Muziki wa Injili
Muziki wa injili ni hisia yafuraha ya kiroho ambayo hutoka kwa Roho Mtakatifu. Inaleta mabadiliko ya moyo
Miaka iliyopita nilisikiliza mahojiano ya redio ya daktari kijana aliyefanya kazi katika hospitali katika Nchi ya Navajo. Alielezea kuhusu tukio lililomtokea usiku mmoja wakati mzee wa Asili ya Kiamerika akiwa na nywele ndefu zilizosukwa alipokuja katika chumba cha dharura. Daktari huyu kijana alichukua kibao cha kuandikia, akamkaribia mzee huyo, na kusema, “Nikusaidieje? Mzee akamwangalia na hakusema kitu. Daktari kijana, akihisi kutokuwa na subira kiasi, akajaribu tena. “Siwezi kukusaidia kama hautaongea na mimi,” alisema. “Niambie kwa nini umekuja hospitalini.”
Mzee huyu baadaye alimwangalia na kusema, “Je! Wewe ucheza ngoma?” Kadri daktari huyu kijana alivyokuwa akifiria swali hili geni, ilikuwa kama vile labda mgonjwa wake alikuwa mganga wa kienyeji ambaye, kulingana na mila na tamaduni, alitaka kuponya wagonjwa kupitia nyimbo na kucheza ngoma badala ya kupewa dawa zilizoandikiwa na daktari.
“La,” alisema daktari, “Sichenzi ngoma. Je! Wewe unaweza kucheza ngoma?” Mzee akatikisa kichwa na kusema ndio. Baadaye daktari akasema, “ Unaweza kunifundisha kucheza ngoma?”
Jibu la mzee limenisababishia kufikiria kwa miaka mingi. “Ninaweza kukufundisha kucheza ngoma,” alisema, “lakini inabidi uusikie muziki.”
Wakati mwingine katika nyumba zetu, tunafundisha miondoko ya kucheza ngoma lakini hatufanikiwi katika kuwasaidia watoto wetu kuusikiliza muziki. Na kama mzee wa mganga alivyojua, ni vigumu kucheza ngoma bila muziki. Kucheza ngoma bila muziki inashangaza na hairidhishi—na inatia aibu. Ulishawahi kujaribu?
Katika mlango wa 8 wa Mafundisho na Maagano, Bwana aliwafundisha Joseph Smith na Oliver Cowdery, “Ndio, tazama, nitakujulisha wewe akilini mwako na katika moyo wako, kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye atakujia na ambaye atakaa moyoni mwako” (mstari 2). Tunajifunza hatua za kucheza ngoma kwa kutumia akili zetu, lakini tunausikiliza muziki kwa mioyo yetu. Hatua za kucheza mgoma za injili ni vitu tunavyovifanya; muziki wa injili ni furaha ya kiroho ambayo hutoka kwa Roho Mtakatifu. Inaleta mabadiliko ya moyo na ni chanzo cha matamanio ya haki. Hatua za kucheza ngoma zinahitaji nidhamu, lakini furaha ya dansi utakuja kuisikia tu pale unapokuja kusikia muziki wake.
Kuna wale wanaowakejeli waumini wa Kanisa kwa mambo tunayoyafanya. Hiyo inaeleweka. Wale wanaocheza ngoma mara kwa mara huonekana kama wako tofauti au wa ajabu au, kwa kutumia neno la kiinjili, “wa kipekee” (1 Peter 2:9) kwa wale ambao hawawezi kuusikia muziki. Ulishawahi kusimamisha gari yako kwenye taa za kuongozea gari karibu na gari ambapo dereva anacheza ngoma na kuimba kwa sauti ya juu? Lakini hauwezi kusikia sauti kwa sababu dirisha zako zimefungwa mpaka juu. Je! Si alionekana wa kipekee kweli? Kama watoto wetu watajifunza kucheza ngoma bila kujifunza kusikiliza na kuona uzuri wa muziki wa injili, mwishowe hawatakuwa na hamu ya kucheza ngoma na labda wataacha au kwa ubaya Zaidi, wataendelea kucheza ngoma kwa sababu tu ya kulazimishwa kutoka kwa wengine ambao wanacheza ngoma karibu na nao.
Changamoto kwetu sote ambao tunatafuta kufundisha injili ni kupanua wigo zaidi ya hatua za kucheza ngoma tu. Furaha ya watoto wetu inategemea katika uwezo wao wa kusikiliza na kupenda uzuri wa muziki wa injili. Tunawaweza kufanya vipi?
Kwanza, lazima tuweke maisha yetu katika kusikiliza masafa sahihi ya kiroho. Siku zilizopita, kabla ya karne ya digitali, tuliipata redio yetu tuliyoipenda kwa kutafuta kwa umakini stesheni mpaka ilipofikia na kusikika vizuri na masafa ya stesheni yetu. Tulipoikaribia namba, tuliweza kusikia mikwaruzo tu. Lakini mwishowe tulipotafuta stesheni vizuri, muziki wetu tunaoupenda ulisikika vyema. Katika maisha yetu, lazima tujifungamanishe na masafa sahihi ili kuusikiliza muziki wa Roho.
Tunapopokea kipawa cha Roho Mtakatifu baada ya ubatizo, tunajazwa na muziki wa mbinguni ambao unakuwa nasi katika uongofu wetu. Mabadiliko makuu ndani yetu au mioyoni mwetu, hata kwamba hatuna tamaa ya kutenda maovu tena, lakini kutenda mema daima” (Mosia 5:2). Lakini Roho hawezi kuwepo mahali penye ukali au kiburi au wivu. Kama tutapoteza ushawishi huo mzuri katika maisha yetu, upatanifu tele wa injili unaweza kwa haraka sana kupoteza sauti na mwishowe kuwa kimya kabisa. Alma aliuliza swali hili la kugusa: “Ikiwa mmesikia kuimba wimbo wa upendo wa ukombozi, ningewauliza mnaweza kuhisi hivyo sasa? (Alma 5:26).
Wazazi, kama maisha yetu hayako sambamba na muziki ya injili, tunatakiwa kuyaweka sawa. Kama Rais Thomas S. Monson alivyotufundisha Octoba iliyopita, lazima tufikirie njia za miguu yetu (ona “Ponder the Path of Thy Feet,” Ensign au Liahona, Nov. 2014, 86–88). Tunajua jinsi ya kufanya. Lazima tutembee katika njia sawa ambayo tuliitembea wakati tuliposikia kwa mara ya kwanza sauti za mbinguni za muziki wa injili. Tunafanyia kazi imani katika Kristo, kutubu, na kupokea sakramenti; ndipo tunaposikia kwa nguvu zaidi ushawishi wa Roho Mtakatifu, na muziki wa injili unaanza tena kucheza katika maisha yetu.
Pili, tunapoweza kusikia muziki wenyewe, tunalazimika kujaribu kwa bidii kuucheza katika nyumba zetu. Siyo kitu ambacho tunaweza kukilazimisha au kulazimishwa. “Hakuna nguvu wala uwezo unaoweza au upaswao kudumishwa kwa njia ya ukuhani”—au kwa kuwa baba au mama au mkubwa na mwenye sauti—“isipokuwa tu kwa njia ya ushawishi, kwa uvumilivu, kwa upole na unyenyekevu, … [na] kwa upendo usio unafiki” (M&M 121:41–42).
Kwa nini tabia hizi zinaongoza katika kuongezeka nguvu na ushawishi katika nyumba? Kwa sababu ni tabia ambazo zinaalika Roho wa Roho Mtakatifu. Ni tabia ambazo zinaweka mioyo yetu katika muziki wa injili. Zinapokuwepo, hatua za kucheza ngoma zitachezwa kwa urahisi kabisa na kwa furaha kwa wachezaji ngoma wote katika familia, bila haja ya vitisho au kushurutishwa au kulazimishwa.
Wakati watoto wetu ni wadogo, tunaweza kuwaimbia wimbo wa kubembeleza mtoto wenye upendo usioisha, na wanapokuwa watukutu na kugoma kwenda kulala usiku, tunaweza kuimba wimbo wa kubembeleza mtoto kwa uvumilivu na saburi. Wanapokuwa vijana, tunaweza kudharau sauti za hasira na mabishano na vitisho na, badala yake, kuimba wimbo mzuri wa kushawishi—na labda kuimba wimbo wa pili wa kubembeleza mtoto wa uvumilivu na saburi. Wazazi wanaweza kuimba katika upatanifu ulio kamili wenye tabia za utulivu na unyenyekevu. Tunaweza kuwakaribisha watoto wetu kuimba pamoja nasi katika umoja tunavyofanyia mazoezi ya wema kwa jirani ambaye anahitaji msaada.
Haitakuja yote kwa mara moja. Kama vile kila mwanamuzi aliyefanikiwa anavyojua, inachukua mazoezi yenye umakini kucheza muziki mzuri. Kama juhudi za mapema katika kutengeneza muziki zinaonekana kushindwa au kutokuwa na radha, kumbuka kwamba kutokuwa na radha hakuwezi kurekebishwa kwa hukumu Kukosekana kwa radha nyumbani ni sawa na giza katika chumba. Haisaidii kukaripia kiza. Tunaweza kuondoakiza kwa kuleta mwanga.
Hivyo kama besi katika kwaya ya familia yako iko juu sana na hawavumiliki, na kama sekisheni ya gita katika okestra ya familia yako ina ukemi au ina sauti kali kidogo au kama zile zumari tukutu zimetoka kwenye tuni au hazithibitiki, kuwa na subira. Kama hausikii muziki wa injili katika nyumba yako, tafadhali kumbuka maneno haya: endelea kufanya mazoezi. Kwa msaada wa Mungu, siku itafika ambapo muziki wa injili utajaza nyumba yako na shangwe isiyo na kifani.
Hata kama umechezwa vizuri, muziki hautatatua matatizo yako yote. Kutakuwa bado na vilele na vilindi katika maisha yako, utulivu na midundo. Hiyo ndio asilia na maisha yetu ya hapa duniani.
Lakini tunapoongeza muziki katika hatua za kucheza ngoma, wakati mwingine kuna midundo migumu ya ndoa na maisha ya kifamilia huenda kuelekea kwenye uwiano sawia. Hata changamoto zetu zitaongezea wingi wa sauti ya kuunga mkono vipande vya muziki vinavyotia moyo. Mafundisho ya ukuhani yataanzaa kutona tona kwenye mioyo yetu kama umande kutoka mbinguni. Roho Mtakatifu atakuwa mwenza wetu wa kila wakati, na mwenza—kielelezo sahihi cha nguvu na ushawishi—atakuwa mwenza asiyebadilika wa haki na ukweli. Na mamlaka yetu yatakuwa utawala wa milele. Na pasipo njia ya kulazimisha utatiririka kwetu milele na milele (ona M&M 121:45–46).
Na iwe hivyo katika maisha ya kila mmoja wetu na katika kila moja ya nyumba zetu ni maombi yangu katika jina la Yesu Kristo, amina.