2010–2019
Kujaza Nyumba Zetu na Nuru na Kweli
Aprili 2015


10:25

Kujaza Nyumba Zetu na Nuru na Kweli

Ili sisi na familia zetu tuweze kuhimili shinikizo la ulimwengu, ni sharti sisi tujazwe na nuru na ukweli wa injili.

Moyo wangu ulijawa na Roho nilivyosikiliza familia hizi zikifundisha ukweli huu mtakatifu, “Familia ni ya Mungu.” 1 Muziki wenye maongozi ni mojawapo wa njia nyingi ambazo tunaweza kumsikia Roho ikitunong’ozea, kutujaza nuru na ukweli .

Woman with 1 can of soda that is crushed and one that is not.

Dhana ya kujazwa nuru na ukweli ilikuwa muhimu hasa kwangu kwa sababu ya tukio nililopata miaka mingi iliyopita. Nilihudhuria mkutano ambapo wanachama wa bodi kuu ya Wasichana walifundisha juu ya kujenga familia na nyumba zenye nguvu ya kiroho. Ili kuonyesha hii, kiongozi wa Wasichana alishikilia makopo mawili ya soda. Kwa mkono mmoja alibeba kopo tupu na katika upande mwingine alibeba kopo lililofungwa na limejaa soda. Kwanza, akabonyeza lile kopotupu; lilianza kubonyea na kisha kukunjika kwa ajili ya presha. Kisha, kwa mkono wake mwingine, akabonyeza kopo lililiofungwa. Lilikuwa imara. Halikukunjika au kubonyea kama lile kopotupu---kwa sababu lilikuwa limejaa.

Tulifananisha maonyesho haya na maisha yetu binafsi na nyumba na familia zetu. Tunapojazwa na Roho na ukweli wa injili, tuna uwezo wa kuhimili nguvu za nje za ulimwengu unaotuzunguka na unaoshinikiza dhidi yetu. Hata hivyo, tusipojazwa kiroho, hatuna nguvu ya ndani ya kupinga shinikizo za nje na tunaweza kuanguka wakati nguvu hizo zinashinikiza dhidi yetu.

Shetani anajua kwamba ili sisi na familia zetu kuweza kuhimili shinikizo za dunia, lazima tujazwe na nuru na ukweli wa injili. Hivyo anafanya kila kitu katika uwezo wake kudhoofisha, kupotosha, na kuharibu ukweli wa injili na kututenga na ukweli huo.

Wengi wetu wamebatizwa na wamepata kipawa cha Roho Mtakatifu, ambaye jukumu lake likiwa ni kudhihirisha na kufundisha ukweli wa mambo yote. 2 Kupitia fursa ya kipawa hicho huja wajibu wa kutafuta ukweli, kuishi ukweli tunaoujua, na kuueleza na kutetea ukweli huu.

Sehemu moja ambapo tunatafuta kujazwa na nuru na kweli ni katika nyumba zetu wenyewe. Maneno katika kibwagizo cha wimbo tunaousikia yanatukumbusha, “Mungu alitupa familia ili kutusaidia kuwa kile Yeye anataka tuwe.” 3 Familia ni karakana ya Bwana duniani ya kutusaidia kujifunza na kuishi injili. Tunaingia katika familia zetu na wajibu mtakatifu wa kusaidia kuimarishana kiroho.

Familia za milele zenye nguvu na nyumba zilizojawa na Roho hazitokei tu. Zinahitaji juhudi kubwa, zinachukua muda, na zinahusisha kila mwanafamilia kutekeleza sehemu yake. Kila nyumbani ni tofauti, lakini kila nyumba ambako mtu mmoja anatafuta ukweli inaweza kuleta tofauti.

Tunaendelea kushauriwa kuongeza maarifa yetu ya kiroho kwa njia ya maombi na kwa kusoma na kutafakari maandiko na maneno ya manabii walio hai. Katika maongezi yake ya mkutano mkuu juu ya kupokea ushuhuda wa nuru na ukweli, Rais Dieter F. Uchtdorf alisema:

“Mwenyezi Mungu wa Milele ... atazungumza na wale ambao wanamwendea kwa moyo wa dhati na dhamira ya kweli.

“Atazungumza nao katika ndoto, maono, mawazo, na hisia.”

Rais Uchtdorf aliendelea: “Mungu anawajali ninyi. Atawasikiliza, na atajibu maswali yenu binafsi. Majibu kwa maombi yenu yatakuja katika njia yake mwenyewe na kwa wakati Wake mwenyewe, na kwa hiyo, mnahitaji kujifunza kusikiliza sauti Yake.” 4

Historia fupi ya familia inaonyesha ushauri huu.

Miezi kadhaa iliyopita nilisoma ushuhuda wa dada ya babu yangu mkubwa Elizabeth Staheli Walker. Kama mtoto Elizabeth alihamia Marekani kutoka Uswisi na familia yake.

Baada ya Elizabeth kuolewa, yeye pamoja na mumewe na watoto waliishi katika Utah karibu na mpaka wa Nevada, ambako waliendesha kituo cha barua. Nyumba yao ilikuwa ni mahali pa kupumzika kwa wasafiri. Mchana wote na usiku wote iliwabidi kujitayarisha kupika na kuwapa chakula wasafiri. Ilikuwa ni kazi ngumu, ya kuchosha, na walikuwa na mapumziko kidogo. Lakini jambo kubwa lililompa wasiwasi Elizabeth ilikuwa nimazungumzo ya watu walioshirikiana nao.

Elizabeth alisema hadi kufikia wakati huu yeye alichukulia kwa mzaha ya kwamba Kitabu cha Mormoni kilikuwa cha kweli, kwamba Nabii Joseph Smith alikuwa amepewa mamlaka na Mungu kufanya aliyoyafanya, na kwamba ujumbe wake ulikuwa ni mpango wa maisha na wokovu. Lakini maisha aliyokuwa akipitia hayakuwa yale ambayo yangeimarisha imani kama hiyo.

Baadhi ya wasafiri waliopitia hapo walikuwa wasomi sana, walioelimika, watu waungwana na kila mara majadiliano kwenye meza yake yalikuwa kwamba Joseph Smith alikuwa “mdanganyifu mjanja” aliyeandika Kitabu cha Mormoni mwenyewe na kisha kukisambazwa ili kutengeneza pesa. Walijifanya ni kama kufikiria kitu kingine chochote kilikuwa upuuzi, wakidai “kwamba Umormoni ulikuwa ni upuuzi mtupu.”

Mazungumzo haya yote yalimfanya Elizabeth kujisikia kutengwa na mpweke. Hakukuwa na mtu wa kuzungumza naye, hapakuwa na muda hata wa kusema sala zake---ingawaje aliomba alipokuwa akifanya kazi. Alikuwa na hofu mno kusema chochote kwa wale ambao waliidharau dini yake. Alisema yeye hakujua kama kile walichokuwa wakisema kilikuwa ni kweli, na alihisi hangeweza kutetea imani yake kama angejaribu.

Pioneer Family in front of a log home

Baadaye, Elizabeth na familia yake walihama. Elizabeth alisema alikuwa na muda mwingi wa kufikiria na wala hakuvurugwa mawazo wakati wote. Mara nyingi alienda kwenye ghala ya chini na kuomba kwa Baba wa Mbinguni kuhusu kile kulichokuwa kikimsumbua---kuhusu zile hadithi ambazo wale watu walioonekana kama waungwana walimwambia kuhusu injili kuwa ni upuuzi mtupu na kuhusu Joseph Smith na Kitabu cha Mormoni.

Usiku mmoja Elizabeth alikuwa na ndoto. Alisema: “Ilionekana kama nilisimama kando ya barabara nyembamba ya gari, ambayo ilielekea chini mwendo nusu kilimani, katikati ya mlima niliona mtu akiangalia chini na kuzungumza, au kuonekana anazungumza na kijana ambaye alikuwa amepiga magoti, na akiegemea juu ya shimo ardhini. Mikono yake Ilinyooshwa na alionekana kama alikuwa anafikia kitu kutoka shimoni. Ningeiliona funiko la mawe lililoonekana kutolewa kutoka shimoni ambako kijana alikuwa ameinama. Barabarani kuliwa na watu wengi, lakini hakuna hata mmoja wao aliyeonekana kuvutiwa na vijana wawili waliokuwa juu ya mlima. Kulikuwa na kitu kilichofuatana na ndoto kilichonivutia kiajabu mpaka nikaamka; ... Sikuweza kumwambia mtu yeyote ndoto yangu lakini nilihisi kuridhika kwamba ilimaanisha malaika Moroni akimfundisha kijana Joseph wakati ule alipoyapata ya mabamba.”

Katika majira ya kuchipua ya 1893, Elizabeth alienda Mji wa Salt Lake kwa kuwekwa wakfu hekalu. Alielezea uzoefu wake: “Huko ndani niliona picha hiyo hiyo ambayo nilivyoona katika ndoto yangu, nadhani ilikuwa ni dirisha la kioo lenye rangi. Nahisi kuridhika kwamba niliona Kilima Kumora chenyewe, haingekuwa halisi zaidi ya hivyo. Nahisi kuridhika kwamba nilionyeshwa katika ndoto picha ya malaika Moroni akimpa Joseph Smith mabamba ya dhahabu.”

Old portrait of Elizabeth Staheli

Miaka mingi baada ya ndoto hii na miezi kadhaa kabla ya kufariki karibu umri wa miaka 88, Elizabeth alipokea msukumo mkali. Alisema, “Wazo lilinijia kwa wazi ... ni kama mtu alikuwa ameniambia, ... ‘Usizike ushuhuda wako ardhini.’”5

Vizazi baadaye, uzao wa Elizabeth unaendelea kuchota nguvu kutoka katikaushuhuda wake. Kama Elizabeth, tunaishi katika ulimwengu wa wenye kutilia mashaka wengi na wakosoaji ambao hukejeli na kupinga ukweli tunaoshikilia kwa dhati. Tunaweza kusikia hadithi zenye kukanganya na jumbe za kutatanisha. Pia kama Elizabeth, itabidi tufanye tuwezavyo ili kushikilia nuru na ukweli wowote tulionao kwa sasa, hasa katika mazingira magumu. Majibu kwa maombi yetu hayawezi kuja kwa kasi, lakini ni lazima tupate wakati mtulivu wa kutafuta nuru kuu na ukweli. Na tunapoipokea, ni jukumu letu kuiishi,kuishiriki, na kuitetea.

Nawaachieni na ushuhuda wangu kwamba najua tunapojaza mioyo yetu na nyumba zetu na nuru na ukweli wa Mwokozi, tutakuwa na nguvu ya ndani ya kuhimili katika kila hali. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. “The Family Is of God,” in 2014 Outline for Sharing Time: Families Are Forever (2013), 28–29.

  2. Ona Moroni 10:5.

  3. “Familia ni ya Mungu”

  4. Dieter F. Uchtdorf, “Receiving a Testimony of Light and Truth,” Ensign au Liahona, Nov. 2014, 21.

  5. Ona Elizabeth Staheli Walker, “My Testimony, Written for My Children and Their Children after I Am Gone,” 1939, 22–26, University of Nevada, Las Vegas, Special Collections; vituo vya uandishi, erufi kubwa na tahajia ni za kipeo sanifu.