Mfariji
Ninatoa ushahidi wangu kuwa Kristo anayeishi humtuma Roho Mtakatifu, Mfariji, kwa wale tunaahidi kumsaidia Yeye kufariji.
Dada zangu wapendwa, ni furaha kwangu kuwa nanyi. Mimi nimemfikiria mama yangu, mke wangu, mabinti zangu, mabinti wakwe zangu, mabinti wajukuu---wengi wao ambao wako hapa leo. Mpangilio huu wa ajabu umenifanya niwathamini zaidi. Nimegundua kupata kuwa na familia kama hiyo na maisha ya familia ya ajabu kama hayo uja kutokana na Mwokozi kuwa kitovu cha kila mmoja ya maisha yao. Tumemkumbuka usiku wa leo katika muziki, maombi, na kupitia mahubiri. Moja ya sifa za Mwokozi ambayo tunashukuru zaidi ni huruma Wake wa kipekee.
Usiku wa leo mmehisi kwamba Yeye anawajua na kuwapenda. Mmehisi upendo Wake walio karibu nanyi. Ni dada zenu, dada wa kiroho wa Baba yetu wa Mbinguni. Yeye anawajali kama anavyowajali ninyi. Anaelewa huzuni wote waliyonao. Anataka kuwasaidia.
Ujumbe wangu usiku wa leo ni kwamba mnaweza kuwa na sharti iwe ni sehemu muhimu Yake kutoa faraja kwa wale wanaohitaji faraja. Mnaweza kutekeleza sehemu yenu vyema Zaidi ikiwa mnajua jinsi anavyowajibu yale maombi kwa usaidizi
Wengi wanaomba kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya faraja, kwa ajili ya msaada wa kuibeba mizigo yao ya huzuni, upweke, na woga. Baba wa Mbinguni huyasikia maombi hayo na kuelewa mahitaji yao. Yeye na Mwanawee Mpendwa, Yesu Kristo mfufuka, wameahidi msaada.
Yesu Kriso ametupa ahadi hii tamu.
“Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo mizito, nami nitawapumzisha.
“Jifungeni nira yangu, na mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu.
“Maana nira niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”1
Mizigo ambayo watumishi Wake waaminifu lazima waibebe katika maisha inafanywa kuwa miepesi kwa Upatanisho Wake. Mzigo wa dhambi unaweza kuondolewa. Lakini majaribu ya maisha ya duniani dhidi ya watu wema bado yanaweza kuwa mizigo mizito.
Mmeona majaribu ya aina hii katika maisha ya watu wema muwapendao. Mkaguswa na tamaa ya kuwasaidia. Kuna sababu ya kuonyesha huruma dhidi yao.
Wewe ni muumini wa ahadi wa Kanisa la Yesu Kristo. Mabadiliko makubwa yalianza moyoni mwako pale ulipokuja katika Kanisa Lake. Uliweka agano, na ulipokea ahadi ambayo ilianza kubadilisha asili yako.
Alma alielezea, kwa maneno yake katika Maji ya Mormoni kile ulichokiahidi wakati wa ubatizo wako na kitakachomaanisha kwako na kila mtu aliye karibu nawe---hasa katika familia yako. Alikuwa akiongea na wale ambao walikuwa karibu kufanya maagano uliyofanya, nao pia walipokea ahadi ambayo Bwana ameiweka nawe.
“Tazameni, hapa kuna maji ya Mormoni (kwani hivi ndivyo yaliitwa) na sasa, kwa vile mnatamani kujiunga za zizi la Mungu, na kuitwa watu wake, na mko radhi kubeba mizigo ya mmoja na ya mwingine, ili iwe miepesi;
“Ndio, na mko tayari kuomboleza na wale wanaoomboleza; ndio, na kufariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa, na kusimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote, na katika mahali popote mlipo, hata hadi kifo, ili kuweza kukombolewa na Mungu, na kuhesabiwa pamoja na wale wa ufufuko wa kwanza, ili mpokee uzima wa milele.”2
Hii ndiyo sababu una mawazo ya kutaka kumsaidia anayetaabika kusonga mbele chini ya mzigo wa huzuni na mateso. Uliahidi kwamba utamsaidia Bwana kuifanya mizigo yao iwe miepesi na kufarijiwa. Ulipewa uwezo wa kuwasaidia kupunguza uzito wa mizigo hiyo pale ulipopokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Alipokaribia kusulubiwa, Mwokozi alielezea njia ambayo kwayo Anasaidia kufanya mizigo kuwa miepesi na kutoa nguvu za kuibeba. Alijua kuwa wafuasi Wake wangehuzunika. Alijua kuwa wataogopa. Alijua wangejisikia hofu juu ya maisha yao ya usoni. Alijua wangehisi wasiwasi juu ya uwezo wao wa kusonga mbele.
Hivyo akawapa hiyo ahadi ambayo anatupa sisi na kwa wafuasi Wake wote wa kweli:
“Na nitamwomba Baba, naye atawapa Mfariji mwingine, ili aweze kuwa nayi daima;
“Hata Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu hawamwoni, wala kumjua: ila ninyi mnamjua; kwani anakaa ndani yenu, na atakuwa nanyi.”3
Kisha Akaahidi:
“Lakini Mfariji, ambaye ni Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisheni kila kitu na kuwakumbusheni yote niliyowambieni.
“Ninawaachieni amani, nawapeni amani yangu: siwapi ninyi kama vile ulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi moyoni mwenu, wala msifadhaike.”4
Kwenye wiki chache zilizopita tu nimeiona ahadi hiyo ikitimizwa na katika maisha ya watoto waliokuwa wakiomba ili mizigo yao iwe miepesi. Muujiza wa mizigo kuwa miepesi inakuja katika njia aliyoahidi Bwana. Yeye na Baba Yake wa Mbinguni walimtuma Roho Mtakatifu kama Mfariji kwa wafuasi wake ili kusaidia.
Hivi majuzi vizazi vitatu vya familia vilikuwa vinaomboleza kifo cha mvulana wa mwenye umri wa miaka mitano. Alikufa kwa ajali akiwa na familia yake kwenye likizo. Nilipewa nafasi kutazama tena jinsi Bwana hubariki walio waaminifu na usaidizi na nguvu ya kuvumilia.
Nilitazama jinsi Bwana alivyofanya mizigo mikubwa kuwa miepesi. Nilikuwa hapo pamoja nao kama mtumishi wa maagano wa Bwana –na kadiri wewe utakavyokuwa daima katika maisha yako – “kuomboleza na wale wenye kuomboleza …na kuwafariji wale wanaohitaji faraja.”5
Kwa kuwa nilijua kuwa hiyo ilikuwa ukweli, nilifurahi na kuwa mwenye amani wakati mababu waliponialika kukutana nao na wazazi wa yule mvulana mdogo kabla ya mazishi.
Niliomba kujua jinsi ningemsaidia Bwana kuwafariji. Walikaa chini sebuleni mwetu. Niliweka joto kwenye chumba usiku huo uliokuwa wa baridi kwa moto mdogo kwenye meko.
Nilikuwa nimehisi kuwaambia kwamba niliwapenda. Niliwaambia nilikuwa nimehisi upendo wa Bwana kwao. Kwa maneno machache nilijaribu kuwaambia kuwa niliomboleza nao lakini kwamba Bwana pekee alijua na angepata uzoefu mkamilifu wa uchungu na huzuni wao.
Baada ya kusema maneno machache nilihisi msukumo kuwasikiliza kwa upendo wakizungumza kuhusu hisia zao.
Kwa muda tuliokaa pamoja, waliongea zaidi yangu mimi. Niliweza kuhisi katika sauti zao na kuona macho yao kwamba Roho Mtakatifu aliwagusa. Waliongelea jinsi ilivyotokea na jinsi walivyojisikia katika maneno rahisi ya ushuhuda. Roho Mtakatifu tayari alikuwa amewapa amani inayokuja na maneno ya matumaini ya uzima wa milele, wakati mwana wao alipokufa bila dhambi angekuwa wao milele.
Nilipowapa baraka za ukuhani, nilitoa shukrani kwa ajili ya uwepo wa Roho Mtakatifu pale. Mfariji alikuja akileta matumaini, ujasiri na ongezeko la nguvu kwa ajili yetu sote.
Usiku ule, niliona onyesho la jinsi Bwana anavyofanya kazi pamoja nasi ili kurahisisha mizigo ya watu wake. Unakumbuka katika Kitabu cha Mormoni wakati watu wake walipokaribia kuzidiwa na mizigo waliyotwishwa migongoni mwao na wasimamizi wakali.
Watu walisihi wapate msaada, kama wengi tuwapendao na kuwatumikia wanavyofanya. Hii ni kumbukumbu, ambayo ninajua ni ya kweli.
“Na pia nitawapunguzia mizigo ambayo imewekwa mabegani mwenu, hata kwamba hamtaisikia kamwe migongoni mwenu, hata mkiwa utumwani; na nitafanya haya ili muwe mashahidi wangu hapo baadaye, na kwamba mjue kwa hakika kwamba mimi, Bwana Mungu, huwatembelea watu wangu katika mateso yao.
“Na sasa ikawa kwamba mizigo ambayo ilikuwa wamewekewa Alma na ndugu zake ilipunguzwa, ndio, Bwana aliwapatia nguvu kwamba wabebe mizigo yao kwa urahisi, na walinyenyekea kwa furaha na subira kwa mapenzi ya Bwana.”6
Nimeona miujiza hiyo tena na tena. Tunaipunguza mizigo ya wengine kwa kumsaidia Bwana kuwaimarisha. Ndio maana Bwana ametujumuisha na kutuamuru kuwafariji wengine ili kuwa mashahidi muda wote na mahali pote.
Baba na mama wa mvulana yule mdogo walitoa ushuhuda wao wa Mwokozi jioni ile katika sebule yangu. Roho Mtakatifu alikuja. Wote tulifarijika. Wazazi walitiwa nguvu. Mzigo wa huzuni haukutoweka, lakini waliwezeshwa kubeba huzuni. Imani yao iliongezeka. Na nguvu zao zitaendelea kukua kadiri wao wanavyoomba na kuishi kwa ajili hiyo.
Ushahidi wa Roho Upatanisho uliokuja usiku huo pia ulimuimarisha Ayubu kuubeba mzigo wake:
“Kwani ninajua kwamba mkombozi wangu anaishi, mwishowe yeye atanipa haki yangu hapa hapa duniani:
“Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivyo, lakini katika mwili huu nitamwona Mungu.”7
Ilikuwa ni ushahidi huo wa Roho ambao ulimpa nguvu ya kuvumilia. Aliweza kukesha hadi asubuhi na ukosefu wa faraja toka kwa watu waliomzunguka kuona furaha ambayo inaweza kuja kwa waaminifu baada ya kuyapita majaribu yao kwa imani.
Ilikuwa kweli kwa Ayubu. Baraka zilimjia katika maisha haya. Habari za Ayubu zinaishia katika muujiza huu:
“Hivyo mwishowe Bwana alimbariki Ayubu kuliko hapo mwanzo. …
“Katika nchi yote hiyo hakukuwa na wanawake waliokuwa wazuri kama mabinti wa Ayubu: na baba yao akawaachia urithi kama alivyowaachia kaka zao.
“Baada ya hapo, Ayubu aliishi miaka mia moja arobaini, akawaona wajukuu na vitukuu vyake vyote hadi kizazi cha nne.
“Basi Ayubu akafariki akiwa mzee wa miaka mingi.”8
Ulikuwa ni kutoka kwa ushahidi wa Roho wa Upatanisho ambaoulimwezesha Ayubu kupitia kwa majaribu ya maisha ulidhamiriwa kujumuisha kila mmoja wetu. Hii ni sehemu ya mpango wa furaha ambao Baba ametupa. Alimruhusu Mwanae kujitolea, kama sadaka ya upatanisho tumaini ambalo linatufariji bila kujali ugumu ili turudi nyumbani Kwake ungekuwa vipi.
Baba na Mwana walimtuma Roho Mtakatifu ili kuwafariji na kuwaimarisha wafuasi wa Bwana katika safari yao.
Niliona muujiza huu wa faraja nilipowasili nje ya kanisa mahali ambapo msiba wa mvulana mdogo ungefanyika. Nilisimamishwa na mwanamke mwema ambaye sikumtambua. alikuwa akija kwa mazishi ili kuombolea na kuwapa faraja kama angeweza.
Alisema alikuwa amekuja mazishini kwa sababu kwa upande mmoja alitaka faraja mwenyewe. Aliniambia mwanawe wa kwanza amefariki hivi majuzi. Alikuwa akibeba mikononi mwake msichana mdogo mzuri. Niliegemea kwake kutazama kwenye uso wa tabasamu wa yule msichana mdogo. Nilimwuliza mama mtoto, “Jinalake nani?” Jibu lake la haraka na la furaha lilikuwa “Jina lake ni Furaha. Furaha mara nyingi huja baada ya huzuni.”
Alikuwa anatoa ushuhuda wake kwangu. Niliweza kuona faraja hiyo imekuja kwake ikitokea kwenye chanzo cha kweli. Ni Mungu Pekee aijuaye mioyo, na ndiye awezaye kusema katika kweli, “Ninajua unavyojisikia.” Hivyo ninaweza kufikiria furaha na huzuni yake iliyotangulia, lakini Bwana ampendaye anaijua.
Ninaweza kujua tu sehemu ya jinsi Yeye anavyohisi furaha kila wakati wewe, kama mfuasi Wake, unapomsaidia Yeye kuleta wakati wa amani na furaha kwa mtoto wa Baba Wetu wa Mbinguni
Ninatoa ushahidi wangu Bwana ametuomba kila mmoja wetu, wafuasiWake, kusaidia kuibeba mizigo ya mmoja kwa mwingine. Tumeahidi kufanya hivyo. Ninatoa ushuhuda wangu kwamba Bwana, kupitia Upatanisho Wake na Ufufuko, amevunja nguvu za kifo. Ninatoa ushahidi wangu kwamba Kristo aliyehai anatuma Roho Mtakatifu kwa wale tulioahidi kumsaidia kuwafariji.
Ninyi nyote ni mashahidi, kama nilivyo, wa ukweli wa maandishi kwenye bejiambayo mama yangu alivalia kwa Zaidi ya miaka 20 kama mshiriki wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Ilisoma “Hisani Haikosi Kufaulu Kamwe.”9 Bado sijui hasa maana ya maneno haya. Lakini nimeweza kutazama sehemu nilipomwona akiwafikia wale waliokuwa na haja. Maandiko yanatuambia “hisani ni upendo msafi wa Kristo.”10
Upendo wake haukosi kufaulu na hatukomi kuhisi katika mioyo yetu haja ya “kuomboleza na wanaoomboleza … na kuwafariji wanaohitaji faraja”11 Wala amani ambayo anaahidi kutuachia kamwe tunapowahudumia wangine kwa ajili Yake.
Kama shahidi Wake, ninatoa shukrani kwa yale mtendayo vyema katika kumsaidia Bwana Yesu Kristo anayeishi na Roho Mtakatifu, Mfariji kuimarisha magoti yaliyodhaifu na kuinua mikono iliyolegea.12 Ninashukrani, kwa moyo wangu wote, kwa wanawake wote katika maisha yangu ambao wamenisaidia na kunibariki kama wafuasi wake wa Yesu Kristo. Katika jina la Yesu kristo, amina.