili kwamba waweze kubariki mataifa yote ya ulimwengu (ona Mwongozo wa Maandiko, “Uchaguzi”). Hii ilikuwa kulingana na ujuzi wa Mungu wa kujua mapema utayari wa watoto Wake wa kumfuata Yesu Kristo na kuwa kama Yeye (ona pia Waefeso 1:3–4; 1 Petro 1:2). Hata hivyo, Paulo alisisitiza katika Warumi 9–11 kwamba bila kujali ni kwa jinsi gani tunakuja katika nyumba ya Israeli—au kuwa muumini wa Kanisa—watu wote lazima wapokee wokovu kila mtu binafsi kupitia imani katika Yesu Kristo na utiifu kwa amri Zake.

Kwa maelezo zaidi, ona Alma 13:1–5; “Kutawazwa kabla ya kuzaliwa,” Mada za Injili (topics.lds.org).

Warumi 12–16

Paulo ananialika kuwa Mtakatifu na mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo.

Sura tano za mwisho za Warumi zina idadi kubwa ya maelekezo mahususi kuhusiana na jinsi gani Watakatifu wanapaswa kuishi. Hutaweza kutumia ushauri huu wote kwa mara moja, lakini msikilize Roho, na Yeye atakuwezesha kupata ushauri mmoja au miwili ambayo unaweza kuanza kuifanyia kazi leo. Elezea matamanio yako kwa Baba yako wa Mbinguni katika sala, na omba msaada Wake.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia.

Mawazo ajili kwa ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:

Warumi 7:23

Kuisaidia familia yako kuelewa zaidi kuhusu “kupiga vita” kulikoelezwa na Paulo katika mstari huu, fikiria kushiriki hadithi kuhusu mbwa mwitu katika makala ya Mzee Shayne M. Bowen “Uhuru wa Kuchagua na Uwajibikaji” (New Era, Sept. 2012, 8–9).

Warumi 9:31–32

Ujumbe wa Mzee Wilford W. Andersen “Muziki wa Injili” (Ensign au Liahona, Mei 2015, 54–56) unaweza kuelezea kwa mfano kile Paulo anachofundisha kuhusu sheria, matendo, na imani. Familia yako inaweza kufurahia kujadili hotuba yake na kujaribu kucheza pakiwepo na bila kuwepo muziki. Ni kwa jinsi gani kucheza bila kuwepo muziki ni kama kutii injili bila kuwa na imani?

Picha
Baba na binti wakicheza

Mzee Wilford W. Andersen alifundisha, “Muziki wa injili ni hisia ya furaha ya kiroho.”

Warumi 10:17; 15:4

Ni kwa jinsi gani kujifunza maneno ya Mungu kumetuletea baraka zilizoelezwa katika mistari hii? Pengine wanafamilia wanaweza kushiriki baadhi ya maandiko wanayoyapenda zaidi (ona pia 2 Nefi 25:26).

Warumi 12

Inamaanisha nini kujifanya wenyewe “dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kukubalika kwa Mungu”? (Warumi 12:1).

Warumi 14:13–21

Familia yako inaweza kunufaika kwa kujifunza ushauri wa Paulo kuhusu kuhukumu na kubishana kuhusu upendeleo binafsi wa wengine? Pengine mnaweza kujadili njia sahihi za kujibu wakati chaguzi za wengine zinapotofautiana na zenu. Ni kwa namna gani tunaweza kukumbuka zaidi juu ya jinsi gani chaguzi zetu huwaathiri wengine? Video “Kuhukumu Wengine? Acha! na “Kuangalia kupitia Madirishani” (LDS.org) zinaweza kutoa utambuzi wa ziada juu ya mada hii.

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wape watoto nafasi ya kuonyesha ubunifu wao. Wakati unapowaalika watoto kubuni kitu kinachohusika na kanuni ya injili, unawasaidia kuelewa vyema kanuni hiyo. … Waruhusu kujenga, kuchora, kupaka rangi, kuandika, na kubuni” (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Chapisha