“Je, Saumu Niliyoichagua, Siyo ya Namna Hii?”
Toleo lako la kufunga litafanya zaidi ya kusaidia kulisha na kuvika nguo miili. Litaponya na kubadili mioyo.
Wapendwa akina kaka na dada zangu, ni furaha kwangu kuelezea upendo wangu kwenu katika mkutano huu mkuu wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Furaha hiyo inakuja kutokana na ushahidi wa Roho kwamba upendo wa Mwokozi unafikia kila mmoja wenu na kwa wototo wote wa Baba wa Mbinguni. Baba yetu wa Mbinguni anatamani kubariki watoto Wake kiroho na kimwili. Anaelewa mahitaji yao yote, maumivu yao, na matumaini yao.
Tunapotoa usaidizi kwa yeyote, Mwokozi anaona ni kama tulijitolea kumsaidia Yeye.
Alituambia hiyo ilikuwa kweli alipoelezea muda wa siku zijazo sote tutakuwa nao tutakapomuona baada ya maisha yetu katika dunia hii kukamilika. Picha akilini mwangu ya siku hiyo imekuwa dhahiri zaidi katika siku ambazo nimeomba na kufunga ili kujua kile cha kusema asubuhi hii. Maelezo ya Bwana juu ya mahojiano ya siku za usoni yalitolewa kwa wanafunzi Wake, na yanaelezea juu ya nini tunachokitaka kwa mioyo yetu yote kuwa ni kweli hata kwetu sisi pia:
“Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini mfalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu:
“Kwa maana nilikuwa na njaa, mkanipa chakula; nilikuwa na kiu, mkaninywesha; nilikuwa mgeni, mkanikaribisha:
“Uchi, mkanivika, nilikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama: nilikuwa kifungoni, mkanijia.
“Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha? Au una kiu tukakunywesha?
“Ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha? Au u uchi tukakuvika?
“Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
“ Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”1
Wewe na mimi tunataka karibisho hilo la upendo kutoka kwa Mwokozi. Lakini tunawezaje kustahili? Kuna wengi wa watoto wa Baba wa Mbinguni ambao wananjaa, hawana makazi na wana upweke kuliko wale tunaoweza kuwasaidia. Na idadi inakuwa kubwa zaidi na zaidi kuliko tunavyoweza kuwasaidia.
Hivyo basi Bwana ametupa kitu ambacho sote tunaweza kufanya. Ni amri rahisi sana kiasi kwamba hata mtoto anaweza kuielewa. Ni amri iliyo na ahadi nzuri kwa walio na shida na kwetu sisi.
Ni sheria ya mfungo. Maneno katika kitabu cha Isaya ni maelezo ya Bwana ya amri na baraka inayopatikana kwa ajili yetu sisi tulio wa Kanisani Lake
“Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
“Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
“Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
“Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;
“Na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
“Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.”2
Hivyo basi Bwana ametupa amri rahisi na ahadi ya ajabu. Kanisani siku za sasa tunapewa fursa ya kufunga mara moja kwa mwezi na kutoa toleo karimu la mfungo kupitia kwa askofu wetu ama rais wa tawi kwa ajili ya kuwasaidia masikini na walio na shida. Kiasi fulani kitatumiwa kuwasaidia wale walio karibu nawe, pengine mtu katika familia yako mwenyewe. Watumishi wa Bwana wataomba na kufunga kwa ajili ya ufunuo kujua wa kuwasaidia na msaada wa kutoa. Kile ambacho hakihitajiki kusaidia watu katika tawi la Kanisa la eneo lako kitapelekwa kuwabariki waumini wengine wa Kanisa duniani kote, walio na shida.
Sheria ya mfungo kwa ajili ya maskini ina baraka nyingi zinazoambatana nayo. Rais Spencer W. Kimball alikuita kushindwa kufuata sheria hiyo ni dhambi ya kutotenda iliyo na gharama kubwa. Aliandika: “Ahadi mzuri zinatolewa na Bwana kwa wale wanaofunga na kusaidia walio na shida. ...Ushawishi na uongozi wa kiroho utakuja kupitia wema na kuwa karibu na Baba wa Mbinguni. Kupuuza kufanya kitendo hiki chema cha kufunga kutatunyima baraka hizi.”3
Nilipokea moja ya baraka hizo siku chache tu zilizopita. Kwa kuwa mkutano mkuu unaangukia wikendi ambayo kwa kawaida ingejumuisha mkutano wa mfungo na ushuhuda, nilifunga na kuomba ili kujua jinsi ambavyo mimi ningeweza bado kutii amri ya kuwajali walio na shida.
Jumamosi, nikiwa bado ninafunga, niliamka saa 12:00 asubuhi na kuomba tena. Nilihisi kuvutiwa kuangalia habari ya dunia. Hapo nilisoma ripoti hii:
“Kimbunga cha Kitropiki Pam kiliharibu nyumba nyingi kilipogonga Port Vila, mji mkuu wa Vanuatu. Kiliua takribani watu sita kule Vanuatu, taarifa ya kwanza kuthibitishwa ya vifo vilivyotokana na dhoruba yenye nguvu sana iliyowahi kuipiga nchi.
“Ilikuwa vigumu kuona mti ulio simama wima kimbunga kilipokuwa kinapita nchi hiyo ya kisiwa cha Pasifiki.4
“Timu ya World Vision ya kutathmini dharura ilipanga kuangalia uharibifu baada dhoruba kukoma.
“Waliwashauri wakaazi watafute makazi katika majumba imara kama vile vyuo vikuu na mashule.
And kisha wakasema: “Kitu imara zaidi walicho nacho ni makanisa yaliyojengwa kwa saruji, ’ alisema Inga Mepham kutoka CARE International. Baadhi yao hawana hivyo. Ni vigumu kupata jumba ambalo ungedhani linaweza kuhimili dhoruba ya kiwango cha 5.”5
Niliposoma hayo nilikumbuka kutembelea nyumba kule Vanuatu. Niliweza kuvuta taswira katika akili yangu na kuona watu wakiwa wamerundikanaa katika nyumba zilizoharibiwa na upepo. Na kisha nikakumbuka makaribisho ya upendo kwangu niliyopewa-na watu wa Vanuatu. Niliwafikiria na majirani zao wakikimbia kuelekea mahali pa usalama kwenye kanisa letu la-saruji.
Kisha nilipiga taswira akilini na kumwona askofu na rais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wakitembea miongoni mwao, wakitoa faraja, blanketi, chakula, na maji ya kunywa. Nilipiga taswira akilini nawaona watoto walio na hofu wakiwa wamekusanyika pamoja.
Wako mbali sana na nyumba ambapo nilisoma ripoti hio, na bado nilijua Bwana angefanya nini kupitia watumishi Wake. Nilijua kile kilichowawezesha kuwasaidia watoto wale wa Baba wa Mbinguni kilikuwa matoleo ya mfungo, yaliyotolewa kwa hiari na wanafunzi wa Bwana ambao wako mbali sana lakini karibu na Bwana.
Hivyo basi sikusubiri hadi Jumapili. Nilipeleka toleo la mfungo kwa Askofu wangu asubuhi hiyo. Najua toleo hilo linaweza kutumika na Askofu na rais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kusaidia mtu katika kitongoji changu. Toleo langu ndogo huenda lisihitajike karibu na ambapo familia yangu na mimi tunaishi, na toleo langu la ziada huenda lisifike Vanuatu.
Lakini dhoruba zingine na majanga yatakuja duniani kote kwa watu ambao Mungu anawapenda na ambao huzuni yao anaijua. Sehemu ya toleo lako la mfungo na langu la mwezi huu litatumika kumsaidia mtu, mahali fulani, msaada ambao Bwana ataona kama anasaidiwa Yeye mwenyewe.
Toleo lako la mfungo litafanya zaidi ya kusaidia kulisha na kuvika nguo miili. Litaponya na kubadili mioyo. Tunda la kutoa kwa hisani binafsi huenda ikawa nia katika moyo wa mpokeaji ili kuwafikia wengine walio na shida. Hicho hutendeka duniani kote.
Kilitendeka kwa maisha ya Dada Abie Turay, ambaye anaishi Sierra Leone. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza mwaka 1989. Viliikumba nchi kwa miaka. Sierra Leone tayari ilikuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani. Wakati wa vita haikuwa wazi ni nani aliyeidhibiti nchini---benki … zilifungwa, ofisi za serikali ziliharibiwa, vikosi vya polisi vilikuwa [havifui dafu dhidi ya vikosi vya waasi], … na kulikuwa na machafuko, mauaji, na huzuni. Makumi ya maelfu ya watu walipoteza maisha yao, na zaidi ya watu milioni mbili walilazimika kuhama makazi yao ili kuepuka kuuawa.6
Hata katika nyakati kama hizo, Kanisa la Yesu Kristo wa Watakatifu wa Siku za Mwisho lilikua.
Tawi moja la kwanza liliundwa katika mji ambapo Dada Turay aliishi. Mume wake alikuwa rais wa kwanza wa tawi. Alihudumu kama rais wa wilaya wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
“Wakati wageni wanapotembelea nyumbani mwa Dada Turay [sasa,] anapenda kuwaonyesha [hazina] mbili kutokana na vita: shati iliyo na mistari ya bluu-na-nyeupe [alilipata] kutoka mitumba ya nguo zilizotumika [iliyotolewa na waumini wa Kanisa] na blanketi, sasa imezeeka na kujawa na matundu.”7
Anasema: “Shati hili ni vazi la kwanza … [nililopokea]. … Nilikuwa ninaivaa kwenda kazini [na]---lilikuwa zuri sana. [Linifanya kujisikia mrembo sana] na sikuwa na nguo nyingine.”
“Wakati wa vita, blanketi hili lilitupa joto, mimi na watoto wangu. Wakati waasi [wangekuja] kutushambulia, hiki kilikuwa kitu cha pekee [ningeweza] kubeba mikononi mwangu [tukikimbia msituni kujificha]. Hivyo basi [tungechukua] blanketi hili pamoja nasi. Lingetupa joto na kutukinga dhidi ya mbu.”8
“Dada Turay anazungumzia shukrani yake kwa ajili ya rais wa misheni ambaye angekuja katika nchi iliyoharibiwa na vita na [pesa] mfukoni.” Fedha hizo, kutoka mchango wa toleo la mfungo wa mtu kama wewe, ziliruhusu Watakatifu kununua chakula ambacho wengi wa Wasierra Leone hawangeweza kununua kwa bei ambayo wangemudu..9
Dada Turay, akizungumza juu ya wale ambao walikuwa wakarimu vya kutosha kuchangia kwa ajili ya wao kuishi, anasema, “Ninapofikiria juu ya watu ambao walifanya hivi ninahisi kwamba walitumwa na Mungu, kwa sababu wanadamu wa kawaida walionyesha ishara hii ya ukarimu kwetu sisi.”10
Mgeni kutoka Marekani aliketi na Abie si muda mrefu uliopita. Muda huo akiwa pamoja naye, macho yake yakawa “yanavutiwa na seti ya maandiko ambayo ilikuwa juu ya meza.” Aliweza kuona kwamba maandiko haya yalikuwa hazina, “yalikuwa yamewekewa alama vyema na maelezo pembeni yake. Kurasa zilikuwa zimezeeka; baadhi zilikuwa zimeraruka. Jalada lilikuwa limetoka.”
Alishika maandiko mkononi mwake na polepole akafungua kurasa. Akifanya hivyo, alipata nakala ya slipu ya manjano ya michango ya zaka. Akaona kwamba katika nchi ambapo dola ilikuwa ya thamani sana, Abie Turay alikuwa amelipa dola moja kama zaka yake, dola moja kwa mchango kwa wamisionari, na dola moja kama toleo la mfungo, kwa wale ambao, kwa maneno yake, walikuwa “maskini kweli.’”
Mgeni alifunga maandiko ya Dada Turay na kuwaza, akisimama pamoja na huyu mama Mwafrika mwaminifu, kwamba alikuwa katika ardhi takatifu .11
Kama tu vile upokeaji wa baraka za toleo lako la mfungo na langu zinaweza kubadili mioyo, ndivyo pia kufunga kwa ajili ya mema ya mwingine. Hata mtoto mdogo anaweza kuihisi .
Watoto wengi, na baadhi ya watu wazima, huenda kwa sababu moja ama ingine wanaona mfungo wa saa 24 kuwa ni vigumu. Inaweza kuwa hivyo, kwa maneno ya Isaya, wakahisi kwamba mfungo “umetaabisha nafsi zao.” Wazazi wenye hekima wanatambua uwezekano huo na hivyo basi wako makini kufuata ushauri wa Rais Joseph F. Smith: “Bora kuwafundisha kanuni na kuwaacha waifuate wakati wakiwa watu wazima wataweza kuchagua kwa busara.”12
Niliona baraka katika ushauri huo hivi karibuni. Mmoja wa wajukuu wangu aliona mfungo wa saa 24 kuwa vigumu kwake kuvumilia. Lakini wazazi wake wenye hekima bado walimhimiza kanuni moyoni mwake. Mmoja wa marafiki zake shuleni alipoteza binamu mchanga kwa kifo cha ajali. Mjukuu wangu alimuuliza mama yake siku ya mfungo, karibu na wakati ule ambao daima alikuwa anona mfungo ni jambo gumu sana, kama yeye kuendelea kufunga kungemfanya rafiki yake aliyekuwa anaomboleza kujisikia vizuri zaidi.
Swali lake lilikuwa uthibitisho wa ushauri wa Rais Joseph F. Smith. Mjukuu wangu alikuwa amefikia kiwango ambacho hakuelewa tu kanuni ya mfungo, lakini ilikuwa imepandwa moyoni mwake. Alikuwa amekuja kujua kwamba kufunga kwake na sala kungeelekeza baraka kutoka kwa Mungu kwenda kwa mtu aliye na shida. Kama akiishi kanuni hii mara nyingi vya kutosha, italeta athari nzuri katika maisha yake mwenyewe yaliyoahidiwa na Bwana. Atakuwa na baraka ya kiroho ya uwezo wa kupokea maongozi ya kiuungu na uwezo mkubwa wa kushinda majaribu.
Hatujui sababu zote kwa nini Yesu Kristo alienda nyikani kufunga na kusali. Lakini tunajua angalau tukio moja: Mwokozi alishinda kabisa majaribu ya Shetani ya kutumia vibaya uwezo Wake wa uungu.
Muda mfupi tunaofunga kila mwezi na kiasi kidogo tunachotoa kwa ajili ya maskini huenda ukatupatia sehemu ndogo tu ya mabadiliko katika asili yetu kuwa na kutokutamani kufanya maovu. Lakini kuna ahadi kubwa, hata kadiri tunavyofanya yote tunayoweza kwa kiwango cha maana kufanya kwa kusali, kufunga, na kuchanga kwa ajili ya wale wenye shida:
“Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
“Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa.”13
Ninaomba kwamba tutafanya bidii tupokee baraka hizo kuu kwa ajili yetu na familia zetu.
Ninatoa ushuhuda wangu kwamba Yesu ndiyeKristo, kwamba katika Kanisa Lake tunaalikwa tumsaidie anapowasaidia maskini kwa njia Yake, na kwamba anaahidi baraka za milele zitakuja kutokana na kumsaidia Yeye. Katika jina la Yesu Kristo, amina.