Kuhusu kuwa mkweli
Mimi ninaomba kwamba tutaweza kushinda majaribu ya kuvuta usikivu kwetu wenyewe na, badala yake, jitahidi kwa heshima kuu: kuwa wanyenyekevu, wafuasi wakweli wa Yesu Kristo.
Mwishoni mwa karne ya 18, Catherine Mkuu wa Urusi alitangaza kwamba angetembelea sehemu ya kusini ya himaya yake, akifuatana na mabalozi kadha wa kigeni. Gavana wa eneo, Grigory Potemkin, alitaka sana kuwavutia wageni hawa. Na aliweka juhudi kubwa katika kujaribu kusisitiza mafanikio ya nchi.
Kwa sehemu ya safari, Catherine alielea akielekea sehemu ya chini ya mto Dnieper, kwa majivuno akiwaonyesha mabalozi vijiji vidogo vyenye ufanisi kando kando ya ufuo vilivyojaa wachapa kazi na watu wa mjini wenye furaha. Kulikuwa na tatizo moja tu: yote yalikuwa kwa maonyesho tu. Imasemekana kwamba Potemkin alikuwa amekusanya maduka na nyumba za bandia zilizotengenezwa kutoka mbao nyembamba. Yeye hata aliwaweka wakulima wachapakazi ili kuonyesha uchumi unaostawi. Mara tu walipopita kupiga kona yam to, Watu wa Potemkin wabomoa kijiji bandia na na kukiharakisha mbele katika matayarisho hadi pale Catherine angepitia.
Ingawa wanahistoria wa sasa wamehoji ukweli wa hadithi hii, neno “Potemkin Village” limeingia katika msamiati wa ulimwengu. Sasa linahusu jaribio lolote la kufanya wengine waamini sisi ni bora zaidi kuliko tulivyo.
Je! Mioyo Yetu iko kwenye Sehemu Sahihi?
Ni sehemu ya hulka ya binadamu kutaka kuonekana kuwa bora zaidi. Ndiyo sababu wengi wetu tunafanya kazi kwa bidii nje ya nyumba zetu na ndiyo sababu makuhani wetu wa Haruni vijana wana hakikisha kila unywele upo katika sehemu yake, isije wakakutana na mtu fulani maalum. Hakuna ubaya wowote kwa kuving’arisha viatu vyetu, kunukia vizuri, au hata kuficha vyombo vyetu vichafu kabla mwalimu wa nyumbani hajafika. Hata hivyo, wakati inapofanywa kupita kiasi, tamaa hii ya kutaka kuvutia inaweza kubadilika kutoka kuwa ya manufaa na kuwa ya ulaghai.
Manabii wa Bwana wakati wote wamepaza sauti za kuonya dhidi ya hao ambao “wanakuja karibu [kwa Bwana] kwa vinywa vyao na pamoja na midomo ina mheshimu [Yeye], lakini wametoa mioyo yao mbali kutoka [Kwake].”1
Mwokozi alikuwa mwelewa na mwenye huruma kwa wenye dhambi ambao mioyo yao ilikuwa minyenyekevu na ya kweli. Lakini alipandwa na hasira ya haki dhidi ya wanafiki kama waandishi, Mafarisayo na Masadukayo---wale ambao walijaribu kuonekana wenye haki ili kupokea sifa, ushawishi na utajiri wa ulimwengu, na wakati huo huo wakidhulumu watu ambao wangekuwa wakiwabariki. Mwokozi aliwafananisha na “makaburi meupe, ambayo kwa kweli yanaonekana mazuri kwa nje, lakini yamejaa mifupa ya watu walio kufa, na unajisi wote.”2
Katika siku zetu, hali kadhalika Bwana ana maneno makali kwa wenye kushikilia ukuhani wanao jaribu “kuficha dhambi [zao], au kufurahisha kiburi[chao], au malengo [yao] ya bure yasiyofaa.” Wanapofanya hivi, Alisema “mbingu zina zinajitoa zenyewe; Roho wa Bwana anahuzunishwa; na wakati anapoondolewa, amina kwa ukuhani au mamlaka ya mtu yule.”3
Kwa nini hii inatokea? Kwa nini sisi wakati mwingine tunajaribu kuonekana watendaji, wenye kustawi, na kujiweka wema kwa nje wakati ndani yetu---kama Mfunuaji alivyosema juu ya Waefeso---“tumeacha upendo [wetu] wa kwanza”?4
Katika baadhi ya masuala, tumepoteza fokasi yetu kwenye kusudi kuu la injili, kukosea “umbo la kumcha Mungu” na kwa“nguvu yake.”5 Hii hususani ni hatari wakati tunapoelekeza mwonekano wetu wa nje wa ufuasi kuwavutia wengine kwa faida binafsi au ushawishi. Kisha ndipo kwamba tuko hatarini ya kuwa kama Mafarisayo, muda ni sasa kutathimini mioyo kufanya mabadiliko mara moja ambayo yanahitajika.
Mipango ya Potemkin
Jaribu hili la kuonekana bora kuliko tulivyo linapatikana katika maisha yetu binafsi lakini pia linaweza kupatikana katika kazi za Kanisa letu vile vile.
Kwa mfano, ninajua kuhusu Kigingi ambako viongozi waliweka tamaa ya malengo makuu kwa mwaka ule. Wakati malengo yote yalionekana ya kufaa, walisisitiza ama kwa ufahari na matangazo ya kuvutia au kwenye namba na asili mia.
Baada ya malengo haya kujadiliwa na kukubaliwa, kitu fulani kikaanza kumletea matatizo Rais wa Kigingi. Alifikiri kuhusu waumini wa kigingi chake---kama vile mama kijana mwenye watoto wadogo ambaye hivi karibuni aliachwa mjane. Alifikiri kuhusu waumini ambao walikuwa wakipambana na mashaka au upweke au hali mbaya za afya na bila bima ya afya. Alifikiri kuhusu waumini ambao walikuwa wanashughulikia ndoa zilizovunjika, wenye uteja, wasio na ajira, wenye magonjwa ya akili. Na zaidi alivyozidi kufikiria kuhusu wao, na zaidi alijiuliza mwenyewe swali la kinyenyekevu: malengo yetu mapya yataleta mabadiliko katika maisha ya waumini hawa?
Alianza kushanga jinsi malengo ya kigingi chao yangeweza kuwa tofauti kama kwanza wangekuwa wameuliza, “Huduma yetu ni nini?”
Kwa hiyo rais huyu wa kigingi alijadili tena na mabaraza, na pamoja walihamisha msisitizo wao. Waliamua kwamba hawataruhusu “wenye njaa, … wenye mahitaji, … walio uchi, wagonjwa, na wanaoteseka, kuwapita bila wao kuwaona.”6
Waliweka malengo mapya, wakitambua kwamba mafanikio ya malengo haya mapya yasingeweza siku zote kupimwa, angalau sio na mtu---kwani ni kwa jinsi gani mtu aweza kupima ushuhuda binafsi, upendo wa Mungu, au huruma kwa wengine?
Lakini pia walijua kwamba “vitu vingi unavyoweza kuhesabu sio vya muhimu, na vitu vingi usivyoweza kuhesabu ni muhimu.”7
Ninashangaa kama utaratibu wetu na malengo binafsi yanaweza wakati mwingine kuwa mfano wa kisasa wa kijiji cha Potemkin. Je yanaonekana ya kuvutia kutoka kwa mbali lakini yanashindwa kutoa msaada kwa mahitaji halisi ya wapendwa binadamu wenzetu?
Marafiki zangu wapendwa na wenza mnaoshililia ukuhani, kama Yesu Kristo angeketi chini pamoja nasi na kuomba maelezo ya usimamizi wetu, sina uhakika angesisitiza zaidi mipango na takwimu. Kile Mwokozi angetaka kujua ni nini hisia za moyoni mwetu. Angetaka kujua tunavyopenda na kuhudumia wale tulio na majukumu nao, vile tunavyoonyesha mapenzi kwa wenza na familia zetu na jinsi tunavyoifanya mizigo yao ya kila siku kuwa miepesi, na mwokozi angetaka kujua jinsi mimi nawe tunavyoweza kumkaribia Yeye na Baba yetu wa Mbinguni.
Kwa nini tupo hapa?
Inaweza kuwa ya kufaa kuchunguza mioyo yetu wenyewe. Kwa mfano, tungeweza kujiuliza wenyewe, kwa nini tunahudumia katika Kanisa la Yesu Kristo?
Tungeweza hata kuuliza, kwa nini tupo hapa kwenye mkutano huu leo?
Nadhani kama ningejibu swali hilo kijujuu, ningeweza kusema nipo hapa kwa sababu Rais Monson alinipanga nizungumze.
Na hivyo kwa kweli sikuwa na uchaguzi.
Licha ya hayo, mke wangu ananitazamia nihudhurie. Na jinsi gani naweza kusema hapana kwake?
Lakini sote tunajua kuna sababu nzuri zaidi kwa kuhudhuria mikutano yetu na kuishi maisha yetu kama wafuasi wenye msimamo wa Yesu Kristo.
Nipo hapa kwa sababu natamani kwa moyo wangu wote kumfuata Bwana wangu, Yesu Kristo. Ninatamani sana kufanya yote ambayo ananitaka mimi katika kusudi hili kubwa. Nina tamani kubadilishwa na Roho Mtakatifu na kusikia sauti ya Mungu wakati anaposema kupitia watumishi wake waliotawazwa. Nipo hapa kuwa mtu bora zaidi, kuinuliwa na mifano ya kuvutia ya ndugu zangu na dada katika Kristo, na kujifunza jinsi ya kwenda kiutekelezaji kuhudumia kwa hao wenye shida.
Kimsingi, Nipo hapa kwa sababu nampenda Baba yangu wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo.
Nina hakika hii ndiyo sababu yako vile vile. Hii ndiyo sababu tupo tayari kufanya dhabihu na sio tu matangazo ya kumfuata Mwokozi. Hii ndiyo sababu kwa nini tunabeba kwa heshima ukuhani Wake mtakatifu.
Kutoka Cheche mpaka Moto mkubwa.
Kama ushuhuda wako unastawi na wenye siha au shughuli zako katika Kanisa kwa karibu sana zinafanana na Kijiji cha Potemkin, habari njema ni kwamba unaweza kujenga kwa nguvu yako yeyote uliyonayo. Hapa katika Kanisa la Yesu Kristo unaweza kukomaa kiroho na kukaribia karibu kwa Mwokozi kwa kutumia kanuni za injili siku baada ya siku.
Kwa uvumilivu na ung’ang’anizi, hata tendo dogo sana la ufuasi au kiasi kidogo cha imani kinaweza kuwa moto mkubwa anaowaka wa maisha yaliyowekwa wakfu. Kwa kweli, hivyo ndivyo, karibu mioto mikubwa yote inavyoanza---kama cheche ndogo.
Kwa hiyo kama unajihisi mdogo na mdhaifu, tafadhali njoo kwake Kristo, ambaye anafanya vitu dhaifu kuwa vyenye nguvu.8 Aliye mdhaifu zaidi miongoni mwetu, kupitia neema ya Mungu, anaweza kuwa na nguvu kiroho, kwa sababu Mungu “haogopi watu.”9 Yeye ni “Mungu wetu mwaminifu ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake.”10
Ni imani yangu kwamba kama Mungu anaweza kunyoosha mkono na kumwidhinisha mkimbizi wa Kijerumani maskini kutoka familia isiyojivuna katika nchi iliyoharibiwa na vita mbali sana kutoka makao makuu ya Kanisa, aidha anaweza kunyoosha mkono wake kwako.
Ndugu zangu wapendwa katika Kristo, Mungu wa Uumbaji, aliyepumulia uhai ulimwengu, kwa hakika ana uwezo wa kupumua uhai kwako wewe. Kwa hakika anaweza kukufanya wewe kuwa mkweli, kiumbe wa kiroho mwenye nuru na ukweli unaotamani kuwa.
Ahadi za Mungu ni za uhakika na zisizo na shaka. Tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kusafishwa uovu wote.11 Na kama tukiendelea kukubali kwa ukamilifu na kuishi kufuatana na kanuni za kweli katika hali zetu za binafsi na katika familia zetu, mwishowe tutafika mahali ambapo hatutakuwa na “njaa tena, wala kuwa na kiu tena. … Kwa kuwa Mwana kondoo ambaye yupo katikati ya kiti cha enzi atatulisha [sisi], na atatuongoza [sisi] katika chemchemi ya maji ya uzima: na Mungu atapangusilia mbali machozi yote kutoka kwenye macho [yetu].”12
Kanisa ni Mahali pa Uponyaji, Sio Kujificha
Lakini hii haiwezi kutokea kama tukijificha nyuma ya sura za kinafi za kibinafsi, dini, taratibu. Hivyo ufuasi wa bandia hautuzuii tu kujiona sisi wenyewe kama tulivyo kikweli lakini pia unatuzuia kubadilika kikweli kupitia muujiza wa Upatanisho wa Mwokozi.
Kanisa sio chumba cha maonyesho ya magari---sehemu ya kujiweka wenyewe kwenye maonyesho ili kwamba wengine waweze kutazama na kupendezwa na mambo yetu ya Kiroho, uwezo, au baraka. Ni kama kituo cha huduma, ambako magari yanayohitaji kukarabatiwa yanakuja kwa matengenezo na kutengenezwa upya.
Na si, sisi wote, tunahitaji ukarabati, matengenezo, na ketengenezwa upya?
Tunakuja Kanisani sio kwa kuficha matatizo yetu bali yaponywe.
Na katika wajibu wetu kama tunaoshikilia ukuhani,t una wajibu wa ziada=== wa “kulisha kundi la Mungu… , sio kwa kukwazo, bali kwa radhi; sio kwa [faida binafsi], bali ya akili iliyo tayari, wala kama kuwa mabwana juu ya urithi wa Mungu, bali kuwa mifano kwa kundi.”13
Kumbuka, ndugu, “Mungu anapinga wenye kiburi, lakini anawapa neema wanyenyekevu.”14
Mashuhuri sana, hodari mno, mtu stadi sana ambaye aliwahi kutembea dunia hii alikuwa pia mnyenyekevu sana. Alifanya baadhi ya huduma zake za kuvutia sana katika wakati wake faragha, akiwa na waangalizi wachache tu, ambao aliwaambia “wasimweleze mtu yeyoyote” nini alichokifanya.15 Wakati mtu fulani alipomwita “mwema” haraka alielekeza kwingine hiyo sifa, akisisitiza kwamba Mungu pekee ni mwema kikweli.16 Kwa uwazi sifa ya ulimwengu haikumaanisha chochote Kwake; kusudi Lake la kipekee lilikuwa kumhudumia Baba Yake na “kufanya siku zote vitu hivyo ambavyo vinamfurahisha Yeye.”17 tungefanya vyema kufuata mfano wa Bwana wetu.
Na tupende kama Alivyopenda
Ndugu zangu, huu ni wito wetu wa juu na mtakatifu---kuwa wawakilishi wa Yesu Kristo, tupende kama alivyopenda, kuhudumia kama alivyo hudumia, “Kuinua juu mikono inayoning’inia na kuimarisha magoti dhaifu,”18 kuwatunza maskini na wenye mahitaji,”19 na kuwatunza wajane na yatima.20
Ninaomba, ndugu, kwamba wakati tunapohudumia katika familia zetu, akidi, kata, vigingi, jamii, na mataifa tutashinda majaribu ya kuvutia macho kwetu wenyewe na badala yake tutajitahidi kwa heshima kubwa: kuwa mnyenyekevu, wafuasi wa kweli wa Bwana na Mwokozi, Yesu Kristo. Wakati tunapofanya hivyo, tutajikuta wenyewe tukitembea katika njia ambayo inaelekea kwenye ubora wetu, ya kweli zaidi, na yenye hadhi zaidi. Kwa haya ninashuhudia katika jina la Bwana wetu,Yesu Kristo, amina.