Kumsubiri Mwana Mpotevu
Na ninyi nami tupokee ufunuo wa kujua namna nzuri ya kuwafikia wale kwenye maisha yetu waliopotea.
Mwokozi Yesu Kristo alitumia muda wake wa huduma hapa duniani kufundisha kuhusu uponyaji wake na nguvu ya ukombozi. Wakati fulani katika Luka mlango wa 15 katika agano Jipya, hasa alilaumiwa kwa kula na kutumia muda na watenda dhambi (ona Luka 15:2). Mwokozi alitumia shutuma hii kama fursa kuwafundisha wote jinsi ya kuwajibu wale waliopotea kutoka kwenye injili.
Aliwajibu wapinzani wake kwa kuwauliza maswali mawili muhimu:
“Hivi, mtu akiwa na kondoo mia, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate?”(Luka 15:4).
“Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha, akipoteza moja, Atawasha taa, aifagie nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate”(Luka 15:8).
Mwokozi baadaye anafundisha fumbo la mwana mpotevu. Fumbo hili halihusu kondoo 100 au sarafu kumi za fedha; ni kuhusu mwana mmoja wa dhamani aliyepotea. Kupitia fumbo hili, nini Mwokozi anatufundisha kuhusu jinsi ya kujibu wakati wanafamilia anapopoteza mwelekeo?
Mwana mpotevu alimjulisha baba yake kwamba anataka urithi wake sasa. Anataka kuondoka kwa usalama nyumbani kwao na familia yake na aende kutafuta mambo ya kidunia (ona Luka 15:12–13). Tafadhali jua kwamba katika fumbo la Mwokozi baba kwa upendo aliitikia kwa kumpa mwanae uridhi wake. Nina uhakika baba yake atakuwa alifanya kila anachoweza kumshawishi mwanae kubaki. Ingawaje, mara tu mtu mzima anapofanya maamuzi yake, baba mwenye hekima humuacha aende. Hivyo baba anaonyesha upendo wa dhati, na kumuangalia mwanae na kusubiri (ona Luka 15:20).
Familia yangu ilikuwa na uzoefu unaofanana na huo. Kaka zangu wawili waaminifu, dada zangu wazuri, na mimi tulilelewa na wazazi wenye mifano mizuri. Tulifundishwa injili katika nyumba yetu, na tukafanikiwa katika ukubwa wetu, na sisi wote wanne tuliunganishwa hekaluni na wenza wetu. Hata hivyo, mnamo 1994 dada yetu, Susan, alikosa furaha na Kanisa na baadhi ya mafundisho. Alishawishiwa na wale waliomdhihaki na kuwashutumu viongozi wa kwanza wa Kanisa. Aliruhusu imani yake katika manabii wanaoishi na mitume kupotea. Baada ya Muda, shaka zake zikawa juu ya imani yake, na akachagua kuachana na Kanisa. Susan amenipa ruhusu ya kuwaelezeeni hidithi yake kwa tumaini kwamba liweze kuwasaidia wengine.
Kaka zangu na mimi na mjane mama yetu tulijawa na huzuni. Hatukuweza kufikiria ni kitu gani ambacho kilichomsababisha kuiacha imani yake.
Kaka zangu na mimi tumetumikia kama maaskofu na marais wa akidi, na tulipata uzoefu wa furaha ya mafanikio kwenye kata na washiriki wa akidi tupowaacha wale tisini na tisa na kumfuata yule mmoja. Ingawaje, kwa dada yetu, juhudi zetu endelevu za kumuokoa na kumkaribisha tena zilimpeleka mbali na mbali zaidi.
Tunapotafuta mwongozo wa mbinguni kwamba ni jinsi gani ya kumjibu sawa sawa, ilikuwa dhahiri kuwa tufuate mfano wa baba katika fumbo la mwana mpotevu. Susan alikuwa amefanya maamuzi yake, na tulitakiwa kumuacha aende—lakini si bila yeye kujua na kuhisi upendo wetu wa dhati kwake. Na pia, kwa upendo na huruma uliofanywa upya, tuliangalia na kusubiri.
Mama yangu hakusita kamwe kumpenda na kumjali Susan. Kila mara mama yangu alipohudhuria hekaluni, aliweka jina la Susan katika mzunguko wa maombi, bila kupoteza tumaini. Kaka yangu mkubwa na mke wake, ambao waliichi karibu sana na Susan huko California, walimualika katika shughuli za kifamilia. Waliandaa chakula cha jioni katika nyumba yao kila mwaka katika siku ya kuzaliwa ya Susan. Walihakikisha walikuwa katika mawasiliano naye na alijua kuhusu upendo wao wa dhati.
Mdogo wangu wa kiume na mke wake waliwaendea watoto wa Susan huko Utah na kuwajali na kuwapenda. Walihakikisha kwamba watoto wake walialikwa katika mikusanyiko ya familia, na ilipofikia wakati wa mjukuu wa kike wa Susan kubatizwa, kaka yangu alikuwepo kufanya ibada hiyo. Susan pia alikuwa na walimu watembeleaji wenye upendo ambao hawakukata tamaa.
Watoto wetu walipoenda kutumika misheni na walipota wenza kwenye ndoa, Susan alialikwa na kuhudhuria sherehe hizi za kifamilia. Tulijaribu kwa umakini kutengeneza matukio ya kifamilia ili kwamba Susan na watoto wake wawe pamoja sisi na wajue kwamba, juu ya yote haya, tunawapenda na tulikuwa sehemu ya familia. Susan alipopokea shahada ya juu katika Chuo Kikuu cha California, tulikuwepo wote kumuunga mkono kwenye sherehe za mahafali. Ingawa hatukuweza kukubali maamuzi yake yote, kwa hakika tuliweza kumkumbatia. Tulimpenda, kumuangalia, na kusubiri.
Mnamo 2006, baada ya miaka 12 kupita baada ya Susan kuliacha Kanisa, mtoto wetu wa kike Katy alihamia yeye na mme wake California ili aweze kuhudhuria katika chuo cha sheria. Walikuwa mji mmoja na Susan. Wenza hawa wachanga walimtegemea shangazi yao Susan kwa msaada na uungwaji mkono, na walimpenda. Susan alisaidia kumlea mjukuu wetu wa kike wa miaka miwili, Lucy, na Susan akajikuta akimsaidia Lucy na maombi ya kila usiku. Katy alinipigia simu siku moja na kuniuliza kama alifikiria kwamba Susan angeweza kurudi kanisani tena. Nilimuhakikishia kwamba nilihisi angeweza kufanya hivyo na kwamba tulihitajika kuendelea kuwa na subira. Jinsi miaka mingine mitatu ilivyopita, kwa upendo endelevu, tuliangalia na kusubiri.
Miaka sita iliyopita juma hili mke wangu, Marcia, na mimi tulikuwa tumekaa mstari wa mbele kwenye Ukumbi wa Mikutano. Nilikuwa nisimikwe kama Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka siku hiyo. Marcia, ambaye mara zote ana mawasiliano ya karibu na Roho, aliandika kijikaratasi ambacho kilikuwa kinasoma, “Nafikiri ni wakati wa Susan kurudi.” Mtoto wangu Katy alishauri kwamba niondoke na kumpigia Susan kumualika kuangalia mkutano mkuu siku hiyo.
Kwa ushawishi wa wanawake hawa wakuu wawili, nilitembea kwenye baraza na kumpigia simu dada yangu. Nilikutana na ujumbe wa kurekodiwa na kwa urahisi tu nikamualika kuangalia hicho kikao cha mkutano muu. Alipata ujumbe. Kwa mshangao wetu, alipata hamasa ya kuangalia mkutano mkuu wote. Alisikia kutoka kwa manabii na mitume aliokuwa amewapenda miaka kadhaa iliyopita. Alikutana na majina mapya ambayo hakuwahi kuyasikia kabla, kama vila Rais Uchtdorf na Mzee Bednar, Cook, Christofferson, na Andersen. Katika kipindi hiki na vipindi vya kipekee vilivyoshushwa toka mbinguni, dada yangu—kama mwana mpotevu—alijirudia (ona Luka 15:17). Maneno ya manabii na mitume na upendo wa familia ulimgusa na kugeuka na kuanza kurudi tena nyumbani. Baada ya miaka 15 binti yetu na dada yetu ambaye alikuwa amepotea amepatikana. Kuangalia na kusubiri vilikuwa vimekwisha.
Susan anaelezea uzoefu huu kama vile Lehi alivyouelezea katika Kitabu cha Mormoni. Aliachilia fimbo ya chuma na kujikuta katikati ya kiza kinene (ona 1 Nefi 8:23). Anasema kwamba hakujua kwamba amepotea mpaka imani yake ilivyokuwa imeamshwa na nuru ya Kristo, ambayo kwa iliweka bayana sana kati ya kile alichokuwa akikipata duniani na kile ambacho Bwana na familia yake walikuwa wakimpa.
Miujiza imetokea katika kipindi cha miaka sita. Susan amepata ushuhuda mpya wa Kitabu cha Mormoni. Amepokea kibali chake cha hekaluni. Ametumikia kama mtoa ibada hekaluni, na kwa sasa hivi anafundisha darasa la Mafundisho ya Injili katika kata yake. Madirisha ya mbinguni yamefunguliwa kwa watoto na wajukuu wake, na ingawa kumekuwa na matokeo magumu, inaonekana kama vile hakuwahi kuondoka.
Wengi wenu, kama familia ya Nielson, mna wanafamilia ambao kwa wakati wamepotea kwenye njia. Maelekezo ya Mwokozi kwa wote wenye kondoo 100 ni kuacha wale tisini na tisa na kwenda kumuokoa yule mmoja. Maelekezo yake kwa wale wenye vipande 10 vya fedha na kupoteza kimoja ni kutafuta mpaka ukipate. Kama aliyepotea ni mwanao au binti yako, kaka yako au dada yako na yeye ameamua kuondoka, tunajifunza katika familia kwamba, baada ya yote tunayoweza kuyafanya, tunampenda yule mtu kwa moyo wetu wote na kumuangalia, tunaomba, na kusubiri kwa ajili ya mkono wa Bwana kudhihirika.
Labda somo la muhimu sana Bwana amenifundisha katika mchakato huu iliotokea wakati wa kusoma maandiko kama familia baada ya dada yangu kuliacha Kanisa. Mtoto wetu David allikuwa anasoma wakati tunajifunza pamoja Luka 15. Aliposoma fumbo la mwana mpotevu, Nilisikia tofauti siku hiyo zaidi ya nilivyowahi kulisikia kabla ya hapo. Kwa sababu kadhaa, nilikuwa nalinganisha na mtoto aliyebaki nyumbani. Jinsi David alivyokuwa anasoma asubuhi ile, nikagundua kwamba kwa namna nyingine mimi nilikuwa mwana mpotevu. Sisi sote tumepungukiwa na utukufu wa Mungu (ona Warumi 3:23). Sisi sote tunahitaji Upatanisho wa Mwokozi kutuponya. Sisi sote tumepotea na tunahitaji kutafutwa. Ufunuo huu siku ile ulitusaidia kujua kwamba dada yangu na mimi wote tulihitaji Upendo wa Mwokozi na Upatanisho Wake. Susan na mimi kwa hakika tulikuwa katika njia moja kurudi nyumbani.
Maneno ya Mwokozi katika fumbo kama alivyoelezea baba kumlaki mwana mpotevu yana nguvu, na naamini yanaweza kuwa maelezo ya uzoefu ambao mimi na wewe tunaweza kuwa nayo na Baba yetu tunaporudi kwenye nyumba yetu ya Mbinguni. Yanatufundisha juu ya baba ambaye anapenda, anasubiri, na kuangalia. Haya ni maneno ya Mwokozi: “Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu” (Luka 15:20).
Na ninyi na mimi tupokee ufunuo kujua jinsi gani kuwafikia wale katika maisha yetu ambao wamepotea na, itakapohitajika, kuwa na subira na upendo wa Baba yetu wa Mbinguni na Mwanae Yesu Kristo, tunapowapenda, kuwaangalia, na kusubiri mwana mpotevu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.